Mwanahabari aliyekejeli ushindi wa Kipchoge akemewa mtandaoni

“Binadamu hadhibitiki akiamua kutenda”

Hiyo ndiyo ilikuwa kaulimbiu ya bingwa wa riadha ya masafa marefu Eliud Kipchoge alipoandikisha historia ulimwenguni kwa kukimbia mbio hizo chini ya masaa mawili.

Eliud Kipchoge ambaye alikata utepe baada ya saa 1.59.40 aliweka historia katika ulingo wa riadha kuwa mwanariadha wa kwanza kumaliza  mbio za masafa marefu kukatika kuda huo.

Chicago Marathon: Mkenya Brigid Kosgei Avunja Rekodi Ya Ulimwengu

Hata hivyo, shirika la riadha ulimwenguni IAAF ilikosa kuhalalisha na kuthibitisha rekodi hiyo mpya ikisema kwamba Kipchoge hakukimbia katika mandhari ya kawaida. IAAF ilisema kwamba hakukuwa na mshindani mwingine katika riadha hiyo pamoja na kukosa kutimiza sheria zingine za IAAF.

Kipchoge  ambaye alipongezwa kote ulimwengumi akiwemo  rias wa zamani wa Marekani Barack Obama kwa juhudi zake na kuonesha ulimwengu kwamba hakuna kisichowezekana katika maisha ya binadamu.

Lakini kwa mwanahabari Paul Bisceglio,  mafanikio ya Kipchoge katika ulingo wa spoti hayakuwa na manufaa yoyote. Katika kauli yake kwenye mtandao, Biscegilo alikejeli ushindi wa Kipchoge akisema kwamba ushindi ulikuwa bandia.

Maneno hayo yaiibua gumzo huku akikemewa na mashabiki wake Kipchoge ambao wanamtazama kama kielelezo bora katika maisha yao.

Architect Kyaka@jackaloh
The author should be reminded that the current World Marathon Record is held by the same person. He was not running to break his own record but to inspire and show others it can be done in under two hours.
“Mwandishi anafaa kukumbushwa kwamba yeye ndiye mmliliki wa rekodi ya dunia katika mbio hizo. Hakuwa anakimbia kuvunja rekodi tena, bali alitaka kuthibitishia dunia kuwa inawezekana chini masaa mawili.
 Gathoni @I_am_Gathoni
“Where were these thoughts BEFORE the race? Bile because a black man did it”
Alimwuliza kwamba mbona hangetoa maoni haya kabla ya riadha hiyo ? Au ana kinyongo kwa sababu ni mwafrika alishinda.
Japheth Odonya @odonya   Kamati ya roho chafu

 

@AfroMelanated alimkejeli kwa swali kwamba iwapo anasingizia kwamba maziwa mala ilimpa nguvu zaidi.

Timu Ya Raga Ya 7s Ya Kina Dada Yafaulu Kushiriki Olimpiki 2020

Matukio ya Spoti Wikendi: Tazama jinsi Kenya ilivyotamba ulimwenguni

Imekuwa wikendi ya kufana sana katika ulingo wa spoti baada ya Wakenya kuonyesha ubora wao ulimwenguni  mzima na  kwamba binadamu hadhibitiki akiamua kutenda.

Mnamo Jumamosi asubuhi  Eliud Kipchoge alisababisha macho ya ulimwengu mzima kutua kwa siku nzima kushuhudia azimio la ufanisi wake.

Alionyesha  ulimwengu mzima  kwamba binadamu hadhibitiki akiamua kutenda.

Haya ni baadhi ya matukio muhimu yaliyosababisha bendera ya Kenya kupeperushwa ughaibuni:

 

Eliud Kipchoge – Ineos 1:59 Challenge

Mnamo Jumamosi asubuhi  Eliud Kipchoge alisababisha macho ya ulimwengu mzima kutua kwa siku nzima kushuhudia azimio la ufanisi wake.

Alionesha  ulimwengu mzima  kwamba binadamu hadhibitiki akiamua kutenda.

Ulimwengu ulishuhudia mkenya Eliud Kipchoge kuwa binadamu wa kwanza duniani kukimbia mbio za kilomita 42 chini ya masaa mawawili.

Kipchoge ambaye alikata utepe baada ya saa 1.59.40 aliweka historia katika ulingo wa riadha kuwa mwanariadha wa kwanza kumaliza riadha hiyo katika kuda huo.

 

Timu ya raga ya 7s kwa kina dada yafuzu kwenye Olimpiki 2020

Aidha, wachezaji wa raga 7s kina dada waliwapiga wenyeji Tunisia katika nusu fainali na kufuzu katika michuano ya Olimpiki ya Tokyo Japan manmo 2020.

Timu ya  raga ya 7s ya kina dada imejipatia tiketi ya kushiriki katika Olimpiki ya Tokyo Japan 2020, baada ya kufuzu katika  fainali ya mashindano hayo nchini  Tunisia Jumapili.

Kenya ambao  ni mabingwa watetezi waliwapiga  wenyeji Tunisia 19-0 kwenye  michuano ya nusu finali  na  kujikatia tikiti  ya moja kwa moja kwenda Japan

Timu hiyo ya Kenya, maarufu kama Lionesses   ilikuwa timu ya nane kufuzu kwenye michezo ya Olimpiki ya 2020.

 

Lawrence Cherono Ashinda Debele

Lawrence Cherono aliibuka mshindi katika mbio za marathon chicago kwa muda wa saa 2:05:45. Alikata utepe   kwa sekunde moja kutoka mbele ya  Debela amabye aliibuka wa pili.

Mengstu alikuwa wa tatu karibu kwa muda wa 2:05:48. Kinyume na ilivyokuwa na mbio za wanawake,  ushindano baina ya wanaume ilikuwa pambano la karibu zaidi.

Mo Farah na Karoki waliondoka nje ya mashindano  hayo kabla kabla ya raundi ya mwisho, wakiwaacha Cherono, Debela na Mengstu waking’ang’ania  ushindi wakiwa mstari wa kumalizia.

 

Rekodi ya 2003 yavunjwa na Brigid Kosgei

Brigid Kosgei  ndiye bingwa wa dunia katika marathon ya kina dada  baada ya kumaliza katika muda wa 2:14:04, zaidi ya dakika sita mbele ya Ababel Yeshaneh, ambaye alikimbia masaa mawili, dakika 20 na sekunde 51, na Gelete Burka ambaye alikimbia masaa mawili, dakika 20 na sekunde 55 wakati Ethiopia ilimaliza la pili na la tatu.

Kipchoge atoa siri kuhusu mapenzi yake ya riadha

Gwiji Eliud Kipchoge ambaye anatarajiwa kuvunja rekodi yake kwenye mbio za marathon kule Austria Vienna Jumamosi, amesema kwamba kukimbia huimarisha  afya mwilini na  husaidia akili kufikiria vizuri.

“Ninapenda kukimbia kwa sababu husaidia mwili kuwa na afya njema na  kufanya akili yako ifikirie vizuri, bingwa wa dunia wa Olimpiki Eliud Kipchoge alisema.

Akijibu maswali kutoka kwa mashabiki wake, Kipchoge alisema kwamba alianza kukimbia  tangu akiwa na miaka 17 iliyopita baada ya kupewa motisha na kocha wake.

“Nilitiwa moyo na mkufunzi wangu mnamo 2003. Kuwa na subira na kujitolea ni mambo kuu yanayoniongoza na nimejifunza kama mkimbiaji,” alisema.

Nyota Eliud Kipchoge Kutimua Viena Kesho, Ineos Ina Maana Gani?

Alipoulizwa kuhusu utaratibu wa amzoezi yake kabla ya kukimbia, Kipchoge alisema kila anachofanya ni kunyoosha  viungo vya mwili wake mwanzo

“Ninafanyia mazoezi yangu nchini Kenya … kwa viatu  aina toafuti kutoka Pomelo hadi Pegasus .. hivyo ni viatu vyangu  vinavyovipenda,” Kipchoge  alisema.

Kwa Eliud Kipchoge kukimbia 1:59, anahitaji kukimbia kwa kasi ya wastani ya;

100 m kwa sekunde 17.08

200 m kwa sekunde 34.17

400 m kwa dakika 1 sekunde 8

800 m kwa dakika 2 sekunde 16

1500 m kwa dakika 4 sekunde 16

Dakika 5000 dakika 14 sekunde 13

10,000 m 28 dakika 26 sekunde 26

Nusu marathon dakika 59 sekunde 59

Marathon 1 hr dakika 59 sekunde 59

Wakati wa mkutano na waandishi wa habari Alhamisi, Kipchoge alisema anahisi yuko tayari zaidi na amejiandaa na mbio za Vienna vyema.

“Ninajiamini kwa sababu nimekuwepo hapo awali. Kilomita zote kwenye riadha ni muhimu na ninachukua umbali wote nitakimbia kuwa muhimu,”  bingwa huyu wa dunia alisema

Kipchoge Akiri Kuwa Mtulivu Kabla Ya Jaribio Lake La Ineos1:59 Challenge

Ineos 1.59: Wakenya wamuombea Eliud Kipchoge mema

Bingwa wa dunia katika Olimpiki Eliud Kipchoge anatazamiwa kuvunja rekodi yake kwa kukimbia mbio za masafa marefu kwa muda wa masaa mawili maarafu kama Ineos 1.59 Challenge.

Kipchoge ambaye anatarajiriwa kushiriki katika mbio hiza kilomita 42, Jumamosi amezidi kutiliwa dua huku Wakenya pamoja na mashirika mbali wakiwa na matumaini tele.

Naibu wa rais William Ruto pamoja na mkwewe mama Rachel Ruto waliondoka Alhamisi kuelekea Austria huku wakisubiri kumshabikia Kipchoge atakaposhiriki mbio hizo.

Nyota Eliud Kipchoge Kutimua Viena Kesho, Ineos Ina Maana Gani?

“Kama jinsi tulivyofanya katika Monza Italy 2017, wakati Kipchoge alivunja rekodi kna kushinda mbio za marathon kwa muda was saa 2.00.25,  Tutashuhudia na kumshabikia katika Vienna Austria kama bingwa wa mbio wa kila wakati,” Mama Rachel Ruto alisema.

@nasil Mburu atuma ujumbe wake wa heri njema huku akimwambia  kuwa yeye ni mkenya mwenzao na anastahiki ushindi

 

Naye William Chepkut ambaye ni mbunge wa Ainabkoi alimsifia sana na kuonyesha upendo na matumaini makubwa kwamba Kipchoge atavunja rekodi hiy

Usitie Guu Mkoa Wa Magharibi, Wabunge Wamwonya Ruto

Nyota Eliud Kipchoge kutimua Viena kesho, Ineos ina maana gani?

Jina la Ineos limeteka anga huku mahiri na bingwa wa Olimpiki katika mbio za masafa marefu Eliud Kipchoge akisubiriwa kutwaa ushindi hapo kesho.

Nyota huyu aliondoka kwenda Vienna ndani ya jeti la kifahari aina ya Gulfstream G280.

Eliud alisema kuwa ana matumaini sana ya kuvunja rekodi hiyo anayotarajiwa kukimbia mbio hizo kwa chini ya saa mbili wikendi.

Soma hadithi nyingine:

Jinsi dhoruba kali ni kero kwa juhudi za uokoaji Likoni feri, lalama za wanamaji

Ineos ni kampuni nambari moja duniani na ya kibinafsi inayohusika na utengenezaji wa kemikali na mafuta iliyopo nchini Uingereza na ina makao makuu mjini London.

Kampuni hii ina ofisi zilizosajiliwa Lyndhurst, Hampshire, na Uingereza.

Jim Ratclifee ndiye muasisi na mwenyekiti.

Jina la Ineos lina maana ya (Inspec Ethylene Oxide Specialties)

Baada ya kuwasili Uingereza, Eliud Kipchoge alianza siku yake ya kwanza huko Vienna kwa kufanya mazoezi ya mbio hizo pamoja na wanariadha wenzake wa pembeni.

Soma hadithi nyingine:

(+Picha) Jacque Maribe na Letoo Road House, bata batani

Kipchoge ambaye alifika Vienna Jumanne  alionekana mchangamfu huku akianza maandalizi hayo kwa kufanyia mwili wake mazoezi maalum ana kunyosha viungo.

“Nina hamu sana ya kushiriki mbio hizi na ni matumaini yangu kuwaona wote wikendi hii.” Kipchoge alisema.

 

[PICHA] Maandalizi ya Kipchoge Vienna kabla ya Ineos1:59 Challenge

Bingwa wa Olimpiki katika mbio za masafa marefu Eliud Kipchoge ambaye aliondoka kwenda Vienna ndani ya jeti la kifahari aina ya Gulfstream G280, amesema ana matumaini sana ya kuvunja rekodi hiyo anayotarajiwa kukimbia mbio hizo kwa chini ya saa mbili wikendi.

 

unnamed (8)

Baada ya kuwasili, Eliud Kipchoge alianza siku yake ya kwanza huko Vienna kwa kufanya mazoezi ya mbio hizo pamoja na wanariadha wenzake wa pembeni.

Kipchoge ambaye alifika Vienna Jumanne  alionekana mchangamfu huku akianza maandalizi hayo kwa kufanyia mwili wake mazoezi maalum ana kunyosha viungo.

 

Thamani, sifa na upekee wa Gulfstream G280, ndege aliyosafiria Kipchoge

Anatazamiwa kuvunja rekodi yake katika mbio za masafa marefu kwa chini ya saa mbili maarufu kama INEOS 1:59 Challenge alipewa hadhi ya hali juu sana na bwanyenye Sir Ratchliffe ambaye anafadhili mbio hizo.

unnamed (6)-compressed

Nimefurahiya sana kuwa hapa Vienna. Kwa sasa nimeona kozi hiyo kwa mara ya kwanza na inaonekana kuwa nzuri, “Kipchoge alisema.

“Nina hamu sana ya kushiriki mbio hizi na ni matumaini yangu kuwaona wote wikendi hii.” Kipchoge alisema.

PICHA: Tazama jinsi Eliud Kipchoge alivyopewa mapokezi ya kifalme

Thamani, sifa na upekee wa Gulfstream G280, ndege aliyosafiria Kipchoge

Jeti aina ya Gulfstream G280 yenye thamani ya bilioni 2.4 ilitua katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Eldoret.

Bingwa wa Olimipiki na mbio za masafa marefu Eliud Kipchoge alipewa hadhi ya upekee Jumatatu usiku aliposafiria ndege inayomilikiwa na bwenyenye billionea maarafu sana wa Uingereza, Sir Jim Ratcliffe.

Kipchoge ambaye anatazamiwa kuvunja rekodi yake ya mbio za masafa marefu kwa chini ya saa mbili maarufu kama INEOS 1:59 Challenge alipewa hadhi ya hali juu sana na bwanyenye Sir Ratchliffe ambaye anafadhili mbio hizo.

 

eliud kipchoge

PICHA: Tazama Jinsi Eliud Kipchoge Alivyopewa Mapokezi Ya Kifalme

Mamlaka ya Uwanja wa Ndege wa Kenya (KAA) kwenye uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Eldoret jana usiku walipokea ndege ya Sir Jim’s , ambayo iliendeshwa na marubani wawili kutoka makao yake ya Uingereza na kumsafirisha Kipchoge kwenda mji mkuu wa Austria.

Ni huko Vienna ambako Kipchoge, mwenye umri wa miaka 34, anatarajiwa kushirki katika mbio za masafa marefu chini ya saa mbili. maarufu kama “INEOS 1:59 Challenge” iliyothaminiwa na Sir Jim, mmiliki wa kampuni ya kemikali ya INEOS.

‘Nia Yangu Ilikuwa Kuwanyamazisha Mahasidi!’ Asema Bingwa Kipruto

Ndege aina ya Ghubastream G280, nambari ya usajili M-INTY ilisajiliwa Uingereza mnamo Machi 4, 2016, na mara ya mwisho ilionekana katika visiwa vya Uingereza ambayo ni makao makuu ya Sir Ratcliffe.

Ndege hiyo inaaminika kuwa na dhamani ya bilioni 2.5.

Mjumbe wako yupo? Wabunge wanaokosa vikao vya kamati wamulikwa