Kimanzi asifu Eritrea baada ya Harambee Stars kunyukwa 1-4

Kocha wa Harambee stars Francis Kimanzi anasema kikosi cha Eritrea kilionyesha mchezo bora zaidi kuliko vijana wake jana baada ya kuwabwaga mabao manne kwa moja katika robo fainali ya kombe la CECAFA inayoendelea mjini Kamapala Uganda.

Stars walikua mabingwa watetezi walijipata taabani licha ya kushinda mechi zao zote za kwanza kwani vijana wa Red sea waliwaonyesha kivumbi.  Eritrea itacheza na Uganda katika fainali, baada ya wenyeji kuilaza Tanzania 1-0.

Kikosi ya Kenya cha riadha kwa vijana wasio zaidi umri wa miaka 20 kitakita kambi huko Nyeri kwa mazoezi ya mbio za dunia za mwaka 2020 kwa wanariadha wasiozidi umri wa miaka 20 zitakazoandaliwa Nairobi.

Wanariadha 50 wataelekea Nyeri, ili kuhakikisha kikosi hicho kiko imara zaidi.  Kenya itakua inawania kunyakua taji hilo.

Aston Villa ililaza Liverpool mabao 5-0 na kufuzu kwa nusu fainali ya kombe la ligi ya Uingereza, usiku wa jana ugani Villa Park. Huku kikosi cha kwanza cha  Liverpool kikiwa nchini Qatar  ambako watacheza na Monterrey katika kombe la klabu bingwa duniani, Liverpool walichezesha kikosi changa zaidi katika historia yao huku vijana wasio zaidi umri wa miaka 23 wakipiga shughuli.

Viongozi wa iigi ya Itaila  wameomba radhi kwa kutumia picha za nyani katika kampeini za kupambana na  ubaguzi wa rangi dhidi ya wachezaji weusi. Picha hiyo iliyonuia kuwaweka pamoja wachezaji imezua ghasia baada ya timu kadha zikiwemo AC Milan na Roma kudai kuwa hawaku husishwa katika kampeni hiyo na haikua bora.

Mchoraji aliyechora picha hiyo alidai alinuia kuwaweka wachezaji wa rangi zote sawa kwa kuwachora nyani hao mmoja mzuungu, mwengine wa kiafrika na yule wa ki Asia.

Kocha wa zamani wa Real Madrid, AC Milan  na Chelsea Carlo Ancelotti anatarajiwa kutajwa kama kocha mkuu wa Everton siku ya Alhamisi ama Ijumaa, baada ya kuafikiana na wenyeji kuchukua hatamu.

Mazungumzo yanaendelea baada ya mzaliwa huyo wa Italia kuwasili Uingereza, siku kadha baada ya kufutwa kazi kama kocha wa Napoli. Ancelotti atachukua  mahala pa Marco Silva ambaye alichujwa wiki mbili zilizopita.

Harambee Stars na Togo watoka sare ugani Kasarani

Harambee Stars walitoka sare ya 1-1 jana na Togo katika mechi ya kufuzu kwa AFCON mwaka 2021 iliyochezwa uwanjani Kasarani.

Kiungo wa kati Johanna Omollo anayesakata soka Ubelgiji alifungia Stars kunako kipindi cha kwanza kabla ya Hakimu Oura-Sama kusawazishia Togo kunako dakika ya 64.

Matokeo haya yana maana kuwa vijana wa Francis Kimanzi hakuweza kupata ushindi waliohitaji kuwapandisha hadi kileleni mwa kundi G.

PATANISHO: Gidi kama uko upande wa Nancy nitakata simu!

Uhispania walimaliza kampeni yao ya kufuzu kwa Uro mwaka 2020 kwa ushindi wa 5-0 dhidi ya Romania. Fabian Ruiz aliwapa mabingwa hao mara tatu wa Uropa uongozi wa mapema kabla ya Gerard Moreno kufunga kutoka kwa pasi ya Santi Cazorla.

Lionel Messi alifunga penalti ya dakika za lala salama, Argentina walipotoka sare ya 2-2 na Uruguay.  Mchezaji mwenza wa Barcelona Luis Suarez, alikua amewapa Uruguay uongozi kunako kipindi cha pili.

Nahodha huyo wa Argentina kisha akafunga bao lake la pili katika mechi za kimataifa. Edinson Cavani alianza kufunga lakini Sergio Aguero akasawazishia Argentina.

Wakati huo huo Italia walirekodi mojawapo ya ushindi mkubwa zaidi katika historia ya kufuzu kwa kipute hicho, kwa kuwaadhibu Armenia 9-1.

ODM kuhamia katika makao makuu mapya

Shirika la maadili ya wanariadha limefuta marufuku ya mwanariadha wa marathon mkenya Jacob Kendagor. Kendagor alipigwa marufuku kwa kukwepa, kukataa na kukosa kuwasilisha sampuli zake kwa vipimo, ambayo ni kinyume cha kanuni za IAAF za kupambana na dawa za kusisimua misuli. Kendagor hata hivyo alikanusha mashtaka hayo.

Shirikisho la riadha nchini AK limetangaza kuwa majaribio ya Olympiki yatafanyika mjini Eldoret kati ya Juni tarehe 19 na 21 mwakani. Hii itakua mara ya pili majaribio hayo yameandaliwa mjini humo, baada ya kuandaliwa humo mwaka wa 2016. Jana AK ilitangaza kalenda yake ya msimu mpya iliyothibitisha kuwa timu ya Kenya ya Olympiki itaingia kambini ugani Kasarani Juni tarehe 24.

Harambee Stars wajikakamua na kutoka sare na wenyeji Misri

Harambee Stars jana walitoka sare ya 1-1 na wenyeji Misri katika mechi yao ya kwanza ya kufuzu kwa AFCON mwaka 2021.

Kenya walijipata nyuma ya the Pharaohs kufikia muda wa mapumziko kufuatia bao la Mahmoud Abdel-Moneim. Bao la kusawazisha la Kenya lilifungwa katika dakika ya 67 na Michael Olunga.

Mechi inayofuata ya Stars itakua dhidi ya Togo jumatatu uwanjani Kasarani.

Huenda Lionel Messi akachezea Argentina katika mechi ya kirafiki na Brazil nchini Saudi Arabia hii leo. Mahasimu hao wa Amerika Kusini watakutana jijini Riyadh huku Messi akicheza mechi yake ya kwanza ya kimataifa tangu Julai.

Kiungo huyo wa Barcelona alipigwa marufuku ya miezi mitatu kwa kusema kuwa ligi ya Copa America ina ufisadi. Neymar hatacheza kutokana na jeraha la mguu lakini Gabriel Jesus yuko kwenye kikosi.

Uingereza walifuzu kwa Uro mwaka 2020 kwa kucharaza Montenegro mabao 7-0 ugani Wembley. Nahodha Harry Kane alifunga mabao matatu na kupanda hadi katika nafasi ya tano katika orodha ya wafungaji mabao mengi, Uingereza, akiwa amefunga magoli 31 huku Alex Oxlade-Chamberlain, Marcus Rashford na Alexandar Sofranac wakifunga mabao hayo mengine.

Mshambulizi wa Chelsea Olivier Giroud alifunga bao la ushindi kupitia mkwaju wa penalti mabingwa wa dunia Ufaransa walipotoka nyuma na kuwanyuka Moldova 2-1 katika mechi yao ya kufuzu kwa Uro mwaka 2020 na kupanda hadi kileleni mwa kundi H.

Kufuzu kwa Ufaransa kulijiri kabla ya mechi hio kuanza kutokana na Uturuki kutoka sare na Iceland. Vadim Rata walifungia Moldova dakika tisa baada ya mechi kuanza kabla ya Raphael Varane kusawazisha na Giroud kufanya mambo kuwa 2-1.

Cristiano Ronaldo sasa amesalia na mabao mawili awe na jumla ya mabao100 katika mechi za kimataifa baada ya kufunga mabao matatu jana dhidi ya Lithuania katika mechi ya kufuzu kwa Euro 2020.

Ureno ilishinda mechi hiyo mabao 6-0. Kiungo huyo wa Juventus mwenye umri wa miaka 34 huenda akawa mchezaji wa pili kufikisha mabao 100 ya kimataifa iwapo atafunga mabao mawili dhidi ya Luxembourg jumapili.

Manchester United ina nafasi nzuri ya kumsajili mshambuliaji wa Red Bull Salzburg na Norway Erling Haaland kinda wa miaka 19, ambaye alifunzwa na Ole Gunnar Solskjaer akiwa Molde. Wakati huo huo United inatarajia kuafikiana na Juventus kuhusu usajili wa mshambuliaji wa Croatia Mario Mandzukic mwenye umri wa miaka 33, kufanya mazoezi na klabu hiyo mwezi ujao kabla ya uhamisho wa Januari.

Kiungo wa AFC Leopards Moses Mburu ameeleza kufurahishwa na kuregelea mazoezi na timu yake baada ya kukaa nje kwa takriban mwaka mmoja akiuguza jeraha.

Mlinzi huyo alifanyiwa upasuaji mwezi Septemba mwaka uliopita na kuregelea mazoezi miezi minne baadae kabla ya kupata jereha la mguu. AFC Leopards iko katika nafasi ya saba katika ligi ya KPL wakiwa na alama 15 baada ya mechi 9. Wtakabana na Bandari mjini Mombasa alhamisi wiki ijayo.

Kocha wa Chemelil Sugar Francis Baraza ameteuliwa kama kocha mkuu wa timu ya Tanzania Biashara United Mara. Baraza ameondoka Chemelil Sugar, ambao wako katika nafasi ya mwisho katika jedwali la KPL na hawajashinda mechi hata moja tangua kuanza kwa maimu mpya.

Alijiunga na timu hiyo Mei mwaka 2018 na ameshawahi pia kufunza Muhoroni Youth, Sony Sugar na Western Stima.

 

Soma jinsi serikali ya Misri ilivyowaokoa Harambee Stars mjini Cairo

Serikali ya Misri iliwaokoa Harambee Stars waliokua nusura wafurushwe kutoka kwa hoteli yao jijini Cairo kutokana na kutolipwa kwa ada.

Stars wako jijini humo kwa mechi yao ya kufuzu kwa AFCON ya kundi G dhidi ya the Pharaohs leo usiku. Rais wa FKF Nick Mwendwa ameilaumu serikali kwa hali hio ambayo anasema inatishia kusambaratisha mechi yao dhidi ya Misri.

Serikali hata hivyo kupitia kwa katibu wa michezo Kirimi Kaberia ilirushia lawama FKF huku Kaberia akisema hawakuipa serikali taarifa muhimu na kuwa walitaka kupewa pesa taslim.

Harambee Starlets wamewasili salama nchini Tanzania kabla ya kipute cha ubingwa wa kinadada cha CECAFA mwaka 2019 kinachopangiwa kuanza jumamosi.

Hii ni siku moja tu baada ya kinadada hao kuwasili nchini kutoka Zambia ambapo walibanduliwa nje ya michuano ya kufuzu kwa olimpiki ya bara mwaka 2020 na She Polopolo.

Starlets wanatumai kushinda taji hilo ambalo limekua likiwaponyoka katika miaka ya hivi majuzi, watakapoanza kampeni yao dhidi ya Ethiopia jumapili tarehe 17.

Meneja wa Uingereza Gareth Southgate anasema hatasita kumchagua kiungo Raheem Sterling kwa mechi ya jumapili ya kufuzu kwa Uro mwaka 2020 huko Kosovo.

Sterling alichujwa kutoka kwa mechi ya leo baada ya kulumbana na mwenzake Joe Gomez. Uingereza inahitaji alama moja tu dhidi ya Montenegro ili kufuzu. Sterling anayechezea Manchester City Sterling atacheza mechi ya jumapili huko Kosovo.

Wing’a wa Chelsea Callum Hudson-Odoi anasema aliongea na meneja Frank Lampard kumshawishi asalie Stamford Bridge. Kinda huyo wa miaka 19 aliwasilisha ombi la kutaka kuhama mwezi Januari baada ya Chelsea kukataa ofa ya pauni milioni 35 kutoka kwa Bayern Munich.

Hata hivyo Odoi amemfurahisha Lampard aliyechukua uskani msimu wa joto. Odoi atakosa mechi za msimu huu baada ya kupata jeraha la mguu alipokua akicheza katika mechi yao dhidi ya Burnley mwezi Aprili.

Aliyekuwa meneja wa Arsenal Arsene Wenger anaregea katika ulingo wa soka baada ya kukubali kuwa mkuu wa ukuzaji soka duniani wa FIFA. Hatua hii inamaliza uvumi uliomhusisha mfaransa huyo na kurudi kama meneja wa Bayern Munich.

Wenger aliondoka Gunners Mei mwaka 2018, baada ya miaka 22 mamlakani. Wadhfa wake mpya utasaidia kukuza soka ya kinadada na wanaume na vilevile masuala ya kiufundi.

 

Furaha kwa Kenya? Salah huenda akakosa mechi dhidi ya Harambee Stars

Kiungo wa Liverpool Mohamed Salah atakosa mechi ya Misri ya kufuzu kwa AFCON dhidi ya Kenya na Comoros kwa kuwa ana jeraha la mguu. Salah aliungana na timu hio jijini Cairo jana ili kufanyiwa uchunguzi wa jeraha hilo.

Mo Salah aregea katika kikosi cha Misri kitakachopambana na Kenya

Salah alikosa mechi ya Liverpool waliyotoka sare na Manchester United mwezi Oktoba baada ya kugongwa na Hamza Choudhury wa Leicester. Meneja Jurgen Klopp, aliyekasirishwa na Choudhury anasema Salah bado alikua akiuuguza mguu huo kabla ya kugongwa tena. Mechi ifuatayo ya Liverpool itakua ugenini dhidi ya Crystal Palace Novemba tarehe 23.

FKF jana ilizindua mkataba wa ufadhili wa shilingi milioni 90 na kampuni ya kamari ya Betika. Kufuati hili ligi ya daraja la pili humu nchini sasa itajulikana kama  Betika Super League kwa kipindi cha miaka mitatu ijayo. Kwa mujibu wa masharti ya mkataba huu timu zote 20 katika mashindano hayo zitapokea ufadhili wa shilingi elfu 750 kila msimu. Vlabu hivyo pia vitapokea vifaa vingine vya soka.

Kutana na Mo Salah ‘feki’ anayetumiwa katika matangazo ya runinga

Bingwa wa mbio za Marathon duniani Brigid Kosgei ni mmoja kati ya wanariadha watano wa kike waliorodheshwa kuwania tuzo la mwanariadha bora zaidi wa kike duniani, mwaka huu. Mwezi uliopita Kosgei aliipiku rekodi ya muingereza Paula Radcliffe ya miaka 16 kwa kukimbia kwa muda wa masaa mawili dakika 14 na sekunde nne na kushinda mbio za Chicago Marathon.

Kosgei pia alikua mshindi mchanga zaidi wa mbio za London Marathon mwezi Aprili. Wanariadha hao wegine ni pamoja na mwamerika  Dalilah Muhammad, mjaamaica Shelly-Ann Fraser, raia wa Venezuela Yulimar Rojas na wa Uholanzi  Sifan Hassan.

Ghost Mulee aitetea Harambee Stars, ataja sababu za kupoteza

Ghost Mulee ametaja sababu za timu ya kitaifa ya Harambee Stars kupoteza moja kwa nunge.

Katika kipindi kinachoruka katika kituo hiki kila asubuhi cha Patanisho, Ghost amesema kuwa uwanja kuteleza ulichangia timu ya kitaifa kupoteza.

IAAF kukataa ushindi wa Eliud Kipchoge, Ghost na Gidi watoa tamko

Kuteleza kwa uwanja kulisababishwa na mvua mkubwa iliyonyesha kabla mechi kuanza

Harambee Stars walikabana koo na timu ya soka ya Msumbiji katika mechi ya kirafiki Alasiri jana.

Hii ilikuwa jaribio kubwa la kutia makali kwa michuano ya kufuzu kwa AFCON mwaka wa 2021

Gari, Miili ya Mariam Khagenda na mtoto yatolewa, nyufa za serikali zatajwa

Kabla mechi hiyo kuanza, Francis Kimanzi alikuwa na matumaini makubwa zaidi huku akisema wachezaji hao ambao wamekuwa kambini kwa siku tano katika mazoezi ya kina.

Ghost amesema kuwa timu ya kitaifa haifai kupoteza matumaini yoyote.

Harambee Stars kukabana na Msumbiji leo, Kasarani

Harambee Stars watakabana na Msumbiji katika mechi ya kirafiki alasiri ya leo uwanjani Kasarani, kujitayarisha kwa michuano ya kufuzu kwa AFCON mwaka wa 2021.

Nahodha Victor Wanyama atacheza huku Farouk Shikhalo huenda akaanza kama kipa kwani Patrick Matasi hayuko. Kocha mkuu Francis Kimanzi anasema wachezaji hao ambao wamekuwa kambini kwa siku tano, wako katika hali nzuri na atawabadilisha ili kujaribu wachezaji wapya.

Mechi hiyo inaanza saa kumi kamili huku tikiti zikiuzwa kwa shiilingi 200.

Uganda yapanga kunyonga wapenzi wa jinsia moja

Hayo yakijiri, timu ya raga ya kinadada Kenya Lionesses itakabana na Zimababwe katika michuano ya kufuzu kwa Olimpiki ya raga ya wachezaji 7 saa sita mchana baada ya kuongoza kundi A na rekodi ya kutoshindwa.

Kinadada hao waliwacharaza Ghana 36-0, baada ua kuwanyuka Botswana 51-0 na Senegal 36-0. Kenya iliorodheshwa ya kwanza na jumla ya alama 121.

Tukielekea ulaya, Nemanja Matic huenda akajumuika tena na kocha Antonio Conte, iwapo Inter Milan itajaribu kumsajili kiungo huyo wa kati msimu huu, kutoka Manchester United.

Mchezaji huyo wa umri wa miaka 31 raia wa Serbia amecheza mara tatu katika ligi ya Primia msimu huu, tangu kuteuliwa kwa Ole Gunnar Solskjaer. Matic alichezea Chelsea kwa miaka mitatu, msimu wa mwisho chini ya Antonio Conte kabla ya kujiunga na United kinyume na alivyotaka Conte Agosti mwaka 2017.

Orodha ya Wanaume mashuhuri wanaojivunia kuwa wazazi

Italia waliwanyuka Ugiriki 2-0 na kufuzu kwa fainali ya michuano ya Uro mwaka 2020. Baada ya kutoka sare tasa katika kipindi cha kwanza Jorginho waliwaeka mbele kupitia kwa bao kunako dakika ya 63 kabla ya Federico Bernadeschi kufunga la pili.

Wakati huo huo Uhispania ilikaribia kufuzu kwa michuano hiyo walipotoka sare ya 1-1 na Norway.

 

Mtalipa! FKF yaagizwa kumlipa aliyekuwa kocha wa Harambee Stars 108M

Mahakama ya kushughulikia masuala ya spoti imeiagiza FKF kumlipa aliyekua kocha wa Harambee Stars Adel Amrouche Shilingi milioni 108 kama malipo ya kumfuta kazi kimakosa.

Kocha huyo raia wa Ubelgiji alifutwa kazi na aliyekuwa rais wa FKF wakati huo Sam Nyamweya baada ya kupoteza kwa Lesotho katika mechi ya kufuzu kwa AFCON mwaka wa 2015. Aliishtaki FKF kwa FIFA na kuwawadiwa shilingi milioni 60 lakini hakutosheka na kuwasilisha kesi yake kwa mahakama ya spoti.

Wema Sepetu azirai na kuanguka ghafla, akimbizwa hospitali

Rais wa sasa wa FKF Nick Mwendwa alipinga rufaa hiyo lakini akapoteza.

Hayo yakijiri, mshambulizi kinda Gabriel Martinelli alifunga mabao mawili na kuwapa Arsenal ushindi dhidi ya Standard Liege katika ligi ya Uropa.

Kulikua na pengo la chini ya dakika tatu kati ya mabao ya kinda huyo wa miaka 18 raia wa Brazil, huku mwenzake Joe Willock wa miaka 20, akifanya mambi kuwa 3-0 kabla ya muda wa mapumziko. Martinelli, alisajiliwa kwa kititta cha pauni milioni 6 msimu huu joto. Arsenal sasa wako kileleni mwa kundi F.

Kiungo wa Arsenal Pierre-Emerick Aubameyang ametumia mtandao wa Twitter kuwasuta wanaosema kua aliondoka Borrusia Dortmund kwa sababu ya pesa tu.

Kenya yashuka hadi nafasi ya 5 katika ubingwa wa dunia – Doha Qatar

Madai hayo yalitolewa na afisa mkuu wa Dortmund Hans-Joachim katika mahojiano na jarida moja la Ujerumani. Aubameyang mwenye umri wa miaka 30 raia wa Gabon alihamia Arsenal kutoka klabu hio ya Ujerumani kwa kitita cha pauni milioni 56 mwezi Januari mwaka 2018.

Aliyekuwa mshambulizi wa Nigeria Isaac Promise ameaga dunia akiwa na umri wa miaka 31. Klabu yake ya Marekani Austin Bold inasema alifariki jumatano usiku lakini hawakueleza chanzo cha kifo chake. Promise alikuwa nahodha wa Nigeria waliposhinda nishani ya fedha katika Olimpiki ya mwaka 2008 jijini Beijing. Alitumia muda mwingi wa tajriba yake Uturuki huku pia akicheza Saudi Arabia.

 

 

Harambee Stars: Kimanzi amtema kipa Matasi, Shakava ajumuishwa

Kocha wa Harambee Stars Francis Kimanzi amemwondoa Patrick Matasi kutoka kwa kikosi chake cha wachezaji 23 kwa mechi ya kirafiki dhidi ya Msumbiji itakayochezwa Oktoba tarehe 13 jijini Nairobi.

Kimanzi amewaweka wachezaji waliokua katika kikosi kilichotoka sare ya 1-1 na Uganda. Eric Johanna anayesakata soka Uswidi pia amewachwa nje huku Harun Shakava, Ian Otieno na Masud Juma wakijumuishwa.

Yusuf Mainge na Joseph Okumu pia wamejumuishwa. Timu hiyo itaripoti kambini Oktoba tarehe 7.

Hayo yakijiri, Kenya jana iliweza kupata medali moja tu katika fainali tatu za mbio zainazoendelea za ubingwa wa dunia huko Qatar.

Mourinho atoa sababu mbona Eto’o alihitaji kushinda Ballon d’Or

Beatrice Chepkoech aliongoza kutoka mwanzo hadi mwisho wa mbio za mita elfu 3 kwa kinadada, kuruka viunzi na maji.  Juhudi za kupata medali katika mbio za wanaume za mita elfu 5 zitaendela leo baada ya Ethiopia kutamba katika fainali ya jana.

Jacob Kirop na Nicholas Kimeli walishindwa kuwapiku waEthiopia huku Muktar Edris akitetea taji lake na Selemen Barega akishinda nishani yafedha.

Hakukuwa na medali katika fainali ya mbio za kinadada za mita 800 kwani Eunice Sum alimaliza katika nafasi ya tano huku Mganda Halimah Nakaayi akishinda dhahabu.

Tukielekea kwenye kadanda, Ole Gunnar Solskjaer anasema Manchester United wana kibarua kigumu baada ya kutoka sare ya 1-1 na Arsenal.

Bao la kusawazisha la Pierre-Emerick Aubameyang lina maana kwamba United sasa hawajashinda mechi tatu za ligi msimu huu ambapo wamekua wakiongoza 1-0 kufikia muda wa mapumziko.

United wamekua na mwanzo mbaya wa ligi katika kipindi cha miaka 30 iliyopita.

Manchester United wanatarajiwa kujaribu tena kumsajili mshambuliaji wa timu ya taifa ya Croatia na klabu ya Juventus Mario Mandzukic mwenye umri wa miaka 33, ambaye alikuwa kwenye mipango yao wakati wa dirisha la usajili lililopita.

Juve wanatarajiwa kutaka ada ya uhamisho ya pauni milioni 9, huku Mandzukic akitarajiwa kukataa ofa yoyote ya mshahara chini ya kiwango anacholipwa sasa cha pauni milioni 4.5 kwa mwaka.

Chanjo itakayomaliza maambukizi mapya ya HIV yazinduliwa

Kiungo wa kati wa Wales Aaron Ramsey huenda akaanza katika mechi yake ya kwanza ya ligi ya mbaingwa kwa Juventus dhidi ya Bayer Leverkusen hii leo.

Ramsey, mwenye umri wa miaka 28, aliingia kama akiba katika mechi ya Juventus waliyotoka sare ya 2-2 dhidi ya Atletico Madrid mwezi September. Lakini ameanza mechi tatu za Serie A matches, ingawaje bado hajacheza kipindi cha dakika 90.

 

 

Harambee Stars na Uganda Cranes wakabana koo

Harambee Stars na Uganda Cranes jana walicheza mechi ya kusisimua uwanjani Kasarani. Uganda walianza kufunga kunako dakika ya 22 kupitia kwa Emmanuel Okwi.

Francis Kimanzi alimuondoa Michael Kibwage baada ya muda wa mapumziko huku Johnstone Omurwa akichukua mahala pake. Kenneth Muguna alifunga bao la kusawazisha kunako dakika ya 51. Kimanzi alikisifu kikosi chake akisema amefurahishwa zaidi na wachezaji aliowaita.

VIDEO + Picha: Harmonize afanya harusi, WCB yatemwa nje ya milango

Bingwa wa London Marathon Brigid Kosgei jana aliweka historia kwa kushinda taji la Great North Run huko Uingereza kwa kukimbia kwa saa moja 1 dakika 04 na sekunde 28. Kosgei alivunja rekodi ya awali ya mkenya mwenzake Mary Keitany aliyoweka mwaka 2014.

Muingereza Mo Farah alishinda taji la wanaume kwa mara ya sita mfululizo mbele ya muethiopia Tamirat Tola huku raia wa Uholanzi Abdi Nageeye, akimaliza katika nafasi ya tatu.

Henrikh Mkhitaryan alifunga mabao mawili na kusaidia mengine mawili Armenia walipiwanyuka Bosnia-Herzegovina mabao 4-2 katika mechi ya kufuzu kwa Euro 2020.

Kiungo huyo wa kati wa Arsenal ambaye anachezea Roma kwa mkopo alifunga bao la kwanza kunako dakika ya tatu. Alifunga la pili baada tu ya Edin Dzeko kusawazisha. Amer Gojak alisawazishia Bosnia tena lakini Hovhannes Hambard-zumyan akafunga kutokana na pasi ya Mkhitaryan.

Kauli ya siku 9th September 2019

Matokeo haya yanapiga jeki matumaini ya Armenia ya ubingwa wa Euro lakini yanawawacha Bosnia wakiwa mashakani. Armenia wako alama tatu nyuma ya Finland ambao wako katika nafasi ya pili.

Kwingineko, Juventus wanataka kufungua majadiliano ya mkataba na David de Gea mapema mwaka ujao iwapo mzozo wake na Manchester United hautakua umetatuliwa.

Raia huyo wa Uhispania atakua bila mkataba msimu ujao wa joto na hajatia saini mkataba wa pauni elfu 350 kwa wiki aliopewa na Manchester United.

Imeibuka kua wamiliki wa Juventus wanaweza kumtwaa De Gea bure bilash, na kumaanisha kua United watakosa kitita kikubwa cha ada ya uhamisho.