Bifu yaibuka baina ya Harmonize na Diamond kuhusu ni yupi mkali kati yao

NA NICKSON TOSI

Harmonize amekua akifanya bidii zaidi tangu aondoke lebo ya WCB inayoongozwa na Diamond, na sasa wasanii hao wameonekana kama watu ambao hawapatani siku hizi  licha ya Diamond kusifia hatua ya Harmonize ya kutoa albamu ya nyimbo 18.

Kama mkurugenzi mkuu wa lebo ya Konde Music Worldwide, Harmonize alimshukuru Mola kwa kumwezesha kuwa na kampuni yake kibinafsi na hata mafanikio ambayo ameyafikia tangu aanze muziki.

Hata hivyo hatua ya Harmonize ya kufunganya virago na kutoka lebo ya WCB, ilichukuliwa kama hatua ya kujiendeleza kimuziki japo uamuzi huo wake ulimfanya kupoteza marafiki katika lebo ya WCB.

91858059_2302796276689690_3610394646334949909_n

Siku chache tu baada ya Diamond kuonyesha kwenye mitandao ya kijamii kasri lake ambalo anaishi kwa sasa, Harmonize hakusalia nyuma kwani alitundika picha ya msanii ambaye amemwandika chini ya Lebo yake kisha kuonyesha jumba la kifalme ambalo anaishi ndani, swala ambalo lilionekana kama njia ya kumjibu Diamond kuwa wapo wengi waliofanikiwa zaidi ya yeye.

Harmonize amemsajili msanii Ibraah ,ambaye kando na kuimba ni mwandishi wa nyimbo tena.

 

 

92708372_632859727567836_5106212880359356991_n

Baadhi ya picha alikuwa ametundika Diamond akiwa kwa makazi yake ndizo hizi hapa.

82046196_1786498221480206_6066164588906833824_n

Harmonize hakusita kuonyesha wafuasi wake naye kasri ambalo anaishi ndani na baada ya kuona picha hiyo ya Diamond, alimua kufichua ukubwa wa nyumba yake.

Inadaiwa kuwa bifu baina ya wasanii hao wawili ilianza baada ya Harominze kuanza kuwasajili wasanii wapya, hali iliyomfanya Diamond kusema kuwa amemsajili Zuchu msanii chipukizi na mwanawe Hadija Kopa kwenye Lebo ya WCB.

 

MHARIRI: DAVIS OJIAMBO

Anaweza ama hawezi? Kutana na Malkia wa WCB Zuchu, saunti mpya ya Bongo fleva

Lebo ya wasafi  ina kipusa mpya, Zuchu  ambaye amekuja kwa kasi na nguvu zote. Zuchu amejiunga na lebo hiyo ya msanii Diamond Platinumz na  ni  binti yake mwanamuziki maarufu wa taarab kutoka Bongo Khadija Kopa.

Alikiba amchokoza Diamond kwa kufichua anavyompenda ‘baby mama’ wake Hamisa katika video mpya

zuchu 2

Good life: Mkewe Mike Sonko Primerose Mbuvi aonyesha jumba lake la kifahari

Kupitia kumbi zao za mitandao ya kijamii  WCB wamemtambulisha Zuchu kwa mashabiki wao kwa kuandika ;

WE INTRODUCE TO YOU THE NEW QUEEN OF BONGO FLEVA||

ZUCHU Ni mtoto wa Malkia Mwenye Sauti ya Kasuku @khadijakopa.
Amepikwa akapikika
Sasa Ni Muda wa Dunia Kufurahia kipaji Hiki Kipya kutoka Tanzania.

Ladies & The Gentleman Rasmi Tunamtambulisha Kwenu Msanii Mpya @officialZuchu Katika Label Yetu Ya @wcb_wasafi .

Tafadhali kwa Heshima na Taazima Tunawaomba Watanzania Mumpokee na Kusheherekea Kipaji chake. .

Wicked Family! Jinsi Diamond na familia yake ilivyomhadaa Tanasha kwamba yeye ndiye Tosha


#TheNewQueenOfBongoFleva #KaribuZuchu #WelcomeZuchu
#Wcb_wasafi
#WCB4LIFE
Cc @boomplaymusic_tz

Mtazame Malkia huyu anayeleta sauti freshi katika bongo fleva

 

zuchu 3

 

MHARIRI: DAVIS OJIAMBO

Covid 19 Survivors: Wafahamu Baadhi ya watu waliopona Virusi vya Corona

Virusi vya Corona vimesababisha  msukosuko mkubwa kote duniani huku nyanja zote zikiathiriwa na kila  upeo wa maisha ya  binadamu ukitikiswa. Licha ya maafa ya watu  zaidi ya  48,000 kote duniani ,  zaidi ta watu laki mbili wamepona ugonjwa huo . Hii hapa orodha  ya watu unaowajua ambao wamepona virusi vya Corona

Masaibu ya Corona! Mfalme wa Thailand ajifungia kwenye karantini na wanawake 20

BRENDA AND BRIAN

 Brenda Cherotich na  Brian

Brenda Cherotich na Brian  ni miongoni mwa watu  watatu nchini Kenya ambao wamepona virusi vya Corona .Wawili hao siku ya  Jumatano walizungumza na rais Uhuru Kenyatta kupitia njia ya video na kulitangazia taifa jinsi walivyojipata na virusi hivyo na muda wao katika karantini. Brenda alieleza jinsi ugonjwa huo unavyoweza kukabiliwa na kuwahimiza wakenya walio na daalili za virusi vya Corona kuwa na ujasiri wa kujitokeza mapema ili kupata usaidizi wa matibabu .

MWANA FA

Mwana FA

Mwanamuziki huyo wa  bongo aliwashangaza  mashabiki wake kwa kutangaza kupitia instagram kwamba alikuwa amepatikana na virusi vya Corona . Alijitega katika karanti kwa muda alioshauriwa na madaktari na baadaye akatangaza kupona . Waziri wa Afya wa Tanzania Ummy Mwalimu  alithibitisha kwamba Mwana FA ndiye aliyekuwa mgonjwa wa kwanza nchini humo kupona virusi vya COVID 19 .

‘Tutakutana tena’ Kipusa Mjane amkumbuka mume wake Bilionea Reginald Mengi

 

salaaam sk

 Salaam SK

Maneja huyo  wa msanii wa Bongo Diamond Platinumz  alikuwa  miongoni mwa watu mashuhuri waliopatikana na virusi vya Covid 19 . Tangazo kwamba Salaam  alikuwa na virusi  hivyo lilimpelekea Diamond pia kuingia karantini  ili kujitenga na uwezekano wa kuambukizwa. Baadaye hata hivyo Salaama aliibuka na habari njema kwamba ameweza kupona virusi vya Corona .

 

Kenya hadi Bongo: Collabo 5 bora zaidi mwaka huu

Mwaka wa 2019 umekuwa wa kufana sana katika sekta ya sanaa nchini kwani kando na miaka iliyopita, wasanii wetu wamejikakamua kisabuni. Kutoka wasanii waliokithiri, kina Khaligraph, Sauti Sol, Nameless, Wahu hadi wasanii wa kizazi kipya kina; Ethic, Ochungulo family na Sailors wote wameonesha ubabe wao kupitia nyimbo walizozindua.
Isitoshe, baadhi yao wameonesha uhodari wao na kuvuka mipaka ambapo wameweza kufanya collabo na wasanii kutoka mataifa jirani, huku Tanzania ikiwa kivutia kikuu cha wasanii hawa.
Radio Jambo hii leo tunakupa orodha ya collabo kumi bora zilizofanywa na wasanii kutoka Kenya na Bongo mwaka huu.
1. Nandy ft Sauti Sol – Kiza Kinene
Kusema wimbo huu ulizinduliwa wiki moja tu iliyopita na kulingana nami, tayari huu ni wimbo wa mwezi! Nandy amewashirikisha magwiji hawa wa Afrika na kuonesha upande tofauti sana, kwani watu wamezoa nyimbo zao huwa za party ama zimejaa vidosho wenye makalio kweli.
Wimbo huu tayari umetazamwa zaidi ya mara milioni moja, Youtube.

2. Nandy willy paul – Hallelujah
Kwa mda sasa, kumekuwa na tetesi kuwa Willy Paul ambaye sasa hivi ni bayana kuwa sio msanii wa nyimbo za injili, anachumbiana na Nandy. Hili lilifuatwa na collabo murwa kwa jina Hallelujah ambayo hadi sasa hivi imeshika Kenya na Tanzania na kama kawaida, Nandy aliwakilisha Bongo vilivyo.
Video ya wimbo huu tayari imetazamwa zaidi ya mara milioni saba.

3. Ali kiba Ommy Dimpoz, Willy Paul – Nishikilie
Willy Paul ambaye tayari amekuwa na mwaka wenye mafanikio mengi kimziki licha ya scandal kibao, alishirikiana na King Kiba na mwenzake kutoka Tanzania bwana Ommy Dimpoz kwenye kibao hiki.
Watatu hawa ambao ni marafiki sugu wa gavana wa Mombasa, mheshimiwa Hassan Joho, waliwapa wanadada kibao cha kunengulia viuno na ambacho kimewateka wengi.
Hata hivyo, video ya ngoma hii haikuvuma sana kwani imetazamwa mara milioni moja nukta tano pekee kufikia sasa.

4. Rose Muhando Ringtone – Walionicheka

Wimbo huu ambao unatumika kama ushuhuda wake bi Muhando baada ya kupambana na ugonjwa kwa siku nyingi, unamshirikisha bwana Ringtone kutoka humu nchini. Ringtone amabaye amekuwa akigonga vyombo vya habari kwa mda, kwa sababu ya mambo ayafanyayo kwenye mitandao ya kijamii, anasifiwa sana na mashabiki kwa ustadi wake.

Wimbo huu ambao ulizinduliwa wiki moja pekee iliyopita, umetazamwa mara 750,000.

5. Willy Paul Ft Rayvanny – Mmmh

Miezi sita sasa tangu wawili hawa wazindue wimbo huu, wakenya na watanzania bado wanaupenda kwa ustadi na upole wake. Wimbo huu ambao unazungumzia tu mapenzi yao kwa wapenzi wao tayari umetazamwa zaidi ya mara milioni kumi.

6. Gabu Ft Mbosso – Mastory

Gabu ambaye kitambo alikuwa wa kikundi cha P-Unit alirudi na kishindo mwaka huu, yeye pia akimshirikisha mtanzania kwa jina Mbosso mwezi Januari. Wimbo huu licha ya kuchezwa sana kwenye klabu humu nchini, ulitizamwa mara milioni moja pekee.

Baadhi ya nyimbo zingine ambazo ziliwashirikisha wasanii kutoka mataifa haya mawili, ni Wakati wa mungu wimbo wake Paul Clement na Guardian Angel na Bahati ft Mbosso – Futa, nyimbo ambazo pia zilionesha ushirikiano mwema dhidi ya wasanii kutoka mataifa haya.

“Yaani Tanzania tumesha wai kabisa,” Willy Paul

Staa wa muziki wa injili nchini Willy Paul ametangaza kuwa sasa ameiteka soko la muziki la nchi jirani ya Tanzania. Kupitia nyimbo alizowashirikisha wasanii Nandy na mkali Rayvany kutoka lebo ya WCB inayomilikiwa na staa mkubwa afrika Diamond Platnumz, sanaa yake imepenyeza kwa urahisi na kueleweka freshi na watanzania.

Tazama nyimbo yake hapa na Rayvanny;

Kwa utafsiri wa haraka, michambo ya wakenya katika mitandao ya kijamii huenda ilimpa nguvu staa huyu kuzidi kupambana na kujitafutia nafasi nzuri ya muziki afrika mashariki.

Pata uhondo hapa:

“Amekula matofali mbili na mimba ikona mwezi mmoja”- Mulamwah

Willy M Tuva katika kipande kifupi cha video alichokiposti Pozze anaonekana akimpa shavu kubwa katika shoo iliyofanyika Dar Tanzania.

Tazama hapa:

Willy Paul ni kati ya wasanii wanaopevuka kwa kasi nchini akiwemo staa wa kike Nadia Mukami, Masauti na kundi la muziki la Ochungulo. Wasanii wengi wamezungumza swala la pozze kuonekana kuasi dini na kufanya muziki wa kidunia.

Soma hapa:

Je, Willy Paul kamkosea mungu? Wakenya watoa maoni

“Willy paul kama anataka kufanya muziki wa kidunia yupo huru. Ni uamuzi wake.” alisema HopeKid.

Staa wa muziki kutoka nchi ya Jamaica Alaine alimtetea Willy paul juzi kati kipindi na ambapo wakenya walikuwa  wanatokwa na povu katika mitandao ya kijamii kumhusu msanii huyu wa injili kuwa na tabia na mienendo inayokinzana na neno la mungu.

“Watu wamkosoe Willy paul kwa upole na kwa upendo. Jamani tusimkosoe kwa chuki na kwa ukali.” alisema Alaine.

Zari Hassan apata kipenzi kipya

Baada ya ukimya wa muda mrefu, Zari ameweza kutokea katika mitandao ya kijamii na mwanaume ambaye amtamrithi msanii na mkurugenzi wa WCB Diamond Platnumz. Katika chapisho siku ya ijumaa, mrembo huyu na mama wa watoto watano amesema kuwa mwanamume aliyempata kwa sasa ni baraka kubwa kwake.

Zari na Diamond waliachana mwaka uliopita tarehe 14 Februari siku ya wapendanao kwa kuchapisha ua jeusi lililoambatana na ujumbe mzito wa kuonyesha hawapo tena katika mahusiano.

zariposeswithdiamond
Zari na mpenzi wa zamani Diamond

Mama Tiffah alionekana kukasirishwa na tendo la mzazi mwenzake kukiri katika runinga na redio kubwa nchini Tanzania kuwa aliweza kufanya tendo la ndoa na kupata mtoto na mwanamitindo Hamisa Mobeto.

Patanisho: Jombi aapa kutopiga bibi yake

Zari The Bosslady ametupia picha ya mpenzi wake mpya katika mtandao wake maridhawa wa Instagram. Katika chapisho  hilo, mama Tiffah ameonekana kummiminia sifa kedekede mume huyu mpya na kubana jina lake kabisa na kumwita Bwana M.

Mrembo huyu ambaye ni msanii kutoka nchi jirani ya Uganda baada ya kumtema staa wa muziki Chibu Dangote alionekana kusononeka sana kwa kumpoteza mpenzi aliyempenda kwa dhati.

From Verona to Venice! Check out how Massawe Japanni is slaying in Italy

Katika mitandao ya kijamii, anadokeza kwamba mshikaji wake mpya amemkubali pamoja na watoto wake watano. Zari amezaa watoto wawili na Diamond platnumz na watatu na aliyekuwa mmewe marehemu Ivan Ssemwanga.

Zari amefunguka sana maneno matamu kwa mpenzi wake.

“Nimebarikiwa sana kukupata wewe. Nakupenda sana Bwana M… Sio kwa vitu unazoninunulia wewe kwa kuwa nimeona tena kubwa na nzuri maishani mwangu ila naupenda moyo wako na jinsi unavyonifanya nijihisi vizuri pamoja na watoto wangu.” Anasema mrembo huyu.

Akionekana kuwa amepitia katika mahusiano ya mateso,  mrembo huyu amesema kuwa yeye huwajenga wanaume na wala sio sampuli ya wanawake wanaotegemea kupewa na wanaume.

“Mimi sio sampuli ya wanawake wanaochukua kutoka kwa wanaume ila nawajenga.”

zari with teddy bear
Zari Hassan

Anasema Bwana M ni tofauti na wapenzi wa jadi na kwamba ana upole na utulivu mwingi ambao unafanya ampende zaidi. Mzazi mwenza Simba  anaonekana kuzama katika mahaba mazito na mtangazaji wa redio Tanasha Donna kutoka hapa nchini.

Penzi lake diamond na Tanasha linaonekana kunoga zaidi baada ya mkali huyu kumpeleka Donna nyumbani Madale na kumtambulisha kwa  familia. Dadake Platnumz anapenda sana mahusiano haya na anajuta kuwa wawili hawa wangekutana zamani.

Bongo star Aslay falls off stage while performing in Kisumu (VIDEO)

Bongo star Aslay had a weekend to forget after the superstar fell off stage while performing in Kisumu.

Bongo Flava queen Lady Jaydee reveals she was on the brink of committing suicide

The ‘Mhudumu’ hit maker took to his social media page to assure his loyal fans that he miraculously escaped the accident without being hurt.

He then went on to praise Kisumu fans for an electrifying atmosphere throughout the show.

He wrote;

It’s normal for celebrities and performers to encounter some challenging moments while on stage and mine came through yesterday, I slipped on stage but miraculously I wasn’t hurt, I came back on stage and gave one of the most electrifying performance, #Kisumu you guys are AMAZING the Energy was insane.

Bongo star Ommy Dimpoz spills details about Avril’s newborn baby

Mwenyezi Mungu Awabariki !!! …….. Ni Kawaida kwa Wasanii kupatana na changamoto jukwani, na Jana ilikuwa zamu yangu, yalitokea Haya punde tu nilipopanda jukwani kwa bahati nzuri sikuumia ,nilirejea jukwani na kuburudisha Mashabiki wangu wa Kisumu waliyojitokeza kwa wingi. Asanteni sana nyote Mwenyezi Mungu Awabariki!!!

Watch the moment Aslay fell off the stage below.

Diamond Platnumz Brings The House Down At His ‘A Boy From Tandale’ Album Launch (PHOTOS)

Tanzanian superstar, Diamond Platnumz is arguably the biggest star in East Africa right now and this attributed to his hot collaborations which features artists from across the world as well as his massive fan base across the region.

The boy from Tandale has been in the country promoting the Songa music app, a chance which he took to launch his most anticipated ‘A boy from Tandale’ album at Kenya National Theatre.

The ‘Mbagala’ hit maker brought the house down in front of 300 invite-only guests. Diamond was also joined on stage by American superstar Omarion with the two sending the crowd into musical ecstasy.

Check out the photos below.

 

diamond a boy from a boy fr a boy f dia

 

Jamaa Akamatwa Na Kilo Kumi Ya Bangi Ya Thamani Ya Shilingi Milioni Nne – Migori

Polisi huko Rongo kwenye kaunti ya Migori wamemkamata mtu mmoja anayedaiwa kupatikana na bangi ya kilo kumi ya thamani ya shilingi milioni nne katika kizuizi cha magari cha mji wa Rongo usiku wa kuamkia leo.

Kwa mujibu wa OCPD wa Rongo, Jonathana Kisaka Muganda, mwanamme huyo Morris Odhiambo mwenye umri wa makamu anadaiwa kupatikana akisafirisha bangi hiyo kwa gari aina ya probox lilillokuwa likielekea mjini Nairobi kupitia mjini Kisii ambako kuna soko la kuuza bangi hiyo.

Aliongeza kuwa mshukiwa huyo ambaye alikuwa pekee yake kwenye gari hilo amezuiliwa katika kituo cha polisi cha Kamagambo mjini Rongo akisubiri kufikishwa mahakamani kujibu mashtaka dhidi yake.

VIDEO: Diamond Analyses Opening Weekend Fixtures Of 2015/16 Premier League Season

Watch Diamond Okusimba briefly describe what his expectations for the 2015/16 Premier League season are after the fixtures were released on Wednesday. Okusimba will be keeping a keen eye on how his favourite Manchester United, defending champions Chelsea, Liverpool and the promoted teams will perform on the opening weekend.