Peter kutoka Machakos alituma ujumbe akiomba apatanishwe na mkewe wa miaka kumi,bi Irene ambaye alitoweka na kurudi kwao, tangia mwezi wa Julai.
“Mtoto wetu alichomeka na baada ya kumpeleka hospitalini akakaribia kupona, na mama mkwe akamuambia mke wangu arudi nyumbani na mtoto ili amuone.
Baada ya kwenda kule mama mkwe akasema kuwa nafaa kwenda kule na wazazi wangu. Tangia wakati ule hata simu zangu hashiki na isitoshe alirudi akabeba watoto wote.” Alijieleza Peter mwenye umri wa miaka 32.
“Kama angejua yeye ni baba mtoto mbona hakuja kututembelea?” Aliuliza bi Irene huku akidai kuwa kwa mda wa wiki mbili ambapo mtoto alikuwa amelazwa mumewe hakuwai watembelea hata mavazi ya kubadilisha hawakuwa nayo.
Sasa baada ya yale mamangu aliniambia nisirudi kwake kamwe kwani alikasirishwa na yale.” Aliongeza.
Hospitali za kibinafsi na za umma zinachunguzwa kwa madai kwamba zimekataa kutoa huduma za dharura kwa wagonjwa wanaokimbizwa katika taasisi hizo.
Gavana wa Nairobi Evans Kidero amesema hospitali zitakazopatikana na hatia, hazitopewa leseni mpya za kuhudumu. Hii ni baada ya mwanamme mmoja kuaga dunia wiki jana baada ya kungoja kwa zaidi ya saa 18 ili kupewa huduma za dharura katika hospitali ya kitaifa ya Kenyatta na zingine za kibinafsi.
NOW PLAYING
Loading Track...
Loading Artist...
SEND A SHOUTOUT!
to Gidi and Ghost
Connect with us!
PROMOTIONS
Kiss TV’s The Search Finally Crowns The Winner Of The Competition
After a long and hard search for Kenya’s most talented and shining...