Patanisho: Alitoka na ugali nilipoenda kumtembelea

Bwana Dennis Gisaka, 35 aliomba apatanishwe na mkewe Jackie 31, baada ya mkewe kutoroka ndoa yao iliyokuwa imedumu kwa zaidi ya miaka kumi.

“Mkewe wangu alikosana na wazazi wangu mwaka wa 2015 mwezi disemba na  kisha tukaenda na kusuluhisha hayo mambo. Siku nne baadaye alitorokea kwao na nilipomwendea yeye alisema hatarudi tena.”

Bwana Dennis anasema kuwa mkewe alitoroka na watoto wao wote ila yeye alimwendea mwanae wa kiume kwani mila na destruri hazikubali mtoto wa kiume kuishi na nyanyake. Hata hivyo, mwaka mmoja baadaye Dennis alimpata tena mkewe.

“Nilimtafta na siku moja nikampata Kitengela. Alinikaribisha na kunipikia ila niliposema ntalala kwake alikataa na akatoka na ugali  nami nikasema sitoki huko. Yeye alienda kulala kwa jirani yake na mimi nikalala kwa kitanda chake. Niliamka asubuhi na kuchukua tuktuk na nikambebea vitu zake zote.”

Jackie, mkewe Dennis hata hivyo ameapa kutomrudia bwanake,

“Huyo jamaa alinikosea sana. Alikuja kwangu akabeba kila kitu. Mimi ni kama ile wimbo ya dunia haina huruma na mimi sina huruma yoyote kwako. Huyu jamaa siku moja aliambia babangu akuje anioe na sasa wazazi wangu wameniambia nikimrudia mimi sio mtoto wao tena.”

Jackie anasema kuwa Dennis hawezi sameheka na hivyo yeye anachokifanya sasa ni kuwataftia wanawe karo na hataki tena mambo yake.

Soma mengi hapa

Patanisho: Mpango wa kando wa bibi yangu anampigia simu tukiwa tumelala

Steve wa miaka 36, na bibi yake Beryl, 36, walitengana mwaka moja ijao, baada ya mvutano na hawajaweza kupatana.

Kisa na maana? Steve anasema ni sababu ya mpango wa kando.

Steve alisimulia kilichotendeka

nituu hi mabao ya mpango wa kando, na sio mimi ni yeye. mimi ni mtu mwaminifu, na 2011 ndio tulijuana na nilikuwa nafanya kazi Nairobi na yeye alikuwa Siaya. Tulielewana tuaowana, na nikambwambia apige transfer Nairobi, na akasema ni vigumu juu alikuwa na mtoto mwignine.

nilimpata na mtoto mmoja, na sikuwa na mapato mazuri na kuongelea hii mambo ya transfer ilikuwa ngumu. 

 

‘No one else paid her fees but her parents’ Ivy Wangechi’s mother denies rumors

Beryl aliweza kushika simu na kukataa huku akisema ako kazini na hawezi kuongea na Gidi.

Lakini Gidi hakukufa moyo, na akapiga mara ya pili,

‘My issue is I don’t talk my issue over the radio, na huyo mwanaume awachane na mimi, sitaki mambo yake kabisa, aendele na maisha yake.’

Je Bwana Steve alikubali kwamba chenye alikuwa anataka Beryl, yani kumfuata Siaya waongee, Steve alishuku na kuonelea hawezi kumfuatilia na mbio na wazazi wake pia watulie.

‘Naonelea ni kama bado kuna mambo mengine ananifichilia’.

Ikiwa Bi Beryle anamsikiza, Steve angependa asikie nini?

‘Excorsed’ gospel singer Rose Muhando is feeling better

‘Wenye wameonaana kwanza wanasameheana na kama akohuko kwao tuongee, turudiane, na tuendelee na maisha yetu vile tulikuwa tunafanya. Watot siwaoni na sijui vile naweza wasaidia.’

Je wanajambo ni ushauri gani ambapo unaweza patia Bwana Steve?

Also read more here

Patanisho: Bwanangu alinifungia mlango akaniambia niende niolewe kwingine

 

Ikiwa mume hataki bibi, je mke anaweza kujilazimisha kwake? Hili ndilo changamoto Bi Susan anapitia, huku akiomba Patanisho kupitia RadioJambo Ijumaa.

Gidi huwa anapenda wakati wanawake wanaomba msamaha katika kitengo cha Patanisho, kwani wa Kenya wengi hudai kuwa wanawake hawapendi kuomba msamaha.

Na hivi leo desturi ilikuwa hiyo, kwa maana Bi Susan alikosana na mzee wake Johnson last week.

Kisa na maana?

‘Alikuwa na uhusiano na mtoto wa shule, 13 years.

Aligundua aje?

Nilifanya kuambiwa na nikachunguza mimi mwenyewe. 

Aliambiwa na nani na aliweza kufuatilia?

‘watu tuu wa plot, niliwapata huko nje walikuwa wamewekeleana mikono kwa mabega. 

Kisha akachukuwa hatia gani?

Nilimuuliza akanichapa nikafanya tuu kutoka kwake juu niliambiwa na wazazi nihepe kwanza akituliza atanirudia. Vile nilitoka hakunipigia simu tena alalfu jana nikajitoa kwa pale nilikuwa naishi nikajileta huko vilealiniona akakfunga nyumba na kuingia huko ndani Akanitumia message akaniambia niende niolewe 

Kwa hivyo anataka kusaidiwa nama gani?

Nataka tuu turidiane naye. Mimi sitaki kuwacha boma yangu.

Je wamekaa kwa ndoa muda gani?

Mwaka na miezi mbili, na tuna mtoto mmoja, alijibu Bi Susan.

Tangu hiyo siku, washa wahi ongea?

Nampigianga simu na hachukuangi. 

Lakini inaonekana kama hii patanisho ilileta shida kidogo kwasababu bwanake alizima simu kabisa.

Ndoa ni kitu ambacho watu waelewe, na hawa vijana vidogo wanaingi kwa uhusiano na hawajajipanga, pia wazazi hawajui. Je ni chnagamotozipi zinazokumba ndoa?

Hawa vijana ni mwongozo wamekosa na ni nani wa kulaumiwa? Gidi na ghost walichangia hili swala. Skiza kanda:

 

 

 

 

Patanisho: Bibi yangu amenuna na tunazungumza kupitia watoto wetu

Wycliffe alikosana na mke wake Evelyne wakati kazi ilikatika ambapo mke wake akachukuwa majukumu pale nyumba anachangia kila kitu, kwa hivyo Wycliffe anahisi huenda labda hiyo ndio ilileta shida pale nyumbani.

Wycliffe alielezea Gidi

ni upande wa fiancial, kazi ilikukosekana na yeye alikuwa kazi by that time, so ilifika mahali amechange. Si uonaona sasa anaone amesimamia kila kitu sasa hapo ndio akaanza kunyamaza na mimi, na nikamwabia kama haniongeleshi, nikambia tunyamziane.

Ni kwan nini anaifikiria ni mambo ya pesa ilifanya furaha iishe huko nyumbani?

Unajua mimi kulingana na vile nimekaa na yeye hiyo miaka yote, nafikiri ni hiyo. Gidi nahsindwa kidogo. Hapo awali tulikuwa tunaelewana kila kitu ilikuwa inaenda tuu shwari, so hapo wakati job iliisha ndio niliona amechange, so sielewi. 

Je amemkalisha chini kumwongelesha? kumuuliza kama hiyo ndio shida na vile wanaweza tatua?

Sasa kama alinyamaza unajua mtu akiamua kunyamaza hata mimi nikamwambia kama umeamua kunyamaza then wacha ata mimi ninyamaze. Hakuna kitu nitafanya. 

Je shuguli zingine za kinyumbani anafanya?

yeah hizo anafanya Saa hii nimepata kazi ingine, na bado hajabadilika.

Wyclife, 28 na bibi yake, 25 wamekaa kwa ndoa miaka mbili na wana watoto wawili.

Watarejesha uhusiano wao? Skiza kanda

 

Patanisho: Mke wangu alinipiga ngumi kama ya GSU

Tulianza rasmi kitengo cha patanisho na yule aliyeomba patanisho ni Kirinya aliyetuma SMS kwa Gidi huku akisema ndoa yake iko karibu kusambaratika akongeza ‘my wife Wangari is not talking to me help me please please.

Doh, kisa na maana. Bwana Kirinya alimwelezea Gidi kilichotendeka

‘Mimi nampigia simu kuna wakati aliniambia anataka kwenda kwao nyumbani na watot ashapeleka huko nimpatie fare. Unajua mimi ni driver wa shule. nikamwambia nitapitia kwake kazi nimpatie pesa an viatu nilinunulia watoto. Kupitia huko nikapata nimwekwa blacklist hata jana nilikuwa nimempigia akaniambia nisiwahi mpigia tena akaniweka mpaka kwa blacklist hata leo sikuenda kazi nione kama mnaweza kunisaidia. 

Mbona Bibi yake Wangari alikuwa amepeleka watoto ushago hapo awali?

Bwana Kirnya alimwelezea, ‘Unajua yeye alisema watot huku ni shida mimi niakmwabia angoje nipeleke numbai kwetu alikataa akaniambia anataka kupeleka watot kwao mimi nikamwambia wapeleke tuu mimi sina shida nitakuwa natoa pesa ya shule na kila kitu Heh naye alinipiga ngumi kama ya GSU bwana. 

Kwa hivi sasa, mke wake Wangari ako wapi?

‘Yeye ako kazi lakini mimi niko nyumbani leo sikuenda kazi Akitoka kazini anarudi nyumbani. Mimi naona hii ndoa ikeinda kuenda tuu. 

Licha ya haya yote Kirinya bado angependa kurejesha uhusiano kati yake na Wangari.

Kirinya ana miaka 32 na Wangari ni 28 na wamebarikiwa na watoto wawili. Ndoa wamekaa kwa miaka nne.

Wangari aliweza kushika simu ya Gidi na kufichua kama yeye ‘si kichwa ngumu’ na mengineo kwa ufupi.

‘Ati mimi ni kchwa ngumu. Sasa nikuulize Gidi, kama hajawahi nipeleka nyumbani kwao na ni kama hajinitambua rasmi kama mke wake’.

Ombai langu ni anipeleke kwao na apange safari nitambulike rasmi.

Skiza kanda usikie maneno matamu kati ha hawa wawili

 

 

 

 

Patanisho: Bibi yangi huchukua simu zangu ninapomtumia mia tano

Katika kitengo chap Patanisho hivi leo, Gidi alipokea ujumbe kutoka bwana Geoffrey, aliomba asave ndio yake ya miaka kumi, baada ya mke wake kutoroka miezei mnne iliyopita.

Alieleza kwamba, ‘ ndio alitoka nyumbani. Kuna siku aliita mshichana cousin yake akuja akae na watoto wetu kabla wafungue shule. Sasa siku moja nikapata watot hawako wamepelekwa reserve. Kumuuliza akasema ndio wameenda reserve, nikamuuliza kwanini hakuniambia. Hapo ndipo tulikosana nikamwabia atoke aeendee watoto akaniambia atenda asubuhi. Asubuhi kuammka sikupata mtu. Akafuta nmba za familia yake yote kwa simu yangu, sasa kutoka siku hiyo hatujawahi onana.

Kutoka siku hiyo, je washawahi ongea?

Anachukuanga simu yangu wikendi tuu wakati anangoja pesa za kusaidia watoto. Lakini katikati ya wiki hachukuangi simu. Bado nampenda nataka turudiane.

Je anahakika hakuma mambo ingine tena alifanya ni hayo tuu ya watoto?

Geoffrey alisema, ; Kitambo alikuwa analalamika nilikuwa namtusi, na niliwacha. Nilimwomba msamaha.

Hakuwa na mpango wa kando?

Hapana. Sijawahi.

Geoofrrey miaka 34, na mke wake Wacera, 29 wako na watoto wawili.

Utamu wa patanisho ni kuskiza mpaka mwisho. Skiza kanda ujue kwanini Wacera hakuchukua simu ya Gidi na ikabidi Geoffrey achukue ushauri kutoka wanajambo.

Patanisho: Na hisi nimetengana na bwanangu juu ya kutoweza kupata mtoto

Tulianza rasmi rasmi kitengo cha patanisho saa mbili unusu, ampbapo ujumbe aliyetuma ni Bi Rile ambaye alisema ndoa yake ya miaka kumi imesambaratika pale kwasabanabu hajaweza kubarikiwa na mtoto.

‘Ameniacha baada ya miaka kumi. ilitokea lini. aliondoka mwezi wa kwanza akienda kazi, akaniacha kwa boma na sasa haji nyumbani tena, ni mwalimu na hadi sasa shule zimefunga na hajarudi. Nikimpigia simu ananiharakisha akisema niongee haraka. Lakini nimesikia tayari ameoa, na mkewe amejifungua. 

Tangu Januari sijamuona. Na anajuaje kwamba ni ile swala la mtoto limeleta hii shida yote?

wakati kabla atoke, kuna comments ambazo alifanya kwamba wakati wenzake a umri wake wanalipa school fees na yeye bado tuu kwa nyumba ananunua mkate ya watu wazima. 

Bi Rile angependa kujua nini kuhusu bwanake katika patanisho?

ok tunaongea kwa simu once in a while anaweza kuchukua simu lakini haongei kama vile mtu huongea na mke wake.

Alieleza Gidi ukweli wa mambo kupitia simu bwana Robert alisema

Inaeza kuwa shida ya mtoto nimekaa na this lady for ten years, na saa hizi kuna pressure from all corners na huu mrembo mimi nimempeleka hospitali ikapatikana yey ndiye akona shida na nimempeleka through IVF sessions mara tatu with various doctors na unaona hiyo kitu ilichukua almost 450,000 shillings sasa mi namwambia ukweli labda through radio jambo kwamba mimi niliamua kutafuta mke wa pili as much as I hated to do it to her.

Skiza kanda ifuatayo

Patanisho: Niliharibu kikoi cha bibi yangu akanikasirikia

 

 

Obilo kutoka Nyakwere aliomba kupatanishwa na mama Delvin aliyetoroka mwezi wa pili.

Sasa hivi ako nyumbani kwao. I was one of the lecturers in Homabay, so hakukuwa na nafasi ya kwenda nyumbani. so vile nilienda nyumbani, nilienda usiku hivi, na kupita hivi tena, nikapata simu, manager alikuwa ananiuliza ati nikowapi. so it forced me to go back the same same day, unfortunately I took hizi shuka za masai na hiyo ilikuwa yake, so from that day upto now we’ve not been in good terms. unfortunately when I was ironing my clothes ilichomeka Ilileta shida, mpaka ikabidi nikabuy mpya.

Je, bwana Obila anahakika ni hii shuka ambayo ilileta shida ua kuna jambo lingine?

‘Sidhani ni hiyo hiyo tuu.

Tangu aende February, wameongea?

ehh kuongea tunaongeanga.

Anasema nini?

Kuna siku aliniambia nitarudi hata leo asubuhi nilimpigia, akaniongeleza tuu vizuri. Lakini mambo yake ya kurudi ni kama imekuwa balaa.

Na wamekaa kwa ndoa miaka ngapi?

4 years.

Je Gidi aliweza kurejesha uhusiano wao. Skiza kanda ifuatayo

 

Patanisho: Bwanangu alialika mpango wa kando kumpikia nilipoenda ushago

Doh!

Ili huyu mwanadada aweze kutulia roho yake ukiskiza vile anazungumza angependa kujua ukweli au msimamo wa huyu jamaa wake ili aweze kuamua kama aendelee kukaa pale kwao ama arudi nyumbani kwao, ilibidi Gidi apige simu mara kadha.

Bi Cynthia alituma ujumbe akiomba apatanishwe na mme wake ambaye ni kama amepotea Nairobi kwasababu hapigi simu anashangaa nini imefanyika.

Tangu February Lawrence amewacha mke wake huko nyumbani na haongei na yeye na inaleta shida kidogo.

“Tulikosana mwezi wa pili. Nilimwambia nataka kwenda nyumbani akaniambia kama utaenda nyumbani hakuna shida Sasa katika hizo harakati mzee wangu akaanza kufuatiliwa kwa nyumba mara SMS, anaandikiwa na SMS na wanawake anapigiwa simu na wanawake nikamuuliza shida ni nini ni venye tuu umesikia nimeenda nyumbani akasema hapana. Sasa hiyo wiki ya kwenda nyumbani nikamwomba simu yake nitumie torch kuogea. Nikachukua simu nikaenda kwa bafuni kuoga. Sasa kitu ikaniambia angalia kwa hii simu nikapata ameandikiwa message ameandikia mwanamke mwingine ati baeb utakuja kunipikia usiku wife wangu anaenda nyumbani. Sasa nikamrudishia simu yake, ata kunisindikiza akakataa. 

Sasa nikafika nyumbanihanipigii simu sasa nikashindwa shida ni nini siku tatu zikapita hanipigii simu. Nilikuwa nimeshika number ya simu ya huyo msichana, sasa nikampigia simu kumuuliza kama anajua Lawrence. Akasema hmajui.

Sasa huyo msichana akareply kwa mzee wangu akamwambia namtusi. Sasa mzee wangu akanipigia simu akaniambia kuanzia leo ujuwe wewe sio bibi yangu. Niakaambia wazazi wangu na imagine nilikuwa na mimba ya miezi mbili. Wazazi wangu wakaniambia nipigie wazazi wake na wao wakaniambia niende kwao. Babangu akapigia huyo mzee wangu simu na kumwabia anitumie fare niende kwao. Kwa hizo harakati ya kuafuta pesa, mimba ikatoka, juu huyo mshichana alikuwa ananitusi sana.

So kumalizia ni kwamba kutoka February sijamuona hajarudi nyumbani alisema nikiwa kwao hawezi kanyanga nyumbani. Ananiandikia SMs za matusi ananiambia akona bib, nisiende nikae tuu.

Cynthia wa miaka 23, na Lawrence, miaka 30 wamekaa kwa hii uhusiano kwa miaka tatu na nusu. Wako na mtoto mmoja, na mwenye anagharamia maisha ni wazazi wake.

Je, Gidi aliweza kumpata Lawrence kupitia simu? Skiza kanda ifuatayo.

 

 

 

 

 

Patanisho: Nikijaribu kumhoji bwanangu, anasema mimi si mwaminifu

Katika kitengo cha Panisho, yule ambaye angependwa kupatanishwa ni Jacqueline ambaye anasema alikosana  na bwanake Cheruiyot juu ya maneno ya watu na yeye Cheruiyot kuwa suspicious.

Jaquiline alituma SMS kwa Gidi akisema watu wanampigia simu na anaamini vile anambiwa.

‘Na yeye saa zingine anakubali. Yeye hayuko nyumbani hautko na yeye ako kazi mbali sana. so anapigiwa simu na brother yake ama majirani wakimwambia maneno, labda siko nyumbani yenye ni uwongo.Na yeye anakubali, anaanza kunigombanisha kwa simu, ananipigia makelele. Na yeye huwa haniamini.

Na hii mambo ya kununa ilianza lini?

‘Alitoka nyumbani three motnhs ago. sasa vile alienda kazi ndivyo alianza kunipigia simu aliniambia hio maneno. 

Wawili hawa wamekaa kwa ndoa miaka tatu na wana mtoto mmoja.

Cheruiyot na Jacqueline waliweza kuongea na kutoa hakikisho wanapendana sana, na ni watu wanajaribu kuwatenganisha.

Skiza kanda: