Watu 13 wafariki huku 218 wakipatikana na Corona

Watu  218  wamepatikana na virusi vya corona  baada ya sampuli 5,424 kupimw akatika saa 24 zilizopita  na kufikisha jumla ya visa hivyo hadi kufikia sasa kuwa 37,707.

Polisi Vietnam wamenasa zaidi ya mipira 300,000 ya kondomu iliyokuwa ikiuzwa baada ya kutumika

Idadi ya sampuli zilizopimwa sasa ni 532,729. Visa vyote ni vya wakenya  isipokuwa vinane.159 ni wauame ilhali  59  ni wanawake .Mgonjwa wa umri wa chini sana  ni mtoto wa mwaka mmoja ilhali wa umri wa juu ana miaka 78 .

Nairobi ndio inayoongoza kwa visa 68  ikifuatwa na  Kisii  28,Mombasa 21,Kisumu 19,Kimbu 13  Kajiado 11,Busia 10,Machakos 8,Tharaka Nithi 6 ,Garissa 6, Taita taveta visa 5  Nakuru visa  4 ,Uasin Gishu visa 3,Narok visa 2,Laikipia visa 2 Kakamega visa 2,Kericho visa 2, Murang’a,Bomet,Kilifi  ,Migori ,nyandarua na Nyeri zina kisa 1 kila moja.

5 Wafariki huku visa vipya 141 vya covid 19 vikiripotiwa

 Watu 170 wamepona ugonjwa huo na kufikisha 24,504 idadi ya wote waliopona corona nchini hadi kufikia sasa .

Leo watu 13 wameaga dunia na kufikisha 682 watu waliofariki kutokana na ugonjwa huo .

 

 

 

Watu 9 waaga dunia huku visa vipya 139 vya corona vikiripotiwa

Kenya siku ya Jumanne imesajili visa 139 vya ugonjwa wa corona  na kufikisha jumla ya visa hivyo nchini kuwa  37,218,  katibu wa utawala wa afya  Mercy Mwangangi  amethibitisha.

Sossion awashauri walimu kutii agizo la kurejea shuleni

Idadi hiyo ni kutokana na  sampuli 1774 zilizopimwa katika saa 24 zilizopita. Kati ya visa hivyo vipya 125 ni vya wakenya ilhali 14 ni vya raia wa kigeni. Wanaume ni 112 ilhali wanawake wakiwa 27. Mgonjwa wa umri wa chini ana  miaka mine ilhali wa umri wa juu ana  miaka 82.

Watu 198 wamepona ugonjwa huo na kufikisha jumla ya idadi ya walipona kuwa 24,147.

Hata hivyo taifa limewapoteza watu 9 kwa ajil ya ugonjwa huo na kufikisha idadi ya walioaga dunia hadi sasa kuwa 659

 

 

 

Corona: Kenya yaandikisha visa 188 vipya huku idadi ikifikia 36,157

Wizara ya afya kupitia ujumbe kwa vyombo vya habari ilitangaa kuwa Kenya meandikisha visa 188 vipya vya coronavirus katika masaa 24 yaliyopita.

Kufikia sasa visa vya Corona vimefikis 366,157 tagia mwezi mechi ambapo kisa cha kwanza nchini kutangazwa.

Ujumbe huo kutoka kwa waziri wa afya Mutahi Kagwe ulisema kuwa sampuli 3,092 zilichukuliwa huku idadi ya sampuli zilizopimwa kuwa 497,652.

Wakti hu huo wazri huyo alisema kuwa wagonjwa watatu wa  Corona waliaga dunia huku idadi ya walioaga ikifikia 622.

Katika visa hivyo vipya wotw ni wakenya ispokuwa raia watano wa kigeni. Kati ya idadi hiyo, 149 ni wanaume huku 39 wakiwa wanawake.

Mgonjwa mchanga zaidi ana umri wa miaka miwili huku mgonjwa mzee zaidi akiwa na miaka 78.

Idadi ya waliopona imefikia 23, 067 baada ya wagonjwa 296 kupata nafuu.

Magoha kukutana na wadau huku pakiwa na kampeini za kutaka shule zifunguliwe

Waziri wa elimu George Magoha  ameitisha mkutano wa kushauriana na washka dau katika sekta ya elimu wiki ijayo  kujadil  mwongozo wa kufunguliwa kwa shule .

Mkutano huo utafanyika katika taasisi ya kustawishaji mtaala wa elimu  na utajadili tena suala tata la kufunguliwa kwa shule wakati huu wa janga la corona .

Magoha aonya kuhusu ufisadi katika mradi wa madawati wa shilingi bilioni 1.9

Mwezi julai ,wizara ya elimu   ilitangaza kwamba huenda shule hazitafunguliwa hadi januri mwaka ujao . Magoha hata hivyo  amesema uamuzi huo unaweza kubadilishwa  kulingana na jinsi kenya inavyokabiliana na janga la virusi vya corona .

Katika wiki moja  iliyopita kumekuwa na ongezeko la wito wa kufunguliwa kwa shule  huku wanaomiliki shule za kibinafsi  wakiitaka serikali kuzingatia kuzifungua shule mapema kuliko ilivyokuwa imetangaza hapo awali .

Hatua hiyo imetokana na kupungua kabisa kwa visa vya Covid 19 vinavyoripotiwa kila siku huku watu wengi pia wakipona ugonjwa huo na kurejelewa kwa shughuli za kawaida katika sekta nyingi za uchumi .

Rais Uhuru Kenyatta anatarajiwa kutoa mwongozo mpya  mwishoni mwa mwezi huu  kama sehemu ya mikakati ya kufungua uchumi ambao umelamazwa na janga hilo tangu mwezi machi mwaka huu .

Shule zitafunguliwa lini? Magoha atakiwa kujibu

Mnamo agosti tarehe 25  mzazi mmoja aliwasilisha kesi kortini akitaka kuishurutisha wizara ya elimu kuzifungua shule .

Shule zilifungwa mwezi machi  wakati Kenya ilipothibitisha kisa chake cha kwanza cha ugonjwa wa corona .

Mwenyekiti wa muungano wa wamiliki wa shule za kibinafsi Mutheu Kasanga amesema wanapinga pendekezo la kuwataka watahiniwa kurudia madarasa kwa mwaka mzima .

 

 

 

 

Covid-19: Watu,83 wapatikana na corona huku 72 wakipona

Hii leo kenya imesajili visa 83 vipya vya maambukizi ya corona na kufikisha idadi jumla ya 35,103 kutokana na sampuli 3,093 zilizopimwa kwa saa 24 zilizopita.

Katika maambukizi hayo mapya 77 ni wakenya huku 6 wakiwa raia wa kigeni,58 ni wanaume ilhali 25 ni wanawake amesema waziri wa afya Mutahi Kagwe.

Covid-19: Watu 136 wapatikana na corona huku 99 wakipona

Nairobi inazidi kuongoza katika maambukizi hayo huku leo ikisajili visa 27 hukuikifuatwa na kaunti ya busia na visa 15.

Vile vile watu 72 wamepona virusi hivyo na kufikisha idadi jumla ya 21,230 ya watu waliopona kutokana na virusi hivyo,39 wamepona wakipoea matbabu ya nyumbani na wengine 33 wameruhusiwa kuenda nyumbani kutoka hospitali tofauti huumu nchini.

Pia watu 3 wamepoteza maisha yao kutokana na corona na kufikisha idadi jumla ya 597 ya watu walioa dunia kutokana na virusi vya corona.

Covid-19: Watu 136 wapatikana na corona huku 99 wakipona

Watu 136 hii leo wamepatikana na maambukizi ya corona na kufikisha idadi ya jumla 35,020, hii ni baada ya sampuli 3,707 kupimwa kati ya saa 24 zilizopita.

Kati ya maambukizi hayo 85 ni wanaume huku 5i wakiwa wanawake, pia 124 ni wakenya ilhali 12 ni raia wa nchi ya kigeni, mgonjwa umri wa chini ana miezi tisa na mwenye umri wa juu ana miaka 75.

Hayo yakijiri watu,99, wamepona kutokana na virusi hivyo na kufikisha idadi jumla ya 21,158 waliopona maambukizi ya corona tangu kisha cha kwanza kutipotiwa.

Vilevile watu 5 wamepoteza maisha ya kutokana na virusi hivyo na kufikisha idadi jumla ya 594 walioaga kutokana na corona, Mungu azilaze roho zao mahali pema.

Watu 544 wapatikana na virusi vya corona huku 13 wakiaga dunia – Aman

Watu 544 wamepatikana na virusi vya corona baada ya sampuli za watu 2,653 kupimwa chini ya saa 24.

Idadi hiyo sasa inafanya taifa kuwa na watu  22, 597 walio na virusi hivyo kufikia sasa.

Aidha wagonjwa wengine 13 wametangazwa kufariki na kufikisha watu 382 waliofariki kufikia sasa kutokana na ugonjwa huo

Katibu wa utawala wa wizara ya Afya  Rashid Aman amesema kuwa watu 263 waliokuwa wamelazwa katika hospitali tofauti nchini wameruhusiwa kwenda nyumbani na kufikisha watu  8,740 waliopona.

Image

Aman pia amethibitisha kuwa wahudumu  wanane  wa afya hadi kufikia sasa wamefariki kutokana na virusi hivyo huku  wa hivi punde kupoteza maisha yake akiwa Mariam  Awuor kutoka kaunti ya Kisii.

Kati ya visa hivyo vipya Nairobi imeandikisha visa 412 , Kiambu 27, Machakos 17, Kajiado 17, Garissa 16, Uasin Gishu 14, Mombasa 9, Nakuru 8, Nyeri 5, Narok 5, Makueni 4 Laikipia 2, Muranga, Kilifi, Busia, Embu, Bungoma, kisii, Kwale na  Meru  zote zikiwa zimeandikisha kisa kimoja.

Wakati huo huo Aman akana madai kuwa kuna baadhi ya wahudumu wa afya ambao wamekosa kulipwa mishahara yao akisema serikali kuu pamoja na zile za kaunti  nchini zimekuwa zikishirikiana ili kufanikisha malipo ya wahudumu hao  .

Image

Serikali ya Homa Bay yasubiri ripoti ya kubaini kilichosababisha kifo cha Mariam Awuor

  Ameongeza kuwa serikali imeweka mikakati mwafaka ya kuajiri wahudumu zaidi ili kusaidiana na wenzao wanaokabiliana na janga hilo.

Amesisitiza umuhimu wa wakenya kuendelea kuzingatia masharti yaliyowekwa na wizara ya afya kama njia ya kupunguza msambao wa corona.

Akisoma takwimu hizo mpya za maambukizi ya corona, Aman ametuma risala za rambirambi kwa familia ya Mariam Awuor ambaye alitangazwa kufariki kutokana na virusi hivyo.

 

 

Watu 690 wameambukizwa maradhi ya corona ndani ya saa 24, idadi ya jumla ya waathiriwa yafikia watu 22,053

Wizara ya afya imethibitisha kuwa na visa 690 vipya vya Corona katika masaa 24 yaliyopita.

Visa hivyo vipya viliripotiwa baada ya vipimo vya sampuli 5,393. Kesi hizi zinafikisha idadi ya sampuli zilizopimwa kuwa 315,723.

Idadi ya kesi ya virusi vya Corona vilivyoripotiwa nchini imefikia 22,053 tangia Machi 13,2020.

Hali ya maabukizi ya virusi vya Corona Afrika Kusini ni ya kutisha

Zaidi ya watu nusu milioni wamethibitishwa kuwa na maambukizi ya virusi vya Covid-19 nchini Afrika Kusini, kulingana na wizara ya ya afya nchini humo

Waziri Zwelini Mkhize ametangaza kuwa watu wapya 10,107 wamepatwa na maambukizi kwa siku moja tu ya Jumamosi, na hivyo kuifanya nchi hiyo kuwa na jumla ya watu 503,290 maambukizi ya virusi hivyo, pamoja na vifo 8,153.

Afrika Kusini ndio nchi iliyoathiriwa zaidi na maambukizi ya Covid-19 barani Afrika ambapo idadi ya maambukizi yake ni sawa na nusu ya maambukizi yote kwa ujumla yaliyoripotiwa katika nchi zote za Afrika.

Pia ni nchi ya tano yenye visa vingi zaidi vya maambukizi dunaini baada ya Marekani, Brazil, Urusi na India.

Maafisa wa wizara ya afya nchini Afrika Kusini wamesema kuwa viwango vya maambukizi vinaongezeka kwa kasi kubwa mno, huku watu wengi wanaopata maambukizi hayo kwa sasa wakiwa ni wakazi wa mji mkuu.

Zaidi ya theluthi moja ya maabukizi yameripotiwa katika jimbo la Guateng ambalo kwa sasa ni kitovu cha mlipuko nchini humo.

Maambukizi hayo hayatarajiwi kuongezeka kupita kiwango hicho, wanasema maafisa wa afya.

Afrika kusini iliweka amri ya kutotoka nje miezi ya Aprili na Mei Sambayo ilipunguza kusambaa kwa virusi vya corona.

Ilianza kufungua shughuli za kiuchumi taratibu mwezi Juni lakini masharti yaliyowekwa – iliwa ni pamoja na kupiga marufuku mauzo ya pombe- yalirejeshwa tena nwezi uliopita baada ya idadi ya maambukizi kuongezeka tena. Hali ya dharura pia imetangazwa kuanzia tarehe 15 Agosti.

Kuongezeka kwa idadi ya wagonjwa kupita kiwango cha uwezo wa hospitali nchini humo pia ni mzigo mkubwa kwa hospitali na taarifa ya uchunguzi ya BBC ilibaini kushindwa kwa mfumo wa afya kwa ujumla jambo ambalo limewafanya wahudumu wa afya kufanya kazi ya ziada na hivyo kuchokana kuufanya mfumo mzima kukaribia kuvunjika.

Mwezi uliopita rais wa nchi hiyo Cyril Ramaphosa alisema kuwa vitanda 28,000 vya hospitali vimepatikana kwa ajili ya wagonjwa wa Covid-19 lakini nchi bado inaklabiliwa na upungufu mkubwa wa madaktari na wauguzi/ manesi

Wiki iliyopita Shirika la Afya Duniani- WHO lilionya kuwa inachoitokea Afrika Kusini huenda ikawa ni dalili za kile kitakachotokea kote barani Afrika.

-BBC

Covid-19:Watu 667 wapatikana na virusi vya corona huku 11 wakiaga dunia

Watu 667 wamepatikana na virusi vya corona  katika saa 24 zilizopita na kufikisha jumla ya watu16,268, baada ya sampuli  5,075 kupimwa.

Katibu wa utawala wa wizara ya Afya Mercy Mwangangi amesema  kwamba watu 11, wameaga dunia na kufikisha 274 jumla ya waliofariki kutokana na virusi hivyo. Watu 311, wamepona  na kufikisha jumla ya waliopona ugonjwa huo kuwa 7446.

Wataalam wa afya wamshauri Uhuru kutofunga nchi kwa sababu ya corona

Kaunti ya Nairobi imezidi kuongoza katika maambukizi hayo.

Msemaji wa serikali Cyrus Oguna athibitisha kuwa na virusi vya corona

Kulingana na Mwangangi 393 ni wanaume  na 274 ni wanawake huku walioambukiza kwa miaka mwaka wa chini ni mtoto wa mwezi moja na mwaka wa juu ana miaka 67.