Harmonize aonyesha dalili za kupoteza umaarufu. Mashabiki wampa shavu kavu (+Video)

Nyota ya staa wa bongo Harmonize kwa sasa anaashiria dalili za kupoteza umaarufu wa kimuziki na ustaa.

Hii ni baada ya yeye kuingia katika ukumbi wa kutazama mechi kati ya Taifa stars ya Tanzania na timu ya kitaifa ya Burundi.

Soma hadithi nyingine hapa:

Hela iliyopotea ATM ya Standard Chartered na G4S. Jinsi simu zilinaswa Thogoto

Harmonize na mpenzi wake Sarah walisimama na kuanza kunengua nyimbo za staa huyu.

Je, huenda Harmonize anapoteza ustaa wake baada ya kuitema WCB?

69234512_128762718473963_5693449161584447397_n__1568104638_65557

Lebo hii inaaminika kuwa kubwa Afrika mashariki na mashabiki wanapenda nyimbo za mastaa wanaofanya chini yake.

Soma hadithi nyingine hapa:

Susan afichua A-Z siri za Willy Paul. Kuchepuka na utumizi wa dawa za kulevya

 Hii inajiri baada ya KondeBoy kufanya harusi bila kuwashirikisha mastaa wakubwa Tanzania hususan kutoka familia aliyokulia ya Wasafi.
Harmonize alipopigiwa kudhibitisha iwapo ni kweli alifanya harusi au ni shughuli ya kushoot video mpya hakuweza kupatikana katika laini ya simu.

Wengi wanadhania labda staa huyu alikuwa location kurekodi video ya ngoma mpya.

Soma hadithi nyingine hapa:

Ogopa sana hawa watu maishani ! Chunga pesa zako kabla ukopeshe

Ila je, Harmonize anaweza kufanya harusi bila kuwashirikisha waliokuwa marafiki wake Diamond Platnumz, Rayvanyy na Lavalava na wengineo?

Swali hili linaweza kujibiwa kwa dalili za ushikaji kuzima kati ya wasanii hawa.

Soma hadithi za mwandishi huyu

 

 

Rich Mavoko ‘aheshimu’ Harmonize kwa kutoka wasafi

Rich Mavoko akataa madai kuwa wimbo wake mpya ‘Babilion’ alikuwa amemwimbia Harmonize.

mavoko

Kwa ufupi, mwanzamziki huyu Rich Mavoko, aliwaambia mashabiki wake wasikazane kuuchambua wimbo wake Babilion wakidai kwamba alimwimbia Harmonize baada ya kutoka lebo ya Wasafi, kwani huo ni uongo mtupu.

Wasafi Records ni lebo ya muziki iliyoanzishwa na staa Diamond Platnumz ambaye pia amebobea kwa mziki wake.

Dennis Itumbi Ashtakiwa kwa kutogharamia ulezi wa mtoto wake

Rich Mavoko ndiye aliyekuwa wa kwanza kutoka Wasafi, baada ya kuwa na vurugu kati yake na meneja wa lebo hiyo.

Mbali na hayo, Rich Mavoko alisema kuwa ,alikuwa asharekodi wimbo wake, Babilion na hakujua kuwa wimbo huo ulikuwa umeambatana na wakati ambao Harmonize alikuwa ametoka Wasafi.

“I had already recorded that song and I didn’t know the timing of the song went hand in hand with Harmonize leaving WCB,” alisema.

‘Sikufa hata baada ya kunywa sumu’ Bwana Kinoti Gatobu

Zaidi ya hayo, Mavoko alisema kuwa, alitoa wimbi wake na mashabiki ndio walioandika maoni yao kuhusu Harmonize, lakini kwake yeye, wimbo huo unahusu maisha tu.

“I gave people the song but they wrote a caption to it. It’s all about the fans’ comments because I do read them. The song is generally about life.”alisema.

Vile vile, Mavoko amesema kuwa, anaheshimu uamuzi wa Harmoize kuamua kutoka kwenye chama cha Wasafi, na hana mambo mengi ya kusema.

“I respect Harmonize’s decision. I can’t say more about it.”

Hata hivyo, maneno ya wimbo huu unaonyesha wazi kuwa, Rich Mavoko ameiimbia chama cha Wasafi.

Wakenya mashuhuri waliochukua talaka ili waokoe maisha yao!

Konde Gang ya Harmonize yaachilia mdundo. WCB yadondosha ya Mbosso

Staa na fundi wa muziki nchini Tanzania Harmonize amedondosha ngoma ya kwanza Inabana tangu adondoshe barua ya kuvunja mkataba wake na lebo inayoongozwa na Diamond Platnumz. Ngoma hii iliyochapishwa kwenye mtandao wa YouTube masaa 10 yaliyopita amemshirikisha Eddy Kenzo kutoka nchi jirani ya Uganda.

Soma hapa:

Eric Omondi atokwa na povu insta. Afunguka jinsi Ebru ilivyomtesa Chipukeezy

Harmonize ameanzisha lebo yake Konde Gang ambayo anapania kuwasaini mastaa wengine wa muziki. Aidha, katika mahojiano Meneja wa WCB Babu Tale alisisitiza kuwa chochote Harmonize atakwenda kuanzisha kinachohusiana na burudani, kutakuwepo na pato itakayokuwa inaingia Wasafi.

Hii ni kufuatia makubaliano katika mkataba wao na staa huyu ambao unatajwa kama ulikuwa wa miaka 15. Katika mahojiano hayo, Tale alitoa tamko kuwa mtu yeyote hawezi siku moja dhubutu kung’ara zaidi ya bosi wake. Hii ni ishara kuwa labda kinachopelekea mtifuano katika Wasafi na Konde Boy huenda dogo alionyesha makali ya kumtoa Diamond Platnumz kwenye game.

Soma hapa:

Inspekta Mwala anusurika kichapo cha umati. Agonga na kuua mtu papo kwa hapo

Kando na kuchonganishwa na vyombo vya habari, Harmonize anapata kero kubwa kwa mashabiki katika mitandao ya kijamii baadhi yao wakihapa kuzima stima za ushabiki kwake.

Lebo ya WCB imedondosha ngoma Shilingi ya Mbosso akimshirikisha Reekado masaa 5 baada ya Harmonize kutoa. Hii inaweza kutafsiriwa kama njia moja ya kufunika ngoma ya Harmonize. Mondi pia anatarajiwa kudondosha ngoma yake muda usio mrefu ili kuonyesha ubabe katika tasnia ya muziki wao.

 

Harmonize aiandikia barua Wasafi akitaka kujiuzulu kirasmi

Msanii Rajab Abdul Kahali kwa jina maarufu Harmonize hatimaye ameandika rasmi kwa kundi la Wasafi Classic Baby WCB akitaka kandarasi yake kuvunjwa. Akizungumza na runinga ya Wasafi, afisa mkuu mtendaji wa WCB Sallam SK alias Mendez alifichua kwamba msanii huyo ameandika rasmi kwa kundi hilo akisema anataka kujiondoa.

Dr Fred Matiang’i aamrisha mabaa yote yafungwe tarehe 24 na 25

 Sallam amesema kwamba kwa sasa moyo wa msanii huyo haupo tena na WCB na ameitisha mkutano na usimamizi wa WCB katika harakati yake ya kukubaliana na hatua hiyo.

“Harmonize kwa sasa moyo wake haupo WCB, kimkataba bado yupo. Kwa nini nasema hivo? Harmonize ameshatuma barua ya maombi ya kuvunja mkataba na yuko tayari kupitia vipengele vyote vya sheria kusitisha mkataba wake na ni kitu ambacho tumependezewa nacho. Yeye mwenyewe ameridhia na ameomba kikao na uongozi,” alisema Sallam.

Harmonize na aliyekuwa meneja wake Mr. Puaz

Hatahivyo amesema kwamba muimbaji huyo wa wimbo ‘My Boo’ bado yupo katika mkataba wa WCB na kusisitiza kwamba ingekuwa heri iwapo Harmonise angetoka bila kuzua zahama.

“Sisi kama taasisi ya WCB tuko radhi kwa kile ambacho ataamua, hatuwezi kupinga chochote. Akiamua kufuata maelezo hayo ana baraka asilimia 100 za Wasafi na akitaka kushirikiana na Wasafi wakati wowote tuko wazi. Wajua unapoondoka kwa mazingira mazuri inasaidia uhusiano usalie pale pale,” alizungumza katika .

Mahakama yakosoa DCI kwa kumkamata bwenyenye, Humphrey Kariuki

 Kulingana na Sallam, tangazo hilo kwamba Harmonize amejiondoa rasmi WCB litatangzwa rasmi baada ya mchakato wote huo kufuatwa na kukamilishwa

“Siku ambayo atatoka kimkataba tutaangazia umma. Kwa sasa hivi ameandika barua. Nafasi yake imetoka WCB. Kufanya kazi ndani ya WCB, ndani ya moyo wake, haiko radhi tena,” aliongezea Sallam.

Msanii wa bongo Fleva Harmonize

Sallam amesema katika tamasha la wasafi lililofanyika mjini Mwanza, kwamba Harmonise alitumia usafiri wa kibinafsi kufanya baadhi ya mambo yaliotoa tafsiri kwamba amejitenga.

”Alitufanyia mambo mengi ambayo hatukutarajia ikiwemo kumsimamisha msanii ambaye hana kibali chetu. Sisi hatupendi kuleta matabaka katika kundi letu lakini kama ilivyokuwa Harmonise aliingia kivyake, sio kwamba Diamond hawezi kufanya hivyo au Rayvany ni ile heshima kwamba WCB ina umoja na kwamba tunafuata sheria zilizopo”.

”Hatahivyo tumependezwa na hatua yake kwa sababu labda kuna vitu ameona akivifanya atafika mbali”, amesema Sallam akinukuliwa na gazeti la Mwananchi Tanzania.

Kuhusu kujitenga na wenzake Sallam amesema kwamba: Hili jambo sio sawa kulingana na maudhui ya tamasha hilo.

Maudhui ya Wasafi festival ni umoja. Msanii akiamua kuacha kuandamana na wasanii wenzake ambao wapo katika tamasha ni kwenda kinyume.

Meneja huyo amewaomba radhi wasanii wote walioshiriki tamasha la Mwanza kutokana na Harmonise kufanya jambo hilo na kwamba uongozi wa Wasafi haukuwa na taarifa.

Harmonize amsifu rais Pombe magufuli kwa wimbo mpya

Harmonize amekuja na lingine jipya na raundi hii ameamua kumsifu rais wa tanzania John Pombe Magufuli kwa njia spesheli baada ya kuachia kibao kipya kwa jina la ‘Magufuli’. Harmonize amefanya jambo hilo licha ya kuwepo na mzozo baina ya lebo ya WCB na rais huyo mwaka uliopita.

magufuli

Kwenye wimbo huo, Harmonize anamshukuru Raisi kwa mambo aliyofanya tangu achukue hatma za uongozi wa taifa la Tanzania. Elimu ya bure kwa watoto, ujenzi wa barabara na hata kuimarisha utendakazi wa wafanyakazi wa serikali.

Pamoja na hayo, Harmonize anamwahidi Magufuli kumpigia kura mwaka ujao kwenye uchaguzi mkuu wa jamuhuri ya Tanzania.

Mume wangu alinilazimisha kutoa mimba kisha akanifukuza

Kabla ya kuachia kibao hicho, Harmonize alimshukuru Magufuli kwenye mtandao wake wa Instagram
“Hebu Leo Tuzungumze Serious Kidogo Ndugu Zangu Hili Swala Linahusu Maendeleo Ya Taifa letu Ambalo Manufaa Yake Ni Faida Kwa Vizazi Na Vizazi…!! Ukiwa Kama Mtanzania Wa Kawaida…!!!! Nikitugani Unachojivunia Katika Utendaji Wa Serikali Yetu Ya Awamu Ya (5) …??? Au Kitu Gani Ambacho Rais Wetu MHE. John Pombe Magufuli Amekifanya Ambacho Unatamani Siku Ukipata Nafasi Ya Kukutana Nae Umwambie Au Umpongeze…?????? .”

Hata hivyo, Harmonize sio mwanamziki wa pekee kumshukuru Magufuli kwani pia  mkubwa wake Diamond Platinumz ndiye aliyetunga kibao kinachotumika na na chama cha mapinduzi huko nchini Tanzania ili kumsaidia Magufuli kupata urais kwa mara ya pili.

Harmonize ni mmoja wa wanamuziki tajiki nchini Tanzania na hivi juzi alipata tuzo la dhahabu kutoka kwa kampuni ya Youtube baada ya kufikisha wafuasi millioni moja.

Soma mengi hapa

Harmonize amzawadi msanii mwenzake na gari jipya

Msanii wa Wasafi, Harmonize amemzawadi msanii mwenzake na gari baada ya kufahamu kuwa msanii yule alikuwa anayapitia mambo magumu.

“Nilianza kuvuta madawa nikiwa kidato cha kwanza,” Zaituni afichua

Siku ya Jumatatu Harmonize, alimwacha mwimbaji Abubakar Kitwala anayejulikana kama Q Chillah akidondokwa na machozi baada ya kumzawadi gari jipya na kumuahidi kufanya kazi ya kimziki pamoja naye.

Akiongea na vyombo vya habari, Harmonize alisema kuwa alimsaidia Q Chillah kwani aligundua kuwa alikuwa anapitia mambo magumu.

Waziri wa fedha Henry Rotich afikishwa mahakamani

Harmonize aliendelea na kusema kuwa Q Chillah alimhamasisha na kuwa wataifanya kazi pamoja.

Soma mengi hapa

20686642_751553508382684_2895548908082036736_n

Q Chillah

66183719_372359300146737_7689680652099039708_n (1)

gari aliyozawadiwa

 

 

Orodha: Tazama mastaa wanaoishi chumba kimoja bila kuoana

Kuna mastaa wengi ambao ni vioo vya jamii wanazowakilisha duniani. Waimbaji hawa wa muziki ni wapenzi na wanaishi pamoja ila harusi au ndoa yao hawajaweza kuifanya. Tunakusogezea hapa baadhi yao:

Soma hadithi nyingine hapa:

Miyeyusho ya insta! Willy Paul ampiga kijembe shabiki

Khaligraph Jones na Georgina Muteti

trgfg

 

Papa Jones na mpenzi wake walijaliwa mtoto wa kike juzi kati . Staa huyu anatamba na kibao Leave Me Alone

Chipukeezy na Kibanja

chipukeezy-and-kibanja3

Wawili hawa walitangazaja uhusiano wao mapema mwakani.

Henry Desagu na Jackie Mbugua

desagu-5

Wawili hawa wanajihusisha na ucheshi katika mitandao ya kijamii. Juzi kati Desagu alifunguka kuwa huwa anafurahi sana Jackie akimvalisha nguo kabla atoke kwenye mikutano kuashiria wanaishi pamoja.

Soma hadithi nyingine:

“Nitwange? Nikule? Nitetemeshe? Ama ni kanyage Hamisa Mobeto”- Eric Omondi

Burna Boy na Stefflon Don

Capture

Harmonize na Sarah

harmonize

Uhusiano wa Konde Boy na Sarah ni wa karibu zaidi. Harmonize ameweza kuchora bonge la tatoo la mwanamke huyu kwenye mkono wake. Sarah amehamia Tanzania ili awe karibu na staa huyu.

Diamond Platnumz na Tanasha Donna

errs

 

Wawili hawa wanasubiria mtoto hivi karibuni.

Mr Seed na Nimmo Gachuiri

dfvfv

 

 

 

 

Harmonize awanunulia wazazi gari mpya

Staa wa muziki Tanzania Harmonize jana amewatunuku zawadi ya kifahari wazazi wake. Msanii huyu ambaye anafanya vizuri na nyimbo kubwa ya Never Give Up ame3dondosha nyimbo mpya na mshikaji wake wa karibu Dully Sykes.

Katika wimbo wa Never Give Up, Konde Boy anafunguka kuhusu maisha yake ya awali. Zaidi ya hapo pia anaeleza jinsi babake mzazi alikwazika alipoanza kuimba.

Harmonize ni kati ya mastaa katika lebo ya WCB wanaofanya vizuri katika tasnia ya muziki Afrika mashariki na Afrika ya kati. Mkurugenzi wa lebo hiyo Diamond Platnumz amenukuliwa akisema kuwa harmonize anaingiza hela nyingi katika muziki na uwekezaji katika Zoom production na Kenny.

Tazama hapa magari mapya kwa wazazi wake:

View this post on Instagram

Best Couple In My Life..!!! 🤴👸

A post shared by KONDEBOY (@harmonize_tz) on

Rich Mavoko : Sioni mtu wa kuomba msamaha WCB

Staa wa muziki wa Bongo fleva Rich mavoko amedokeza kuwa haoni wa kumwomba msamaha katika lebo ya WCB. Mavoko alitoka ghafla katika lebo hiyo inayoongozwa na nyota na mwanamuziki mkubwa Afrika Diamond Platnumz.

Wasanii wengine walio chini ya usimamizi wa lebo hiyo ni pamoja na Harmonize, Rayvanyy, QueenDarleen na mkali Mbosso.

Soma hadithi nyingine:

HopeKid : Nilifukuzwa kanisani kisa skendo yangu na DK kwenye Beat

download

Mgogoro na mvutano mkubwa ulifuata kuhusu mtakaba aliokuwa ameingia na usimamizi wa lebo hii ya Wasafi. Kulingana na Mavoko, mkataba wake na WCB ulivurugika kipindi baadhi ya vitu alivyotaka havikufanywa na lebo hiyo.

Soma upate uhondo hapa:

Hopekid reveals student in threesome scandal with DK Kwenye Beat was suicidal

” Mkataba bado haujaisha ata kama nimetoka. Kuna baadhi ya vitu havikwenda sawa na nilivyotaka mimi. Nilikaa sana na nyimbo na ambazo nilitakiwa nizitoe ila sikuweza. Kuna kipindi mamangu alinipigia kuniulizia mbona sitoi nyimbo. Sikuona kabisa maisha mazuri ya usoni nikiwa WCB.” alisema Mavoko.

Staa huyu anayetamba na nyimbo mpya inayofanya vizuri Usiguze amesema kuwa hawezi kurudi lebo aliyotoka katika mahojiano na kituo kimoja nchini Tanzania. Kuhusu kuomba msamaha na kukubali kurudi katika lebo hiyo kubwa Afrika mashariki, staa huyu alisema hawezi kabisa.

“Nilipoingia WCB sikuona msanii mkubwa hapo ukiweka kando mkubwa wa lebo hiyo. Naomba msamaha wa nini? Kosa gani nilifanya mimi? Sina matatizo na yeyote WCB.”

 

lucy2

Diamond Platnumz na babake wakutana na kuzima tofauti zao

Msanii na staa mkubwa Afrika Diamond Platinumz ameweza kukutana katika redio ya Wasafi FM na babake na kuonekana kuzima tofauti zao za awali.

Mzee Abdul alimtaliki mkewe miaka ya awali kijana huyu akiwa kidato cha kwanza. Naseeb alitangulia kwa kusema kuwa ubaridi unaonekana kati yao na baba mzazi umechochewa na kutokua pamoja kwa kipindi kirefu.

“Kiukweli siwezi kusema nina ukaribu na mzee. Hatujakuwa na bond kubwa naye ila mimi sina matatizo naye…tukiwa kuna issue tutakutana naye tuongee” Diamond alisema katika mahojiano.

diamodn and his parents
Diamond Platnumz na wazazi

Ukaribu wa Naseeb na mamake umeonekana kwa muda mrefu kunoga huku babake akionekana kusahaulika na msanii huyu.

Katika kitengo cha Block 89 cha shoo ya redio ya Wasafi, babake Platnumz anaonekana kutokea ghafla katika mahojiano  ya mtoto wake na kituo hiki.

Mwanae anamiliki chumba hiki cha habari pamoja na runinga bila kusahau lebo ya Wasafi (WCB)  inayojivunia kusimamia wasanii wakubwa Afrika mashariki na Afrika ya kati kama Rayvany,  Harmonize, Lavalava, Mbosso na Queen Darleen.

Baada ya kuugua kwa muda mrefu, babake Chibu alipata ufadhili kutoka kwa mtendawema aliyeguswa na hali yake ya ugonjwa.

diamondplatnumzinyellow
Diamond

Yule sio mtoto wangu kunizaa ila niseme kuna watu hawana wazazi na wana hela.Aliniangalia katika mitandao ya kijamii katika hali sio nzuri na akatokea kutoa usaidizi”

Diamond anadai kuwa baadhi ya vyombo vya habari vinamtumia babake kupata ufuasi mkubwa wanapokwenda kumhoji kuhusu tofauti zao.

“Naamini vyombo vya habari vinakuzakuza na kutengeneza matatizo kati yangu na baba.”

diamond platnumz madale
Bongo singer Diamond Platnumz

Kwa upande mwingine anaona kuwa babake anamweka katika kicheko kwa watu wengi hususan wapinzani wake anapoonekana kama hamsaidii mzazi.

Babake alimwomba msamaha na wote kuonekana wameridhiana katika mazungumzo yao

Kama nimekukosea naomba unisamehe na ujaribu kuangalia utanisaidia vipi mimi babako.”

Diamond alionya kuwa kuna baadhi ya vyombo vya habari vinavyomtumia babake kwa maslahi yao na hawamsaidii. Mkali huyu wa kibao kipya The one  alimaliza kwa kuomba msamaha.

“Well mimi siwezi kusema nina  matatizo na babangu. Naamini utofauti wake na mama unafanya tuwe hatuna ukaribu…Naomba anisamehe pia kwa sababu sijui akiwa na mama walikosana kwa misingi gani.”

Also read more here