Ghost na Arocho wapanga kukuza vijana kupitia kadanda

Watangazaji wa Radio Jambo, Fred Arocho na Jacob ‘Ghost’ Mulee ni miongoni mwa watangazaji ambao taaluma zao za uanahabari zimejengwa kwa msingi wa kadanda.

Kwa mfano, Afrika mzima, yajua kuwa Ghost Mulee ni mmoja wa makocha maahiri na humu nchini anatambulika kama gwiji kwa ujuzi na mafanikio aliyoletea nchi hii.

PICHA: Mwanawe Arocho asafiri hadi China kwa mafunzo ya soka

Arocho ama ukipenda ‘Twiga’ pia anaheshimika nchini kwa mchango wake kama mchezaji, enzi zile na hata pia ndani na nje ya uwanja na studioni, ambapo anatetea maswala ya wachezaji.

Pamoja, wawili hao wameshirikiana ili kukuza talanta na isitoshe, ni mpango wao kuonesha fahari yao kwa Nairobi na haswa Eastlands, mtaa ambao walilelewa.

Moja wapo ya mipango wao ni kuandaa shindano la kadanda la wachezaji 11 kila upande, shindano ambalo litaleta pamoja timu nane kutoka mitaa tofauti ya Nairobi.

Shindano hili ambalo limedhaminiwa na OdiBets, ni la siku moja, linafanyika hii leo katika uga wa Camp Toyoyo, Jericho.

Isitoshe, wawili hao wameshirikiana na ajenti kadhaa kutoka Sweden wakiwemo; Patrick Murk na Johan Sandohl na pia Jamal Ibrahim, ambao watakuwa wakitafuta talanta ambazo watakuza.

Story za Ghost: Jamaa atoroka hotelini alipomuona DCI Kinoti

“Ghost Mulee nami tulileta vichwa vyetu pamoja kama watu walioanzia Eastlands, watu ambao walipata fursa ya kucheza kadanda na kufika tulipo. Sasa tunataka kupatia wengine fursa kama ile ili wajikuze.” Alisema Arocho.

Aliongeza,

Tumechukua timu nane kutoka Nairobi kote ambazo ndio timu bora kabisa Nairobi ili waoneshe talanta zao. Na wakibahatika watajipata bara Uropa. Shindano lile litaanzia robo fainali, kisha nusu fainali hadi fainali.”

Shindano hilo liitwalo ‘Champions of champions’ tayari limeanza na litakamilika saa kumi na moja jioni.

Washindi watazawadiwa kitita cha elfu 50,000 huku watakaopoteza katika fainali watapokea elfu 20,000.

 

Ghost Mulee, Raila wahudhuria mazishi ya Joe Kadenge

Mtangazaji Jacob ‘Ghost’ Mulee ambaye ni alikuwa rafiki wa karibu wa Joe Kadenge ni miongoni mwa wageni mashuhuri waliohudhuria mazishi ya mwenda zake.

Mazishi ya Kadenge yanafanyika nyumbani kwake katika kaunti ya Vihiga.

abbas.kadenge

 

Joe Kadenge alipenda nambari saba na alifariki Julai 7 – Mwanawe

Mwenda zake Kadenge ni gwiji wa kadanda nchini, na aliaga dunia yapata wiki mbili zilizopita akiwa na umri wa miaka 84, na alisifiwa na wengi kama mwanasoka ambaye aliiletea Kenya hadhi kuu katika nyanja ya soka.

Mulee aliandamana na rafiki zake wa karibu akiwemo, Mahmoud Abbas ambaye alikuwa kipa maridadi wa timu ya Harambee Stars, na wengineo.

Aliyekuwa waziri mkuu Raila Odinga pia ni miongoni mwa wageni na inatarajiwa wachezaji wa soka wa zamani na wa sasa pia watahudhuria mazishi hayo.

ghost mulee joe kadenge

Siku ya Junatano, wanasiasa, marafiki wa karibu na familia yake Joe Kadenge, walikusanyika kwenye Kanisa la Friends International kumpa heshima zake za mwisho shujaa huyo.

Wageni waheshimiwa wahudhuria misa ya wafu ya Joe Kadenge

Binti yake Esther alisema,

Joe alipenda nambari saba, jeresi yake ilikuwa namba saba, gari yake ilikuwa na nambari saba, namba yake ya nyumba pia ilikuwa ni saba na alifariki tarehe saba ya Julai.

raila.kadenge (1)

Joe Kadenge alikuwa mwanasoka mahiri sana siku zake na aliichezea timu ya taifa Harambee stars kwa miaka 14 baada ya kuanza kusakata boli  miaka ya sitini.

Baada ya kustaafu kutoka soka, Joe alijitosa katika usimamizi wa kandanda ambapo pia alipaa na kuwa kocha wa timu ya Harambee Stars mwaka wa 2002.

Mwenyezi mungu na aijalie nafsi yake na kuipa ujasiri familia na rafiki zake.

Happy birthday! Ghost Mulee asherehekea kuhitimu miaka 54

Kila mwaka siku ya kumi na saba, mwezi Julai, huwa siku ya kufana sana kwa mtangazaji Jacob ‘Ghost’ Mulee kwani ndio siku huadhimisha kuzaliwa kwake.

ghost birthday

Families With The Most Unique Birthday Dates Featuring Ghost Mulee!

Kama ilivyo desturi, Mulee hupata fursa ya kukata keki pamoja na wafanyi kazi wenza na kusherehekea mwaka mwingine chini ya makali ya jua.

Mwaka huu, Ghost alipata zawadi kemkem na keki zimemngoja alipomaliza show yake ya Gidi na Ghost Asubuhi. Alizingirwa na marafiki na wafanyi kazi wenza akiwemo, Gidi Gidi.

gidi and ghost cake

Kwa furaha na vicheko vyake vya kuumiza mbavu, Mulee alikata keki akiadhimisha miaka 54 tangu azaliwe na kula na kila mmoja.

Kabla ya hafla hiyo fupi, mwenzake na boss wake, Gidi alimtumia ujumbe wa kusherehekea mafanikio yake huku akimtaja kama mwanaume kamili.

Gidi Reduces Birthday Boy Ghost Mulee To ‘Tears’ After Surprising Him On Air

Gidi alimuombea mwenzake miaka nyingi na uzee ambao utamuacha kocha huyo wa zamani wa Harambee Stars, bila meno.

ghost birthday

Gidi alichapisha kwa mtandao wake wa Instagram akisema,

Let me take this earliest opportunity to wish this gentleman and colleague @ghost_mulee a Happy birthday. May you grow to be toothless 😂😂😊

 

Mashabiki wa Mulee nao hawakusita ila kumuminia ujumbe wa heri njema.

PHOTOS: Ghost Mulee’s Wife Treats Him To A Romantic Red-themed Birthday Dinner

paul.koskei: Happy Birthday Ghost. You guys promote a very natural platform on Radio for common Mwanainchi to air their views.

denniskayaviri: Happy born day coaches….may u leave to blow 100001 candles

njue_kami: Happy birthday day kicheko.. May u leave to blow 100001 candles..

ak1jcc1: Happy birthday to you, Ghost mzee wa kicheko

 

Sherehe hii yaja siku moja tu baada ya mtangazaji wa Mazungumzo waziwazi, Bramwell Mwololo pia kusherehekea siku ya kuzaliwa. Bramwell pia alipata fursa ya kukata keki pamoja na wafanyi kazi wenzake na marafiki kwa jumla.

Wamlambez! Tazama ujumbe wake Ghost Mulee kwa wanajambo

Leo ni Friday ama ukipenda, furahi day na mtangazaji Ghost yuko kwenye mood ya sherehe huku wikendi iking’oa nanga rasmi.

Katika kanda aliyochapisha katika mtandao wake wa Instagram, Mulee anaonekana akijiburudisha na kinywaji cha juisi ya miwa baada ya kutoka kazini.

Wakenya hawapaswi kufikiria Tanzania ni timu ovyo – Ghost Mulee

Kwenye kanda hiyo, mtangazaji huyo wa Gidi na Ghost asubuhi, anawashauri mashabiki wake kutobugia pombe na kisha kuendesha magari.

Hata hivyo aliwakumbusha kuwa kama ni lazima wanywe na waendeshe magari basi wajaribu kunywa juisi ya miwa.

“Usione wivu ni ile tu nakunywa sugarcane juice ni Friday, na ndio mimi huwaambia kama unataka kunywa usinywe na uendeshe magari na kama unakunywa juisi ya miwa basi waweza endesha magari wakati wowote.” Alisema Mulee kabla ya kuangua kicheko anachotambulika nacho.

Baadaye, Mulee alimalizia ujumbe wake kwa kuwatakia mashabiki wake wikendi njema akisema ‘Wamlambez’.

Ghost Mulee amshauri Victor Wanyama kabla ya kipute cha AFCON

Tazama kanda hiyo hapa.

View this post on Instagram

Enjoy your Friday

A post shared by Jacob "Ghost" Mulee (@ghost_mulee) on

 

Wakenya hawapaswi kufikiria Tanzania ni timu ovyo – Ghost Mulee

Kocha wa zamani wa Harambee stars Ghost Mulee anadai vijana wa Kenya walikua na uwoga kidogo katika mechi yao ya kwanza dhidi ya Algeria katika kipute cha AFCON nchini Misri lakini wana uwezo wa kufanya vyema katika mechi ya pili dhidi ya Tanzania kesho na pia dhidi ya Senagal Jumatatu.

Ghost Mulee amshauri Victor Wanyama kabla ya kipute cha AFCON

Stars walipoteza 2-0 katika mechi ya ufunguzi lakini bado wa uwezo wa kufuzu kwa awamu ya pili kwa mara ya kwanza katika historia ya Kenya.

Kulingana na mkufunzi huyo wa zamani wa timu ya taifa, alisema kuwa mechi hiyo ilikuwa na vipindi viwili tofauti kwani hakupendezwa na jinsi Harambee Stars walikuwa wanapoteza mipira mingi na pia mikakati yao ya kuzuia mpira sana.

Hata hivyo, Mulee bado anashikilia kuwa bao la kwanza lililofungwa kupitia mkwaju wa penati halikuwa halali kwani mlinzi Dennis Odhiambo hakumguza Youcef Atal.

Gidi left elated after Ghost Mulee did this for Marie-Rose

Sikupendezwa sana na jinsi tulivyoshindwa kupeana pasi kila tulipopata mipira. Tulicheza mchezo wa kuzuia sana katika kipindi cha kwanza na pia hatukuwa tunajiamini kila tulipo pata mpira. Alisema Ghost Mulee.

Aliongeza,

Pia sina furaha kwani CAF wameamua kutumia teknolojia ya VAR kuanzia robo fainali kwani ukiangalia bao la kwanza, Dennis hakumguza mchezaji wa Algeria lakini sasa Kenya hawawezi lalamika.

Kenya sasa ina kibarua kigumu kwani itabidi wameshinda mechi yao dhidi ya Tanzania hapo kesho na kuomba kuwe na matokea mema katika mechi dhidi ya Senegal na Algeria.

Ingawa Mulee ana imani kuwa Kenya itawabwaga Tanzania, hata hivyo mtangazaji huyo aliwaonya wakenya ambao wanadhani kuwa Tanzania ni timu rahisi.

Mtindo mpya wa mlinzi wa Harambee Stars Joash Onyango wasisimua wakenya

Wakenya wanadhani Tanzania ni timu tu nyingine, hapana. Nafikiria kuwa twafaa kuwa makini sana na pia hatujatemwa nje ya mashindano bado.

Kuna uwezekano kuwa Kenya itawabwaga Tanzania halafu mechi ya mwisho dhidi ya Senegal huku tukitarajia kuwa mechi yao na Algeria itazaa matokeo mema.

Naamini tukichapa Tanzania, wachezaji wetu watajikakamua dhidi ya Senegal kwani watajua kuwa watahitaji pointi moja ili wafuzu. 

Michuano hiyo ya Ubingwa bara Africa itaingia siku ya sita leo huku mechi tatu zikichezwa nchini Misri.

Viongozi wa kundi B Nigeria watacheza dhidi ya Guinea saa 5.30pm huku wakitafuta ushindi ili kufuzu kwa awamu ya pili. Mechi hio itafuatwa na mechi ya kundi A kati ya Uganda na Zimbabwe saa 8pm.

Waganda wanahitaji angalau sare ili kuwa na matumaini ya kufuzu huku Zimbabwe wakitafuta ushindi baada ya kupoteza dhidi ya Misri katika mechi ya ufunguzi.

 

Ghost Mulee amshauri Victor Wanyama kabla ya kipute cha AFCON

Kipute cha ubingwa bara Afrika, AFCON kinang’oa nanga hii leo huku wenyeji misri wakikabana koo na Zimbabwe.

Misri al maarufu the pharaohs, wakiongozwa na mshambulizi matata wa Liverpoool, Mo Salah wana rekodi ya mataji saba na watakuwa wananuia kuongeza la nane baada ya kunyukwa katika fainali ya mwaka 2017 na Cameroon.

Kila la heri! Raila Odinga atembelea Harambee Stars kabla ya AFCON

Mara ya mwisho Kenya ilishiriki katika michuano ya AFCON ilikuwa miaka kumi na mitano iliyopita, chini ya uongozi wake kocha Jacob ‘Ghost’ Mulee.

Kocha huyo ambaye sasa ni mtangazaji wetu, ana imani kuwa vijana wa Harambee Stars wataleta hadhi kuu nchini na kuwa watafuzu hadi raundi ya mchujo.

Kenya iko katika kundi ‘C’ na Algeria, Tanzania na pia Senegal.

Baada ya Wanyama kufuzu kwa fainali za kombe la mabingwa bara uropa dhidi ya Liverpool, Mulee alimshauri nahodha huyo kuwa anapaswa kuuleta msukumu huo huo kwa timu ya taifa.

Mtindo mpya wa mlinzi wa Harambee Stars Joash Onyango wasisimua wakenya

Soma ushauri wake,

Kwanza nampongeza Victor Wanyama kwa kusaidia Tottenham kufuzu hadi fainali za kombe la mabingwa bara uropa. Kama nahodha ameongoza kwa mfano na hakuna tuzo kuu kwa mchezaji kama kucheza katika kombe la dunia na pia katika fainali za kombe la mabingwa bara uropa.

Huo ushawishi, huo msukumo na maadili mema twaomba ulete katika timu ya taifa katika kombe la ubingwa bara Afrika.

Watu wengi wasema kuwa ndoto ya Kenya tayari imedidimia lakini mimi naamini kuwa tutaizaba Algeria kisha tutoke sare na Tanzania katika mechi ngumu, na pointi nne zitakuwa tosha kutupeleka katika raundi ya mchujo.

 

My wife is a nice banker and a good chef! – Ghost Mulee

Mother’s Day is just around the corner, and we sat down with our very own Ghost Mulee who has fond memories of his late mom as well as a special respect for the mother of his kids.

Mulee says Mother’s Day is very special to him because every human being comes from a mother.

TBT : Pata kumjua mtangazaji Jacob ‘Ghost’ Mulee Zaidi

“Mothers are patient. They carried us in their wombs, although they had an option of not giving birth, and even after they gave birth to you, they still had an option of deciding on whether you should stay with them or not,” Mulee told Word Is yesterday.

The vocal radio king celebrates his late mum for raising him. “I have a special place in my heart for my dear mama for raising me single-handedly and teaching me a lot of values, which includes reading the word of God,” he said.

Mulee remembers how his mother would read the Bible every day, saying she loved the book of Proverbs.

The breakfast presenter also paid tribute to his gorgeous wife Carol, whom he met over 26 years ago.

Photo Of The Day: Ghost Mulee meets Brazilian legend, Ronaldinho

He said he they met in a matatu, and he stole her heart with his contagious laughter. And, like they say, the rest is history.

“My wife is also a special person in my life, and for the last 26 years we have been together, we have done so many things together. She is a nice banker and a good chef,” Mulee said.

Every time he eats out, he reminds her how good she cooks and makes sure he eats home as well.

“She is very hardworking. Every day she wakes up very early and packs my breakfast, and for all the love she has for me, I appreciate,” he said, adding that he is planning to surprise her differently from what he did last year.

“Vioja Mahakamani actors are my favourite comedians,” says Ghost Mulee

We all grew up watching our favorite actors Olexander Josphat, Ondiek Nyuka Quarter among others on KBC.

They filled our homes with laughter, and this is what warms the heart of Radio Jambo’s Ghost Mulee.

The Gidi na Ghost Asubuhi co-host took to Instagram to show some love for his favourite comedians who have acted in KBC popular tv series Vioja Mahakamani and Daktari.

View this post on Instagram

My best comedians

A post shared by Jacob Ghost Mulee (@ghost_mulee) on

Here are some of the pictures for these comedians.

1606433

kw

mama-kayai

4675d3871cf111a671cabb268e432015_L

 

STORY ZA GHOST: Sponsor Alia Kwikwi Baada Ya Kunyang’anywa Kipusa

Ni katika kipindi tu cha Gidi na Ghost Asubuhi ambapo vioja na vituko vya kila aina hushuhudiwa. Kuanzia kauli ya waskilizaji kutoka pembe zote za Kenya, wageni na hata pia watangazaji ambao wamebarikiwa na ucheshi si haba.

Sio kila mara tunaskia kuhusu wanaume wazee almaarufu ‘sponsor’ ambao wana tabia za kutembea au kuchumbiana na wanadada wadogo ki umri haswa wa chuo kikuu, lakini yote unayapata katika mchuzi mtamu wa redio Jambo huku ukichanganya na kachumbari iitwayo, Patanisho.

Basi katika stori za bwana Ghost Mulee, tukio moja lililomhusisha sponsor na mpenziwe lilitokea mjini na kuwaacha wengi vinywa wazi.

Akielezea tukio hilo, Ghost alisema kuwa mwanaume mmoja alikuwa na mpenzi mmoja jijini Umoji ambaye alimfanyia kila kitu ikiwemo kumkodishia nyumba.

Huku akidhani yeye ndiye mpenzi tu wa yule kipusa, alimtembelea siku mmoja bila kumuarifu na alichokutana nacho kilimwacha akibubujikwa na machozi.

“Sasa si jamaa anajua kule ni kwake akaenda siku mmoja akipiga mbinja akija anabisha nyumba kuingia akampata mwanadada yule ametulia na jamaa mwingine kitandani akivuta sigara… hakuamini macho yake na hakuwa na la ziada ila kulia.” Alisimulia bwana Ghost.

Pata uhondo kamili na tuwache tabia za sponsor jameni.

Patanisho: Tulipeleka mtoto kwa mganga akamnyonya damu, nikatoroka nyumbani

Je ikiwa mme wako anaamini mambo ya mganga baadala ya hospitali una weza mshauri vipi?

Jackie na bwanake walikosana akamwachia mtoto, baada ya kisa cha kuhuzunisha.

Anatuelezea kilichotokea:

‘ilikuwa tuu kwa hasira nikawacha mtoto lakini sasa ilifanyika mwezi wa nne. Tulikusana na yeye Januari nikaenda kwetu then nikarudi mwezi wa tatu ikienda kuisha hapo. so huyu mtoto alikuwa mgonjwa wakati tulikuwa pamoja na yeye, wakati tulirudi huyu sasa bwanangu akaniambia kuwa kuna mtu mwenye anaomba na anaweza ombea huyo mtoto apone, so tuka enda na yeye so tulipo fika hapo tukaingia kwa huyo mtu huyo mtu hakukuwa tukaka kakaa then akaniita mimi na mtoto kwa room ingine hivi aka tusurround akachukuwa kitambaa ya red kufunika mimi na mtoto so huyo mwanume akaanza kuomba ameakisha candles kila aina akachukuwa ringi yenye amevaa ya red akaniambia nitoe mtoto tshirt yenye amevaa na akamwekea kwa tumbo akaanza kufinya akatuma baba ya huyu mtoto aende kwa duka anunue wembe akaleta akampea. so mimi nikaanza kutetemeka akaniuliza mbona natetemeka nikamwambia sijawahi amini maombi kama haya na chenye kiko ndani ya roho yangu hakijawahi niruhusu niamini.

so akachukuwa wembe akakata mtoto kidogo then akwa anafinya hiyo ring kwa tumbo akaweka mdomo wake penye amekata na damu. katema damu na hiyo damu ilikuwa na kitu kama glass akaniambia eti hizi vitu ndizo mtoto wako alikuwa ametumiwa. so bwanangu akachukuwa shillingi mia saba akampea, na tukaambiwa kesho yake turudie dawa.

Vile tulienda kwa nyumba tukaanza kubishana akanichapa mbaya sana juu nilimwanbia huyo si mtu wa mungu ni mtu anaabudu madevil na hiyo ni kama sacrifice tulikuwa tunatoa kwa mtoto. 

Wawili hawa waliendelea kubishana hadi mumewe akamtoa nywele, na bibi akatoroka nyumba akihofia maisha yake. Mwezi wa nne ndio ali pigia bwanake simu kumuomba msamaha na warudiane.