‘Nimeishiwa nguvu kwa kupoteza chanzo cha kipekee cha kunitia nguvu.’- Mamake Walibora azungumza

Mnamo tarehe, 15/04 mwaka huu wananchi, viongozi jamaa na hata marafiki  walikumbana na habari za kuhuzunisha baada ya kutangaziwa kifo cha mwanahabari ken Walibora.

Mwili wake ulipatikana katika chumba cha kuhifadhi maiti cha Kenyatta huku jamaa wakipigiwa simu ili waje watambue mwili huo.

Kunani? Ken Walibora ndiye mwanahabari wa tatu kupoteza maisha yake kwa kugongwa na matatu

Walibora 1

Ken Walibora alitokewa Ijumaa ya pasaka huku nguvu za kumtafuta na kumpigia simu zikiambulia patupu, kulingana na ripoti Walibora aligongwa na matatu kisha kuaga dunia.

Eunice ambaye ni mama wa mwendazake akizungumza alisema kuwa familia na jamaa wamempoteza mtu na mwana wa maana katika maisha yao.

Gwiji ambaye kazi yake haitasahaulika kamwe! Rais Kenyatta amwomboleza Walibora

Mama huyo aliyekuwa amejawa na majonzi alisema kuwa Walibora amekuwa wa msaada kwa familia hasa kwa wadogo wake baada y kifo cha baba yake.

“Nimeishiwa nguvu baada ya kupoteza chanzo changu pekee cha kunitia moyo na mtu wa kutegemewa baada ya kifo cha marehemu mume wangu.” Eunice Alisema.

Rais Uhuru Kenyatta aliwaongoza marafiki, viongozi na hata jamaa kwa kumuomboleza Gwiji Walibora huku wengi wakimsifia mwenye kupenda elimu na sifa njema.

Kulingana na mmoja wa binamu wa Ken alisema kuwa alikuwa mtu mpole na mwenye kupenda elimu na mengi zaidi.

“Ken alikuwa mtu mpole, angesafiri hadi nyumbani ambapo alijiunga na wazazi wangu siku kadhaa. Alipenda sana mboga za kienyeji, alikuwa akimuomba mama amuandalie akiwa kijijini. Ni jambo ambalo limewaacha wengi na sintofahamu kuhusu mwanamume aliyeishi maisha ya faragha.” Alisema.

Ken walibora alikuwa mfano mwema kwa wengi na wengi walipenda kumuiga kwa matendo yake.

Kutoka kwetu wanajambo Mola ailaze roho yake mahali pema peponi.

PATANISHO: Hata akini block sitamsahau kwani nampenda – Saphan

Saphan, 31, kutoka Utawala alituma ujumbe akidai kuwa angependa kupatanishwa na mkewe bi Eunice, 24,  na kusema kuwa shida ni kuwa siku moja alimuachilia akatembee na kurudi nyumbani akiwa amechelewa, ambalo halikufurahisha wazazi wake.

Anasema mkewe aliondoka na kwenda Kisumu ambapo sasa anaishi na dadake.

Ataponea? Mo Farah atuhumiwa upya na swala la madawa ya kusisimua misuli

“Nampenda sana na sitaki kumuachilia hivyo. Wakati wa holiday alisema anataka kwenda kumuona dadake na badala ya kurudi siku hiyo akarudi siku iliyofuata jioni jambo ambalo halikumfurahisha babangu.” Alisimulia Saphan.

Alikasirika na kuondoka na kwenda kwa dadake, sasa hivi najaribu kumpigia lakini ameni block pia kwa Whatsapp. Niko tayari kumpokea na tuishi kwa maisha yetu mazuri.” Aliongeza.

Wawili hao wamekuwa kwa ndoa ya miaka miwili na bado hawajajaliwa na watoto.

“Mwambie awe mwanaume awache mambo ya kuskiza wazazi wake, wakati nilikuwa nafukuzwa alikuwa hapo mbona alikuwa amesimama tu hapo?.” Aliuliza Eunice.

‘Niliacha ukahaba baada ya babangu kuja lodging’

Eunice aliongeza,

Mume wangu nilimwambia naondoka na nitalala kwa dadangu na babake ndiye aliniuliza kwenye niliko na kuuliza mbona nimelala nje. Isitoshe aliniambia narandaranda nje na niliporudi akaniamrisha nifunge virago niondoke.”

Kwa upande wake, Saphan anasema kuwa mkewe alimrushia maneno kwa gate na kumuamrisha asimtete mbele ya wazazi wake.

“Sirudi! Nishaamua, yeye aishi maisha yake na wazazi wake!”

PATANISHO: niliangukia mume ambaye hakuwa anasoma katiba

Eunice,25, kutoka Teso alituma ujumbe akiomba apatanishwe na mumewe bwana Ronald.

“Yeye alikuwa anataka niishi nyumbani naye mjini ila hataki niende mjini. Kisha nikaskia fununu kuwa analeta wanawake kwa nyumba ila mimi naishi nyumbani na wazazi wake.” Alisema Eunice.

PATANISHO: Nilimvulia mume wangu nguo baada ya kumtusi mama

Eunice anasema baada ya kutoka kwake, alipendana na mwanaume mwingine na kwa bahati mbaya alipata mwanaume ambaye wanalala kitandani pamoja kama wanawake wawili kwani hawasomi katiba.

Alisema wazi kuwa ana miss katiba ya bwanake na anampenda sana.

Kabla ya kutengana kwao wawili hao walikuwa kwa ndoa ya miaka miwili unusu na walijaliwa mtoto mmoja na alipopigiwa simu bwana Ronald alisema kuwa atafanya maamuzi kivyake kisha atamjulisha mkewe.

PATANISHO: Kondoo ndio ilitutenganisha na mke wangu

“Kurudi sio tatizo lakini tatizo ni kuwa alishaolewa yeye kwani mke wa mtu akikurejelea sio jambo nzuri. Ninacho kifahamu ni kuwa bado yuko kwa bwanake.” Alisema Ronald.

Bwana Ronald naye alisema kuwa tayari ana mke na amejaliwa na mtoto na hangependa Eunice aondoke kwa ndoa yake ili amrudie na pia hangependa kuwa na wake wawili.

Upande wake Eunice, alikubali uamuzi wa Ronald na ameamua kuendelea na maisha yake na kutafuta mpenzi mwingine.

Patanisho: Amekuwa mkali kama simba ninapoitisha tendo la ndoa

PATANISHO: Nili promote mpango wa kando kuwa mke

Kelvin alituma ujumbe akiomba apatanishwe na mkwewe bi Eunice, ambaye walikosana na kutengana mwaka mmoja uliopita.

“Nilikuwa na mpango wa kando ambaye nilimuoa kama mke wa pili na hapo ikaleta shida kwa ndoa. Mke wangu akakasirika na hapo nikawachana na mke wa pili lakini tukakosa maisha ya kuaminiana.

Yeye akitoka haniamini nami akitoka simuamini na ilipofikia mwezi wa tano akaondoka na kuniachia watoto.” Alisimulia Kelvin.

Mama mkwe alinishauri nimtafute mke wangu kupitia patanisho – Kiragu

Anadai wawili hao hulea watoto pamoja lakini hapendelei watoto kuishi mahala kwingine lakini kila anapompigia mkewe bado ana ugumu wa kurudi.

Wawili hao wamekuwa kwa ndoa ya miaka kumi na wawili hao walioana wakiwa na umri mchanga sana.

Alipopigiwa simu bi Eunice alidai kuwa mumewe amechelewa kwani walikuwa wamemaliza kutatua maneno yao.

“Kwa uamuzi wangu ni eti tulikuwa tumezungumza, kwanza mahala amekosea ni kuwa ameenda kunianika Radio Jambo.” Alisema Eunice akisisitiza kuwa watoto watalea pamoja lakini hatorudiana naye.

PATANISHO: Nimepoteza watoto wanne kwa sababu ya mama mkwe