AUDIO: Kasisi Azuiliwa Na Polisi Baada Ya Kunajisi Na Kupachika Wanafunzi Wawili Mimba

Kasisi mmoja anazuiliwa katika kituo cha polisi cha Voi kwa tuhuma za kuwanajinsi na kuwatunga mimba wanafunzi wawili wa shule moja ya upili wenye umri wa miaka 16 huko Voi kaunti ya Taita Taveta.

Mlinzi Wa Kanisa Auwawa Huku Kasisi Akinusurika Kifo

 Kwa mujibu wa kamanda wa polisi kaunti ya Taita Taveta, kasisi huyo kutoka Wongonyi eneo la Tausa anadaiwa kuwanajisi wanafunzi hao tangu mwaka jana.

Makasisi wapinga ndoa za jinsia moja

Polisi wameomba mahakama siku tatu kufanya uchunguzi kabla mshukiwa kujibu mashtaka.

Skiza kanda ifuatayo

Mlinzi Wa Kanisa Auwawa Huku Kasisi Akinusurika Kifo

Mlinzi mmoja wa kanisa katoliki la Nangina kwa jina Fredrick Ouma aliuwawa na watu wasiojikana usiku wa kuamkia jana.

Kulingana na walioshuhudia kisa hicho, watu wanne waliokuwa wamejihami kwa panga walivamia nyumba ya kasisi wa kanisa hilo na kuiba simu pamoja na shilingi elfu tatu kabla ya kasisi huyo kupiga kamsa kuitisha usaidizi.

Akithibitisha kisa hicho kamishona wa kaunti ya Busia bwana Mongo Chimwaga alisema mlinzi huyo aliuwawa kwa kukatwa katwa akiwa katika juhudi za kumsaidia kasisi wa kanisa hilo ambaye alinusurika kifo baada ya kufanikiwa kutoweka.

Aliongezea kuwa juhudi za kuwatia nguvuni washukiwa hao tayari zimeng’oa nanga huku akiwataka wakazi kuwasaidia katika uchunguzi.