Kipchoge, Kenyatta wafanya mazoezi Ikulu, katika uzinduzi wa Beyond Zero

Mama wa Taifa Margaret Kenyatta alijumuika na bingwa wa olimpiki wa mbio za masafa marefu Eliud Kipchoge kwenye ikulu ya Nairobi katika uzinduzi wa mbio za Beyond Zero.

Hafla ya Beyond Zero Half Marathon inatarajiwa kufanyika Machi tarehe 8, 2020 jijini Nairobi.

Moses Kuria Apuuzilia Mbali Ripoti Ya BBI, Adai Ni ‘Feki’

Katika uzinduzi huo, Mama wa taifa alidhihirisha kujitolea kimasomaso katika kutetea huduma za afya kwa watoto na wanawake kote nchini.

Aidha, Margaret Kenyatta alifanya mazoezi ya riadha katika ikulu pamoja na Eliud Kipchoge na mkewe Grace mwendo wa asubuhi.

 

kipchoge beyond zerro campaing-compressed

Mama wa taifa pia alitangaza kuongezwa kwa nafasi za watakaonufaika na ufadhili wa masomo kutoka 100 hadi 200 hapo mwakani.

Alisema kuwa fedha zitakazo changishwa katika hafla hiyo zitatumika kuimarisha vifaa vya kliniki pamoja na ujenzi wa maeneo ya kimatibabu ya Beyond zero.

Miongoni mwa waliokuwapo ni mawaziri Amina Mohammed na Margaret Kobia pamoja na Seneta Beth Mugo na  Ida Odinga mkewe kiongozi wa upinzani Raila Odinga.

 

 

 

 

 

 

 

Picha ya siku: Eliud Kipchoge aburudika na bingwa wa F1 Lewis Hamilton

Baada ya kutuzwa kama mwanariadha bora duniani mwaka wa 2019, Eliud Kipchoge amekuwa akitumia mda wake wa mapumziko, kujibamba na kutalii nchi tofauti.

Wikendi iliyopita, Kipchoge alichapisha picha akiwa Abu Dhabi alipokuwa ameelekea kushabikia bingwa wa F1, Lewis Hamilton, kupitia mualiko spesheli kutoka kwa kampuni ya Mercedes.

Bingwa huyo wa mbio za marathon kisha alipata nafasi murwa kabisa kutangamana na kuburudika na Hamilton ambaye alituzwa kama bingwa wa mbio hizo.

Eliud kupitia mtandao wa Twitter aliandika,

A very inspiring weekend with

at the Grand Prix of Abu Dhabi. A pleasure meeting Lewis, Valtteri and the entire team and see their focus, discipline and hard work from up close.

kipchoge q kipchoge 2 kipchoge

Kipchoge awasili kimyakimya, fahamishwa mbona hatachinja ng’ombe kusherehekea

Bingwa wa dunia katika mbio za masafa marefu Eliud Kipchoge aliwasili nyumbani kutoka Austra Vienna kimya kimya baada ya kuweka historia kwa kukimbia marathon kwa muda wa chini masaa mawili.

Kipchoge  aliwasili nchini bila mapokezi ya kitaifa na sherehe mnamo Jumatano asubuhi.

Kinyume na vile ilivyotarajiwa, Wakenya walitamani sana kupewa fursa ya kumuenzi bingwa huyu wa riadha. Hata baadhi wakitaka sikukuu kutengwa kwa ajili yake, lakini Kipchoge  anasema: “Sitasherehekea kwa kuchinja ng’ombe. Hayo hayatawaHifanyika katika maisha yangu. Sherehe yangu kubwa huishia uwanjani ninapokata utepe”

Kutana Na Mo Salah ‘Feki’ Anayetumiwa Katika Matangazo Ya Runinga

Anatarajiwa kupokelewa  pamoja na familia yake na timu yake katika kambi yake na mazoezi Global Communications.

“Kwa sasa tunapanga mikakati ya kusherehekea. Ni vizuri kusherekea ushindi, kutulia, kupongeza timu yangu na kujiandaa kwa shughuli zijazo,” Kipchoge alisema.

Hata hivyo bingwa huyu alifutilia mbali wito wa kufanyiwa sherehe za kitaifa.

“Nitasherehekea bali kimya kimya. Kwa njia ya unyamavu, sio kwa kishindo” Kipchoge alisema.

Hata hivyo Kipchoge hakutoa maazimio yake iwapo atashiriki katika michezo ya Olimpiki jijini Tokyo Japan mwaka ujao.

Alisema kwamba ingali mapema kusema hatua yake ijayo.

“Sitaki kuzungumzia mashindano ya Tokyo sasa, lakini natumai nitakuwa katika mstari wa  kuanzia. Bado ninayo miezi kadhaa kabla ya Tokyo na ninahitaji kusherekea mwanzo.” alisema.

“Ninawapongeza wakenya wote walionishabikia kwa muda huo wote  wa 1:59:40.  Ninawaambia wajipe motisha na wajue kwamba binadamu hadhibitiki akiamua kutenda” Kipchoge alisema.

Orodha ya mali 10 inayomilikiwa na mjane Sarah Wairimu

 

 

Je atawahi? Kipchoge ateuliwa kwa tuzo la mwanariadha bora wa mwaka

Bingwa wa dunia wa mbio za marathon Eliud Kipchoge na bingwa wa dunia wa mbio za mita 1500 Timothy Cheruiyot wameteuliwa kwa tuzo la mwanariadha bora wa mwaka wa IAAF.

Kuteuliwa kwake Kipchoge kumejia siku kadhaa tu baada ya kuandikisha historia kama binadamu wa kwanza kukimbia na kumaliza mbio za nyika chini ya masaa mawili.

Martial anatarajiwa kucheza dhidi ya Liverpool baada ya kuregelea mazoezi

Kipchoge na Cheruiyot ni miongoni mwa wanariadha 11 walio kwenye orodha iliyotolewa na IAAF kwa hafla hiyo ya kila mwaka itakayoandaliwa November tarehe 23 jijini Monaco, Ufaransa.

Wawili hao watakabiliwa na ushindano mkali kutoka kwa wamarekani Donavan Brazier, Christian Coleman na Noah Lyles.

David Rudisha ambaye ndio bingwa wa mita 800 na anayeshikilia rekodi ya mbio hizo na bingwa mara mbili wa olimpiki, ndiye mkenya pekee amewahi shinda tuzo hizo.

Rudisha alituzwa mwaka wa 2010.

Upigaji kura wa mwanariadha bora wa kiume utafungwa Novemba tarehe 4. Baadae wanaume na wanawake 5 watatangazwa na shirika la riadha duniani, IAAF.

PATANISHO: ‘I am busy muache kunilazimisha kuzungumza!’ – Paul

Matukio ya Spoti Wikendi: Tazama jinsi Kenya ilivyotamba ulimwenguni

Imekuwa wikendi ya kufana sana katika ulingo wa spoti baada ya Wakenya kuonyesha ubora wao ulimwenguni  mzima na  kwamba binadamu hadhibitiki akiamua kutenda.

Mnamo Jumamosi asubuhi  Eliud Kipchoge alisababisha macho ya ulimwengu mzima kutua kwa siku nzima kushuhudia azimio la ufanisi wake.

Alionyesha  ulimwengu mzima  kwamba binadamu hadhibitiki akiamua kutenda.

Haya ni baadhi ya matukio muhimu yaliyosababisha bendera ya Kenya kupeperushwa ughaibuni:

 

Eliud Kipchoge – Ineos 1:59 Challenge

Mnamo Jumamosi asubuhi  Eliud Kipchoge alisababisha macho ya ulimwengu mzima kutua kwa siku nzima kushuhudia azimio la ufanisi wake.

Alionesha  ulimwengu mzima  kwamba binadamu hadhibitiki akiamua kutenda.

Ulimwengu ulishuhudia mkenya Eliud Kipchoge kuwa binadamu wa kwanza duniani kukimbia mbio za kilomita 42 chini ya masaa mawawili.

Kipchoge ambaye alikata utepe baada ya saa 1.59.40 aliweka historia katika ulingo wa riadha kuwa mwanariadha wa kwanza kumaliza riadha hiyo katika kuda huo.

 

Timu ya raga ya 7s kwa kina dada yafuzu kwenye Olimpiki 2020

Aidha, wachezaji wa raga 7s kina dada waliwapiga wenyeji Tunisia katika nusu fainali na kufuzu katika michuano ya Olimpiki ya Tokyo Japan manmo 2020.

Timu ya  raga ya 7s ya kina dada imejipatia tiketi ya kushiriki katika Olimpiki ya Tokyo Japan 2020, baada ya kufuzu katika  fainali ya mashindano hayo nchini  Tunisia Jumapili.

Kenya ambao  ni mabingwa watetezi waliwapiga  wenyeji Tunisia 19-0 kwenye  michuano ya nusu finali  na  kujikatia tikiti  ya moja kwa moja kwenda Japan

Timu hiyo ya Kenya, maarufu kama Lionesses   ilikuwa timu ya nane kufuzu kwenye michezo ya Olimpiki ya 2020.

 

Lawrence Cherono Ashinda Debele

Lawrence Cherono aliibuka mshindi katika mbio za marathon chicago kwa muda wa saa 2:05:45. Alikata utepe   kwa sekunde moja kutoka mbele ya  Debela amabye aliibuka wa pili.

Mengstu alikuwa wa tatu karibu kwa muda wa 2:05:48. Kinyume na ilivyokuwa na mbio za wanawake,  ushindano baina ya wanaume ilikuwa pambano la karibu zaidi.

Mo Farah na Karoki waliondoka nje ya mashindano  hayo kabla kabla ya raundi ya mwisho, wakiwaacha Cherono, Debela na Mengstu waking’ang’ania  ushindi wakiwa mstari wa kumalizia.

 

Rekodi ya 2003 yavunjwa na Brigid Kosgei

Brigid Kosgei  ndiye bingwa wa dunia katika marathon ya kina dada  baada ya kumaliza katika muda wa 2:14:04, zaidi ya dakika sita mbele ya Ababel Yeshaneh, ambaye alikimbia masaa mawili, dakika 20 na sekunde 51, na Gelete Burka ambaye alikimbia masaa mawili, dakika 20 na sekunde 55 wakati Ethiopia ilimaliza la pili na la tatu.

”Nitakusaidia kukula pesa”Huddah ataka kuwa mpango wa kando wa Kipchoge

Amini Usiamini, katika mtandao wa kijamii wa Instagram binti Monroe aliandika ujumbe wa kuwaomba mashabiki wake wamuunganishe na bingwa Eliud Kipchoge ili amsaidie kutumia pesa alizoshinda.

Uganda yapanga kunyonga wapenzi wa jinsia moja

Katika posta nyingine alisema kuwa anataka kuona kama Eliud ni bingwa wa mbio katika ‘sekta nyingine’ yaani sekta ya michezo ya chumbani.

Ghost Mulee aitetea Harambee Stars, ataja sababu za kupoteza

 Kidosho Monroe aliandika ujumbe huu siku moja tu baada ya kukamatwa kwa sababu ya kuendesha gari akiwa mlevi.
Monroe alilala kwenye kituo cha polisi usiku wote.

”Nitakusaidia kukula pesa”Huddah ataka kuwa mpango wa kando wa Kipchoge

Alichokisema Obama kuhusu Eliud Kipchoge, Eliud aomba wakutane

Rais mstaafu wa Marekani Barack Obama ametoa tamko la ushindi na kuunga mkono ushindi wa Eliud Kipchoge.

Kupitia mtandao wa Twitter, Obama amesifia ushindi wa wakenya hawa wawili.

“Hapo jana (Jumamosi), Mkiambiaji Eliud Kipchoge amekuwa wa kwanza kuvunja rekodi ya masaa mawili. Hii leo (Jumapili)  Chichago, Brigid Kosgei ameweka rekodi mpya ya kidunia ya wanawake….Wawili hawa ni mfano mzuri wa uwezo wa binadamu kufaulu…” Obama

Je, Mariam Kighenda alipanga kujitoa uhai? Mmewe John afunguka

Kama Eliud Kipchoge, Obama mwenyewe alitoa motisha kubwa zaidi kwa dunia baada ya kuchaguliwa kuiongoza Marekani.

 

Eliud ameingia katika historia ya binadamu wa kwanza kumaliza mbio za kilomita 42 kwa masaa mawili.

Kwa sasa Eliud anaomba kukutana na Obama baada ya pongezi hizo.

(+Video yavuja) Mariam Kighenda akicheza Kainama ya Harmonize kabla ajali Likoni Feri

“…Ahsante kwa maneno yako ya busara. Kwa haya maisha huwa tunaishi kuwapa moyo wengine. Ningefarijika zaidi iwapo tungekutana na tujadili jinsi tunavyoweza kufanya ulimwengu huu uwe wa kukimbia…” Eliud alimwandia Obama katika Twitter.

Haya yanajiri baada ya Eliud Kipchoge kutwaa ushindi mkubwa katika mbio za Marathon mjini Vienna, Austria.

Fahamu mbona rekodi ya Kipchoge haitambuliki kama rekodi ya dunia

Hapo jana, gwiji wa marathon Eliud Kipchoge aliiweka jina lake katika vitabu vya historia , akimaliza kilomita 42 za mbio za marathon kwa saa moja dakika 59 na sekunde 40 katika shindano la Ineos siku ya Jumamosi nchini Austria Vienna.

Hatahivyo muda huo bora uliowekwa na bingwa huyo hautatambulika kama rekodi ya dunia.

Man City, Rio Ferdinand na wanasiasa wampongeza Eliud KIpchoge

Kulingana Shirika la Riadha duniani IAAF , kwa mbio yoyote kufikia sheria zake na hivyobasi kutambulika kama rekodi ya dunia kuna masharti yanayopaswa kufuatwa kulingana na chombo cha habari cha AFP.

  • 1.Kwanza mbio hizo lazima ziwe zimeandaliwa na shirika la riadha duniani IAAF ama shirikisho la raidha la nchini ambapo riadha hizo zinaandaliwa.
  • 2.Wanariadha wanaodhibiti kasi hawawezi kuingia katika mbio hizo kwa zamu na kutoka.
  • 3.Lazima wanariadha wafanyiwe vipimo vya matumizi ya dawa za kusisimua mwili
  • 4. Vinywaji vinapaswa kutoka kwa vituo rasmi na sio kupewa mwanariadha na wasimamizi wake.
  • 5. Ni Sharti kuwepo zaidi ya washindani watatu katika mbio hizo.
  • 6. Mwanariadha hafai kudhibitiwa kasi na gari lililopo mbele yake.
  • 7. Njia itakayotumika ni sharti ifanyiwe ukaguzi na kupimwa na maafisa wa IAAF.

Wakati wa jaribio la kwanza la mbio hizo za marathoni huko Monza nchini Itali miaka miwili iliopita, Kipchoge alipatiwa vinywaji huku wadhibiti mbio hizo wakibadilishwa mara kwa mara, hatua iliokiuka masharti ya IAAF.

Siku ya Jumamosi , alipewa vinywaji kila baada ya kilomita 5 na hivyobasi kukiuka sheria hizo za shirikisho la riadha duniani.

Mkimbiaji huyo mwenye umri wa miaka 34 tayari anashikilia rekodi ya dunia miongoni mwa wanaume katika umbali huo akiwa na muda wa saa mbili dakika moja na sekunde 39, ambao aliweka katika mbio za Berlin tarehe 16 mwezi Septemba 2018.

AMEFAULU!! Eliud Kipchoge amaliza mbio chini ya masaa mawili

Kulingana na AFP , barabara hiyo ilikuwa imeandaliwa hali ya kwamba ingemchukua Kipchoge sekunde 4.5 zaidi kulingana na uchanganuzi wa wataalam wa michezo katika chuo kikuu cha Vienna.

Kwa jumla aliweza kushuka mita 26 na kupanda mita 12 , walisema wataalam hao.

Mbio hizo za marathon zimekuwa na ushindani mkali katika kipindi cha miaka 16 iliopita kati ya wanariadha wa Kenya na wenzao wa Ethiopia.

Mataifa hayo mawili ni washindani wakuu wa mbio ndefu uwanjani.

Rekodi ya Kipchoge ilikaribia kuvunjwa na raia Muethiopia Kenenisa Bekele ambaye alikimbia saa 2 dakika moja na sekunde 41 ikiwa ni sekunde mbili pekee kabla ya kuivunja rekodi hiyo.

Mbio hizo za Viena hazikuwa mashindano bali zililenga kuwapa motisha mamilioni ya watu duniani. Na Kipchoge amefanikiwa.

Katika mahojiano na vyombo vya habari , Kipchoge alisema kwamba mbio hizo za Vienna zililenga kuwapatia changamoto wanadamu katika maisha yao ya kila siku.

Pia aliwashutumu wakosoaji wake.

Ninakimbia kuweka historia , ili kuuza #NoHumanLimited na kuwapa motosha zaidi ya watu bilioni 3 . Sio swala la fedha bali kubadilisha maisha ya watu”, alinukuliwa akisema.

-BBC

Man City, Rio Ferdinand na wanasiasa wampongeza Eliud KIpchoge

Dunia nzima sasa inamzungumzia bingwa na mwanariadha hodari zaidi kuwahi shuhudiwa duniani, Eliud Kipchoge.

Hii ni baada ya mwanriadha huyo kuandikisha historia kama binadamu wa kwanza duniani kukimbia na kumaliza mbio za nyika chini ya masaa mawili.

Kipchoge alimaliza mbio hizo baada ya lisa moja, dakika 59 na sekunde 40 pekee. 1:59:40.

Mbio hizo maalum zijulikanazo kama Ineos1:59 challenge zilifanyika Vienna, Austria kuanzia mida ya 9:15  Jumamosi asubuhi na Kipchoge alisindikizwa na zaidi ya waweka kasi 20.

 Miongoni mwa waliompongeza kwa juhudi hizo za kufana ni wakenya kutoka tabaka mbali mbali, wanasiasa, timu za kadanda za uingereza zikiwemo, Tottenham Hotspurs na Man City na wanasoka wa zamani; Rio Ferdinand na Yaya Toure ambao wamewahi tembelea nchi ya Kenya.
Tumeorodhesha baadhi ya timu na watu mashuhuri ambao wamempongeza Kipchoge.

Boniface Mwangi alisema,

Issa a plan. We should line up the entire road from the airport to Nairobi CBD to welcome #eliudkipchoge. Receive him like the HERO he is.

AMEFAULU!! Eliud Kipchoge amaliza mbio chini ya masaa mawili

Amini usimamini! Mkenya na bingwa wa mbio za nyika kote duniani, Eliud Kipchoge amefaulu katika juhudi zake za kukamilisha mbio za Ineos1:59 challenge chini ya masaa mawili.

Kipchoge amemaliza mbio hizo baada ya lisa moja, dakika 59 na sekunde 40 pekee. 1:59:40.

Pombe yauzwa sh159 pekee ili kumshabikia Eliud Kipchoge

Siku hii ndiyo iliyokuwa imengojewa dunia nzima huku kila mmoja akitazamia Eliud Kipchoge kuivunja rekodi yake na kumaliza mbio za kilomita 42, chini ya masaa mawili.

Mbio hizo maalum zijulikanazo kama Ineos1:59 challenge zilifanyika Vienna, Austria kuanzia mida ya 9:15  Jumamosi asubuhi na Kipchoge alisindikizwa na zaidi ya waweka kasi 20.

Kipchoge akiri kuwa mtulivu kabla ya jaribio lake la Ineos1:59 challenge

Hongera Kipchoge!!!