Njia Panda? Je,Kenya itachukua hatua gani huku mataifa mengine yakilegeza vikwazo na mengine yakikaza kamba kuhusu Covid 19?

Wakenya wengi wanangoja kwa hamu leo Jumatatu kujua hatua ambazo serikali itachukua hususan endapo rais Uhuru Kenyatta  atatangaza kufunguliwa kwa  nchi na kuruhusu usafiri au kuzidisha mikakati ya kupambana na maambukizi ya virusi vya corona.

Kuna mgawanyiko ulioibuka wa maoni kuhusu kinachofaa kufanywa huku pande mbili zenye maoni tofauti zikijitokeza kutaka  usafairi uruhusiwe na wa pili ukitaka mikakati hiyo ikazwe kamba zaidi kwani visa vya maambukizi ya virusi vya corona vingali vinaongezeka.

Katiba hotuba yake ya mwisho kuhusu hali ya corona rais Kenyatta alisema kurejelewa kwa hali ya kawaida kutategemea iwapo visa vya ugonjwa huo vitakuwa vimepungua na tangazo lake la kuzidisha kipindi cha kafyu liliwashangaza wengi waliomtaraji kuondoa kabisa  kafyu.

Makali ya COVID 19: Makahaba wachangiwa shilingi 49,000 kununua chakula na kulipa kodi ya nyumba wakati huu wa janga ka corona

Wakati huu, wengi wanapongoja tangazo lake wamejitayarisha kiakili uwezekano wake kuongeza muda huo  ikizingatiwa kwamba  visa vya walio na ugonjwa huo vimeongezeka na sasa wakenya  7,889 wana ugonjwa huo huku 160 wakiaga dunia hadi kufikia sasa.  Siku ya jumamosi Kenya ilisajili visa vingi zaidi kuwahi kuripotiwa kwa siku moja baada ya watu 389 kupatikana na ugonjwa huo hatua ambayo huenda ikafanya kuwa vigumu kwa rais Kenyatta kuamua kulegeza kamba kuhusu masharti  ya kupambana na virusi vya corona.

Je, ni hatua gani zilizochukuliwa na mataifa mengine wakati huu?

 Tanzania

Katika taifa jirani la Tanzania, shule zimefunguliwa ingawaje kuna masharti ya watu kuvalia maski na kuosha mikono katika sehemu za umma. Kenya awali ilikuwa imetanagza kuwa shule zitafunguliwa mwezi Septemba lakini hilo halitawezekana baada ya wizara ya elimu kuzidisha muda huo hadi Januari mwakani. Waziri wa elimu George Magoha amesema walimu, watu takriban laki tatu watapimwa kwanza kabla ya shule kufunguliwa. Hilo huenda likawa jambo gumu kutimiza ikizingatiwa kwamba kwa miezi minne, Kenya imefaulu tu kuwapima watu  189,263.

England

Polisi nchini Uingereza sasa wamesema wamegundua kwamba watu walevi hawana uwezo wa  kujizuia kukaribiana katika usiku ambao maeneo ya burudani yalifunguliwa nchini humo kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miezi mitatu.

Sekta ya utalii na burudani nchini humo imejipata na uchangamfu baada ya   utulivu wa miezi mitatu   na kufunguliwa  siku ya Jumamosi kumewafanya watu kuitaja kama ‘siku ya Uhuru ‘ au super Saturday’

Pesa husumbua watu! Mwanamme wa India anunua maski ya dhahabu kukabiliana na coronavirus

Australia

Australia imetangaza siku ya Jumatatu kwa mara ya kwanza katika miaka 100  kufunga mpaka wa majimbo ya  Victoria na New South Wales. Mara ya mwisho kwa mpaka huo kufungwa ilikuwa 1919 ili kukabiliana na  janga la  Spanish flu

Hatua hiyo hata hivyo huenda ikavuruga uchumi wa  Australia   huku visa vya maambukizi vikipanda katika  mji mkuu wa Victoria  Melbourne  na kuifanya serikali kuanza kutekeleza masharti ya watu kutokaribiana na  hata maagizo ya kutotoka nje yakitolewa .

Watu 149 wamepatikana na virusi vya corona

Katika taarifa ya kila siku na iliyotumwa kwa vyombo vya habari nchini ,Kenya imesajili visa 149 vya maambukizi ya corona baada ya watu 3090 kufanyiwa vipimo ,hivyo,kufikisha wagonjwa 5533 wa virusi hivyo nchini.

Vile vile taarifa hiyo imesama kuwa watu wengine 48 wameruhusiwa kuondoka hospitalini na kufikisha jumla ya watu 1905 waliopona.

Aidha wagonjwa 5 wamepoteza maisha kutokana na virusi hivyo ,na kufikisha watu 137 waliofariki.

Visa hivyo vipya vimetokea maeneo yafuatayo,Nairobi (73), Mombasa (20), Kiambu (8), Machakos (3)

Kati ya waathiriwa hao ,wakenya ni 148 huku raia wa kigeni akiwa mmoja.

Wakati uo huo taarifa hiyo imeonya kuwa watu wanaotumia chang’aa wako katika hatari ya kuambukizwa virusi hivyo.

Waathiriwa ni kati ya mwaka mmoja na 76.

 

Kenya yashinda kiti katika baraza la usalama la umoja wa mataifa kwa kura 129

Kenya  imeshinda kiti cha uanachama katika baraza la usalama la umoja wa mataifa  baada ya kupata kura 129 katika raundi ya pili ua upigaji kura dhidi ya Djibouti.

Uhuru: Sina nia ya kuongeza muda wangu madarakani

Djibouti  ilipata kura 62 katika raundi ya pili baada ya kuinyima Kenya ushindi katika raundi ya kwanza siku ya Jumatano.  Siku ya Jumatano Kenya ilipata kura 113 dhidi ya 78 za Djibouti  na ilihitaji kura 128 ili kupata ushindi wa moja kwa moja kati ya kura 192 za mataifa wanachama

Hatua hiyo ililazimu bunge la  mataifa wanachama kuitisha awamu ya pili ya upigaji kura ili kuamua mshindi kati ya Kenya na Djibouti  kumtafuta mwakilishi wa Afrika katika baraza hilo kwa kipindi cha mwaka mmoja.

Kenya yashindwa kukipata kiti cha baraza la usalama la UN-Raundi nyingine ya kura kufanyika leo

Kenya inaichukua nafasi ya Afrika Kusini  na itahudumu kuanzia mwaka wa 2021 hadi 2022. Nairobi sasa inajiunga na India, Mexico, Norway  na  Ireland  kuwa miongoni mwa wanachama wasio wa kudumu wa baraza hilo ambao ni (Russia, China, UK, US, France) kupitisha maazimio ya kudumisha amani na usalama duniani wakati wa kipindi cha mwaka wa 2021/2022.

 

 

Kenya na Tanzania zakubaliana jinsi ya kuwapima madereva wa masafa marefu

Kenya na Tanzania hatimaye imekubaliana jinsi ya kuendesha shughuli ya kuwapima madereva wa masafa marefu baada ya wiki mbili za vute ni kuvute kuhusiana na upimaji wa madereva hao.Wawakilishi wa serikali kutoka kwa mataifa yote mawaili walikutana ili kutafuta njia mwafaka ya kutatua mzozo ambao umekuwa ukiyumbisha biashara katika mataifa husika .

Sanda Ojiambo ateuliwa kuwa mkurugenzi mtendaji wa jumuiya ya kimataiafa inayoleta pamoja kampuni kufanya biashara

Waziri wa Uchuguzi na usafiri nchini James Macharia na mwenzake kutoka taifa la Tanzania Isack Kamwelwe walikutana katika mpaka wa Namanga na kujadili hatua madhubuti za kutia kikomo kwenye mvutano ambao umekuwepo.

Mazungumzo baina ya mawaziri hao wawili yanajiri siku chache tu baada ya viongozi wa mataifa hayo mawili kuzungumza ili kutatua mvutano huo.

Hatuwezi kuwa kwa Lockown miaka yote, Uhuru asema

Mkutano huo ulichukua saa sita huku ikidaiwa kuwa palikuwepo na makubaliano kutoka pande zote mbili ya jinsi yua kuendesha shughuli hiyo.

Macharia alisema kuwa Kenya na Tanzania ni lazima izike tofauti zake katika kaburi la sahau na kuangazia namna ya kufufua sekta ya biashara ambayo imeathirika pakubwa.

“Kenya and Tanzania are trade partners, recording a turnover of more than $500 million (Sh53 billion) annually. We have reached an agreement that Tanzanian and Kenyan drivers will be subjected to the WHO standard Covid-19 testing in their territories and issued with clearance certificates,” amesema  Macharia.

Magufuli na Kenyatta wazungumza kuhusiana na mgogoro mipakani

Rais Kenyatta na mwenzake wa Tanzania John Magufuli walifanya mazungumzo ili kubaini njia mwafaka ya kutafuta suluhu katika mgogoro ambao umekuwepo kwenye mipaka ya mataifa hayo mawili tangu virusi hatari vya corona kuripotiwa katika mataifa mawili.

Viongozi hao wawili wamekubali wizara zote mbili za usafiri kukutana na kufanya mazungumzo ili kubaini namna shughuli hiyo itakavyoendeshwa kwenye mipaka ya Kenya na Tanzania huku mjadala kuu ukiwa ni kuhusiana na madereva wengi wanaotokea taifa jirani la Tanzania wakiwa wameambukizwa na virusi hivyo.

Felicien Kabuga afikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza baada ya kutiwa mbaroni

Katika video na ambayo tumeiona, Magufuli amesema vita vya mipaka ambavyo vimekuwepo vitayawezesha mataifa hayo mawili kuendelea kushirikiana kiuchumi.

uhurugreetsmagufuli

“Haiwezekani tukawakwamisha waliokuja kufanya biashara. Lakini pia magari ya Tanzania hayawezi yakakwamishwa kwenda Kenya,” alisema Magufuli.

Ameongeza kuwa ni sharti asasi kuu kutoka mataifa husika kuzungumza ili kupata njia mwafaka.

Museveni aamrisha idadi ya madereva waliopatikana na corona kuondolewa katika takwimu kamili za serikali

“Wazingatie uchumi wa nchi zetu. Kwa vile tumezungumza vizuri na Kenyatta, sisi tumeyamaliza. Wakae viongozi watatue hii maneno na watu wafanye biashara katika pande zote mbili,” amesema Magufuli.

magufuli uhuru

 

Jumapili, Tanzania ilisitisha shughuli za usafiri wa madereva wa Kenya kuingia nchini humo siku moja tu baada ya rais Kenyatta kufunga mipaka yake na taifa hilo ili kusitisha maambukizi ya virusi hivyo.

 

Kaunti 20 nchini zimeandiksiha visa vya Corona -Wizara ya afya

Ikiwa kufikia sasa taifa la Kenya limesajili visa vya maabukizi ya virusi vya corona kuwa 781, wizara ya afya imesema kuwa kati ya majimbo 47 nchini, kaunti 20 kufikia sasa zimesajili aghalabu kisa cha viruis hivyo hatari.

Majimbo yaliyoko kwenye mipaka ya Kenya na taifa la Tanzania yakiwa ambayo yanaipa serikali kiwewe kufuatia visaa vingi vinavyoripotiwa kwa watu wanaotoka Tanzania.

Watu 23 wamepatikana na virusi vya corona baada ya kupimwa na serikali

Tazama ubaini kaunti na visa ambavyo zimesajili.

Image

Waliofariki nchini wamefikian watu 45

Dereva wa lori atoweka baada ya kupatikana na corona

Serikali  ya Uganda imeanza kumtafuta dereva wa lori kutoka Kenya aliyekuwa amethibitishwa kuambukizwa virusi vya corona na kutoweka. Dereva huyo aliingia nchini humo tarehe 8, Mei na kupimwa virusi hivyo katika eneo la Malaba.

Coronavirus: Madereva 4 wa malori kutoka Tanzania wapatikana na virusi hivyo Uganda

Dereva huyo aliacha gari lake na kutoweka baada ya kugundua ana virusi vya corona.

Msemaji wa polisi wa Uganda Patick Okemo siku ya Jumapili aliwataka wananchi kujitolea na kutoa habari kumhusu dereva ili atiwe nguvuni.

“Juhudi za kumsaka mgonjwa ambaye ameenda mafichoni zinaendelea. Kikosi cha usalama na maafisa wa afya wanamsaka jamaa huyo.  Vita hivi si vya maafisa wa usalama na wa afya pekee,” Okemo alisema.

Madereva wa masafa marefu watishia kuandamana kutokana na dhulma za maafisa wa usalama Uganda

 

Mnamo tarehe 10, Mei, nchi ya Uganda ilikuwa imethibitisha visa 121 vya corona ambapo watu 55 walikuwa wamepona kutokana na virusi hivyo.

Hatua ya haraka! Kenya yaanza mchakato wa kupima madereva wa masafa marefu mipakani

Uganda ilianza mchakato wa  kuwapima madereva wa masafa marefu baada ya madereva wanne kutoka nchi jirani ya Tanzania kupatikana na virusi hivyo nchini Uganda.

 

MHARIRI: DAVIS OJIAMBO

 

Kenya Vs Uganda! Mbochi mganda alivyompokonya mhadhiri mume wake

Kumekuwa na  dhana ambayo siwezi kujua iwapo ni ya kweli kwamba wanawake wa Uganda ni bora kuliko wa Kenya.

millie Odhiambo

No Sex !Ugonjwa wa zinaa ulinizuia kufanya mapenzi na mke wangu kwa mwaka mmoja’ Jamaa aeleza masaibu yake baadaya kuambukizwa STI

Hivi karibuni,  mbunge  Millie Odhiambo alijipata akipondwa vibaya  katika twitter baada ya kuweka ujumbe ulioonekana kuendeleza dhana hii alipoambatisha ujumbe huo wake na picha iliyowalinganisha wanawake wa Kenya na wenzao wa Uganda. Millie alindika hivi ;

‘It is our responsibility as Kenyan women to teach our daughters how to tend to their future husbands. It might appear unfeminine but God has a reason why we are women and they are men… We have to embrace nature and its dynamics’

Wakenya  hawakumpa mbunge huyo muda wa kujieleza na pindi makombora ya kumkosoa yakaanza kurushwa. Kwa wakati mmoja, ilibidi Millie afafanue  kauli yake kuhusiana na swala hilo lakini alichosema kilizua mengi hasa kuhusiana na mjadala wa chini kwa chini ambao umekuwepo kwa muda mrefu sana kuhusu hadhi, heshima na  tabia za wanawake wa Kenya wakilinganishwa na mvuto wa wenzao kutoka Uganda na hata taifa lingine jirani la Tanzania.

Ujumbe huo wa mbunge Millie Odhiambo ulizua kumbukumbu ya mhadhiri mmoja wa chuo kikuu  jijini  Nairobi ambaye alipokonywa mume na mfanyikazi wake, msichana wa Uganda. Wengi hawakuamini kilichofanyika lakini kwa mujibu wa masimulizi ya pande zote husika, msichana huyo kutoka Uganda alimfanya mume wa mhadhiri kujihisi kama mfalme na muda sio  mrefu, walikuwa washachukuana na jamaa kumuacha mke wake msomi na mhadhiri wa chuo kikuu!

MIA: ‘Alinitoroka siku ya harusi, sasa anataka turudiane, never!” Mwanamke amkemea jamaa aliyehepa siku ya harusi

Yote yalianzia katika vitu ambavyo wanawake wa Kenya husema ni vitu vidogo. Kwa sababu  mume wa mhadhiri alikuwa pia msomi, alikuwa mhandisi na mara nyingi akija nyumbani, hakuwa akimpata mke wake akiwa amewasili na  nyakati zote, yule mfanyikazi wa nyumbani alikuwa ndiye anamshughulikia kuanzia kumuandalia chakula na hata maji bafuni. Ilifika wakati  Engineer  akaanza kumpigia simu mfanyikazi wake  kumjulia hali kwa sababu mkewe alikuwa kajitosa kweli katika shughuli  za taaluma yake na akasahau kabisa jukumu lake lingine kama mke wa mtu .

Is Love Blind? Wengi wanataka kujua kilichomvutia marehemu Tecra Muigai kwa Omar Lali

Muda ulivyodondoka ndivyo Mhandisi  alivyojipata kavutiwa kuwa karibu sana na yule mfanyikazi wa kiganda   ambaye hakuwa na kisomo wala hungefikiria wangeelewana kwa chochote. Mama mwenye nyumba naye, kwa sababu ya jeuri yake, alikuwa hajawahi kumuona yule mfanyikazi kama tishio kwa ndoa yake kwa sababu alikuwa akijiona kafika kweli kwa sababu ya elimu yake. Kufikia wakati alipofumbua macho kujua kilichokuwa kikiendelea, mfanyikazi wake wa   nyumbani, yule mganda alikuwa keshapata mimba ya mumewe na wameanza maisha machoni pake bila haya .

Matumizi ya pesa zenyewe ndio hatufahamu! Kenya yapokea bilioni 78 kutoka IMF

NA NICKSON TOSI

Shirika la Kimataifa la Kutathmini matumizi ya pesa International Monetary Fund IMF limethibitisha mgao wa fedha kwa taifa la Kenya wa bilioni 78 kutumika katika vita dhidi ya coronavirus .

Zikiwa zimetumwa kwa wizara ya afya, bilioni izo za pesa zinatarajiwa kusaidia serikali kulipa baadhi ya madeni ya wizara hiyo na kusaidia kununua vifaa muhimu vya kutumiwa na wahudumu wa afya.

Kenya receives Ksh.78 billion IMF loan to address Covid-19 pandemic

Visa vya coronavirus nchini Kenya vyatimia 607

Kando na ufadhili huo pia Kenya inatarajia kupokea kitita kingine cha pesa takriban  bilioni 106 kutoka kwa benki kuu ya dunia ili kutumiwa katika mchakato wa kupigana na virusi vya Corona.

Bilioni hizo sasa kutoka IMF zitakuwa nguzo muhimu japo serikali imetuhumiwa vikali na wananchi kutokana na ubadhirifu wa mikopo hiyo inayotoka katika mashirika ya kimataifa.

Lockdown bila usaidizi: Mbunge alalamikia kufungwa kwa Eastleigh, Old Town

Siku za hivi karibuni, waziri wa afya Mutahi Kagwe alilazimika kuelezea kamati ya bunge ya afya kuhusiana na matumizi ya pesa hizo.

 

 

 

Ndege ya Kenya yaanguka Somalia na kusababisha vifo vya watu 6

Watu sita wameaga dunia baada ya ndege moja iliyosajiliwa Kenya kuanguka nchini Somalia.

Wizara ya mashauri ya kigeni nchini imeitaka Somalia na  mashirika ya kimataifa kuchunguza kikamilifu kuanguka kwa ndege moja ya  kampuni ya kibinafsi iliyokuwa ikisafirisha misaada ya kupambana na virusi vya corona.

Kunani? Wakuu wa maabara Tanzania wasimamishwa kazi, uchunguzi wafunguliwa dhidi yao

Ndege hiyo ilianguka katika hali ya kutatanisha  katika eneo la Bardale, Baidoa nchini Somalia siku ya Jumatatu tarehe 4. Kenya imeyataka mashirika mengine ya ndege yanayohudumu katika eneo hilo kuchukua tahadhari  kwani hali  iliyosababisha ajali ya ndege hiyo bado haijaeleweka .

Unyama ulioje? Mwanamme amuua mkewe kwa kumkata kichwa Isiolo

Wizara ya mashauri ya kigeni ya Kenya imesema itashirikiana na mashirika mengine kufuatilia kwa karibu uchunguzi  kuhusiana na  tukio hilo na kutafuta suluhisho. Ndege hiyo yenye nambari ya usajili 5Y-AXO ilikuwa ya kampuni ya  African Express na ilisababisha vifo vya watu wote sita waliokuwemo .