Covid 19 : Dawa ya Mitishamba ya Madagascar yashindwa kuzuia maambukizi ya corona

Hospitali nchini Madagascar zimekuwa zikikabiliana na ongezeko la maambukizi ya Covid-19 , huku rais akiendelea kunadi dawa ya mitishamba anayodai ina uwezo wa kutibu ugonjwa wa Covid 19.

Visa vya maambukizi vimeongezeka mara nne zaidi katika kipindi cha mwezi mmoja uliopita katika taifa hilo la kisiwani barani Afrika, huku zaidi ya watu 13,000 wakiambukizwa virusi na wengine na 162 kufariki kutokana na virusi vya corona, ambavyo vimesambaa karibu maeneo 22 ya nchi hiyo.

Licha ya ongezeka hilo la maambukizi, rais Andry Rajoelina amesimama na dawa hiyo ya kienyeji inayofahamika kama Covid-Organics, ambayo ilizinduliwa kwa kishindo mwezi Aprili.

Ilitengenezwana Taasisi ya utafiti ya Madagascar kutokana na mmea wa artemisia – chanzo cha dawa inayotumiwa kutibu malaria – na mimea mingine kutoka Madagascar.

Kinywaji hicho kilinadiwa kama tiba ambayo inaweza kuzuia na kutibu corona miezi minne iliyopita na imekuwa ikitumiwa na watoto shuleni

Mapema mwezi huu rais alionekana akigawanya dawa hiyo pamoja na bidhaa zingine muhimu kama vile mchele, mafuta na sukari kwa watu masikini katika mji mkuu, Antananarivo.

Bwana Rajoelina alikosolewa vikali kwa kusababisha mkusanyiko wa watu wakati wa amri ya kutotoka nje lakini, mtazamo wake kuhusu janga la corona haijabadilika: “Janga hili halitachukua muda mrefu, ni wingu linalopita na tutaishinda.”

Pia alidai kuwa idadi ya watu walioambukizwa haikua juu viungani mwa mji mkuu ambako dawa hiyo ilikua imeanza kusambazwa miezi kadhaa iliyopita.

Shirika la Afya Duniani WHO, inaunga mkono dawa za mitishamba lakini linataka uchunguzi wa kisayansi kufanyiwa dawa hizo kabla ya kuanza kutumiwa

Kufikia sasa hakuna matokeo ya majaribio ya kimatibabu iliyotolewa kwa umma – japo hilo halijazuia dawa hiyo kutajwa kuwa chanzo cha fahari ya tiba asilia katika baadhi ya mataifa ya Afrika. Dawa hiyo imeagizwa na nchi kadhaa za Afrika

 

Iwapo hutaki kuwafunza watoto basi acha:Magoha awakashifu wanaopinga masomo ya ‘kijamii’

Waziri wa elimu George Magoha amewashauri wasiotaka kuwafunza watoto katika mpango wa kutoa mafunzo  ya kijamii majumbani kuacha

Magoha  alikuwa kizungumza kuhusu pingamizi dhidi ya mpango wa kutumia mfumo wa nyumba kumi kuendelea kuwasomesha watoto nyumbani wakati huu wa janga la corona baada ya shule kufungwa kama njia ya kuzuia usambaaji wa virusi vya corona .

Junet atishia kumshtaki Khalwale kwa matamshi kuhusu pesa za Covid 19

” Kugeuka na kuanza kubadilisha mambo kuhusu mpango huo ni jambo la kusikitisha .mpango huu ulifaa kuhakikisha kwamba watoto wanasomeshwa katika maeneo walioko’ amesema Magoha

Akizungumza huko Eldoret  Magoha amesema kuna habari za kupotsha zinazoenezwa kuhusu mpango huo .

” Naskia mambo mengi kuhusu mpango huu… iwapo unaishia katika eneo  lililozizngirwa na kuna watoto 30 , na mwalimu mmoja huo ,unahitaji  PPE’s za nini ?’

” kama hutaki kuwafunza watoto wacha ..Usijisumbue! watoto ni wenu . Ni rahisi kwa njia hiyo

Akisema kwamba serikali haina mpango wa kuzifungua shule Magoha alisema wakenya wanafaa kukomesha dhana kwamba ni serikali ndio iliyoleta virusi vya corona .

Eliud Owalo akihama chama cha Mudavadi cha ANC

” Hatutafungua shule .masomo ya kijamii  sio mpango wa kufungua shule’

” watu wanafikiria kwenda shule ni kuhusu kalamu na karatsi .kuna vitu vingi vya kuwafunza watoto’ alisema

 

Yassin Juma apata corona gerezani, Ethiopia

Mwandishi wa habari Yassin Juma, ambaye alikuwa amezuiliwa nchini Ethiopia tangu mwezi uliopita amepatwa  na virusi vya corona, wakili wake Kedir Bullo amesema

Juma alikuwa anatarajiwa kufikishwa mahakamani katika mji mkuu wa Addis Ababa, lakini alishindwa kwa sababu ya kuugua, aliongeza bwana Bullo.

Covid 19 :Afrika kuanza kufanya vipimo vya cxhanjo dhidi ya coronavirus

Mahakama ilitoa amri ya kuachiliwa kwake kwa dhamana wiki iliyopita lakini polisi wa Addis Ababa walisema bado wanafanya uchunguzi dhidi ya madai yake na hivyo kuendelea kumzuilia kizuizini.

Mwandishi huyo alikamatwa pamoja na waandishi wa habari wawili wa Ethiopia. Walikuwa wanashutumiwa kwa kufanya ghasia na kupanga mbinu za kumuua maafisa wa juu wa Ethiopia.

Waandishi wote watatu walipinga madai dhidi yao.

Covid-19: Afrika kuanza kufanya vipimo vya chanjo dhidi ya coronavirus

Wiki ijayo, mataifa saba ya Afrika yanatarajiwa kuanza kufanya vipimo vya kinga ya mwili dhidi ya virusi vya corona, kituo cha Afrika cha kudhibiti magonjwa (CDC) kimeeleza.

Daktari wa maradhi ya kupumua afariki Covid 19

Vipimo hivyo ni sehemu ya jitihada za kuweza kuelewa ukubwa wa mlipuko wa janga hili katika bara la Afrika.

“Liberia, Sierra Leone, Zambia, Zimbabwe, Cameroon, Nigeria pamoja na Morocco ndio mataifa ya kwanza ya Afrika ambayo yamejishatiti kufanya vipimo hivyo, kiongozi wa CDC John Nkengasong ameeleza.

Alisema bara la Afrika limefanya vipimo vya corona milioni 9.4, idadi ambayo inakaribia milioni 10 ambayo ilikuwa imelengwa.

Dkt Nkengasong alisema Afrika imefanya jitihada nzuri katika kuanzisha chanjo.

Alisema jitihada za bara hili zilianzishwa na taasisi kadhaa ili kufanya jaribio na kuanza kutoa na kufadhili chanjo.

Afrika imerekodi maambukizi 1,084,904 ya virusi vya corona, kwa mujibu wa takwimu ya chuo kikuu cha Johns Hopkins.

Daktari wa maradhi ya kupumua afariki kutokana na Covid-19

Wahudumu wa afya wanaomboleza kifo cha mwenzao  aliyekuwa daktari wa maradhi ya kupumua ambaye alikuwa na ugonjwa wa Covid 19

Ndambuki Mboloi   aliaga dunia kwa ajili ya virusi hivyo siku ya Alhamsi, kimetangaza chama KMPDU.

Muungano huo sasa unaitaka serikali kuzindua huduma za kuwafidia wahudumu wa afya wanaoaga dunia wakiwa kazini

Kufikia wiki jana, Kenya ilikuwa imepoteza  wahudumu wa afya 14 kwa ugonjwa wa Covid 19  huku zaidi ya 600 wakiambukizwa

Kwa ajili ya hilo KMPDU imezindua kampeini mtandaoni ili kutaka kuboreshwa kwa maslahi ya utendakazi ya wanachama wake wote. Kampeini hiyo ni kwa heshima ya Daktari

Visa vya Covid 19 nchini vyaongezeka hadi 28,754 baada 650 kupatikana na virusi hivyo

Doreen Adisa  ambaye aliaga dunia kwa ajili ya Covid 19

“.. Mimi ni Adisa .. tunahitaji vitanda, vifaa na huduma ya bima. Afya yangu, maisha yangu kama daktari  hayapo tena mikononi mwangu’ wamesema katika kampeini hiyo

Madaktari hao wameitaka serikali kuwalinda  na kuwapa huduma za ushauri.

“Adisa  alifanya kila alichoweza lakini ugonjwa huo ulimuangamiza. Huku watu wengi wakiambukizwa, madaktari zaidi wataambukizwa’

Wahudumu hao 14 wa afya walioaga dunia ni kutoka idadi ya watu 423 walioaga dunia kote nchini kwa ajili ya virusi hivyo kuanzia mwezi Machi. Takriban  wahudumu 768 wa  afya wamepatikana na  na virusi hivyo  kufikia Agosti tarehe 10.

 

Visa vya Covid 19 nchini vyaongezeka hadi 28,754 baada 650 kupatikana na virusi hivyo

Kenya leo imesajili visa 650 zaidi vya ugonjwa wa corona na kufikisha visa hivyo kuwa 28,754.

Katibu wa  utawala katika wizara ya Afya Mercy Mwangangi amesema visa hivyo vimetoka kwa sampuli  6,768  zilizopimwa katika saa 24 zilizopita.

Kutoka visa hivyo 633 ni vya  wakenya  ilhali 17 ni raia wa kigeni.

Mwangangi amesema watu 391  ni wanaume ilhali 259 ni wanawake huku mgonjwa mwenye umri wa chini sana akiwa mtoto wa mwaka mmoja na mwenye umri wa juu zaidi akiwa mwenye umri wa miaka 80

Watu 490 wamepona  na kufikisha idadi ya waliopona hadi sasa kuwa  15,100.

Hata hivyo watu wanne zaidi  wameaga dunia kwa ajili ya corona na kufikisha idadi ya walioaga dunia hadi sasa kuwa 460

Covid-19:Watu 679 wapatikana na virusi vya corona

Watu 679 wamepatikana na virusi vya corona na kufikishia idadi ya jumla 28,104 ya watu walioambukuzwa na virusi hivyo,katika saa 24 zilizopita, hii ni kutokana na sampuli 6,590 zilizopimwa Katibu wa utawala wa wizara ya Afra Mercy Mwangangi amesema.

Hayo yakijiri watu 18 wamepoteza maisha yao kutokana na virusi vya corona na kufikisha 456 ya watu walioaga dunia, pia watu 783 wameruhusiwa kuenda nyumbni baada ya kupona corona na kufikisha idadi ya watu

15 waaga dunia huku 497 wakipatikana na virusi vya corona

Wagonjwa 400 ni wanaume ilhali 279 ni wanawake, miongoni mwa walioaga ni mkuu wa wafanyakazi wa KEMRI.

Kati ya wagonjwa hao 658 ni wakenya na 21 ni taia wa kigeni huku mwenye umri wa chini ana mwezi mmoja na wa umri wa juu ana miaka 87.

15 waaga dunia huku 497 wakipatikana na virusi vya corona

Watu 15 wameaga dunia kwa ajili ya virusi vya corona katika saa 24 zilizopita .

Katibu wa utawala wa wizara ya Afra Mercy Mwangangi  amesema hayo wakati akitangaza kwamba Kenya imesajili visa vipya 497 vya ugonjwa huo nchini  kutoka sampuli  4171 na kufikisha jumla ya visa hivyo  nchini kuwa 27425.  Kati ya waliopata ugonjwa huo 467 ni wakenya ilhali 30 ni  raia wa kigeni .

Wagonjwa  312 ni wanaume ilhali 185 ni wanawake . Mwangangi pia ametangaza kwamba 372 wamepona idadi inayofikisha jumla ya watu waliopona ugonjwa huo hadi sasa kuwa 13,867.

Covid 19 : Urusi yapata chanjo ya coronavirus Putin asema imeidhinishwa kwa matumizi

Kati ya watu 15 walioaga dunia ,11 walikuwa na matatizo ya awali ya kiafya na idadi hiyo sasa inafikisha 438 walioangamia kwa ajili ya virusi vya Covid 19 nchini .

Covid 19 : Urusi yapata chanjo ya coronavirus Putin asema imeidhinishwa kwa matumizi

Rais wa Urusi Vladimir Putin amesema kwamba chanjo iliyotengenezwa ndani ya Urusi kwa ajili ya ugonjwa wa Covid-19 imeidhinishwa kwa matumizi baada ya kufanyiwa majaribio kwa binadamu chini ya miezi miwili.

Bwana Putin amesema kwamba chanjo hiyo imepita vigezo vyote vilivyowekwa na kuongeza kwamba binti yake tayari amepatiwa.

Maafisa wamesema kuwa wanampango wa kuanza kutoa chanjo hiyo kwa umma kuanzia Oktoba.

Wataalamu wameonesha wasiwasi wao kuhusu kasi ya kazi ya Urusi na kusema kuwa watafiti huenda wametumia njia za mkato.

Huku wasiwasi ukiendelea kuhusu uwezekano wa usalama kuingiliwa wiki iliyopita Shirika la Afya Duniani (WHO) liliitaka Urusi kufuata miongozo ya kimataifa ya kutengeneza chanjo dhidi ya virusi vya corona.

Chanjo iliyotengenzwa na Urusi sio miongoni mwa orodha ya zile za WHO ambazo zimefika awamu ya tatu ya majaribio kunakohusisha majaribio kwa watu wengi zaidi.

 

Covid-19: Watu 492 wapatikana na virusi vya corona

Kenya hii leo imerekodi visa 492 vipya vya maambukizi ya corona na kufikisha idadi ya jumla 26,928 ya watu walioambukizwa virusi hivyo hii ni kutokana na sampuli 4063 zilizopimwa chini ya saa 24.

Watu 534 wamepona kutokana na virusi hivyo na kufikisha idadi jumla ya 13,495 ya watu waliopona virusi vya corona Mutahi Kagwe alisema.

Kaunti ya Nairobi inazidi kuongoza kwa maabukizi hayo huku hii leo ikifuatwa na kaunti ya Garissa, huku haya yakijiri watu wengine watatu wameaga dunia kutokana na virusi hivyo na kufikisha idadi ya jumla 423 ya watu walioaga dunia kwa ajili ya virusi vya corona.

Huku akizungumza alisema kuwa hospitali zinapaswa kuzingatia kupeana ripoti zifaazo za maambukizi ya corona, pia alisema kuwa mgonjwa wa umri wa chini ana miezi kumi na moja na wa juu ana miaka 83.