Rais Kenyatta apokea risala ya kheri njema kutoka kwa Baba Mtakatifu

Rais Uhuru Kenyatta amepokea risala ya kheri njema na baraka kutoka kwa Baba Mtakatifu Francis.

Baba Mtakatifu alituma risala hiyo alipopita anga ya Kenya akiwa safarini kurejea mjini Roma baada ya kukamilisha ziara yake kwa mataifa matatu ya Msumbiji, Madagascar na Mauritius.

Katika risala yake ilyotumwa kwa njia ya redio na kunukuliwa na wadhibiti wa Safari za Ndege wa Kenya, Baba Mtakatifu ambaye ni kiongozi wa kanisa Katoliki ulimwenguni alitangaza baraka za amani na kheri njema kwa taifa la Kenya.

Pope Francis aanza ziara barani Afrika

“Rais Uhuru Kenyatta, natoa salamu zangu za kheri njema kwako na watu wa Kenya baada ya ziara yangu ya utume katika nchi za Msumbiji, Madagascar na Mauritius.”

“Nawaombea baraka za amani na maisha mema,” kasema Baba Mtakatifu Francis.

Baba Mtakatifu aliwasili jijini Maputo, nchini Msumbiji tarehe 4 Novemba kwa ziara ya siku tano katika mataifa ya kusini mwa Jangwa la Sahara ambapo alizuru Madagascar kwa siku mbili na kukamilishia ziara yake nchini Mauritius.

Baba Mtakatifu Francis alizuru Kenya mwezi wa Novemba mwaka wa 2015 katika ziara yake ya kwanza barani Afrika na kuwa Baba Mtakatifu wa pili kuzuru Kenya baada ya Baba Mtakatifu John Paul II aliyezuru Kenya mara tatu.

‘Kanisa langu ni la wezi na kahaba,’ mchungaji Francis Maina

Baba mtakatifu kufanya mazungumzo na rais Kenyatta wakati wa ziara yake

Picha kwa hisani ya: redpepper.co.ug

Baba mtakatifu Pope Francis atafanya mazungumzo na rais Uhuru Kenyatta siku ya kwanza ya ziara yake.

Pope Francis ambaye atawasili humu nchini tarehe 25 mwezi November pia atakutana na maafisa wa serikali kabla ya kuhutubia taifa.