Ilikuaje:Siwafahamu wazazi wangu tangu utotoni mwangu-Leila Chepkirui

Leo katika kitengo cha ilikuaje Leila Chepkirui alieleza jinsi alivyolelewa na watu tofauti huku akihishi mtaani kwa kukosa wazazi wake na jinsi mwanawe alijiunga na kundi la Alshabaab.

“Hadi sasa sijui wazazi wangu halali, hii ni kwa sababu wazazi wangu walikuwa wnataka kuniavya lakini yaya ambaye alikuwa ameandikwa kwetu alimkataza mama yangu

Ilikuaje: Papa Dennis aliuawa- asema nduguye

Alimwambia anizae na ampe mtoto, sijui kwanini au makubaliano waliokuwa nayo wakati huo, baada ya hapo nyanya huyo alinichukua na kuanza kunilea

Baada ya muda nyanya aliaga dunia na kuachwa katika chumba cha watoto mayatima, ilifika muda tukaambiwa hatupaswi kuwa katika eneo hilo

IMG_5013

Wale wengine walikuwa wanalelewa nami walichukuliwa nami nikaachwa nilienda kuishi mitaani.” Alisimulia Leila.

Alizidi na kuzungumza,

“Kwa sababu sikuwa na chakula mwanaume mmoja alichukua fursa ya kunitumia ili nipate chakula hapo ndipo nilipata ujauzito

Nilijifungua mtoto wa kiume, kwa niliishi mitaani na yeye nilikuwa nasaidiwa na  watu kutoko msikitini na kanisani, watu walichukua nafasi hiyo kumhuzisha katika vitendo mbalimbali

Msikiti uliamua kumsomesha mtoto wangu kwa maana sikuwa na uwezo, kuna mwalimu ambaye alikuwa anajiita wa dini ambapo nilimkubali kijana wangu kujiunga

Lakini hayakuwa masomo ya dini mbali walikuwa wanafunzwa jinsi ya kuwa gaidi, katika kidato cha pili alibadilika ghafla na kuacha masomo

Hii ni kwa sababu nilikuwa nakula miraa, na hata kulewa watoto wangu wakiwa hapo, nilibarikiwa na mtoto mwingine msichana ambaye alikuwa anachapwa sana na ndugu yake baada ya kubadilika

Nilimuongelesha lakini siku moja aliamka na kuniambia anataka kuenda Somalia.” Leila Alisimulia.

Baada ya kijana wake kubadilika Leila alienda kupata msaada kutoka kwa chifu ili kijana wake hasiweze kujiunga na kundi la Alshabaab.

Ilikuaje:hatujajaliwa kupata mtoto na mume wangu wa sasa-Nyota Ndogo

Ilimbidi aende mpaka kwa serikali ili mwanawe abadilike, kijana huyo alifuatiliwa na serikali na mwishowe kubadilika.

“Baada ya kufuatiliwa nilimrudisha shule na kisha akamaliza shule ya upili, na nilimuokoa kwa sasa amebadilika na anaendelea vyema

Nimewalea watoto wangu pekee kati ya vijana ambao waliokuwa na wao yeye tu ndio amesalia na kubadilika.” Alisema.

Kwa mengi zaidi tembelea mtandao wetu wa kijamii wa youtube.

 

Ilikuaje:hatujajaliwa kupata mtoto na mume wangu wa sasa-Nyota Ndogo

Leo katika kitengo cha ilikuaje tulikuwa na msanii wa nyimbo za bongo Nyota Ndogo almaarufu mwanaisha Abdalla na kutueleza jinsi alikuwa baada ya kunyamaza sana kama hajatoa muziki wowote.

Ilikuaje: mchoro wa Uhuru nilimpa kama zawadi-Collins Omondi

“Niliachana na mume wangu wa kwanza mtoto wangu wangu akiwa na miaka minne na sasa yuko na miaka kumi na sita

Mume wangu wa pili uwa ananipa ruhusa ili mtoto wangu mbarack amuone baba yake mzazi, pia mume wangu, na kwa hakika si yeye alifanya niachane na mume wangu wa kwanzanyota ndogo

 

Kwa hakika najuta sana kuenda katika mitandao ya kijamii na kusema kuwa ndoa yangu imevunjika

Hatujajaliwa na mtoto nikiwa na mume wangu

Ni mimi nataka watoto na mume wangu, si kwa sababu ya tamaa wala kutaka mali yake, tukienda  hospitali uwa tunaambiwa tuko sawa

Mama yangu alifanywa apinge ndoa yangu na mume wangu lakini sasa tuko sawa, uwa tunatembeleana naenda nchini Denmark miezi mitatu naye anakuja nchini Kenya miezi mitatu.” Alieleza Nyota.

Nyota alisema alipumzika katika kutoa vibao kwa sababu ya ndoa yake.

“Nilipumzika kwa sababu hakuna vile ningetoa nyimbo zangu na kisha na safiri kila mara.” Aliongea Nyota.

nyotandogocover-e1490774130921

Kwa maoni yake Nyota alisema kuwa angependa kuongeaza watoto wawili na mume wake, msanii Nyota kuna wakati alialikwa kuenda kutumbuiza watu nchini USA.

Ilikuaje:Mke wangu alinimwagia asidi usoni kwa kumzuiya kubeba baadhi ya sehemu za mwili wa mtoto wao aliyekuwa ameaga.

Nyota alisema kuwa mapenzi ya ng’ambo ni ya kudekezwa lakini afrika si rahisi kudekezwa na mpenzi wako.

Hapo ndipo alipopatana na mume wake, kwa mengi zaidi tembelea mtandao wa kijamii wa Youtube. na kwa wimbo wake mpya tazama kwenye youtube

 

Ilikuaje: mchoro wa Uhuru nilimpa kama zawadi-Collins Omondi

Collins Omondi Okello ni msanii ambaye jina lake limetambaa sana wiki hii baada ya kumchora Steve Harvey.

Ndani ya studio katika kipindi cha ilikuaje Okello, 30, alikuwa na haya ya kusema,

Ilikuaje:Mke wangu alinimwagia asidi usoni kwa kumzuiya kubeba baadhi ya sehemu za mwili wa mtoto wao aliyekuwa ameaga.

“Mchoro wangu wa kwanza ulikuwa wa rais Uhuru Kenyatta, baada ya kumchora na kisha kuweka katika mtandao wa kijamii rais mwenyewe alinipigia simu baada ya kuona mchoro huo, hii ni kwa sababu uliambiwa na watu wengi katika mtandao wa kijamii.

Niliamka na nikapata watu wengi walikuwa wamenipigia simu, nilipopigia rais alinialika katika ikulu na nikaenda kumtembelea

Niligundua nina talanta ya kuchora nikiwa na umri mdogo sana.” Alieleza Collins.

Image result for collins omondi okelloImage result for collins omondi okello

Collins alisema kuwa amechora watu kadhaa ikiwemo mtangazaji Jeff Koinange ambaye alimuita na kumshukuru kwa uchoraji wake.

ILIKUAJE:Ilichukuwa miaka mitano ili wimbo wangu wa kwanza uwe maarufu-Gloria Muliro

Baada ya mchoro wa Steve Harvey kuenea , Steve aliouona na kisha akamtumia ujumbe na kumwambia anataka wakutane kwa sababu ya mchoro huo.

“Niliambia marafiki wangu wasambaze picha hiyo katika mitandao ya kijamii, baada ya Steve kuona picha hiyo alinituia ujumbe.

Aliniambia niende nchini humo ili tukakutane, katika chuo kikuu nilisomea maswala ya kifedha, mchoro wa uhuru nilimpa kama zawadi lakini kuna watu walinishukuru.” Alisema Collins.

Image result for collins omondi okelloImage result for collins omondi okello

Collins ana mke mmoja na kubarikiwa na  watoto wawili.

Ilikuaje:Mke wangu alinimwagia asidi usoni kwa kumzuiya kubeba baadhi ya sehemu za mwili wa mtoto wao aliyekuwa ameaga.

Katika kitengo cha ilikuaje Dan alichukuwa fursa yake na kueleza jinsi mkewe alimumwagia asidi[acid] kwenye uso wake hali iliyomfanya kuwa kipofu baada ya kumzuiya kubeba baadhi ya sehemu ya mwili ya mtoto wao aliyekuwa ameaga dunia.

 

“Mzozo wetu ulianza baada ya kifungua mimba wetu wa kwanza kuaga dunia baada ya kuugua, mke wangu alikuja akaniambia kuwa anataka kupeleka viungo vya mtoto wetu nyumbani, nilikataa na kisha tukasuluhisha maneno

IlikuajeTulilawitiwa na watu wa karibu ,wasema john omondi na Henry Karanja wasimulia masaibu yao

IMG_0822

Baada ya hapo nilienda kazini, niliporudi nilienda kulala kilicho nishtua baadae ni uchunguzi wenye ulikuwa usoni mwangu, mke wangu alikuwa amenimwagia asidi.” Alieleza Dan.

Akiwa katika mahojiano Dan alisema kuwa alikaa hospitalini kwa muda wa miezi sita na baada ya kutoka aliambiwa na madaktari hawezi ona tena kutokana na madhara yaliyosababishwa na asidi hiyo.

“Nilipotoka hospitali nilipeleka kesi mahakamani, baada ya kukamatwa aliachiliwa kwa dhamana na yuko huru sasa, nilipomuuliza nini kilicho mfanya afanye kitendo hicho aliniambia alidanganywa

Tangu hiyo siku alinipogia simu akiniomba msamaha, na nikamwambia kuwa nimemsamehe kutoka kwa moyo wangu

Hata dada zake walinipigia simu pia na nikwaambia nishaawasamehe, watu wengi sana walishtuka waliposikia kitendo hicho ambacho aliyekuwa mke wangu alikitenda.

Hii ni kwa sababu ndoa yetu ilikuwa ya kupigiwa mfano tulikuwa tunapendana sana.” Aliongea Dan.

ILIKUAJE:Ilichukuwa miaka mitano ili wimbo wangu wa kwanza uwe maarufu-Gloria Muliro

Wakati huo Dan alipofanyiwa kitendo hicho alikuwa na miaka 26 na mkewe 24  mwaka 2013 /9/21.

“Tulikuwa tumekaa kwa ndoa kwa miaka mitatu nilipofanyiwa kitendo hicho, tangu ni chomwe na asidi ni zaidi ya miaka mitatu 

Kwa sasa sijapata mchumba mwingine lakini nilimsamehe kutoka kwa roho yangu.” Alizungumza Dan.

IlikuajeTulilawitiwa na watu wa karibu ,wasema john omondi na Henry Karanja wasimulia masaibu yao

aKatika kipindi cha ilikuaje John Omondi na Henry Karanja walitenga muda wao na kutueleza jinsi walivyo lawitiwa na watu wa karibu sana na wao.

John alianza  kusimulia masaibu ambayo alipitia mikononi mwa rafiki zake,

“Si kufahamu kama walikuwa mashoga ata rafiki yangu, waliniwekea dawa katika kinywaji changu ili nisijisikie walipokuwa wakifanya kitendo hicho

Walioninajisi walikuwa watano, wazazi wangu walijua niko shuleni nikisoma  kwa maana nilikuwa katika chuo kikuu

Sikuelewa walikuwa mashoga kwa maana nilikuwa nimesomea mashambani, nilipokuwa nafanyiwa kitendo hicho nilikuwa na miaka,21,

IMG_0700

Baada ya kufanya hivyo walitoroka na kuniacha chumbani nikiwa pekee, nilijisikia kesho yake ambapo niliona nikiwa navunja damu sana

Niliamka lakini sikuwa na nguvu hata kindogo, nilizirai tena, niliamka hapo ndipo jirani yangu aliniona na akaenda kuita watu wakanipeleka hospitali.”Alisimulia John.

John aliogopa kusema kitendo ambacho alifanyiwa  na hii hapa sababu yake

“Niliogopa kusema kwa maana niliogopa kukejeliwa na watu wa jamii, kama binadamu tunajua vizuri jinsi jamii ilivyo ukisema kitendo kama hicho ilhali umekuwa san.” Alisema.

Mmoja wa amba walimlawiti alikuwa anaishi na yeye ni shoga, alipofikishwa hospitali hakuwafahamisha wazazi wake.

“Nilipoanza kuchumbiana niliambia mpenzi wangu kilicho nitendekea, nilipopona sikurudi shule kwa maana nilikuwa na haya nilianza kutumia dawa za kulevya kwa maana sikuwa najisikia mimi ni wa maana katika maisha

Niliambia wazazi wangu kilicho nitendekea baada ya kupona, kitendo hicho kiliniadhiri mpaka nilikuwa natumia pampers.” Alieleza.

John hakutembea peke yake mbali alitembea na rafiki yake Henry Karanja ambaye alilawitiwa na mjomba wake na alikuwa na haya ya kusema.

“Nililawitiwa na mjomba wangu nikiwa na miaka ya,15, hapo nilikuwa kidato cha pili,hii baada ya mkutano wa kifamilia na mjomba wangu akambia baba yangu anataka tuende pamoja nyumbani mwake

Alikuwa na miaka,25, alipofanya kitendo hicho sikumwambia mtu yeyote, mbali nilijihisi nimekuwa shoga na nikaanza kutafuta mashoga wenzangu

Nilipata shoga wa Zanzibar, alinitumia nauli na nikakula alinipigia simu tena na kunitumia nauli tena, nilienda huko nikakaa kwa muda wa miezi mitatu huku tukifanya kitendo hicho

Baada ya muda niliokoka na nikaacha vitendo hivyo, nilikuwa nalipwa na shoga huyo pesa nyingi sana, nikiangalia nyuma .” Alisimulia Henry.

Kwa maelezo zaidi kuhusu walicho kipitia John Omondi na Henry Karanja tembelea Channel cha Youtube cha radiojambo.

 

ILIKUAJE:Ilichukuwa miaka mitano ili wimbo wangu wa kwanza uwe maarufu-Gloria Muliro

Katika kipindi cha ilikuaje tulikuwa na mgeni ambaye ni muimbaji wa nyimbo za injili Gloria muliro, akielezea safari yake ya uimbaji.

ILIKUAJE: Nilizaliwa bila mfuko wa uzazi na figo moja – Julian Peter

_J5A3196(2)(2)

Hivi majuzi Gloria  ameutoa wimbo ambao unajulikana kama ‘Look to Jesus’ na kusema kuwa aliimba wimbo huu kwa ajili ya kuwatia watu ambao wamepitia changamoto na kukufa moyo.

“Huo wimbo niliimba kwa ajili ya kuwatia watu moyo ambao wanapitia changamoto nyingi sana.” Alisema.

Aliendelea na kusema kuwa alipoanza kuimba ilimchukua muda wa miaka mitano ili ajulikane na nyimbo zake zij++++++++++ulikane.

“Niling’ang’ana sana kwa kutoa wimbo wangu wa kwanza ambapo ilichukua muda wa miaka mitano ili wimbo wangu ujulikane,

Wimbo wangu uliopokolewa sana na kupendwa sana ni wa ‘omwami’ wimbo ambao ulipokelewa sana na watu wa nyumbani

Hii ni baada ya kuenda nyumbani na kuenda kuimba nyumbani kwetu.” Alizungumza Gloria.

Ilikuaje: Wazazi wangu waliaga dunia kwa sababu ya ukimwi-Revival Manoha

Gloria alizidi na kueleza changamoto alizozipitia baada ya mama yake kuaga dunia na baba yake kuoa mama wa kambo.

“Baada ya mama yangu kuaga dunia baba alioa mama wa kambo, na tuka pitia shida na changamoto nyingi sana, 

Kabla ya kuwa muimbaji nilikuwa mwalimu, na kwa sababu ya wito wa Mungu niliacha kazi hiyo na kuanza kuimba.” Gloria Alisema.

Akiongelelea kuhusu kifo cha msanii mwenda zake Papa Dennis alikuwa na haya ya kusema,

“Kwa hakika hadi waleo hakijawahi bainiwa kiini cha kifo cha Papa, Mila ndiye anajua yote na yale yalitendeka.” Alizungumza.

Msanii Gloria alikuwa katika mstari wa kwanza katika kupanga mazishi ya Papa na hata akaenda na kuhudhuria mazishi yake licha ya wasanii wengi kutojitokeza siku hiyo.

ILIKUAJE: Nilizaliwa bila mfuko wa uzazi na figo moja – Julian Peter

Mwanadada kwa jina Julian peter, ndiye aliyekuwa mgeni wetu katika kitengo cha Ilikuaje akihojiwa na Massawe Japanni.

Story yake Julian ni spesheli sana kwani alizaliwa bila mfuko wa uzazi, njia ya uzazi na figo moja. Kulingana naye, hali hiyo ni ugonjwa unaojulikana kama (MRKH) Mayer-Rokitansky-Küster-Hauser.

Julian alizaliwa kwa familia ya watoto wawili wa kike na dadake sasa hivi ameolewa na amejaliwa na familia.

Julian ambaye ni mwalimu, ni mchangamfu na hali yake haijamuangusha au kumshusha moyo kadri na jinsi wengi wangedhania.

Kulingana na Julian, yuko kwenye kikundi cha wanadada 30 humu nchini walio na hali kama yake.

Patanisho sio ya waluhya pekee! Gidi na Ghost wakosoa wakenya (AUDIO)

Unajihisi aje kama mwanamke?

Mimi niko salama kabisa, maisha yangu ni ya kawaida kama mwanamke yeyote ila siwezi pata damu yangu ya mwezi kwani sina mfuko wa uzazi, hiyo tu ndio tofauti yangu na wanawake wengine.

Je unaweza shiriki ngono?

Baada ya kufanyiwa upasuaji unaweza shiriki mapenzi kwani italingana na wakati umepona na pia unapaswa kuwa tayari kiakili. Kumbuka umewekwa au umetengenezwa njia ya uzazi.

 

Ungependa kuolewa?

Mungu akipenda nitaolewa. Lakini sasa hivi niko tayari kupata mtoto kupitia adoption.

Ushawahi jipata ukijihurumia?

Nilijua miaka 12 iliyopita na nilijihurumia kwa mda mchache na baadaye nikaendelea na maisha ya kawaida. Baada ya shule nikafanya utafiti kuhusu hali hiyo na nikajikubali kwani singebadilisha.

Kuna watu ambao hawajui kuhusu jambo hili ila liko ni watu hawajitokezi kuzungumzia, na wanadhani umerogwa.

Anawashauri wanawake wenzake walio na hali kama yake kutojihisi ni kama wako pekee yao na kuwashauri wajitokeze na waungane na kundi lao.

Ilikuaje: Pesa zangu za kwanza niliwasaidia wazazi wangu-DJ Shiti

Steven Oduor Dede almaarufu kama Dj Shiti alipata fursa ya kuja kueleza jinsi maisha yake yamekuwa tangu alipoanza uigizaji wake.

Alifahamika sana baada ya kuigiza kipindi cha ‘ The real house helps of Kawangwere’

Ilikuaje: Haikuwa rahisi kubali kifo cha mke wangu-Dan Sonko

IMG_0530

“Nilianza uigizaji wangu nilipokuwa mtoto mchanga nilikuwa naiga vile shangazi yangu alikuwa anaongea, binamu zangu walipenda sana

Kila wakati nilikuwa naiga vile watu walikuwa wanaongea, nilipokua mmoja wa binamu zangu alinishauri niwe mcheshi pia muigizaji.” Alieleza.

Alianza uigizaji wake wakati wa mazishi ya mzee Ojwang.

Ilikuaje: Kati ya watoto kumi na wawili tumebaki wawili-Charity Mwamba

“Nilienda kwa mazishi ya mwenda zake Ojwang na mmoja wa marafiki zangu akanikutanisha na Abel Mutua kwa maana wakati huo alikuwa mwandishi wa kipndi cha churchill

Usiku wake alinipigia simu na kuniambia niende katika onyesho la churchill, hapo ndipo nilianza uigizji wangu.” Alizungumza shiti.

Shiti ni mtoto wa sita kati ya watoto nane katika familia yao, alieleza jinsi wlivyoteseka baada ya baba yake kustaafu mapema.

IMG_0521

“Wazazi wangu hawakujua maisha yatabadilika baada ya baba yangu kustaafu mapema kwa kawaida tulikuwa tunaishi katika nyumba ya kampuni

Tulitoka katika nyumba hizo na kuanza kutafuta pesa za kujikimu maishani, nilipotoka nyumbani nilipata wazazi wangu hawajalipa kodi ya nyumba na nyumba yao kupelekwa katika Agenti.” Alileleza Dj Shiti.

Muigizaji huyo anawaletea watoto wa ndugu zake na pia wadogo zake, amekuwa katika uigizaji kwa muda sasa huku akisema pesa za kwanza alizopata alisaidia kuboresha maisha ya wazazi wake.

Ilikuaje:Kukosa baba maishani ni kidonda rohoni mwangu-Martin Githinji

Amesomea ‘public relation’ na hajaweza kumaliza kusomea shahada hiyo kwa sababu ya ukosefu wa pesa

“Pesa ambazo nilipata za kwanza niliwasaidia wazazi wangu na kuboresha maisha yao.” Alisema Shiti.

Ilikuaje: Haikuwa rahisi kubali kifo cha mke wangu-Dan Sonko

Katika kitengo cha ilikuaje Dan Sonko na mpenzi wake Bwire Ndubi walitembelea studio zetu na kisha kueleza vile maisha yao yamekuwa.

Wapnzi hawa waili wote ni waigizaji wa filamu.

Ilikuaje: Mama yangu aliniambia babangu mzazi ni mjomba wangu-Jackie

IMG_0379

 

“Kifungua mimba wangu alizaliwa kupitia oparesheni na wa pili pia alizaliwa na operesheni lakini kwa bahati mbaya aliaga dunia kwa sababu alikuwa amepoteza damu nyingi

Alipotoka kuzaa alipelekwa katika chumba cha hali maututi, alihitaji damu ya hapo kwa papo, watu walijitokeza kwa wingi na watu sita tu ndio walichaguliwa

Baada ya muda mfupi daktari aliniita na kuniambia mke wangu ameaga, ni habari ambazo si kuzichukua kwa urahisi.” Alieleza Dan.

Ilikuaje:Nilikuwamfanyakazi wa nyumba kabla niwe mcheshi-Smartjoker

Imekuwa miaka miwili na miezi tisa tangu alipompoteza mkewe wake.

“Katika kuwalea watoto wangu nmesaidiwa sana wazazi wangu.” Alisema Dan.

Mpenzi wake Bwire alikuwa na haya ya kusema,

IMG_0388

“Nilijuana na Dan katika sekta yetu ya sanaa, na mkewe alikuwa rafiki yangu, kuna watu tofauti humu nchini siewezi sema Dan aliendelea na maisha yake kwa haraka baada ya kumoteza mke wake

Si hisi kama nimemsaliti mkewe kwa maana wakati alikuwa uhai sikuwa na uhusiano wowote na Dan, na hata katika kazi yetu sijawahi muona kama anaweza kuwa mpeni wangu 

Kwa sababu tayari alikuwa na familia yake.” Alieleza Bwire.

Dan alisema kuwa alitoa pete ya ndoa ili kuanzisha uhusiano wake na Bwire na kusema kuwa alimjuwa mpenzi wake kabla amjue mwendazake mkewe.

Wamekuwa katika uhusiano wa kimapenzi kwa muda wa miezi tano.

Ilikuaje: Mume wangu alifariki dakika nne baada ya kunipigia simu-Sarafina DeMathew

”  Uhusiano wangu na watoto wa Dan uko sawa kwa maana kifungua mimba tulikuwa marafiki sana, Dan uwa anamkumbuka mkewe lakini uwa nampa himizo.” Alisema Bwire.

Dan alisema kuwa ni yeye aliuliza Winfred kuhusiana na swala la kuwa na uhusiano swala ambalo alikiri lilichukuwa muda mrefu .

‘Mimi ndio nilimsukuma kwa sana, na marafiki wengi ndio wamenivuta nyuma kwa ajili wanakukejeli ukitaka kuendelea na maisha yako.” Alisema.

 

Ilikuaje: Mama yangu aliniambia babangu mzazi ni mjomba wangu-Jackie

Katika kipindi cha ilikuaje muigizaji Jackie Matubia alieleza jinsi maisha yake yamekuwa tangu utotoni mwake, Jackie alifahamika sana kwa uigizaji wake katika kipindi cha tahidi high.

Ilikuaje:Nilikuwamfanyakazi wa nyumba kabla niwe mcheshi-Smartjoker

IMG_0290(1)

 

“Mama yangu aliolewa tena baada ya kuachana na baba yangu mzazi, katika utotoni mwangu nililelewa na watu tofauti kwa maana mama yangu alipo olewa hakuenda na mimi katika ndoa yake mpya

Hii ni kwa sababu alikuwa anataka watu wa familia hiyo wanikubali, wakati huo alikuwa ananiambia baba yangu mzazi ni mjomba wangu

Baadae nilikuja kujua ukweli ambapo nilimkasirikia mama yangu sana lakini mwishowe nikakuja kumsamehe.”Alieleza Jackie.

Mwaka jana ndoa ya Jackie ilivunjika na alikuwa na haya ya kusema kuhusiana na ndoa yake.

 

IMG_0295(1)

Ilikuaje:Kukosa baba maishani ni kidonda rohoni mwangu-Martin Githinji

“Nilipojua ndoa yako haiendi vyema nilienda kumwambia mama yangu cha kusema alisema historia isiweze kujirudia tena, kwa sababu alinizaa na kuachana na baba yangu

Vilevile nilijifungua na mapema mwaka jana ndoa yangu ikavunjika, tulikimbilia ndoa yetu kwa sababu hatukua na mtu yeyote wa kutupa ushauri.” Alieleza.

Si hayo tu aliongeza na kusema,

“Baba ya mtoto wangu aliniomba msamaha kwa mara nyingi, kuachana na mume wangu kuliadhiri mtoto wangu kwa sababu alikuwa analia sana.” Alizungumza.

Hapo awali kuna uvumi ambao ulienea sana katika mitandao wa kijamii kuwa Jackie na mume wake walitengana kwa maana wote wawili walitoka nje ya ndoa lakini alikana madai hayo.

Ilikuaje: Mume wangu aliambia wakwe wangu nataka kumuua-Mary Princess

” Ni uongo kuwa tulikuwa tunaenda nje ya ndoa, hakuna vile unaeza enda nje ya ndoa mkiwa mmetengana kwa hivo ulikuwa uongo

Kwa kweli nilipatana na mume wangu katika mtandao wa kijamii wa instagram, tukakuwa marafiki kisha wapenzi

Kwa mara ya kwanza aliniambia kuwa ni dereva wa matatu lakini nikampenda hivyo.” Alizungumza Jackie.