Tottenham yawalaza Arsenal mabao 2 kwa 1 huku Gunners ikichukua nafasi ya tisa katika jedwali ya ligi kuu

Ni mchuano ambao wengi walitabiri na kusema Gunners wataibuka washindi. Tottenham waliwapa Arsenal kichapo cha mabao mawili kwa moja.

Tottenham Hotspur wameongeza nafasi yao ya kushiriki mtanange wa Bara Ulaya kufuatia ushindi wao wa 2-1 dhidi ya Arsenal katika debi ya London.

Chelsea yawalaza Crystal Palace mabao 3 kwa 2 na kuchukua nafasi ya tatu kwenye jedwali

Mabao kutoka kwa Son Heung-Min na Toby Alderweireld yalitosha Spurs kusajili ushindi mkubwa nyumbani siku ya Jumapili, Julai 12.

 

Mabao hayo mawili yalipelekea bao la kwanza la Alexander Lacazette kuwa la kufutia machozi huku Gunners wakihangaika kutafuta bao la kusawazisha katika mechi hiyo. Mechi hiyo ilikuwa ya kwanza kwa Jose Mourinho na Mikel Arteta katika debi ya London huku wakufunzi hao wakiingia kwenye mchezo huo wakiwa wametiwa adhabu.

57c5aac838087111(1)

Spurs walikuwa kwenye mchakato wa kuwarejeshea mashabiki wao matumaini kufuatia matokeo yao mabovu tangu kurejea kwa ligi hiyo.

Lakini Gunners ndio walitingisha wavu wa kwanza baada ya Alexander Lacazette kuvurumisha kombora kali lililompita Hugo Lloris na kufanya matokeo kuwa 1-0.

 

Ecvk4BFXoAMOai-

Matokeo hayo yaliwashuhudia Spurs wakisonga mbele ya Arsenal katika nafasi ya nane na pointi 50 huku vijana wa Mikel wakishuka hadi nafasi ya tisa na matumaini yao ya kushiriki mashindano ya bara Ulaya yakizimwa

Arsenal, mashetani wekundu wawika ligi ya EPL

 

Mason Greenwood alifunga mara mbili katika ligi ya premia kwa mara ya kwanza huku Man United ikitoka nyuma na kuilaza Bournemouth 5-2 na kuongeza matatizo ya klabu hiyo inayokaribia kushushwa daraja.

Greenwood mwenye umri wa miaka 18 aliwasawazishia wenyeji baada ya goli lililofungwa na Junior Stanislas kuishangaza Man United kunako dakika ya 15 kabla ya kuifungia United goli lake la nne baada ya kipindi cha kwanza .

Marcus Rashford alikuwa ameiweka United 2-1 juu kutoka mkwaju wa penalti kabla ya Anthony Martial kufunga bao zuri kabla ya kipindi cha kwanza kukamilika.

Katika mechi ilioja mbembwe za kila aina , Joshua King aliifungia timu yake goli la pili kupitia mkwaju wa penalti dakika nne baada ya kipindi cha mapumziko. Kikosi hicho cha Edie Howe , kilifunga goli la kusawazisha ambalo lilikataliwa kwa kuwa la kuotea.

Wakati huohuo Arsenal iliishangaza klabu ya Wolves ugenini na kuimarisha matumaini yake ya kufuzu katika mashindano ya klabu bingwa Ulaya baada ya kuwalaza wenyeji wao 2-0 katika uwanja wa Molineux.

Kinda wa Gunners Bukayo Saka, ambaye alitia saini kandarasi mpya siku ya Jumtano alianza kuifungia klabu yake .

Adama Traore aliharibu nafasi bora zaidi ya kusawazisha , kabla ya Alaxandre Lacazette kuingia kama mchezaji wa ziada na kufunga bao la ushindi.

Arsenal ilipanda hadi katika nafasi ya saba huku ikiwa pointi tatu nyuma ya Wolves.

-BBC

David Luiz: Defenda wa Arsenal asema kushindwa kwao mabao 3-0 na Mancity ni kwa sababu ya makosa yake

Mlinzi wa kilabu ya arsenal  David Luiz  amekubali kuwajibikia  kushindwa kwao mabao 3 kwa  nunge na Manchester City  lakini  akasema yungali ana matumaini ya kuichezea kilabu hiyo.

Luiz,  ambaye mkataba wake unatamatika mwishoni mwa mwezi huu  aliondolewa uwanjani ili kutamatisha kurejea kwake uwanjani kuliozongwa na makosa chungu  nzima .

“Ni makosa yangu, timu ilifanya vyema  hasa ikiwa na wachezaji 10  kocha pia yuko sawa na yote ni kwa ajili ya makosa yangu” amesema mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 33.

“Nataka kusalia hapa. Kocha anafahamu hilo ma anataka nisalie  hapa.”

Luiz alijiunga na Arsenal  kipindi kilichopita cha uhamisho  kutoka Chelsea  kwa pauni milioni 8  na alikuwa ameachwa katika benchi  dhidi ya City kwa ajili ya kutoeleweka kuhusu hali ya mkataba wake.

Aliingia uwanjani katika dakika ya 24  baada ya  kujeruhiwa kwa  Pablo Mari na alifanya masihara yaliompa bao la kwanza   Raheem Sterling.

Kisha baadaye alihusika na kumbwaga chini Riyad Mahrez na kusababisha penalty  na kuonyeshwa  nje ya uwanja. Kufurushwa kwake kutoka mechi hiyo kunamaanisha ameichezea arsenal mchuano wake wa mwisho endapo hatazidisha mkataba wake.

 

Arsenal Yakung’utwa magoli 3 na Man City

Matumaini ya Arsenal ya kumaliza miongoni mwa vilabu nne bora ilipata pigo kufuatia ushindwa wa 3-0 kwa Man City ugani Etihad.

Mechi hiyo ya Jumatano, Juni 17 usiku, ilikuwa siku ya pili tangia Ligi Kuu kurejea baada ya kusitishwa kwa wiki kadhaa.

Huku Man City wakiwa tayari nje ya kinyang’anyiro cha kutwaa taji, Arsenal ndio walikuwa wakikaza kamba ili kujipatia tiketi ya kushiriki Ligi ya Mabingwa.

Hata hivyo, hayo yalitibuka, huku Gunners wakikumbana na majeraha mawili kwa mpigo dakika chache kabla ya mechi hiyo.

Granit Xhaka ndiye alikuwa wa kwanza kuondoka uwanjani dakika tano kabla ya mechi kuanza baada ya kupata jeraha la mguu.

Nafasi yake ilichukuliwa na Dani Ceballos ambaye alijiunga na David Luiz kutoka kwenye benchi dakika 22 baada ya Pablo Mari kupata jeraha.

Lakini kushirikishwa kwa Luiz ndio ilikuwa mwanzo wa mikosi ya Arsenal, huku utepetevu wa difenda huyo Mbrazil ukimruhusu Raheem Sterling kufunga bao la kwanza kabla ya muda wa mapumziko.

City iliwatinga bao lao lingine dakika nne baada ya awamu ya pili kuanza kupitia kwa Kevin de Bruyne ambaye alifunga bao baada ya Luiz kusababisha penalti.

Kisa hicho kilimshuhudua difenda huyo wa zamani wa Chelsea kulishwa kadi nyekundu kwa kumchezea visivyo Riyadh Mahrez.

 

Michezo! Wachezaji wa Arsenal wakataa kupunguza mishahara yao

NA NICKSON TOSI

Kikosi cha Kwanza cha Arsenal kimepusilia mbali pendekezo la Usimamizi wa klabu hiyo la kutaka kupunguziwa mshahara wao kwa asilimia 12.5 kwa muda wa mwaka mmoja kufuatia hasara waliyosajili wakati huu ambapo hakuna shughuli zozote za  ligi kuu ya Uingereza zinazoendelea.

Hatua ya kupunguza mshara wa wachezaji wa Arsenal ilionekana kama ya kupunguzia gharama uongozi wa klabu hiyo haswa wakati huu ambapo ligi takriban zote ulimwenguni zimesitishwa kutokana athari ambazo zimetokana na Corona.

Mesut Ozil is the biggest earner at Arsenal

 Baadhi hya wachezaji wanaolipwa mishahara nono katika klabu hiyo ya Ungereza ni Mesut Ozil anayelipwa £350,000, Pierre-Emerick Aubameyang na  Alexandre Lacazette  £200,000 .

Ligi kuu ya Uingereza ilisitishwa baada ya wachezaji na mameneja wa timu mbalimbali kupatikana na virusi vya Corona, hali iliyofanya shirikisho la soka la Uingereza FA na usimamizi wa Premier league kusitisha ligi hiyo kwa ghafla.

Aidha timu na wachezaji wamekuwa wakishauriwa na wakuu wa serikali kukubali kupunguziwa mishahara kwa asilimia 30 ili kutoa mchango kwa serikali kufanikisha shughuli za kutoa huduma kwa wananchi wa taifa hilo ambalo limeathirika pakubwa na virusi vya Corona.

Wachezaji wa Arsenal kusalia nyumbani licha ya mkufunzi Mikel Arteta kupona

NA NICKSON TOSI

Usimamizi wa klabu ya Arsenali umewataka wachezaji wa klabu hiyo kusalia nyumbani licha ya mkufunzi wao Mikel Arteta  kupona baada ya kuwa chini ya uangalizi kutokana na virusi vya Corona.

Taarifa za awali zilikuwa zimedai kuwa wachezaji wa kikosi cha kwanza na baadhi ya maafisa wa kiufundi walikuwa wanatarajiwa kurejelea mazoezi yao jumanne 14 mwaka huu.

Hatua hiyo ilichukuliwa baada ya serikali ya Uingereza kutaka klabu zote katika taifa hilo kusitisha shughuli za mazoezi kama njia ya kukabiliana na Corona .arteta

Klabu zingine zimedinda kuwarudisha wachezaji wao kwenye kambi baada ya virusi vya Corona kuathiri maeneo kadhaa ya miji ya Uingereza .

Meneja wa Arsenal Mikel Arteta ndiye aliyekuwa wakwanza kuambukizwa virusi hivyo,hatua iliyofanya shirikisho la Soka Uingereza FA kufutilia mbali mitanange kadhaa ili kupunguza virusi hivyo kuenea zaidi kwa wachezaji wengine.

Picha ya siku: Jamaa afunga harusi akiwa amevalia sare ya Arsenal

Jamaa mmoja amewashangaza wengi na kufurahisha wengine baada ya kuchapisha picha zake na mkewe mtandaoni, baada ya kufunga harusi.

Kilicho shangaza na kufurahisha ni kuwa kinyume na bwana harusi wengi ambao huvalia suti, yeye aliamua kuadhimisha siku hiyo akiwa amevalia sare za Arsenal.

Ndoa ya Sekunde; Mwanahabari wa runinga ya Inooro asimulia jinsi ndoa yake ilivunjika

Ni dhahiri kuwa jamaa huyo ni shabiki sugu wa Arsenal na licha ya timu hiyo kuwa na msimu mbaya, aliamua hilo halitamzuia kufurahia harusi yake na timu anayoipenda.

Isitoshe alihakikisha kuwa amevalia sare ya Arsenal ya nyumbani (nyekundu) na ya ugenini (njano)

Alichapisha picha zile na ujumbe uliosema; I Love you home & away (Nitakupenda nyumbani na mbali na nyumbani au ugenini). Kisoka, timu zote duniani lazima zicheze mechi dhidi ya mahasimu wao, nyumbani kwao na pia ugenini.

Dennis Okari na mkewe Naomi washerehekea mwaka mmoja tangu wafunge ndoa 

Tazama picha zifuatazo;

arsenal away Arsenal

Arsenal

Lacazette huenda akahamia Atletico Madrid huku Lemar akijiunga na Gunners

Mshambulizi wa Arsenal Alexandre Lacazette huenda akasajiliwa na Atletico Madrid iwapo watashindwa kumsajili Edison Cavani wa Paris Saint-Germain. Afisa mkuu wa Atletico Miguel Angel Gil Marin alikutana na rais wa PSG Nasser Al Khelaifi jijini Paris jana kujadili uhamisho wa Cavani uliopendekezwa.

Mkataba wowote kati ya Arsenal na Atletico unaomhusisha Lacazette kuhamia Uhispania una maana pia huenda kiungo wa Ufaransa Thomas Lemar akahamia Emirates. Lemar amekua na wakati mgumu tangia kuhamia Madrid kutoka Monaco msimu uliopita.

Liverpool wamepigwa jeki na kuregea kwa Fabinho kwenye mazoezi,  na huenda akacheza katika mechi yao dhidi ya Manchester United wikendi ijayo. Raia huyo wa Brazil amekua nje na jeraha la mguu kwa wiki sita lakini sasa amekamilisha matibabu yake na amekua akifanya mazoezi kwa siku kumi zilizopita. Amesema pia sasa yuko tayari kujiunga na mazoezi kamili na kikosi cha kwanza ili aweze kuregea kucheza.

Shirikisho la FKF jana lilizindua Betways kama mfadhili wao mpya wa kombe la Betways FKF kwa mkataba wa miaka mitatu kwa kitita cha shilingi milioni 45.

Mabingwa Bandari wataanza kutetea taji lao kwa mchuano dhidi ya KSG Ogopa FC  katika raundi ya 32. Katika droo hio Gor Mahia watapambana na mshindi kati ya Kariobangi Sharks ‘B’ na Naivas FC, huku mahasimu wao AFC Leopards wakipambana na mshindi kati ya Elimu FC na KUSCO.

Zoo Youth watapambana na Sindo United huku mshindi akikabana na KCB.

Rais wa FKF Nick Mwendwa anasema ufadhili huo umekuja kwa wakati ufaao na utaboresha soka mashinani. Ufadhili huu unajiri baada ya kampuni ya Sportpesa kujiondoa kutokana na kile walichokitaja kuwa kutozwa ushuru wa juu mno.

 

Tulipeni milioni moja ili tuwachilie Arteta! Man City yaagiza wanabunduki

Manchester City wanataka walipwe pauni milioni moja ili wavunje mkataba na kocha wao msaidizi Mikel Arteta – Arsenal wanataka kumtangaza Arteta kama kocha wao mkuu mpya. (Mail)

Liverpool wanatarajiwa kutupilia mbali mipango ya kumsajili mshambuliaji wa Ujerumani na klabu ya RB Leipzig Timo Werner, 23, baada ya kufikia makubaliano ya kumsajili mshambuliaji wa Japani na klabu ya Red Bull Salzburgforward Takumi Minamino, 24. (Star)

Mwenyekiti wa klabu ya Tottenham Daniel Levy amedai kuwa Spurs “hawaogopi” kumuuza kiungo mchezeshaji raia wa Denmark Christian Eriksen, 27, kwa timu pinzani za England mwezi ujao. (Evening Standard)

Christian Eriksen

Carlo Ancelotti anatarajiwa kutangazwa kama kocha mpya wa Everton baada ya kusaini mkataba wa pauni milioni 11.5 kwa mwaka. (Mirror)

Juventus wanatarajiwa kumbakiza beki wao raia wa Uturuki Merih Demiral, 21, licha ya klabu kadhaa za ligi ya Primia na pia AC Milan kuonesha nia ya kutaka kumsajili. (Calciomercato)

Paris St-Germain wanatarajiwa kusuka mipango ya kumsajili Pep Guardiola kama mbadala wa kocha wao wa sasa Thomas Tuchel. (Le 10 Sport via Daily Mail)

Winga Mjerumani Leroy Sane, 23, anataka kuhamia miamba ya nyumbani kwao Bayern Munich na anapiga hesabu za kuihama Manchester City mwezi Januari. (Bild via Mirror)

-BBC

Man City wakerwa na hatua ya Arsenal kumfuatilia Mikel Arteta

Manchester City wamekerwa na hatua ya Arsenali ya kumfuatilia kocha wao msaidizi Mikel Arteta na wameionya klabu hiyo kuwa itawabidi watoe donge nono ili wamnyakue kocha huyo.

Aidha, Arteta anatarajiwa kukutana na kiongozi mkuu wa Arsenal Josh Kroenke kwa ajili ya kufanya usajili wa tatu na wa mwisho huku akikaribia kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Unai Emery aliyetimuliwa mwezi uliopita.

Hata hivyo, Arteta yuko tayari kuacha wadhfa wake na kuchukua hatamu kama kocha wa Arsenali. Mzaliwa huyo wa Uhispaia ambaye hapo awali alichezea Arsenali alifanya mazungumzo na wasmamizi wa klabu hio ya London na inaaminika bado wanasubiri kumpiga msasa zaidi kabla ya kuteuliwa.

Kocha wa zamani wa Real Madrid, AC Milan  na Chelsea Carlo Ancelotti ameafikia makubaliano na klabu ya Everton ili kuchukua hatamu kama kocha mkuu.

Mazungumzo hayo yalifanyika jana baada ya Muitaliano huyo kuwasili Uingereza, siku kadhaa baada ya kufutwa kazi kama kocha wa Napoli.

Ancelotti amesalia na makubaliano ya sheria na masharti tu kabla ya kuchukua rasmi mahala pa Marco Silva ambaye alichujwa wiki mbili zilizopita.

Hata hivo kocha wa muda Duncan Fergusson atasalia kama msaidizi wake.

Wilfred Zaha alisawazishia Crystal Palace katika dakika ya 76 dhidi ya Brighton na kuhakikisha mechi hiyo ya ligi kuu Uingereza iliishia sare ya 1-1. Neal Maupay alikua ameweka Brighton kifua mbele katika kipindi cha pili ya mechi hio ya kusisimua.

Brighton wamesalia katia nafasi ya 13 kwenye jedwali huku Palace wakiwa katika nafasi ya tisa baada ya mechi 17.