PATANISHO: Bibi yangu anatetea mpango wake wa kando

Paul aliomba apatanishwe na mkewe bi Elizabeth akidai kuwa wawili hao walikosana baada yake kumpiga mpango wa kando.

PATANISHO: Bwanangu alikatwa kichwa na mpango wa kando na bado akamrudia

Akieleza kisa hicho, bwana Paul alidai kuwa wawili hao walikuwa wametengana kwa mda na kila mmoja akaanza uhusiano wa kando na baada yao kurudiana, aliyekuwa mpango wa kando wa mkewe hakusita kumfuata.

Jambo hilo lilimkera haswa baada yake kumtumia picha za mkewe kwa mtandao wa Whatsapp na alipopatana naye alimpa kichapo cha mbwa, jambo ambalo halikumfurahisha mkewe.

Kwa hasira na kero kuu, Paul alimfukuza Elizabeth.

Soma usimulizi wake.

PATANISHO: Nilienda Kuwatch mpira kurudi nyumbani bibi amenuna hadi leo haongei

 

Tulikuwa tumekosana hapo mbeleni na tuka separate kidogo. Katika hali ya ku separate akapatana na mtu mwingine halafu tukaja tukarudiana. Baada ya kuishi naye yule jamaa bado alimfuata na baada ya kuzungumza na mke wangu tukamaliza hayo maneno, na nikampigia yule jamaa na nikamkanya.

Sasa hakuacha na akaendelea kumfuata na ikafika mahali akaanza kutuma picha za bibi yangu kwa Whatsapp na hiyo kitu iliniuma sana.

Nikamwambia bibi yangu anipatanishe na yule jamaa, tukazungumza na nikakasirika zaidi nikampiga yule mwanaume na bibi yangu nikama lile jambo halikumfurahisha na akaanza kumteta yule mwanaume na kwa machungu ikabidi nimfukuze mke wangu. Aliondoka na kwenda kwao nyumbani na hawazungumzi na yule jamaa.

Wawili hao wana watoto wawili mmoja alimuoa naye na wamekuwa kwa uhusiano wa miaka minane.

Bi Elizabeth naye alidai kuwa Paul alimtumia fedha za kununua sare za shule lakini pindi tu zilipofika akazirudisha. Alisisitiza mumewe ana madharau sana na hadai kurudiana naye.

Hata hivyo alimuomba ashughulikie watoto huku akimpa mda.

Patanisho: Nililala kwa sitting room baada ya mke wangu kugeuka kwa kitanda akaface upside down

Pata uhondo wote.

PATANISHO: James Alalamikia Kunyang’anywa Mke Na “Jamaa Wa Maziwa”

 

Siku ya Jumatano tarehe 7/12/2016 bwana James mwenye umri wa miaka 26, kutoka maeneo ya Thome aliomba apatanishwe na mkewe Elizabeth 24, ambao walikosana majuma mawili yaliyopita.

Wapendwa hao wawili wana mtoto mmoja ambaye James alimuoa mkewe naye na wawili hao wamekuwa pamoja tangia mwaka wa 2013.

Kulingana na bwana James, siku moja mkewe alielekea kazini lakini hakurudi. Alipompigia simu mkewe alimwambia kuwa  asisumbuliwe na kukata mawasiliano kati ya wawili hao.

Baada ya hayo, James alihamia chumba kingine katika ploti hiyo hiyo kwa uchungu mwingi na wakti mkewe aliporejea nyumbani, wawili hao waligawana mali na la kuchesha zaidi ni kuwa wawili hao walipatana asubuhi ya leo huku James alipokuwa akielekea msalani naye Elizabeth akielekea bafuni.

Isitoshe James alisema kuwa chanzo kuu cha wawili hao kutengana na kuzua shida chungu nzima, ni mwanaume mmoja aliyekuwa akimletea mkewe maziwa. Hapo alishuku huenda jamaa huyo na Elizabeth wana uhusiano kwani walipotengana, jamaa huyo alianza kumletea mkewe maziwa hadi kwake nyumbani.

Alipopigiwa simu Elizabeth ambaye ni shabiki wa Patanisho alikiri kuwa tabia za bwanake kama kutokuwa mkamilifu na kuwa mwizi ndizo chanzo cha wawili hao kukosana.

“Ana tabia za wizi kwa ploti ananiletea aibu kwa nyumba. Hanunui chochote hata chakula, patipati hamna chochote anafanya ispokuwa kulipa kodi. Niliporudi nyumbani kutoka matembezi nilipata James amehama na singemlazimisha.” Alieleza Elizabeth.

“Jamaa wa kuuza maziwa ni rafiki yangu na ndiye natarajia anioe. Nilianza uhusiano naye kwa sababu yeye alikuwa ananitunza, asiponisaidia mimi na mtoto wangu tunalala njaa. Bwanangu alikuwa anamtuma mtoto wetu chapati ala huku mtoto akimtizama.” Alieleza zaidi bi Elizabeth huku akisema kuwa hataki maneno yake hata kidogo.

Bwana James aliposkia hayo yote alitoweka na kukata mawasiliano. Do!

Skiza uhondo kamili.