Mheshimiwa Jaguar ashambuliwa kuhusu mchipuko wa Corona

NA NICKSON TOSI

Wakenya katika mitandao ya kijamii wamemshambulia mbunge wa Starehe Charles Njagua almaarufu kama Jaguar kutokana na usemi wake kuwa China ndiyo iliyosababisha kuwepo kwa Corona ulimwenguni na hivyo inastahili kutupilia mbali madeni ya Kenya.

Mara nyingine Jaguar amenukuliwa akidai kuwa bilioni 650 ambazo Kenya ilichukuwa kutoka Uchina zinastahili kupewa wafanyabiashara wadogo wadogo na wakaazi wa mitaa ya mabanda nchini ambao wameathirika pakubwa na mkurupuko wa virusi vya corona.

Aidha Jaguar alikiri kwamba itakuwa vigumu kwa serikali kuwalizimu watu kukaa makwao hasa wale wanaofanya vibarua na ambao hulipwa kwa siku ili kujipatia kipato cha siku. Alisema kwamba iwapo serikali inapania kuchukuwa hatua hiyo ni sharti iwalishe wananchi wake.

jaguar

“Virusi vya Corona vilitokea Uchina, nilazima watufutilie mbali madeni yote ya Kenya shilingi bilioni 650, tuwape wafanyibiashara wadogo na wale wanaoishi katika mitaa ya mabanda  pesa hizo, hatuwezi waamrisha watu wanaojituma kila siku eti wasitoke makwao ilhali hawana chakula nyumbani mwao,aliandika Jaguar katika mtandao wake wa Twitter.

Jaguar

Hapa ni ujumbe huo kamili alioutuma Jaguar katika mtandao wake wa Twitter

Hon. Jaguar's tweet

Baadhi ya wananchi waliousoma ujumbe huo walikuwa na hisia hizi za kusema

@Komondi43 Yani umekaa to chini ukafikiria hivi.. manifesto ya jubilee ilikuwa?

@Lazooj Hii ndio inaitwa ujinga wa hali ya juu.

@jimmyabachi Hapa you have umefikiria kama ule Patrick wa SpongeBob

@ThisIsMboya Sisi Kama wasee wa Mukuru tumekataa hilo wazo bana!

Ujumbe wa maana;Jaguar awashauri wasanii

NA NICKSON TOSI

Mwanamziki na ambaye pia ni mbunge wa Starehe Charles Njaguar almaarufu kama Jaguar,amewahimiza wasanii wenzake kuekeza zaidi katika miradi mbali mbali kando na kuishi maisha ya kifalme yanayowafanya wengi wao kupoteza maisha kwa kujiangamiza.

Alizungumza hayo wakati wa hafla ya mchango wa mazishi ya mwendazake Papa Dennis yaliyofanyika katika kanisa la Nairobi Chapel jumatatu eneo la Dagoretti.

Wasani wengi walikusanyika katika hafla hiyo ya mchango wakiwemo ; Gloria Muliro, Dk Kwenye Beat, Ringtone, Mwenye Haki, Kevochi, Dj Euphoric, Gabu from P-unit, Vivian, Mr. Seed na Dj Mo.

Papa Dennis’ body will be transported today all the way to Tala for his burial.v

Kweli aligharamika! Picha ya pete ya mke wake Nyashinski

Jaguar alisema kuwa wakati wasanii wanapata pesa wengi wao wanataka kuishi maeneo ya kifahari kama Kileleshwa na kununua magari ya kifahari kama vile Range Rover ambayo yanawanyonya hela zao.

hakuna kazi ikona pesa kuliko hii ya wasanii, hii muziki hii, ni wewe ujipange vizuri kwa sababu sisi ndio tunfanyanga makosa..wewe unastruggle unakua msanii then after ushapewa hit song unahamia Kileleshwa,kitu ya pili unanunua Range Rover kitu ya tatu unataka mabibi watatu” said Jaguar

Mimi nilisema kwa ile mstari ya watu wanataka kwenda kuona Raias ni tuongee ju ya policies, kwa sa babu hakuna mtu anaeza kupangia Maisha yako. kama mimi niongee hapa niseme ukweli, mimi wakati nlikua msanii number one kwa sababau tunaanzanga na E na wale wako E ndio husumbua sana, ukifika A, one concert mtu unalipwa 1 Million, wewe niambie mama wa sukumua yule ako pale Muthurwa apate 1 million ni mgani ushaiona amehamia pale Kileleshwa?,” aliuliza Jguar.

Jaguar (Instagram)

Mbunge huyo alisema kuwa atasaidia katika mazishi ya Papa Dennis na pia akawasihi wasanii wenza kuungana ili kufanikisha safari yake ya mwisho ya Papa Duniani.

Jaguar aliwashukuru Sadat, Ringtone Daddy Owen, Mash Mjukuu na kuwataka wnzake watupilie mbali wazo kuwa Sadat angejukumika kutokana na pesa zake alizobarikiwa kwa msiba huo.

Msiba na ugonjwa haijai kua ya mtu moja, kwa sababu huezi sema leo nimekua mgonjwa mwachie mtu mmoja mzigo. Kwa hivyo nataka nikushukuru Sadat mimi najua ulijaribu mahali unaeza” Alisema Ringtone

Wasanii wengi wamekataa kutoa pesa - Ringtone Apoko on Papa Dennis’ burial

Jaguar aliwashukuru wasanii Ringtone,Weezdom,Daddy Owen waliofika Pangani wakati tukio hilo lilijiri .

Gavana wa Nairobi Mike Sonko aliwashukuru wote waliofika kwa hafla hiyo na japo hakuwepo alitoa kitita cha shilingi alfu 70,000.

Mwili wa Papa Dennis utasafirishwa leo hadi eneo la Tala Kaunti ya Machakos kwa mazishi  hiyo kesho.

FRENEMIES: Jaguar Atoa ‘Godoro’ kwa Babu Owino Gerezani .

 

Mbunge wa Starehe  Charles Njagua al maarufu Jaguar amempiga vijembe mwenzake wa  Embakasi mashariki Babu Owino  ambaye azmeuiliwa katika gereza la Viwandani . Jaguar alipokuwa akitoa magodoro kwa wafungwa wa gereza hilo amesema  Magodoro hayo pia yatamnufaisha mwenzake Babu ,ambaye yuko katika  gereza hilo hadi jumatatu wiki ijayo.

HELL:Wakili wa Miguna Miguna asema mteja wake anapitia mateso Ulaya

” Leo nimetoa  magodoro 2000 kwa wfaungwa wa  gereza la  Industrial Area .Naamini wafungwa  wanastahili kuwa katika mazingira mazuri wakingoja uamuzi wa kesi zao.Mwenzangu Babu Owino pia ni miongoni mwa watakaonufaoika na magodoro haya ya ubora wa juu’ aliandika katika ukurasa wake wa facebook.

Kenya Ina Mambo! Video ya Jamaa mmoja akipiga punyeto hadharani yawashangaza wanamitandao

Babu ,siku ya jumatu alishtakiwa kwa jaribio la mauaji ya DJ mmoja  Felix Odhambo kwa jina maarufu DJ Evolve katika eneo la burudani la B cLub . Picha ya CCTV katika eneo hilo la burudani inamwonyesha Babu akiitoa bastola yake na kasha kumfyatulia DJ Evolve . Babu amekanusha mashtaka dhidi yake  na amewataka wakenya kungoja kusikia kisa chake kuhusu kilichotokea siku hiyo .” Nawahimiza wakenya kuwa watulivu na kungoja kusikiza upande wangu wa kisa hicho  nikapotoka katika makao yangu ya sasa ya gereza la viwandani’ aliandika katika twitter .

Picha ya siku: Jaguar aapa kumpelekea Babu Owino godoro korokoroni

Mbunge wa Starehe, Charles ‘Jaguar’ Njagua alimkejeli mwenzake wa Embakasi Mashariki, Babu Owino alipotangaza kuwa atapeana magodoro 200 kwa wafungwa wa jela la Industrial area.

Jaguar alisema kuwa atamnunulia Owino ambaye anakabiliwa na kesi ya kumfyatulia DJ Evolve risasi, godoro la hali ya juu ili asiwe na wakti mgumu katika jela hiyo.

Aliandika,

Today I will donate over 200 mattresses to Industrial Area Prison, Starehe. I believe that remandees should be as comfortable as possible as they await the outcome of their cases. My colleague, Hon. Babu Owino, will benefit from one of the heavy-duty mattresses #TuesdayMotivation

rsz_jaguar

Vitu 5 hufai kufanya ukiwa kwenye uhusiano wa kimapenzi

Ni ukweli mtupu jinsi wanamuziki Jaguar na zikki walivyoimba na kusema, mapenzi ni bahari lisilo na mwisho kwani kwa wote ambao wako kwenye uhusiano wa kimapenzi na wapendwa wao, wanaelewa msemo huu.

Hivyo basi, Radio Jambo imewaandalia orodha ya vitu vitano ambavyo hufai kufanya unapo kuwa kwenye mashua hii ya mapenzi.

love.birds

Soma uimarike.

  1. Hufai kuwa mtu wa kumkontroli mpenzi wako.

Nikisema kumkontrol mpenzi wako, ninamaanisha kuwa, hufai kuwa mtu ambaye unataka kujua yote ambayo mpenzi wako anafanya, na endapo mpenzi wako hajafunguka na kukuambia kila kitu anachofanya, utazua vurugu na kuleta shida kwenye uhusiano wenu.

Endapo una mpenzi, unachotakikana kufanya ni kumuacha mpenzi wako awe huru. Si lazima umwombe ruhusa mpenzi wako kila wakati unapotaka kufanya jambo kwani ninaamini nyinyi nyote ni watu wazima na mnajiweza.

2. Katu usijaribu kuamuru mpenzi wako awache kufanya anchopenda kwa sababu yako.

Ni kosa kubwa sana kumfanya mwenzio awache kufanya anachopenda kufanya kwa ajili yako, kwani utakuwa unamshusha mpenzi wako sana.

Uzoefu huu umekithiri katika mapenzi ya watu wachanga na ata kwa wazee kwani, kwa mfano kama mtu amezoea kucheza mpira ama anapenda kutazama mechi za mpira, mara kwa mara, mpenzi wake anaweza muamuru awache kucheza au kutazama mechi za mpira na amini usiamini, mara kwa mara, mambo kama haya huleta vurugu katika uhusiano huu wa kimapenzi.

Wosia wangu ni kwamba, endapo mpenzi wako anapenda kufanya kitu fulani, kuwa mtu wa kwanza wa kumtia moyo, azidi kupenda anachofanya  na mapenzi yenu yatakuwa shwari bila vurugu mara kwa mara.

Jamaa ashtakiwa kwa kuiba furushi tatu za karatasi ya tishu

 

3. Usifikiri kuwa unaweza kurekebisha tabia ya mwezako.

Mara kwa mara, wapenzi wanapoanza uhusiano wao, huona kila kitu kikiwa sawa na kuona kana kwamba mpenzi wake ni kamili. Hata hivyo, natumai tunajua kuwa hakuna mtu duniani ambaye ni kamili kabisa, kwa hivyo, kila kitu kina dosari.

Hivyo basi, wazo la kurekebisha tabia ya mtu linafaa kutupiliwa mbali kwani, ni vigumu sana kufaulu kurekebisha mtu kama si yeye mwenyewe ameamua kuwa anataka kubadili tabia yake.

Unapotaka kuishi maisha ya mapenzi yasiyo na vurugu kila wakati, jaribu sana kumuelewa mpenzi wako na badala ya kujaribu kugeuza tabia yake, zidi kumpenda kama unaona kuwa unaeza vumilia anachofanya, walakini, kama tabia yake ni tabia ambayo hauwezi ishi nayo, basi, kata kauli na kukata ushirikiano huo kwani ni vigumu sana kubadili tabia ya mtu.

4. Usiwe mtu msiri ama mwongo 

Sote ni binadamu na ninajua kuwa ni vigumu sana kwa binadamu kamili kusema ukweli kila wakati.

Mara kwa mara, watu hudanganya ili waweze kujiokoa kutoka kwenye tatizo lakini, tabia hii ya kudanganya inaweza kuweka uhusiano wako na mpenzi wako matatani.

Vile vile, maji yatazidi unga, endapo utakuwa msiri sana na umfiche mpenzi wako mambo muhimu ambayo unafaaa kujua. Amini usiamini, mpenzi wako akigundua siri hiyo, maji yatazidi unga na uhusiano wenu kuwa na changamoto nyingi.

Hivyo basi, usiwe msiri na jaribu sana kuwa mkweli kwani naamini kuwa, sote twajua kua siku za mwizi ni arobaini na mwisho, utapatikana tu!

PATANISHO: Ndugu yangu alinifumania na mke wake

 

5.Usifikiri kuwa, mambo yatakuwa shwari kila wakati

Ni vizuri tujue kuwa hakuna kitu ambacho kinaweza kosa dosari na hivyo basi, wapenzi wanafaa kuelewa fika kuwa, hata katika bahari la mapenzi, mambo huwa hayaendi shwari kila wakati.

Wakati mwingine, mambo huwa hayawi sawa. Vita vitakuwa, na msisahau wahenga walisema, wagombanao ndio wapatanao hivyo basi, endapo kutakuwa na vurugu, mnafaa kuzisuluhisha kama watu wakubwa na mambo yote yatakuwa shwari.

 

Haya ndiyo tuliyo nayo siku hii ya leo na ni ombi letu kuwa mtafaidika vilivyo.

Salaale! Je Jaguar na Hamissa Mobetto wana mtoto pamoja?

 Mtoto wa pili wa Hamisa Mobetto na mtoto wake mheshimiwa Jaguar wanafanana kiasi ambacho watu wanabaki wakishangaa ni vipi vile wawili hawa wanafanana kiasi hicho.
Hamisa and Jaguar's kids

Watoto hawa wana umri wa miaka mitatu na mwana mitindo wa Tanzania Hamisa Mobetto alikataa madai eti baba ya mtoto wake ni Jaguar.

Hamisa Mobetto alisema kuwa ni ukweli mtoto wake anafanana na mheshimiwa Jaguar lakini Jaguar si baba ya mtoto wake kwani hata hajawahi kutana naye ana kwa ana.

IT’S TRUE MY SON DYLAN LOOKS LIKE JAGUAR BUT HE’S NOT THE FATHER. FIRST OF ALL, I HAVE NEVER MET JAGUAR. I HAVE ONLY SEEN HIM ON VIDEOS BUT NEVER MET ONE ON ONE. IF IT COST HIM, THEN I’M SORRY,’ Mobetto alisema.

Diana Marua amfokea shabiki Insta kisa Bahati, Insta yawaka

Jaguar ana watoto watatu amabo kila mmoja ana mama tofauti.

Vilevile, Hamisa ana mtoto mmoja na Diamond Platnumz.

Radio Jambo imewaandalia orodha ya picha za watoto hawa.

Tazama na usisite kutupa maoni yako.

1.Mtoto wa mheshimiwa Jaguar

 

2.Mtoto wa Hamisa Mobetto.

“Rudisha mama ama utafute mtu!” Jaguar amshawishi Eric Omondi

Mheshimiwa Charles ‘Jaguar’ Njagua amemsuta mcheshi na msanii Eric Omondi kumrudisha aliyekuwa mpenziwe, bi Chantal maishani mwake.

Kupitia kwa kanda iliyochapishwa katika mtandao wa Eric Omondi, Jaguar ambaye alikuwa ameenda kumtembelea rafikiye kwake nyumbani.

Akiwa humo, aliandaliwa staftahi na inaonekana hakuridhishwa na hapo akamrai Omondi amrudishe Chantal.

Omondi na Chantal walitengana mwaka huu mwezi wa Mei alipotangaza kuwa njia zilizowaleta wapendwa hao wawili, ziliwapa mielekeo tofauti.

Aliandika,

As you move into your new phase in life with or without me I want to wish you all the best My Love❤️…The paths that brought us together are now facing different directions. The post read in part.

Ingawa Jaguar alishukuru juhudi za Omondi kumuandalia chai, anahisi kuwa ni muhimu amrudisha chantal au hilo likishindikana, basi atafute mpenzi mwingine kwani wako wengi zaidi.
Soma jinsi mazungumzo yao yalivyokuwa;

Jaguar: Rudisha mama

Eric Omondi: Chai ilikuwaje bila mama?

Jaguar: Chai haiko lakini ahsante kwa breakfast, lakini tunaomba urudishe mama. Hata wewe sasa utanona, utaongeza weight ama utafute mtu, watu ni wengi.

Eric Omondi: Nitafute mtu ama mama arudi?

Jaguar: Mama arudi au utafute mtu

Tazama kanda hiyo

Je Jaguar amwinda Lulu Diva? Mwanamuziki apasua mbarika

Mwanamuziki kutoka Tanzania, Lulu Diva amefunguka kuhusu uhusiano wake na mbunge wa Starehe, mheshimiwa Charles “Jaguar” Njagua.
Kupitia mahojiano ya moja kwa moja, Diva alimuambia mwanahabari wa Tanzania Diva The Bawse  kuwa Jaguar amekuwa akimmezea mate na pia yeye amekuwa akimvizia vizia Jaguar.

HATUJATENGANA KWA SABABU MIMI NAYE HATUJAWAHI KUWA NA UHUSIANO WOWOTE.

Aliongeza kuwa,

AMEKUWA AKINIVIZIA NAMI NIMEKUWA NIKIMMEZEA MATE. KWA HIVYO SISI SOTE TUNATAMANIANA TU NA TUKAAMUA KUWA WACHA MAMBO YAWE HIVYO.

Lulu Diva

Hapo awali, ilikisiwa kuwa Lulu alikuwa anachumbiana na aliyekuwa mmoja wa kikundi cha muziki cha Wasafi records, Rich Mavoko.

Hata hivyo, hivi majuzi yeye na Diamond Platnumz wamekisiwa kuwa kwenye uhusiano, madai ambayo mkuu huyo wa WCB alikana.

Alipoulizwa kama anatarajia kujifungua mtoto wa aidha Jaguar au Diamond Platnumz, Diva alikana akisema;

LA HASHA SINA MIMBA.

Serikali yajitenga na mbunge wa Starehe, Jaguar

Serikali inasema matumizi mabaya ya Jaguar ya uhuru wa hotuba kuwafukuza jumuiya za kigeni na kuwahamasisha wanajumuiya wa eneo hilo, inadhoofisha utamaduni wa kukaribisha ambao Kenya unajulikana

Katibu wa baraza la mawaziri, Monica Juma asema kuwa lugha ya fujo na yenye hasira huenda kinyume na tabia za Kenya za kukaribisha jumuiya za kigeni na pia Katiba ya Jamhuri yetu.

Serikali imejitenga kutokana na maneneo yaliosemwa na mbunge wa Starehe, Charles Kanyi anayejulikana kwa jina lake la utani kama Jaguar.

Jaguar alitekwa kwa video ambayo sasa imeenea mtandaoni, akiwaambia wageni wa nchi za kigeni wanaofanya biashara eneo la nairobi, wazifunge na warudi nchi zao la sivyo, wataondolewa kwa nguvu.

Jaguar anahitajika kuwenda mwenyewa kwa kituo cha polisi cha Bunge.

Mbunge, aliyefungwa na wafuasi wake, alikuwa ametishia kuivamia majengo ya wageni, akiwashawishi na kuwapeleka kwenye uwanja wa ndege ambapo Idara ya Mambo ya Ndani na Uhamiaji watawafukuza.

Lakini katibu wa kudumu Macharia Kamau alisema Kenya ina majuto kwa kiasi kikubwa kwa lugha iliyotumika yenye maneno kuchochea umma yaliyotolewa na mbunge huyo..

Alisema lugha hiyo yenye fujo na yenye hasira inaenda kinyume na tabia za Kenya za kukaribisha wageni, na pia inaenda kinyume na Katiba ya Jamhuri yetu.

Serikali ya Kenya inataka kujitenga yenyewe kutoka kwa Mheshimiwa Jaguar na maneno aliyosema.

Macharia Kamau aliwathibitishia wageni wanaofanya kazi na kuishi Kenya kuwa wako salama na nchi ya Kenya itaendelea kushugulikia usalama wao.

Monica Juma aliwasihi nchi zingine ziwakaribishe wakenya na moyo mkunjufu kama walivyofanya hapo awali.

 

Jaguar alala jela usiku wa kuamkia leo, watu mashuhuri wamuunga mkono

Mbunge wa Starehe anayejulikana kwa jina lake la utani kama Jaguar alikamatwa siku ya Jumatano baada ya matamshi aliyotamka.

Jaguar anatarajiwa mahakamani hii leo ili kusomewa mashtaka ya kuchochea wapiga kura wake dhidi ya wageni.

Alilala usiku mzima katika seli za polisi za Kileleshwa.

Alipokuwa anatoa hotuba yake kwa wafanya biashara wa Kirinyaga, mwimbaji huyo alisema,

Ukitathmini masoko yetu yamechukuliwa na waganda na watanzania. Na ikiwepo hawatatolewa baada ya saa 24, tutawatoa kwa nguvu na kuwachapa na hatutaogopa yeyote.

Baada ya kutiwa mabaroni alijitetea akisema,

Matamshi niliyoyatamka jana yalikuwa yakiwalenga wachina ambao wamevamia soko na kufanya biashara za wanaanchi wa Kenya kuwa ngumu.

Maneno ya Jaguar hayaja wagawanya wabunge bali pia wakenya, wengine wame muunga mkono huku wengine wakimkemea.

Haya ni baadhi ya maoni yaliyotolewa

akotheekenya It shall be well

huddahthebosschick We shall Prevail!

terencecreative Pamoja milele

iamfrasha tuko na wewe 💯💯💯💯💯💯

allyabdu Mimi nisha rudi nipo kwetu Tanzania

djtibzkenya @jaguarkenya Nobody’s perfect, we all make mistakes, just apologize to our brothers and we all move on, we need each other now more than ever. Peace & love always.