(+ Video) Harmonize a-copy paste Baba Lao ya Diamond Platnumz, video mpya

Staa wa Bongo Harmonize almaarufu kama Konde Boy ameachilia video ya wimbo wa Kushoto Kulia.

Video hii ina nembo ya lebo yake ya Konde Gang tofauti na kazi za awali zilizokuwa na nembo ya WCB.

WCB inayoongozwa na Diamond imemlea na kumkuza Harmonize.

Rayvanny adondosha Remix ya Tetema na mastaa wakubwa Afrika

 Audio ya Kushoto Kulia imefanywa na producer wawili Bonga huku video ikiongozwa na Hascan.

Idea au concept ya video inaonekana kufanana na ya Baba Lao ya Diamond Platnumz.

Katika video ya Harmonize, kuna sehemu na ambapo yupo katikati mwa watu waliojifunga buibui nyeusi.

Dakika 5 tu niage dunia, Msanii wa nyimbo za injili Roz Haki afunguka

Video ya Baba Lao ilitangulia kudondoka huku Diamond Platnumz akionekana kati ya watu waliovaa suti na kujifunga vitambaa vyeupe.

Ni juzi tu Harmonize alikuwa katika ubishi wa midundo ya UNO na mtayarishaji wa nyimbo Magix Enga almaarufu kama Beat King.

Magix Enga hatimaye alitangaza kumsamehe.

Akichapisha ujumbe kwenye Insta, Enga alitangaza kuwa walimaliza tofauti zao.

Kuna uwezekano pande mbili zilipatana baada ya ubishi kuwepo kuhusu mdundo wa ngoma hiyo.

 Katika video hiyo, Enga anasikika akiuliza maafisa hao “Mnanikamatia nini mazee kama wimbo ya Harmonize tayari iko YouTube.”

Yote tisa, concept ni ileile.

Sio mara ya kwanza Konde Boy kutuhumiwa kumuiga Diamond ata jinsi anavyoimba na kunengua katika video zake.

 

Diamond Platnumz kuiba mdundo wa ngoma ya Soapy, S2Kizzy aelezea

Producer wa mkwaju wa ‘Baba Lao’ ya Mondi ametokezea na kufunguka kuhusu midundo ya ‘Baba Lao’ na ‘Soapy’ ya Naira kufanana.

Akihojiwa na kituo cha Wasafi FM nchini Tanzania, S2Kizzy amesema kuwa waliomba ruksa ya kuimba na mdundo huo.

Producer huyu ameeleza kuwa alivutiwa zaidi na mdundo wa Naira katika ngoma ya Soapy.

(+ Video) Diamond Platnumz ampiga Ali Kiba chambo kali, BABA LAO

“Wakati tukiwa Madagascar mimi Diamond. Tulienda na studio ndogo siunajua sisi ni watu wa muziki tukawa tunagonga mawe tu. Tulikuwa tumekaa tunagonga ngoma fulani slow hivi.” S2Kizzy.

“Pale tulipokuwa tumekaa palikuwa na TV inaonesha chaneli fulani hivi,  mara ikapita ngoma fulani ya Naira Marley ‘Soapy’ tukasema mbona kama ngoma ina vibe fulani hivi..Na siku tunaweza kufanya ngoma kama hii. Basi tukaona ngoja tufanye ngoma kama hii halafu tutawasiliana nao wenyewe. Kwa hiyo tukawa inspired na wimbo wa Naira Marley unaitwa ‘Soapy’, Kwa tukaona tunaweza tukaweka maneno yetu, Vibe letu na vitu vyetu lakini kwenye type ya muziki kama huo.” alisimulia S2Kizzy.

(+ Video ) Mpiga picha Collins Kweyu afunguka baada ya kichapo na Mike Sonko

Aidha, S2Kizzy amesema kuwa ana nyimbo kama 40 zake Diamond Platnumz.

Kwenye ngoma hizi zote ni za kimataifa.

S2Kizzy anasema kuwa kuna producer wengi Afrika wanaomtafuta Diamond Platnumz.

(+ Video) Diamond Platnumz ampiga Ali Kiba chambo kali, BABA LAO

Staa na nyota mkubwa wa muziki Afrika Diamond Platnumz amedondosha mkwaju mpya Baba Lao.

Aidha katika mistari ya Diamond Platnumz, mistari ipo inayoonekana kumlenga Ali Kiba kuhusu bifu yao iliyotamba katika mitandao ya kijamii.

“Ame-force bifu…eeh tumemkwepa…anabaki masononeko”

Jamaa apokea kichapo kwa madai ya kuhonga wapiga kura, Kibra

Huu ni mstari ambao upo kwenye ngoma hiyo.

Midundo ya muziki huu inadaiwa kuwa sawa na wimbo wa Soapy wake Naira Marley.

Kufanana kwa ngoma hizi mbili zimeifanya ngoma ya Diamond Platnumz kupata nafasi kubwa katika soko la muziki Nigeria.

Ngoma yake Diamond ina masaa kumi na 16 tangu iachiliwe kwenye mtandao wa YouTube.

Kati ya mistari kwenye Baba Lao, staa huyu anasifia lebo ya Wasafi na kutoa michambo inayoonekana kumlenga Kiba.

(+ Picha) Levis Saoli atua Citizen TV, alichokisema Nimrod Taabu,Joe Ageyo

 

Je,unadhani Mondi katoka na midundo ya Soapy? Dondosha maoni yako hapo chini?