PATANISHO: Bwanangu alileta msichana kwa nyumba akidai ni cuzo

Monicah alituma ujumbe akiomba apatanishwe na mumewe bwana Joseph, ambaye walikosana baada ya kuleta msichana mwingine kwa nyumba huku akidai kuwa ni binamu yake.

PATANISHO: Mama alimkosea mke wangu akitaka kujionesha yeye ndio kichwa

“Naskia tu maisha yamenilemea. Hakuwa cousin yake juu huyo msichana alikuja tukaanza kuishi naye na tukaanza kugombana naye.

Nilifanya uchunguzi nikajua alikuwa rafiki yake ila sio wa familia yao na isitoshe tuliishi naye wiki tatu.” Alieleza Monicah huku akidai kuwa kuna wakati alikuwa anamuacha mumewe na yule ‘binamu’ mezani bila kushuku lolote.

Yule msichana alikuwa hadi anavaa nguo zangu na kumweleza mume wangu hakuwa anafanya lolote kusuluhisha hilo.” Aliongeza.

Kulingana na Monicah tangia watengane ameskia kuwa mumewe alishikana na mwanamke mwingine lakini bado anampenda yule jamaa na anataka warudiane.

PATANISHO: Bwanangu alioa mfanyi kazi wetu na hajawahi niongelesha miaka saba

Wawili hao wamejaliwa mtoto mmoja.

“Najua kipindi chako, najua Monicah lakini sasa mambo ni ngumu.” Alisema Joseph huku akisema kuna mambo mkewe alifanya yaliyomkera na hatataja hewani.

Natafuta na mtu nitakaye ishi naye na ni mtu atakayeishi vile natarajia kwani Monicah hakuwa anafuata programme yangu pia umri wangu ni mkuu kumshinda.” Aliongeza Joseph.

Hakuna mwanaume aliye na akili timamu anayeweza leta mwanamke mwingine kwa nyumba na kusema ni binamu yake. Hakuwa mwanamke mwenye ushirika nami ila alikuwa mtu wa nyumbani. ”

Hata hivyo alisema alimsamehe kitambo ila haoni wakirudiana kamwe.

Pata uhondo kamili.