Mke wangu hataki tutoe ‘contraceptive’ Bahati na Diana waeleza haya

Huku wakizungumza wakiwa kwenye mitandao ya youtube, msanii Bahati na mkewe Diana Marua walieleza kwa nini Diana alilazimika kutoa mpango wake wa uzazi yaani kwa lugha ya kimombo(Contraceptive).

Wawili hao walieleza kuwa daktari alimshauri Diana aweze kutoa mpango huo wa uzazi ili awache au apunguze uvimbe mwilini mwake.

“Nataka kutoa IUD ambayo nilieka, ukiwa mwanamke utaelewa kwa nini unahitaji mpango wa uzazi, nina historia kuhusu uvumbe katika mguu wangu wa kushoto tangu nikiwa shule ya upili

Bahati
Bahati with Diana Marua

Nimeenda hospitalini mara kadhaa na hata kufanya vipimo lakini hakuna kitu ilikuwa inanionyesha, baadaye iliacha kuvura yenyewe lakini kwa siku tano zilizopita huu mguu ulianza kufura wenyewe na uchungu mwingi

Kwa hivyo daktari alinishauri nitoe mpango wa uzazi kwenye mwili wangu.” Diana Alisema.

Msanii Bahati alijiunga na mazungumzo hayo ambapo alisema kuwa mkewe hataki kutoa kifaa hicho ilhali alishauriwa na daktari atoe.

diana marua
diana marua

“Tulipoenda kwa daktari alishauriwa atoe ili kitu chochote kisitendeke, mke wangu hataki tutoe contraceptive huku akisema hatuwezi ishi bila contaceptive bali mimi ni mfalme wa withdrawal.” Alisema Bahati.

Mkewe Bahati aungana na mashabiki kutuma rambirambi zao kwa msanii Weezdom

Aliyekuwa msajiliwa wa lebo ya EMB msanii Weezdom yuko katika maomboolezi hii ni baada ya kumpoteza rafiki wa karibu na mama lakini si mama mzazi ambaye aliaga dunia mnamo jumapili Agosti,30.

Kupitia kwenye mitandao ya kijamii Weezdom aliposti video huku akieleza jinsi mwendazake Faith Peter alimlea kama mama mzazi.

“Wacha ni seme kuwa zawadi ya maana humu nchini ni uhai, nimepata habari tu saa hii, kuwa nimempoteza mmoja wa watu wa maana katika maisha yangu na ambaye ningetamaini angekaa duniani ili atazame na kuona mafanikio yangu lakini nimempoteza hii leo

Rafiki wa karibu ambaye alikuwa familia kwangu ambaye wakati wangu mgumu alinishika mkono kama mama mzazi lala salama faith peter

Rafiki ambaye alikuwa familia, lala salama mamaa 💔💔💔 utahishi kwa moyo wangu milele.” Alisema Weezdom.

Pia aliposti picha ambazo walipigwa kabla ya kifo chake, inaashiria ya kwamba mwendazake amekuwa na Weezdom hapa na pale.

Mashabiki na mkewe Bahati walichukua fursa hiyo na kutuma risala za rambirambi kwa msanii huyo na hizi hapa baadhi ya jumbe zao;

 

118460925_317260226151552_6034155444832923177_n

diana marua: Pole Sana Weez! It will be well. May She Rest In Power ❤️🙏

vivianne_ke🙏🙏🙏🙏 Take heart. Our prayers go to your family

nanaowiti: Woiye! Saddened. She had such a kind beautiful soul Woiye!!! RIP Faith. Pole Weez. I know how much you guys cared for each other. 💔💔💔💔

ladybee_254May the Lord comfort you family🙏 Poleni sana

118559737_111332433928493_3575436133626634449_n

winnie_shareefaMy deepest condolences Weez🙏🏾 Rest well Mama🙏🏾🙏🏾:

mylee_staicey:May She Rest In Peace🙏🏽

feimutioRest easy beautiful🤗❤️❤️

guardianangelglobal: pole sana kaka

‘Kubali tu kukaliwa na mkeo’ –Bahati atoa siri ya ndoa yenye furaha

Bahati  na  Diana Marua  ni  wanandoa ambao wameangaziwa sana nchini na mengi yamesemwa kuwahusu katika mitandao ya kijamii. Bahati kwa upande wake amelazimika kuzoa  kejeli za kila mara kuhusu tofauti ya umri  kati yake na mkewe ambaye anamshindia kwa miaka mitatu.

Trouble maker?Msanii wa nyimbo za Kikuyu Muigai Njoroge atakiwa kufika mbele ya NCIC kuhusu wimbo wa ‘mashamba’

baha 2

Msanii huyo hata hivyo hajaonekana kujalishwa na hilo kwani anasema umri kwake sio jambo la kutia fikrani kwa sababu wana ndoa yenye furaha sana na mkewe Diana. Hata hivyo, amekiri kwamba wakati mwingi ameamuacha Diana kuthibiti kila jambo katika ndoa yao kwani hiyo ndio njia bora ya kuwa na amani na hata furaha katika ndoa.

Single and Worried: Mbona mahusiano yako hayadumu? Hizi ndio sababu

baha 3

Mashabiki wengi  ambao huchakura picha za Bahati na Diana mitandaoni wamekuwa kila mara wakidai kwamba Diana ni mkubwa sana kuwa mkewe Bahati. Hilo halijawanyima usingizi wawili hao na wamekuwa wakishangaa mbona kuna makali sana ya kuwakosoa. Kuhusu mbinu yake ya kuhakikisha kwamba hapatokei migogoro katika ndoa yao, Bahati amesema;

“Nyumba ni ya mwanamke, nawashauri wanaume  kwamba endapo wanataka kuwa na ndoa zenye furaha basi waacheni wanawake wathibiti nyumba  na wawe katika usukani,” amesema Bahati

baha 4

Hata hivyo amesema hatua hiyo yake haimaanishi kwamba jukumu lake kama baba mwenye nyumba  ameliacha kwani licha ya Diana kuchukua usukani wa mambo mengi, yeye bado ndiye kiongozi wa nyumba yao.

 

 

Bahati aeleza kwa nini alimtumia rafiki ya mkewe kama video vixen

Mkurugenzi ama ukipenda bosi wa lebo ya EMB Kevin Bahati ameeleza kinagaubaga kwa nini alimtumia rafikiye mkewe anayefahamika kama Phoina kama video vixen kwenye kibao chake kipya cha ‘Wanani’.

Akiwa kwenye mahojiano alisema kuwa aliamua kumtumia Phoina kwenye wimbo wake kwa maana ametumia mke wake kwenye nyimbo zake mbili.

Bahati alisema kuwa wimbo mmoja ambao Diana amurua aliutoa miaka michache iliyopita wa ‘mpenzi’ na ule mwingine ambao Diana atakuwa video vixen atautoa mwaka wa 2021.

Screenshot-2020-06-12-at-09.58.05

 

Alizidi na mazungumzo na kusema kuwa kama msanii anapaswa kuwa na mitindo tofauti na kufanya kile atakacho wala si kile watu wengine wanahitaji.

Sikumtumia Diana sababu yupo kwa nyimbo zangu nyingi, nimefanya naye mapenzi na kuna video yangu special inatoka 2021 bado ni yeye yupo. Isitoshe, ndio maana naitwa gospel artiste, nafaa kuwa artistic nisifanye vitu ambavyo watu wanategemea.” Bahati Alisema.

Akiwa kwenye mahojiano aliisema kuwa amemaliza mwaka kama hajahojiwa na kuwa mahojiano hayo ndio ya kwanza baada ya mwaka huo mmoja kukamilika.

Screenshot-2020-06-12-at-09.59.10

“Sijakuwa na sit down for over a year. Mwisho nilikaa na wewe na Mwakideu niliona mnaleta ufala saa zingine.”

Bahati pia aliwahakikishia mashabiki wake kuwa ni msanii wa nyimbo za injili na wala hajabanduka.

Tazama picha za video vixen anayetishia kumuondoa Diana Marua

Inaonekana mtoto wa mama Bahati hakutoshelezwa na pesa za muziki wa nyimbo za injili, huku akianza kuimba muziki wa kidunia. Mnamo tarehe 11 Juni, msanii huyo alitoa kibao kinachofahamika kama ‘wanani toto si toto.’

Baba huyo wa watoto watatu alianza kuimba nyimbo zake akiwashirikisha wasanii au kikundi cha Gengetone, Boondocks ambao wanafaahamika kwa vibao vyao vya nyimbo za kidunia.

Bahati alikuwa mwerevu zaidi baada ya kutumia picha za kanisa katika video ya muziki wake na Gengetone kuwachanganya mashabiki wake wasione kuwa ameanza kuimba nyimbo za kidunia.

Screenshot-2020-06-12-at-10.46.18

Wimbo ambao Bahati ameutoa unathibitisha kuwa ametoka katika dunia ya nyimbo za injili na kuanza kuimba nyimbo zingine.

Hivi ndivyo Willy Paul alianza kabla ya kuanza kuimba nyimbo za kidunia kabisa na kuingia na miguu yote katika nyimbo za kidunia. Haya basi Bahati ametoa kibao hicho na video vixen mmoja anayetishia kumuondoa Diana.

Mbali na hayo, kibao cha wanani toto si toto ni kibao cha mapenzi na inaonekana mwanamke huyo amechukua moyo wa msanii huyo.

Si vibaya Bahati kuanza kuimba nyimbo za kidunia lakini cha kushangaza ni aliweza vipi kumchukua rafikiye Diana awe Vixen katika kibao chake?

Screenshot-2020-06-12-at-09.58.05

Mashabiki wake walimuonya dhidi ya video vixen huyo, hizi hapa baadhi ya hisia za mashabiki wake;

_l.a.v.y.25 Aaai baha Diana aliaccept hiyo video 😢😢

miss_v7922 i feel like diana should be the one

paulahwawira the video vixen is Diana’s best friend she’s called @phoinahaircollection

teddiegodwiller this is business, ukileta wivu kwa job utakua Mawe? 🤣

_poetic_rasta Hivi ndo mtu huachwa😂😂

jennysean3 Akyyyyy Diana utanyaganywa bwanako ukionanga tuuuuu na machoooo,,,,,,huyu Dem n🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥

BeFunky-collage-2020-06-12T112830.375-scaled(1)

Screenshot-2020-06-12-at-09.59.10

‘Diana saidia bwana yako Bahati Kuimba.’ Willy Paul amuambia Diana Marua

  Yaonekana bifu kati ya willy Paul na Bahati imerudi tena kwani wasanii hao wameonekana kutupiana vijembe mitandaoni .

pozze 2

Bahati maajuzi ameandika jinsi alivyokuwa akimsaidia Willy Paul kwa kumuandikia nyimbo  na kusema ;

 “The days I used to write songs for this small boy.  I’ve missed our childish days bro #WillisRadido,”

Akijibu hilo, Willy Paul  alisema katika instagram;

“So, I’m told Bahati mtoto wa Diana said amekuwa akiniandikia nyimbo. Never. What should I tell him? Anyway, that’s me driving with my legs just to pass a little message to that boy.”

 No Hard Feelings: Tanasha Donna amtumia ex wake Diamond  ujumbe mtamu  wa kumshukuru

Posti hiyo baadaye ilifutwa. Wawili hao wamejipata mashakani  baada ya kubadilisha muziki wao kutoka ‘gospel’ hadi midundo ya kisasa .

Katika video nyingine iliyosambazwa mtandaoni, Pozze alidai kwamba  muziki wa Bahati ulikuwa  ukididimia. Pia alimshauri Diana Marua kumsaidia mumewe kutengeza nyimbo nzuri badala ya kutumia pesa zake.

‘Alikuwa akinikojolea na kunifukuza nje uchi.’ Mtangazaji wa zamani wa KBC Rachel Wainaina asimulia masaibu na mume wake wa zamani

“Bwana Diana utatuonyesha mambo kweli. Si uache hata Diana aimbe. Diana saidia Bwana yako. We unataka ulishwe Bwana anapoteza vocals we uko hapo unakula tu. Saidia Bwana.”  Alisema  Pozze

Katika posti nyingine pozze alisema

“My brother Bahati naskia ulikua uniandikia songs….. mimi? Uko sure ni mimi?? Ooh lord, give mtoto wa Diana his memory back!! He’s mistaking me for Weezdom.. Let me remind you Baba:.. Naitwa KING POZZE. Much love… Pitia home kesho kuna maji moto na ndimu atleast itakuhelp… Guys, what should i do to this small boy??”

 pozze 3

 

Double agent? Diana Marua aeleza selfie yake na Victor Wanyama

Diana Marua  ni mwanamke ambaye ameyasikia yote na kuvumilia mashambulizi makali ya mtandaoni dhidi ya mume wake Bahati.

Lakini hakujua kwamba atageuziwa mtutu wa bunduki na kuanza kujitetea akikimbia kuitetea hadhi yake baada ya kuibuka  madai kwamba wakati mmoja alikuwa katika uhusiano wa kimapenzi na mwanasoka Victor Wanyama. Madai hayo yalianzia twitter na picha zikaambatanishwa na madai hayo .

Mistaken Identity?Mrembo katika sakata ya Willis Raburu na Mkewe si mpenzi wa mtangazaji huyo,hata hamjui(Picha)

diana 2

Katika  youtube, wakati wa maswali na majibu  ambapo alijumuika pia na mumewe Bahati  Diana amesema hakuwahi kuwa katika uhusiano na mchezaji huyo wa soka na kwamba walikutana kupitia kwa rafiki yao mmoja.

“ Nilikutana na Victor kupitia kwa rafiki na tukajivinjari kwa muda  na ndiposa zilipigwa zile picha’

diana 3

Diana pia amewalaumu KOT kwa kuanzisha madai hayo  akisema waliamua kuzitumia picha za selfie pekee badala ya picha walizopigwa kwa makundi wakiwa watu wengi .

diana 5

Bahati  alikuwa kimya  wakati mke wake akijitetea na kujaribu kuvunja madhara ya uvumi uliokuwa umesambazwa  na wanamitandao.

‘ Nataka watoto zaidi’ Betty Kyallo afunguka kuhusu ndoa na mipangpo ya siku zijazo

Bahati huenda ndiye akajilaumu kwa makombora ambayo mkewe anarushiwa kwani mwezi jana aliibuka na posti ya dharau kwamba hakuna mwanamume anayeweza kumtunza mke wake kwa sababu ni wa hadhi ya juu. Madai hayo ndio yaliyowachemsha wanamitandao waliozama na kuibuka na picha hizo za jadi za Diana  ili kumpa adabu Bahati kwamba kulikuwa na wanaume wengi mbele yake katika  maisha ya Diana kabla hajakutana naye.

 

MHARIRI: DAVIS OJIAMBO

 

 

 

 

Ndoto Butu? Msanii Bahati asema siku moja atakuwa rais wa Kenya

Mwanamuziki Bahati huenda ana amaazimio mazito kuliko uzani wake .

bAHATI 2

 

Labda uwache kuwa na umama ndio uwe rais! Bahati asema anaweza piga marufuku mtandao wa Twitter akiwa rais

Baada ya kuwa katika ndimi za wengi wa kufaniwa mzaha mitandaoni hivi karibuni kw ajili ya wimbo wa Kaligraph kwa jina ‘ hao’ bahati sasa anasema siku moja atakuwa rais wa Jamhuri ya Kenya . Katika wimbo wake ,Kaligraph alimpiga Bahati kijembe kwa kumtaja kama  ‘Bahati mtoto wa  Diana ,mstari ambao uliwafanya wengi kumpiga kejeli msanii huyo  aliyetamba kwa wimbo ‘mama’.

BAHATI 3

 

Mtoto wa Diana! Bahati afanyiwa kejeli baada ya video yake akidensi na mkewe Diana Marua

Hakusazwa  katika mitandao kwani alianza tena kuchanwachanswa wakati alipotoa video na Diana wakiwadensi huku Bahati akiwa amevalia nguo za mwanamke . Jana msanii huyo aliamua sasa kugonga msumari mwingine katika kidonda cha mashabiki wake katika instagram kwa ujumbe ambao bila shaka ulilenga kuzua majibu ya kila aina .

Niaje mtoto wa Diana? Uko freshi kweli? Bahati amjibu Khaligraph Jones baada ya kumuita mtoto wa Diana

Alitaka kuheshimiwa na watu katika twitter  na kuahidi kwamba siku moja atakuwa rais wan chi  .Ujumbe wake ulisema hivi ;

 “I will be the President of this Country One Day  So Tell those Keyboard Warriors on Twitter to Come Srowwree and Address Me With Respect!… hio Ndio Kitu Ya Kwanza Nitafunga Nikiapishwa  #MrBahati.”

“Twitter is the First thing I will burn Once I’m Sworn in as the President of Kenya. Aki Simnasumbuaaa #BAHATI,”  Bahati alisema

Kilichofuatia ni  kejeli zaidi huku wengfi wakipuuza uwezo wake  kuongoza hata kanisa lolote

BHATI 4

‘Nitakupokonya Diana na niende naye marekani.’ Aliyekuwa mumewe Eunice Njeri amtishia Bahati

Kwa siku kadhaa sasa msanii Bahati na mkewe Diana Marua wamekuwa wakienea sana kwenye mitandao ya kijamii kwa kukejeliwa na mashabiki wao.

Wasanii wengi na mashabiki walimtetea na hata wengine kumkejeli licha ya kuwa ni msanii mwenzao.

Mtoto wa Diana! Bahati afanyiwa kejeli baada ya video yake akidensi na mkewe Diana Marua

94883239_2823619474357913_3546552714589449259_n(1)

Aliyekuwa mume wa mwimbaji Eunice Njeri, Isaac Bukasa almaarufu rapa Izzo amemuomba msanii wa nyimbo za injili Bahati kujirekebisha ama atampokonya mke wake.

Rapa huyo alimuonya Bahati kuwa huenda akamchukua Diana Marua kwa sababu anahitaji mwanamume ambaye amekomaa kiakili.

Kupitia mtandao wa kijamii wa instagram, Izzo alikuwa na ujumbe huu wa kumwambia Bahati, baada ya kuposti picha ya mkewe Bahati.

@Bahatikenya if you wont style up, I will fly in Diana and give her a better Life in the USA, she needs a better mature man not just forced tiny beards with no brains.

Stay warned. You are either fully in God or out completely.
Thank you @Ringtoneapoko for your advice on Gospel artists.” Aliandika Izzo.

Changamoto wanazopitia Bahati na Diana zitaisha – King Kaka

Matamshi yake Izzo yanakuja siku chache baada ya Bahati kuposti video akiwa amevalia vipuli na nguo ya Diana huku akiwa anacheza.

 

Mtoto wa Diana! Bahati afanyiwa kejeli baada ya video yake akidensi na mkewe Diana Marua

Msanii Bahati amejua sana kujiwekea mtego na wiki hii amekula vijembe kwa njia ya kikatili mtandaoni .

bahati 2

Tanasha Donna asilimu na sasa jina lake ni Aisha – Msanii athibitisha safari yake mpya katika Uislamu

Msanii huyo amefanyiwa masimango na kejeli baada ya  rapa  Khaligraph Jones kutoa wimbo wake ambao ulimtaja Bahati kama ‘Mtoto wa Diana’ .

Bahati alijaribu kuteka   mawimbi ya wimbo huo kwa kutoa picha iliyomuonyesha akiwa amebebwa na Diana na hivyo kweli alifaulu kupepezea chini kejeli ambazo zingemfuata. Lakini alipoamua kuvalia kama mwanamke na kushiriki shindano la Tik tok na Diana, Bahati alifungua bomba kubwa la kufanyiwa mzaha na  huenda hakutarajia mlipuko wa hisia kama hizo

 

Bahati 3

Nataka mimba! Mtu ajitokeze- Akothee afichua uchu alio nao wa kupata mtoto

Haya hapa baadhi ya maoni ya wanamitandao

namelesskenya Woiiii…bhangi hiyo haikuwa imekauka vizuri… ‍♂️‍♂️

jalangoo Umechizi

djjoemfalme Bro nilishakushow. Turudi EMB buda….Ama nikustaki kwa @akotheekenya. Hii energy turudishe kwa kazi

akotheekenya Nitahama hii Kenya haki

clemmo25 Corona itatuonyesha mengi!!

gabu_bugubugu Umama umekuingia sasa. Happy mothersday

mzaziwillytuva Mwezi wa mfungo umeanza  Tuzidishe #Maombi

dansonko Vitu kama hizi ndio zimefanya tuongezewe 21 days zingine aki!

wesleytheedj Uko sawa buda?

weezdom254 Unakaa tule tudem hukula fare

yycomedian Halafu unapata tu kuna mwanaume wa Cameroon atanyonga na hii video bila kujua ni ndume…

felistarbrigita   mtoto wa dayana sasa utakuwa mama dayana

munju_ree bahati umeanza umama

goldshine___ Vipe tena bahat ushakuwa dulla makabila

bahati 4