Ilikuaje: Sijawahi sikia pengo ya kutokuwa na baba mzazi – Mammito

Eunice Wanjiku Njoki almaarufu Mammito ni mjeshi wa kipindi cha Churchchill, na ambaye amelelewa na mama pekee katika maisha yake.

Mammito akiwa katika mahojiano na mtangazaji Massawe Japanni alisema kuwa mama yake alikuwa anatia bidii kuhakikisha ameenda shule na pia kumlea ipasavyo.

“Nimelelewa Kibra na mama pekee, mama yangu aliweza kuhakikisha amenilea mzuri nimeenda shule,

“Nakumbuka siku moja mama yangu aliweza kulia mbele yangu kwa sababu hakuwa na pesa ya kulipa karo yangu ya shule nikiwa shule ya upili,

“Ilinibidi nitoke shule ya kulala na nirudi katika shule ya kurudi nyumbani kila siku, sijawahi sikia pengo ya kuwa sina baba,

“kwa sababu mama hajawahi nieka katika hali ile ya kujiuliza kwanini baba yangu hayuko karibu.” Akieleza Mammito.

mammito
comedian Mammito Euniece

Mcheshi huyo ni kifungua mimba wa familia ya watoto watatu, huku akisema kuwa maisha ya ‘ghetto’ si rahisi na aliweza kulelewa na shida nyingi sana.

Akiongeza mcheshi Mammito alisema kuwa hajui baba yake na wala hajawahi sikia pengo kuwa hana baba kwa maana mama yake amekuwa naye kwa kila jambo.

“Mimi sijawahi jua baba yangu wala sijawahi sikia ile pengo ya kuwa sina baba mzazi, sijawahi uliza mama yangu sababu ya kuachana na baba yangu,

“Najua alikuwa na sababu kubwa ya kuachana na baba yangu, huwa tu namuuliza na mzaa baba yangu ni nani, na pia sijawahi jua sababu kuu ya wao kuachana,

“Sipendi kurudisha mama yangu nyuma kwa kumuuliza maswali hayo inaweza kuwa alipitia changamoto nyingi ndio maana waliachana.” Mammito alisema.

Mammito alisema kuwa alianza kazi ya ucheshi akiwa na miaka 22, na alijua kuwa ana talanta ya ucheshi tangu utotoni kwa maana aliweza kumsumbua mama yake sana.

Pia alisema kuwa alikuwa na matumaini kuwa ataweza kutoka katika maisha duni na kuwa mtu wa maana.

“Nilianza kazi ya ucheshi nikiwa na miaka 22, na pia nilianza uhusiano wa kimapenzi nikiwa nimemaliza shule ya upili, kisha baadaye nikaweza kuumizwa roho.” Aliongea Mammito.