Inspekta Generali aanza uchunguzi wake katika idara ya uhamiaji

Inspekta Generali wa polisi Hillary Mutyambai ameelekezwa kuanza uchunguzi kuhusiana na madai ya uhalifu kutekelezwa katika idara ya uhamiaji.

Runinga ya Citizen ambayo ilifichua uhalifu huo uliobandikwa jina “Westlands undercover” ulidai kwamba maafisa katika idara ya uhamiaji na mashirika mengine ya usalama wa serikali walipanga kufukuza familia moja ya kihindi ili waweze kunyakua mali ya familia hiyo.

Barua ghushi ya kuua Ruto, Dennis Itumbi akabiliwa na mashtaka mapya

 Katika taarifa siku ya jumanne, msemaji Wangui Muchiri alisema Mutyambai atatoa ripoti ndani ya siku 14.

Muchiri alizidi kueleza kuwa yeyote yule pamoja na runinga ya Citizen aliye na ushahidi kuhusu suala hilo, wanaweza kufikisha ripoti hiyo kwa mkurugenzi wa kitengo cha mambo ya ndani.

Wanaweza pia kuwasilisha ushahidi huo kwa huduma ya kitaifa ya polisi, Charlton Muriithi ambaye anaweza kufikiwa kwa nambari 0798474619 au barua pepe: @nationalpolice.go.ke

Katika ufichuaji huo, kulikuwa na mpango ambao ulikuwa umepangwa vizuri kwa malengo ya kumfukuza mfanyibiashara huyo na dadake.

PATANISHO: ‘I am busy muache kunilazimisha kuzungumza!’ – Paul

 Madai hayo yamemtaja naibu wa inspekta wa polisi Edward Mbugua, mkuu wa hudumu za uhamiaji Alex Muteshi, mbunge wa Makadara George Aladwa, maafisa wa DCI, na mawakili.

Ufichuaji huo ambao ulieleza na kuweka mambo wazi kuwa wahusika hao walikuwa na lengo la kuondoa familia hilo humu nchini ili wabadilishe umiliki wa mali inayomilikiwa na Dilip Bakrania na dadake Hansa Bakrania.

 

 

Mpelelezi mwingine kuwa mkuu wa huduma ya polisi

Rais Uhuru Kenyatta jana aliweza kumteuwa mpelelezi mwingine ili kuchukua nafasi ya IG Boinnet kama Inspekta mkuu wa polisi. Hillary Mutyambai atakua mkuu wa huduma ya polisi kama ataweza kukubaliwa na bunge.

Hii inaweka kupumzika uvumi nani atakaye fanikiwa kuchukua nafasi ya Boinnet, Mutymbai ni naibu wa mwelekezi katika kitengo cha kumpambana na ugaidi na uratibu wa kitaifa na huduma za akili.

Hillary Mutyambai
Hillary Mutyambai

Mutyambai huwa anajiunga na baadhi ya kundi la wapelelezi, ambalo limeteuliwa kuongoza taasisi muhimu wakati wa umiliki wa rais Uhuru.

Boinnet, DPP Noordin Haji, na mkurugenzi mkuu wa polisi EACC Twalib Mbarak wote walikuwa maafisa wa polisi wa akili.

Muhula na wakati wa miaka nne ya Boinnet ofisini iliweza kuisha Jumatatu.

TBT: When Raila Odinga Met With Didier Drogba And Nicholas Anelka

Huduma ya polisi ya kitaifa iliuliza rais Uhuru ndani ya siku 14 baada ya nafasi kutokea katika ofisi ya inspekta mkuu aweze kumteuwa mtu kwa ajili ya nafasi hiyo, na kisha kupeana jina lake katika bunge.

Kama ilivyo ada ya mkurugenzi mkuu, Boinnet atakuwa katibu tawala wa wakuu katika wizara ya utalii na wanyamapori.

Pia rais aliweza kumteuwa Wycllife Ogalo kuchukua nafasi ya Isaiah Osugo kuwa mkuu wa jumla wa idara ya gereza, Osugo ambaye ni mpelelezi wa kazi aliweza kuwekwa katika idara hiyo mwaka wa 2008.

President Mwai Kibaki aliweza kumtoa katika idara ya DCI.

Jana pia rais alimteuwa Vincent Loonena kuwa mkurugenzi mkuu wa huduma ya ulinzi ya pwani ya Kenya, ni idara ambayo iliweza kuzinduliwa mwaka jana Novemba.

Bride dies from a mystery illness on honeymoon just six days after wedding

Huduma hiyo ni ya kulinda maeneo ya maji ya nchi dhidi ya ugaidi, dawa za kulevya, uvuvi haramu na miongoni mwa uhalifu mwingine.

John Wangui Waweru atakuwa mkurugenzi mkuu wa huduma ya wanyamapori wa kenya (Kenya Wildlife Service), alichukua nafasi ya prof Charles Musyoki.

Waziri wa utalii Najib Balala alimteuwa Musyoka mwaka jana Julai wakati vifaru 11 waliweza kufariki walipokuwa wakihamishwa kutoka Nairobi.

Pia walioteuliwa katika tume ya kitaifa ya huduma ya polisi na waliokubaliwa na bunge ni Eliud Kinuthia atakaye chukua nafasi ya Johnston Kavuludi kama mwenyekiti.

Wengine ni miongoni mwa Lilian Kiambaa, Eusebius Laibuta, Naphtali Rono, Alice Owala na John Moiyaki.