(+ Video) Mahangaiko ya Harmonize, Je lebo ya WCB inamnyanyasa ?

Harmonize amesimulia mahangaiko anayopitia baada ya kutangaza kuitema lebo kubwa Afrika Mashariki y WCB.

Katika mahojiano na Clouds, staa huyu amesimulia jinsi amelazimika kuuza nyumba zake kulipa Milioni 22.5 anazodaiwa na lebo ya Wasafi.

Uongozi wa WCB sasa unamtaka alipe hela iliyotumika kurekodi muziki wake na zaidi ya hapo kununua hatimiliki za jina la Harmonize.

Ikumbukwe kwamba staa huyu anayetamba na mkwaju wa UNO hakuwa na jina hilo alipoingia Usafini (WCB)

Jina la Harmonize , Harmonize mwenyewe ni mali ya WCB kulingana na meneja wa Diamond Sallam SK.\

Kufikia sasa Konde Boy ameuza nyumba zake mbili katika juhudi za kumaliza mkataba wake freshi bila matatizo.

“Nimelipa kiasi lakini mpaka hivi sasa bado nadaiwa na sijamalizia kulipa ila bado kiasi kidogo sana cha kumalizia hela hiyo,” Harmonize alidokeza.

Sikuwa na hela, kwa hivyo nikauza baadhi ya ninavyomiliki. Kuna sehemu nilikuwa najenga nyumba zangu 3, nililazimika kuuza. Nilifanya hivo kwa sababu pesa sio kitu. Nishawatumia mpunga kiasi fulani na salio ni ndogo…” Alisema Konde Boy

Ila je? Kuna uwezekano wowote lebo hii ikawa inamnyanyasa Konde Boy.

Msanii Rich Mavoko alipitia njia sawa na Harmonize.

Je, hela wanayodai wasanii hawa inaweza ikaathiri muziki wao wa njia moja ama nyingine?

Harmonize ni msanii namba moja kwa sasa Tanzania – Q Chief

Staa mkongwe wa Tanzania Q Chief sasa anahoji kuwa Harmonize kwa wakati huu ndiye staa mkubwa Tanzania.

Katika mahojiano, Q Chief ambaye anaonekana karibu sana na Konde Boy amezungumza mengi kuhusu maisha yake ya muziki.

Aidha, staa huyu amesema kuwa kutoka kwa Harmonize WCB ni ishara ya mwana kukua.

“Kuna kipindi mtoto analelewa na baba. Kikubwa unachotakiwa kujua ni kumheshimu baba. Harmonize sijawahi sikia akimzungumzia Diamond vibaya…”

Soma hadithi nyingine:

Rayvanny aweka wazi taarifa za kusaliti Mkewe Fayma kwa Elizabeth Lulu

Q Chief amesema kuwa yupo kwenye usimamizi wa  Konde Gang ya Harmonize.

“Konde Gang ni lebo yangu. Nyuma ya hizo projects yupo mwenyezi Mungu…”

Kama mwandani wa Harmonize, staa huyu amekana taarifa za uhasama kati ya Diamond na msanii aliyemtengeza.

“Tangu hizi issues zianze, Harmonize sijawahi sikia akizungumza kitu negative kumhusu Diamond…”

“Ni kwa sababu anaheshimu. Watu wanatakiwa kuona vile ana akili kubwa.”

Kuhusu iwapo anajua kilichofanyika kupelekea Harmonize kuitema WCB, Q Chief amesema kuwa ana ufahamu wowote.

Soma hadithi nyingine:

Swaleh Mdoe atokwa na povu, siasa za uanahabari zimemchosha

‘Nyuma ya pazia hatujui ni nini kinaendelea. Ukaribu wangu na Harmonize haunipi kujua kabisa kinachofanyika.”

Aidha, amewaonya watu wanaomchamba staa huyu katika mitandao ya kijamii.

“Inaniuma sana mtu anaposema atakwama. Kwa nini mtu hafikirii kuwa Mungu atamsaidia apae juu.”

“Comment mbaya zinamjenga na hata comment nzuri zinamfanya awe imara zaidi.”

“At least naona furaha iliyopotea miaka mingi. Nawashukuru sana waandishi wa habari, nimshukuru Harmonize, Diamond kwa kuipeleka game juu.”

“Lakini sisemi kuwa msanii wangu Harmonize hana mchango wowote. Kama unavyoona sasa,yeye ndiye msanii namba moja Tanzania.”

 

Harmonize ataja mastaa Tanzania waliojunga na Konde Gang, aitaja WCB

Staa na nyota wa Bongo Harmonize ametaja baadhi ya majina ya watu ambao watakuwa katika lebo ya Konde Gang.

Ikumbukwe kuwa staa huyu ndiye kifungua mimba cha lebo kubwa Afrika Mashariki ya WCB iliyopo mjini Dar nchi jirani ya Tanzania.

Harmonize almaarufu kama Konde Boy amekuwa mkubwa kwa kupiga nyimbo hatari na kushirikisha mastaa wakubwa kutoka nchi jirani kama Uganda na Nigeria kati ya nyinginezo.

Matamasha anayoyafanya ni makubwa sawa na bosi wake Diamond Platnumz.

Soma hadithi nyingine;

(+Meseji zavuja ) Willy Paul aonywa, meseji za ufisi Insta

Dogo ana mpenzi wa haiba ya juu sana Sarah.

Ana walinzi sawa na idadi ya Diamond. Kumewahi kutokea vyombo vya habari nchini Tanzania zinazowalinganisha wawili hawa.

Katika mahojiano, staa huyu aliitetea Konde Gang na kutaja watu walio katika lebo hiyo,

“Sisi tunakuwa kila siku na watu wanatupenda. Jamii inatupenda na inatufuatilia sana. Konde Gang ni still WCB.”

“Konde Gang itakuwa na mastaa wa wengine sio mastaa. Nadhani kwa sasa umeona Jose wa Mipango Jabulanti, Choppa,Mnyama Mkali, Budda na Mchachambo .”

“You know Young Money right, you know cash money right. Come on why are you asking?” Alisema Harmonize.

Kwa usemi huu, staa huyu anasema hana matatizo na WCB.

Soma hadithi nyingine;

Zitakavyofanyiwa noti mzee za elfu, M-Pesa kukoma kuchukua Alhamisi

 Hii inatokea kuwa tofauti na matendo yake baada ya kufanya hafla ya ndoa na kukosa kuwaalika mastaa wa WCB

Wanandoa hawa walihakikisha wameipanga hafla hiyo kwa mbwembwe zote na hawakuwaalika mastaa wa WCB.

Soma hadithi nyingine;

Mkali wa “Lubbish” apigwa faini ya 1M kwa kuonyesha video chafu, ajitetea

Mzee Abdul anahoji kuwa dalili za Harmonize kuwa ana uwezo wa kufanya na kusimamia fiesta zake nje ya nchi ni ishara kuwa mwana kashakua na kwa hivo kutoka kwake ni kwema kwa maslahi yake.

Anadokeza kuwa labda dogo kapewa ushawishi na marafiki wake ili kufanya uamuzi huo.

”Kwanza Naseeb alimuangaikia sana. Kamtufuta kampa sapoti kubwa kamtoa kimuziki,” Mzee Abdul.

“Harmonize sio mtoto. Ukiona mtu anatoka kashakomaa tayari.

Babake Diamond asimulia A-Z kilichomfanya Harmonize kutoka usafini WCB. Amtuliza Mondi kwa pigo hilo

Baada ya mzee wa Mondi kukosolewa na mashabiki wake baada ya kuchapisha video ya Harmonize katika mtandao wake wa insta. Sasa Baba Dangote ametokea na mapya na kufunguka A-Z kilichosukumia Harmonize atangaze kuitema lebo ya WCB. Baba Diamond amesema kuwa kutoka kwa staa huyu kutoka lebo sio kitu cha kushtukiza kwani dalili zilikuwepo.

DIAMOND_FATHER__1567597349_80569

Mzee Abdul anahoji kuwa dalili za Harmonize kuwa ana uwezo wa kufanya na kusimamia fiesta zake nje ya chi ni ishara kuwa mwana kashakua na kwa hivo kutoka kwake ni kwema kwa maslahi yake. Anadokeza kuwa labda dogo kapewa ushawishi na marafiki wake ili kufanya uamuzi huo.

Soma hadithi hii:

Babake Diamond Platnumz aposti ngoma ya Harmonize. Aonywa kutengwa(Video)

” Kwanza Naseeb alimuangaikia sana. Kamtufuta kampa sapoti kubwa kamtoa kimuziki,” Mzee Abdul.

“Harmonize sio mtoto. Ukiona mtu anatoka kashakomaa tayari.”

Soma hadithi hii:

Mwendo wa kistaa sana ! Akothee awaacha Lang’ata vinywa wazi

Abdul amesema kuwa simu yake ina nyimbo kibao za WCB na ni shabiki mkubwa sana wa Harmonize.

“Chibu kama Chibu ni mwanangu. Simba tulia bado hujapoteza. Kaa tulia omngeza utapata mwingine zaidi ya huyo. Mwingine alitoka na kama wewe tulia komaa.” Alimtuliza Diamond Platnumz.

Pengo la Harmonize lazibwa usafini WCB. Lavalava abingirisha gari hatari kwenye lebo

Staa wa bongo Lavalava anaonekana kuwa anatengenezwa kuja kuijaza pengo lililoachwa na Harmonize.  Harmonize kwa sasa sio msanii wa WCB na ameanzisha kundi la Konde Gang ambao taarifa zipo kwamba atasaini mastaa wakubwa Tanzania. Ukubwa wake Harmonize unamfanya kutofanya chini ya Wasafi.

Pata hadithi hapa:

McDonald Mariga afunguka kuhusu kustaafu soka. Asema hatumiwi kisiasa

Huenda kuna baadhi ya vijisehemu katika mkataba vinavyombana kufanya kazi za nje na kutanua kama mzazi wake katika tasnia hii Diamond Platnumz. Lavalava anazidi kufanya mauzo mazuri na mkaju wa Saula aliomshirikisha Harmonize.

Stima za ushikaji zinaonekana kuzima ghafla kati ya Harmonize na dogo zake waliokuwa katika lebo moja. Hii ilidhihirika jana baada ya Harmonize ambaye aliwasilisha barua ya kutoka usafini na kuonekana na mikakati ya kuanzisha lebo yake ya Konde Gang.

Pata hadithi hapa:

Rayvanny, Mbosso, Lavalava watakuja kuitema WCB. Afanyeje Mondi

Sifa Salam anazomlimbikizia Lavalava katika mahojiano ni ishara kubwa sasa WCB inapania kumfanya mkubwa ili aje kujaza nafasi hiyo. Staa huyu amezamia insta kuonyesha baraka alizobarikiwa kwa gari ya kifahari.

View this post on Instagram

Kwanza Kabisa Nimshukuru M/Mungu kwamaana Bila Yeye Nisingefika Hapa Nilipo pili Wazazi Wangu Tatu CEO @diamondplatnumz Nauongozi Wote Wa @wcb_wasafi @babutale @sallam_sk @ricardomomo @kameboy_j @mkubwafellatmk kwakuhakikisha Tunapata Haki Zetu Kihalali Ili Nasisi Tuendeshe Maisha Yetu Nakusaidia Familia Zetu NNE Nikushukuru Wewe Shabiki Yangu Uliekuwa Unanisapoti Tangu Nilipoanza Mpaka Sasa Nilipofikia Kijana Wenu Nimeongeza Kausafiri Nahii Sikwasababu Mimi Nitajiri Sana hii Nikwasababu Ya Sapot Yenu Tangu Mwanzo Wa Safari Yangu Ya Muziki Ewe kijana Mwenzangu Dada kaka Nawote Waangaikaji Tusikate Tamaa Mungu Yupo Anatuona Tusali Natufanye Kazi Kwa Bidii Nakumbuka Miaka Mitatu Nyuma Nilkuwa Sina Uwezo Wakununua Hata Baiskel Ila Maombi juhudi Nakumuheshimu Kila Mtu Ndo Nguzo Yamafanikio Tusikate Tamaaa MUNGU ANATUONA #Wcb4Life 💥💥💥💥

A post shared by NINJA (@iamlavalava) on

Harmonize kuitema WCB ni njama ya Mondi kusahaulisha Kiba kwenye tasnia

Idadi kubwa ya mashabiki wa Bongo Fleva mpaka sasa hawaamini kuwa ni kweli staa wa bongo Harmonize kwa kweli ameitema lebo iliyomkuza. Hawaamini ni kosa gani msanii huyu alikosewa ili aamue kufanya uamuzi wa ghafla na wenye uzito kama huo.

diamond-platnumz

Hakuna siku mpaka sasa Harmonize ametokea kusema masaibu yaliyomkuta ili kutoka katika lebo kubwa Afrika Mashariki. Wengi wanahoji kuwa ni njama ya Diamond Platnumz kumfanya Harmonize awe mkubwa ili kutoa dhana ya mashabiki kila mara kumlinganisha na hasimu wake Ali Kiba.

Som hapa pia:

Rayvanny, Mbosso, Lavalava watakuja kuitema WCB. Afanyeje Mondi

Kwa sababu kwa sasa Harmonize anachonganishwa na baadhi ya vyombo vya habari kuwa ni mkali kulika Diamond. Wema Sepetu aliyekuwa mpenzi wa Diamond Platnumz siku za jadi aliwahi kunukuliwa akisema kuwa dogo Konde Boy yuko sawa kimuziki kushindi Diamond.

Sasa mashindano yanatengenezwa na vyombo vya habari kati ya Harmonize na Diamond. Jambo kama hili huenda likasababisha Ali Kiba kupotea masikioni mwa watu na ata kukosa kuonekana mbishi wa karibu wa nyota na staa anayemiliki lebo ya Wasafi.

Som hapa pia:

Babake Diamond Platnumz aposti ngoma ya Harmonize. Aonywa kutengwa(Video)

Je, unaamini hii inaweza kuwa sababu ya Harmonize kuitemana na WCB na mazingira yatengenezwe ya chuki kumtoa Kiba kwenye tasnia ya muziki. Tupe maoni.

Rayvanny, Mbosso, Lavalava watakuja kuitema WCB. Afanyeje Mondi

Harmonize ndiye kifungua mimba cha lebo kubwa Afrika Mashariki ya WCB iliyopo mjini Dar nchi jirani ya Tanzania. Amekuwa mkubwa kwa kupiga nyimbo hatari na kushirikisha mastaa wakubwa kutoka nchi jirani kama Uganda na Nigeria kati ya nyinginezo.

Matamasha anayoyafanya ni makubwa sawa na bosi wake Diamond Platnumz. Dogo ana mpenzi wa haiba ya juu sana Sarah. Ana walinzi sawa na idadi ya Diamond. Kumewahi kutokea vyombo vya habari nchini Tanzania zinazowalinganisha wawili hawa.

Soma hadithi hii:

Wakala wa sensa ahusika densi na watoto wadogo. Video yavuja na kusambaa Twitter

 Diamond Platnumz alipuuzilia mbali kauli hii na kusema media zinajaribu ziwezavyo kukuza ubifu kati yake na wasanii aliowatengeneza. Juzi kati, Harmonize amedondosha barua na kuwapa kwaheri WCB.

Ila je, unaamini kuwa alichokifanya ni kitu kibaya. Mwana anapokua anatakiwa kujitenga mbali na babake mzazi na kuanzisha familia. Ndo maana staa huyu akaanzisha familia ya Konde Gang.

Soma hadithi hii:

Babake Diamond Platnumz aposti ngoma ya Harmonize. Aonywa kutengwa(Video)

Hii ni dalili tosha kuwa wasanii waliopo WCB siku moja watakuja kuwa wakubwa wote kama Diamond Platnumz na watataka kuwa huru kuanzisha lebo zao nje ya Wasafi. Kwa mfano, Lavalava ameanzisha Bite Gang, taarifa pia zipo Rayvanny anamiliki studio yake na ana wasanii dogo zake anaowapa mafunzo ya kuchana.

Soma hadithi hii:

Macdonald Mariga atua ofisi za Jubilee kwa mbwembwe. Jubilee itampa tikiti ?(Video)

 Diamond sasa anapaswa kuamua kati ya umeneja wa lebo na kuimba atachagua kipi? Kwa sababu wasanii waliopo WCB watatanua na kuanzisha lebo zao. Juhudi alizowekeza katika wasanii hawa ingawa zinamletea faida kuu, wasanii hawa watakua na hata kumshinda katika charts kubwa za muziki duniani.

Diamond ni mkubwa kweli. Anamiliki biashara kubwa kama runinga ya Wasafi, redio na nyinginezo. Ni msanii mkubwa Afrika na duniani. Ila achague afanye kitu kimoja. Hakuna mtu aliyewahi kufaulu katika mambo mengi. Una kauli gani kwake Diamond?

Babake Diamond Platnumz aposti ngoma ya Harmonize. Aonywa kutengwa(Video)

Mzee wa Mondi amejipata kukosolewa na mashabiki wake baada ya kuchapisha video ya Harmonize katika mtandao wake wa insta. Kutoka Harmonize atangaze kuitema lebo ya WCB, stima za ushikaji zimekata ghafla. Ushikaji wa zamani wa kuposti kazi za msanii Harmonize hazionekani tena.

Soma hadithi hapa:

Mwendo wa kistaa sana ! Akothee awaacha Lang’ata vinywa wazi

Harmonize mwenyewe aliposti ngoma ya Mbosso aliofanya na Reekado. Hali kadhalika, dogo alipost ngoma yake Rayvanyy Remix Tetema ila wawili hao hawakupost Inabana yake na Eddy Kenzo.

Sasa mzee wa Diamond Platnumz huenda hajapata kuelewa upepo huu wa ubifu na anashobokea kazi za staa huyu kwenye mitandao ya kijamii.

“Mzee utatengwa 😅😂😂😅😅😜, “alisema shabiki mmoja.

Soma hadithi hapa:

Macdonald Mariga atua ofisi za Jubilee kwa mbwembwe. Jubilee itampa tikiti ?(Video)

 Harmonize kwa sasa sio msanii wa WCB na ameanzisha kundi la Konde Gang ambao taarifa zipo kwamba atasaini mastaa wakubwa Tanzania. Ukubwa wake Harmonize unamfanya kutofanya chini ya Wasafi.

Huenda kuna baadhi ya vijisehemu katika mkataba vinavyombana kufanya kazi za nje na kutanua kama mzazi wake katika tasnia hii Diamond Platnumz.

Rayvanny na Mbosso wampa shavu kavu Harmonize. Ushikaji haupo tena

Stima za ushikaji zinaonekana kuzima ghafla kati ya Harmonize na dogo zake waliokuwa katika lebo moja. Hii ilidhihirika jana baada ya Harmonize ambaye aliwasilisha barua ya kutoka usafini na kuonekana na mikakati ya kuanzisha lebo yake ya Konde Gang.

Soma hapa:

Harmonize na Konde Gang ni biashara za lebo ya Wcb. Balaa kubwa kwa Kondeboy

Harmonize aliposti ngoma za Rayvanny na Mbosso, Remix ya Tetema na Shilingi. Kama ilivyo desturi, wawili hawa wangeposti ngoma yake mpya na Eddy Kenzo Inabana kama kuonyesha kuipa nguvu sanaa yake ila wakakosa.

Soma mengine hapa:

Tsunami ya Raila kufagia wabunge wa TangaTanga. Ruto aidharau Tsunami

Harmonize ameanzisha lebo yake Konde Gang ambayo anapania kuwasaini mastaa wengine wa muziki. Aidha, katika mahojiano Meneja wa WCB Babu Tale alisisitiza kuwa chochote Harmonize atakwenda kuanzisha kinachohusiana na burudani, kutakuwepo na pato itakayokuwa inaingia Wasafi.

Soma mengine hapa:

Inspekta Mwala anusurika kichapo cha umati. Agonga na kuua mtu papo kwa hapo

Lebo ya WCB imedondosha ngoma Shilingi ya Mbosso akimshirikisha Reekado masaa 5 baada ya Harmonize kutoa. Hii inaweza kutafsiriwa kama njia moja ya kufunika ngoma ya Harmonize. Mondi pia anatarajiwa kudondosha ngoma yake muda usio mrefu ili kuonyesha ubabe katika tasnia ya muziki wao.

Harmonize na Konde Gang ni biashara za lebo ya Wcb. Balaa kubwa kwa Kondeboy

Baada ya mojawapo ya mameneja wa lebo kubwa Afrika mashariki na Afrika ya kati WCB Sallam kutangaza kuwa msanii Harmonize yupo katika mikakati ya kutemana na lebo hiyo, Babu Tale sasa anasema kuwa swala la Harmonize kutoka katika WCB haiwapigi mshipa katu.

View this post on Instagram

👽

A post shared by KONDEBOY (@harmonize_tz) on

Soma hii hapa:

Chipukeezy atemwa na runinga ya Ebru. Mbona figisu figisu?

Kwa mujibu wa uongozi wa lebo ya Wasafi, mkali wa Never give Up alidondosha barua akitaka kubanduka rasmi. Balaa nzito inaonekana kutokea baada ya taarifa kuwa huenda staa huyo akawa amesaini mkataba wa miaka 15.Hii ina maana kuwa kwa nafsi yake hayupo Wasafi ila anabanwa na mkataba aliousaini. Kulingana na Babu Tale, mkataba wao na msanii huyu unadokeza kuwa chochote Harmonize atakachofanya kinachohusisha burudani au muziki ni biashara yao.

Soma hapa hadithi nyingine:

Chipukeezy apoteza kazi Ebru. Mastaa nchini wamtuliza instagram

 Kwa kauli hiyo, endapo Konde Boy atasaini msanii mpya katika kikundi atakachokwenda kuanzisha Konde Gang ,WCB  itakuwa inatengeneza hela kupitia kikundi hicho.

“Sioni ubaya wa kuweka familia ndani ya familia.mkataba wetu sisi unamface Harmonize. Ukimzungumia Harmonize ile ni biashara yetu kulingana na mkataba wetu. Akiweka chochote kinachohusiana na muziki nacho kinaingia WCB. Anavyotanuka huko kwingine bado kuna mrija unaingia WCB.” Babu Tale

Soma hapa:

Chipukeezy avuruga mkataba akiwasaidia staa chipukizi. Ona anachotakiwa afanye