“Sina maringo wasee…”- Willy Paul

Staa mwenye utata Willy Paul amefunguka na kusema hana matatizo na mtu na yeyote. Katika mtandao wake wa Insta, nyota huyu amechapisha ujumbe kwa wafuasi wake na kudokeza kwamba yupo freshi.

“Sina maringo wasee, ukiniona somewhere just say hi and ill hi back.. and maybe buy you something nice…..” alisema Pozze.

Soma hadithi nyingine:

“Huddah na Vera nawatamani…”, asema Willy Paul

Muimbaji huyu anayetamba na nyimbo inayofanya vizuri katika mitandao ya kijamii, Hallelujah aliomshirikisha Nandy anazidi kupevuka kimuziki.

Pozze analenga zaidi soko la Tanzania kupitia collabo kubwa anazofanya na wasanii kama Rayvanny na Nandy.

 

“Huddah na Vera nawatamani…”, asema Willy Paul

Baada ya shutuma za ukaribu na minenguo hatari kwenye fiesta ya  Choma Na Ngoma na mrembo wa Tanzania Nandy, Willy Paul ametokea kwenye kipande cha video alichochapisha kwenye mtandao wake maridhawa wa Insta. katika video hii fupi, staa huyu anaonekana na kikundi cha marafiki akijaribu kuigiza kitendo alichokifanya Askofu Ng’ang’a kanisani mwake.

61196090_1362417120574999_4257206207397840919_n (1)

Je, Willy Paul kamkosea mungu? Wakenya watoa maoni

“Yaani leo mnaona mnaeza mkatamani Hudda na Vera sababu nawatamani??? Lubish”, anasema Willy Paul.

Kwenye kipande hicho cha video, Pozze anawatusi wanakikundi na upande mwingine wanamwogopa zaidi. Kumekuwepo na maswali mengi kumhusu muimbaji huyu wa nyimbo za injili iwapo kaasi na kubadilika kuimba nyimbo za klabu.

61501565_377021072927921_6685521336903062628_n

Pata uhondo:

Staa Willy Paul na Nandy wafunguka baada ya ajali

Staa wa Jamaica Alaine alipozuru nchini katika tamasha kubwa iliyofanyika Kasarani ya Tomorrow’s Leaders Festival alimtetea kuwa wakenya wamkosoe kwa utaratibu na upendo mwingi ili aweze kujirudi.

Mapema wiki kiongozi wa upinzani Musalia Mudavadi alionekana pia kutoa kumuonya msanii huyu. Musalia alisema kuwa wasanii wa injili wanapaswa kuwa kioo cha jamii na waonyesha mienendo ya kikristo.

 

Rich Mavoko : Sioni mtu wa kuomba msamaha WCB

Staa wa muziki wa Bongo fleva Rich mavoko amedokeza kuwa haoni wa kumwomba msamaha katika lebo ya WCB. Mavoko alitoka ghafla katika lebo hiyo inayoongozwa na nyota na mwanamuziki mkubwa Afrika Diamond Platnumz.

Wasanii wengine walio chini ya usimamizi wa lebo hiyo ni pamoja na Harmonize, Rayvanyy, QueenDarleen na mkali Mbosso.

Soma hadithi nyingine:

HopeKid : Nilifukuzwa kanisani kisa skendo yangu na DK kwenye Beat

download

Mgogoro na mvutano mkubwa ulifuata kuhusu mtakaba aliokuwa ameingia na usimamizi wa lebo hii ya Wasafi. Kulingana na Mavoko, mkataba wake na WCB ulivurugika kipindi baadhi ya vitu alivyotaka havikufanywa na lebo hiyo.

Soma upate uhondo hapa:

Hopekid reveals student in threesome scandal with DK Kwenye Beat was suicidal

” Mkataba bado haujaisha ata kama nimetoka. Kuna baadhi ya vitu havikwenda sawa na nilivyotaka mimi. Nilikaa sana na nyimbo na ambazo nilitakiwa nizitoe ila sikuweza. Kuna kipindi mamangu alinipigia kuniulizia mbona sitoi nyimbo. Sikuona kabisa maisha mazuri ya usoni nikiwa WCB.” alisema Mavoko.

Staa huyu anayetamba na nyimbo mpya inayofanya vizuri Usiguze amesema kuwa hawezi kurudi lebo aliyotoka katika mahojiano na kituo kimoja nchini Tanzania. Kuhusu kuomba msamaha na kukubali kurudi katika lebo hiyo kubwa Afrika mashariki, staa huyu alisema hawezi kabisa.

“Nilipoingia WCB sikuona msanii mkubwa hapo ukiweka kando mkubwa wa lebo hiyo. Naomba msamaha wa nini? Kosa gani nilifanya mimi? Sina matatizo na yeyote WCB.”

 

lucy2

Baadhi ya maneno Massawe huyatumia hewani na maana yake

Utangazaji wa redio ni mojawapo ya sanaa duniani zinazohitaji ubunifu mkubwa na ukakamavu wa kuwashika na kuwagandisha wasikilizaji katika spika za redio zao.

Sanaa yoyote lazima msanii achombeze maneno matamu yanayofanya kazi yake ionekane bora na ya kuvutia zaidi.

Soma hapa:

Massawe afunguka kuhusu ajali – Jumatano

Mwimbaji wa nyimbo za mapenzi atapenda sana kuchonga mistari inayokwenda freshi na maudhui na lengo anayokusudia kwa mashabiki wa jinsia tofauti. Hali kadhalika anapofanya maonyesho jukwaani atakuwa na baadhi ya maneno kinywani ambayo wafuasi wake humtambua nayo.

Mtangazaji Massawe hajaachwa nyuma katika mtindo huu na kuna baadhi ya maneno anayoyatumia katika kipindi chake cha Bustani la massawe ili kuvutia mashabiki.

Pata uhondo hapa:

Sababu Massawe Japanni hatokuwa hewani kwa mda

Tumekusogezea hapa baadhi ya tungo virai (phrases) anazopenda kutumia:

  1. “Nafurahi kuwa tupo pamoja nawe”

Baada ya nyimbo inayocheza hewani kumalizika, mtangazaji huyu anapenda sana kuanza na maneno haya kama kitambulisho cha kufungua shoo.

     2. “Ngwenee”

Hili ni tamko ambalo lina asili ya lugha ya Kikamba na huwa na maana ya ‘Nakuona’. Kwa haraka haraka unaweza toa ubashiri wako na kusema kuwa Massawe husema hivi labda kwa sababu anatoka maeneo ya ukambani au labda ni mbinu ya kugeuza ndimi na kuwavuta wasikilizaji kutoka jamii hiyo.

    3 .” Uko hii town? Au niko hii town au labda hii ni town”

Massawe hutumia maneno haya mara kwa mara. Staa huyu huwa anataka kujua mashabiki wake wanategea kipindi wakiwa maeneo gani.

 

Soma pia:

‘Safiri salama dadangu’ Massawe Japanni mourns her best friend

Gidi amkosoa rapa Khaligraph Jones

Rapa mkubwa Afrika mashariki Khaligraph Jones almaarufu kama Papa Jones ni kati ya wasanii wanaofanya muziki wa kuchana hapa nchini.

Mkali huyu wa nyimbo inayofanya vyema katika mitandao na katika vyombo vya habari ya Superman mapema mwakani alionekana kukerwa na kuona redio na runinga hazichezi nyimbo za wasanii hapa nchini na kuapa kuwapeleka nchini Nigeria ili wajifunze kutoka nchi hiyo ya Afrika magharibi.

khaligrapharms6
Khaligraph Jones

Soma hapa:

“Simama wakuone kijana mfupi round” – Mbusii amuita Uche

Katika mahojiano ya kipekee na kituo cha Jambo, Gidi amezungumzia maswala yanayogusia muziki wa hapa nchini na jinsi wasanii wanavyojituma katika tasnia hii.

Gidi ameonekana sana kumkosoa msanii huyu kwa kutofahamu utaalamu unaotumika katika redio na runinga.

“Khaligraph jones ni msanii mzuri. Lakini huenda kidogo hana ufahamu wa jinsi redio zinafanya kazi. Mtangazaji wa redio hana mamlaka ya kuchagua muziki gani anafaa aucheze. Kila redio ina mtindo inayofuatilia. Miziki tunayocheza redio Jambo huwezi kuicheza Classic Fm kwa sababu wasikilizaji wao wanataka vitu tofauti.”

Soma hapa;

“Nikiingia Mombasani nione Fatuma sitambania” – Mbusii

gidipointing

 Huku akionekana kuwakashifu wasanii wanaofanya nyimbo kujulikana tu na kuwa na sifa bila kuzingatia kutengeneza hela, Gidi alisema kuwa wasanii nchini wanatakiwa waige mfano wa kundi la wasanii la Sauti Sol.

“Kila msanii anajitahidi sana. Sauti Sol naweza nikasema wanaufanya muziki kitaalam sana.Wasanii chini nawaomba sana waweze kuiga kikundi hiki.”

Soma hapa:

King Kaka afunguka kuhusu kufanya collabo na mzazi mwenzake Sage

Gidi anawahimiza wasanii waache mtindo wa kuimba nyimbo kujulikana tu bali watengeneze pesa.

“Wafanye muziki kama biashara na sio kuufanya ujulikane na watu. Ni biashara. Ni kazi.”

Akiwalenga wasanii wanaoipa nguvu hashtegi ya #PlaykenyanMusic, mtangazaji huyu wa kipindi kinachoruka kupitia masafa ya Redio Jambo cha Patanisho, alidokeza kuwa redio nyingi hapa nchini ni biashara za watu binafsi.

“Tusije tukaanza kushurutisha nyimbo kuchezwa katika redio. Redio zingine ni biashara za watu binafsi. Labda serikali inaweza kuwa na sheria zinazohakikisha tunacheza miziki ya hapa nchini kwa kiwango kikubwa.”

 

King Kaka afunguka kuhusu kufanya collabo na mzazi mwenzake Sage

Msanii na rapa mkubwa Afrika mashariki King Kaka amefunguka sana kuhusu kufanya muziki na aliyekuwa mpenzi wake Sage.

Katika mahojiano na mtangazaji Rais Papa katika kipindi kinachoruka katika mtandao wa youtube ya Redio Jambo, mkali huyu ameweza kusema kuwa hana matatizo na mzazi mwenzake baada ya wao kutengana huku akisema nafasi ikitokea wanaweza ingia studio na kufanya ngoma.

“Tukikutana studio tunaweza fanya ngoma. Muziki inafanywa tu si ni muziki.” Alisema King Kaka.

Soma mengine:

Musician Vivian opens up on being in an abusive relationship

Papa Na Mastaa ni kipindi na ambacho kimetengwa kwa mahojiano ya kipekee na mastaa wa muziki, mkali huyu ambaye ni mjasiriamali, rapa na mwimbaji pia ameanzisha juhudi za kuwasaidia wasanii chipukizi inayofahamika kama Empires Gold na tayari wasanii watatu wapo katika mpango huo.

King Kaka pia ameweza kuweka wazi sababu iliyomfanya yeye kuacha kufunza masomo ya biashara katika chuo kikuu cha Zetech. Staa huyu aliweka pembeni kazi hii kwa misingi ya kazi nyingi zinazomwandama.

“Nilikuwa mhadhiri Zetech University. Nilikuwa nafunza business na kwa vile schedule yangu ilikuwa tight nkaacha. For almost 2 years sifunzi.”

Mkali huyu aliweza pia kuzungumzia safari yake ya Marekani inayofahamika kama Eastlando Royalty US Tour. Ziara hii ya marekani iliweza kumfanya aingie studio na kumshirikisha msanii wa kimataifa Cassidy katika nyimbo inayofanya vyema ya Far Away.

“The fact that nikona Cassidy kwa ngoma ni ushindi ukubwa,” King Kaka alieleza katika kikao cha Papa Na Mastaa.

Pata uhondo hapa:

My hubby pinned me down and shaved my hair – Cries Woman

Audio ya nyimbo hii ilifanywa hapa nchini na Musyoka na video ikihaririwa na mkenya anayeishi Marekani, Hussein Njoroge.

King Kaka alifunguka zaidi kuhusu mahusiano yake na msanii Sage na jinsi anavyotenga wakati kuongea na watoto.

“I think you’re talking about sage yeye akona my other daughter. Lazima niende kumwona mtoto wangu ambaye ni Ayana lakini naishi na Nana. You’ve to create time for your kid.”

King Kaka hali kadhalika alisema kuwa yupo freshi na Msanii Khaligraph na kumsifia sana.

“Ni jamaa anafanya vizuri tunashukuru mungu. Tukiona vijana wanatia bidii tunafurahia. Anatia bidii kwa kazi zake. Tunaongeaongea ikifika time tutaingia studio.”

Soma hapa:

‘Kijana fupi amenona..’ Compilation of the best quotes by lonyang’apuo

Diamond Platnumz na babake wakutana na kuzima tofauti zao

Msanii na staa mkubwa Afrika Diamond Platinumz ameweza kukutana katika redio ya Wasafi FM na babake na kuonekana kuzima tofauti zao za awali.

Mzee Abdul alimtaliki mkewe miaka ya awali kijana huyu akiwa kidato cha kwanza. Naseeb alitangulia kwa kusema kuwa ubaridi unaonekana kati yao na baba mzazi umechochewa na kutokua pamoja kwa kipindi kirefu.

“Kiukweli siwezi kusema nina ukaribu na mzee. Hatujakuwa na bond kubwa naye ila mimi sina matatizo naye…tukiwa kuna issue tutakutana naye tuongee” Diamond alisema katika mahojiano.

diamodn and his parents
Diamond Platnumz na wazazi

Ukaribu wa Naseeb na mamake umeonekana kwa muda mrefu kunoga huku babake akionekana kusahaulika na msanii huyu.

Katika kitengo cha Block 89 cha shoo ya redio ya Wasafi, babake Platnumz anaonekana kutokea ghafla katika mahojiano  ya mtoto wake na kituo hiki.

Mwanae anamiliki chumba hiki cha habari pamoja na runinga bila kusahau lebo ya Wasafi (WCB)  inayojivunia kusimamia wasanii wakubwa Afrika mashariki na Afrika ya kati kama Rayvany,  Harmonize, Lavalava, Mbosso na Queen Darleen.

Baada ya kuugua kwa muda mrefu, babake Chibu alipata ufadhili kutoka kwa mtendawema aliyeguswa na hali yake ya ugonjwa.

diamondplatnumzinyellow
Diamond

Yule sio mtoto wangu kunizaa ila niseme kuna watu hawana wazazi na wana hela.Aliniangalia katika mitandao ya kijamii katika hali sio nzuri na akatokea kutoa usaidizi”

Diamond anadai kuwa baadhi ya vyombo vya habari vinamtumia babake kupata ufuasi mkubwa wanapokwenda kumhoji kuhusu tofauti zao.

“Naamini vyombo vya habari vinakuzakuza na kutengeneza matatizo kati yangu na baba.”

diamond platnumz madale
Bongo singer Diamond Platnumz

Kwa upande mwingine anaona kuwa babake anamweka katika kicheko kwa watu wengi hususan wapinzani wake anapoonekana kama hamsaidii mzazi.

Babake alimwomba msamaha na wote kuonekana wameridhiana katika mazungumzo yao

Kama nimekukosea naomba unisamehe na ujaribu kuangalia utanisaidia vipi mimi babako.”

Diamond alionya kuwa kuna baadhi ya vyombo vya habari vinavyomtumia babake kwa maslahi yao na hawamsaidii. Mkali huyu wa kibao kipya The one  alimaliza kwa kuomba msamaha.

“Well mimi siwezi kusema nina  matatizo na babangu. Naamini utofauti wake na mama unafanya tuwe hatuna ukaribu…Naomba anisamehe pia kwa sababu sijui akiwa na mama walikosana kwa misingi gani.”

Also read more here

Zari Hassan apata kipenzi kipya

Baada ya ukimya wa muda mrefu, Zari ameweza kutokea katika mitandao ya kijamii na mwanaume ambaye amtamrithi msanii na mkurugenzi wa WCB Diamond Platnumz. Katika chapisho siku ya ijumaa, mrembo huyu na mama wa watoto watano amesema kuwa mwanamume aliyempata kwa sasa ni baraka kubwa kwake.

Zari na Diamond waliachana mwaka uliopita tarehe 14 Februari siku ya wapendanao kwa kuchapisha ua jeusi lililoambatana na ujumbe mzito wa kuonyesha hawapo tena katika mahusiano.

zariposeswithdiamond
Zari na mpenzi wa zamani Diamond

Mama Tiffah alionekana kukasirishwa na tendo la mzazi mwenzake kukiri katika runinga na redio kubwa nchini Tanzania kuwa aliweza kufanya tendo la ndoa na kupata mtoto na mwanamitindo Hamisa Mobeto.

Patanisho: Jombi aapa kutopiga bibi yake

Zari The Bosslady ametupia picha ya mpenzi wake mpya katika mtandao wake maridhawa wa Instagram. Katika chapisho  hilo, mama Tiffah ameonekana kummiminia sifa kedekede mume huyu mpya na kubana jina lake kabisa na kumwita Bwana M.

Mrembo huyu ambaye ni msanii kutoka nchi jirani ya Uganda baada ya kumtema staa wa muziki Chibu Dangote alionekana kusononeka sana kwa kumpoteza mpenzi aliyempenda kwa dhati.

From Verona to Venice! Check out how Massawe Japanni is slaying in Italy

Katika mitandao ya kijamii, anadokeza kwamba mshikaji wake mpya amemkubali pamoja na watoto wake watano. Zari amezaa watoto wawili na Diamond platnumz na watatu na aliyekuwa mmewe marehemu Ivan Ssemwanga.

Zari amefunguka sana maneno matamu kwa mpenzi wake.

“Nimebarikiwa sana kukupata wewe. Nakupenda sana Bwana M… Sio kwa vitu unazoninunulia wewe kwa kuwa nimeona tena kubwa na nzuri maishani mwangu ila naupenda moyo wako na jinsi unavyonifanya nijihisi vizuri pamoja na watoto wangu.” Anasema mrembo huyu.

Akionekana kuwa amepitia katika mahusiano ya mateso,  mrembo huyu amesema kuwa yeye huwajenga wanaume na wala sio sampuli ya wanawake wanaotegemea kupewa na wanaume.

“Mimi sio sampuli ya wanawake wanaochukua kutoka kwa wanaume ila nawajenga.”

zari with teddy bear
Zari Hassan

Anasema Bwana M ni tofauti na wapenzi wa jadi na kwamba ana upole na utulivu mwingi ambao unafanya ampende zaidi. Mzazi mwenza Simba  anaonekana kuzama katika mahaba mazito na mtangazaji wa redio Tanasha Donna kutoka hapa nchini.

Penzi lake diamond na Tanasha linaonekana kunoga zaidi baada ya mkali huyu kumpeleka Donna nyumbani Madale na kumtambulisha kwa  familia. Dadake Platnumz anapenda sana mahusiano haya na anajuta kuwa wawili hawa wangekutana zamani.