Patanisho: Mume wangu alitaka kujinyonga kanisani

Stephen alituma ujumbe akiomba apatanishwe na mama Faith ambaye ni mke wake na mama wa mtoto wao mmoja.

“Tulikosana tarehe 28 baada ya kusafiri nyumbani. Niliporudi nilipata amefunganya virago na kuondoka bila sababu na sina habari nilimkosea aje.

Alinituma nyumbani na akaniambia nimletee dawa ya kienyeji kwani alikuwa mja mzito na amepoteza mtoto bila kujua kuwa ni uwongo.” Alielezea Stephen.

Kwa nyumba alichukua kile alichoona ni chake na nikamwachia mungu kwani nampenda na mungu ametujalia mtoto mmoja.”

Huyo ni baba wa mtoto wangu, unajua mahali tulikosania ni kwamba kuna siku tulikosana na akachukua kamba akitaka kujinyonga kwa compound ya kanisa. Alieleza mama Faith.

Sasa kila mara tukikosana huwa akidai kuwa niokote nilichotaka kwa ile nyumba na niondoke, hapo siku moja nikaamka nikachukua nilichokinunua na kuondoka.

Tukasuluhisha yote na tukaombewa na tukasahau lakini kuna siku alitaka kuniua kwa kutumia chuma kwani kuna siku alimuumiza mtoto na akafura mguu. Huyu sio jamaa wa kuishi naye.

Aliongeza mkewe Stephen akidai kuwa kuna wakati alilala nje na hakuwa na mavazi na hata alikuwa anaomba hadi mavazi ya ndani.

Alijawa na huzuni akidai kuwa hataki kuzungumza na mumewe kwa hasira kwani amezungumza na watangazaji kwani anawapenda.

Pata uhondo kamili.

Kizazaa Kanisani Baada Ya Mhudumu Wa Klabu Kulalamikia Kutolipwa Na Mhubiri

Basi kama ilivyo ada ya mtangazaji wa kipindi cha asubuhi cha Gidi na Ghost Asubuhi, Ghost alivuka mwaka wa 2017 na uchangamfu si haba.

Kama kawaida hakuwacha ucheshi wake mwaka wa 2016 na basi juzi alisimulia kisa kimoja cha kuchesha ambapo mhubiri aliwachwa mwenye aibu tele baada ya mhudumu wa klabu kudai kuwa mtumishi ule wa mungu alidinda kumlipa fedha alizokuwa amemkopesha hapo awali.

Basi mwanadada yule alipogundua maji yamezidi unga aliamua kufa kupona na kuzua vurugu kanisani mwa jamaa ule huku akidai waumini hawatatoa sadaka iwapo hatalipwa fedha zake. Basi waumini waliwachwa vinywa wazi wasijue jinsi mhudumu yule walivyopatana na mhubiri wake na mbona akakataa na mkopo wake.

Basi kukopa harusi kulipa matanga. Pata uhondo kamili.

JUJA: Waumini Wamfurusha Mchungaji Mpenda Pesa

Leo ikiwa Jumatatu, kama ibada kipindi ukipendacho cha Gidi na Ghost Asubuhi kilirudi hewani baada ya wikendi refu na kama kawaida Ghost Mulee alirudi na uhondo kamili kutoka majimbo tofauti.

Tukizungumzia ibada, kulikuwa na vituko maeneo ya Juja katika kanisa moja hapo jana.

Kulingana na Ghost Mulee, waumini walimtimua mchungaji wao huku wakimkashifu kwa kupenda hela. Kisa hicho ambacho kiliwashangaza wengi, kilizuka baada ya mchungaji huyo ambaye ndiye mwenye kanisa hilo kuwakemea washirika wake kwa kutotoa sadaka wala fungu la kumi.

NAIVASHA: Mwanaume mmoja akamatwa kwa kulawiti na kuua mchungaji mifugo

“Mchungaji huyo aliingia kanisani na kuwaambia washirika kwanza watoe sadaka na fungu la kumi, kabla ibada haijaanza.” Alisimulia Ghost.

“Baada ya watu kutoa sadaka, kuna wengine ambao hawakutoa sadaka na hapo ndipo kisanga kilianza. Mchungaji huyo alianza kuwafokea kondoo wake. ”Hakuna haja ya kuja kanisani na hamtoi chochote, mnakujaje kujaza viti hapa mwakaa tu?” mchungaji alifoka.” Na punde tu muumini mmoja aliposimama na kumkashifu mchungaji huyo kwa matamshi yake, alikipata cha mtema kuni.

Pastor crashes woman to death while attempting miracle

Sikiza kanda ifuatayo.

 

Usalama waimarishwa mjini Mombasa

Maafisa wa polisi wametumwa kulinda doria katika maeneo ya makanisa mjini Mombasa kufuatia tishio la ugaidi pwani ya Kenya. Maafisa hao wanajumusiha maafisa wa CID na polisi wa utawala.

Askofu wa kanisa la Kiangilikana Julisu Kalu pia ametoa wito kwa waumini katika sehemu za kuabudia kuwa macho na kupiga ripoti kwa maafisa hao kuhusu chochote wanachohisi kitatishia usalama wao.