Uhuru: Sikudhani uchaguzi wa Kibra ungekuwa wa amani

Rais Uhuru Kenyatta kwa mara ya kwanza amezungumzia kuhusu kushindwa kwa Jubilee katika uchaguzi mdogo wa Kibra.

Jubilee ilikuwa inampigia upato  McDonald Mariga katika uchaguzi huo uliowavutia wagombeaji 24.

Hata hivyo, Mariga alibwagwa na mgombea wa chama cha ODM.

Watu Sita Wauawa Na Umati Katika Kaunti Ya Busia

Uhuru alikiri kwamba Jubilee ilishindwa ila akasema  cha muhimu ni amani uliodumishwa wakati wa kampeni na hata siku ya ukupigaji kura.

“Katika miaka yangu yote sijawai ona kampeni ya amani Kibra. Kuna baadhi ya watu wachache walirushiwa mawe lakini hatukuona duka likichomwa au watu wakiwa na wakati mgumu wakienda nyumbani,” Uhuru alisema.

“Iwapo uchaguzi unaweza ukafanywa Kibra na watu hawatapoteza mali yao au maisha yao basi hiyo ni ushindi na watu wanafaa kujifunza kutokana na hilo,”

Alizungumza hayo katika ikulu ndogo ya Sagana katika kaunti ya Nyeri wakati alipofanya mkutano na wanasiasa kutoka Mlima Kenya.

Rais Uhuru alitoa mfano wa mfuasi wake ambaye kila wakati wa uchaguzi huvamiwa na kutpoteza mali.

Seneta Cleophas Malala Atimuliwa Chamani ANC

Uhuru alisema kuwa kuna mwanamke aliyepotea mali yake katika uchaguzi wa 2007, 2013 na hata 2017 kutoka na vurugu zilizoshuhudiwa wakati wa uchaguzi.

Alisema kwamba kuwalika watu wengine kujumuik nao haimaanishi kwamba anawafukuza walio karibu na yeye.

Aidha aliwarai viongozi kutoka Mlima Kenya kusahau tofauti zao na kufanya kazi kwa pamoja.

Ugonjwa Anaougua Othuol Othuol , Namba Yatolewa Kuchanga Hela

 

 

 

Boni Khalwale atoa sababu za kujihami na mawe Kibra

Seneta wa zamani wa Kakamega Boni Khalwale amejitetea kwa nini alilazimika kujihami kwa mawe katika uchaguzi mdogo wa Kibra uliofanywa juma lililopita.

Khalwale alipigwa picha akiwa amejihami na mawe huku akikabiliana na umati uliokuwa unazua rabsha.

Waziri Mkuu Wa Lesotho Dkt. Motsoahae Thomas Thabane Kuzuru Kenya

Seneta huyo wa zamani ambaye alikuwa amezuru Kibra ili ‘kulinda kura’ za mgombeaji wa Jubilee McDonald Mariga, aliwarushia mawe wahuni hao waliokuwa wamemkabili.

“Nilikuwa nimetulia  kisha takriban vijana 30 wakajitokeza wakiwa wamejihami kwa mawe. Nilikuwa jasiri na nilitaka kukabiliana nao kama mpiganaji wa mafahali kutoka Ikolomani,” Khalwale alisema.

Akizungumza  mjini Kakamega Jumapili, Khalwale  alimlaumu waziri wa usalama wa ndani Fred Mating’i na Inspekta mkuu wa polisi Hillary Mutyambai kwa utepetevu.

“Nawarai waziri Matiang’i na afisa mkuu wa polisi pamoja na katibu mkuu Karanja Kibicho kumakinikia suala la usalama wa wakenya,” alisema.

Alilalamikia kuwa hata baada ya vurugu hizo, polisi  hawakuchukua hatua za kinidhamu kwa wahuni hao.

“Kwanini wakati wahuni  hao walikuwa wakizua rabsha hakuna yeyote aliyechukua hatua dhidi yao ? Polisi waliniacha nikipigania maisha yangu huku wakinitazama.”

Khalwale alisema kwamba hakuwa na  nafasi nyingine ya kujisitiri  ila  kutumia mawe kuinusuru maisha yake.

(+Picha ) Bintiye Akothee, Vesha Okello Avujisha Picha Ya Babake

“Mimi nikasikia hayo kupitia kwa mtandao kwamba ndio hao wanakuja..wakati walinikaribia, nataka musikie, hakunayeyote atakayewashurutisha Waluyha kuwapigia kura,” alisema.

Khalwale alikuwa miongoni mwa  wanasiasa waliokuwa wakipigia debe mgombeaji wa Jubilee McDonald Mariga ambaye alishindwa na Imran Okoth wa ODM.

 

Waheshimiwa Murkomen na Kamket warushiana cheche za matusi kuhusu Kibra

Seneta wa Elgeyo Marakwet Kipchumba Murkomen amelumbana na  mbunge wa  Tiaty  William Kamket  ambaye alidai kwamba juhudi za naibu wa rais William Ruto kutawala eneo la Kibra zimefeli.

Hii ni kutokana na kushindwa kwa mgombea wa chama cha Jubilee McDonald Mariga ambaye anasemekana kuteuliwa na kupigiwa upato na naibu wa rais William Ruto.

Gavana Wa Mombasa, Hassan Joho Alazwa Hospitalini

Kamket alisema kwamba Ruto amefeli kupanda mbegu Kibra baada ya mgombeaji wa chama cha Jubilee McDonald Mariga kushindwa na Imran Okoth.

Akimkashifu Kamket, Murkomen ambaye pia ni kiongozi wa walio wengi katika Seneti alimtetea Ruto huku akimsifia kwa bidii zake.

Aidha, alimkemea Kamket kwamba umaarufu wake katika Baringo umedidimia.

Malumbano hayo yalitokea muda mfupi tu baada ya Ruto kupongeza Jubilee kwa kinyang’anyiro hicho cha Kibra.

Ruto alimpongeza McDonald Mariga na chama cha Jubilee kwa kuvamia na kudhibiti ngome ya Raila.

Ijumaa asubuhi, Imran Okoth wa ODM alitangazwa kuwa mbunge mteule wa eneobunge la Kibra.

Mariga Akubali Kubwagwa, Amualika Imran Chakula Cha Mchana – Video

 

 

Baada ya Kuikomboa ‘Bedroom’ Babu Owino asema wanalenga ‘Sitting room’

Baada ya chama cha ODM kuwabwaga wana Jubilee katika uchaguzi mdogo wa eneobunge la Kibra, kwa sasa mbunge wa Embakasi Mashariki Babu Owino anasema wataka kuikomboa “Sitting room” ya ODM, eneo hilo likiwa Langata.

Eneo bunge la Langata linaongozwa na Mbunge Nickson Korir ambaye aliteuliwa kutoka chama cha Jubilee.

Kupitia mtandao wake wa Twitter, Babu Owino aliishangalia juhudi za ODM kuwapandua wana Jubilee katika uchaguzi wa Kibra kwa kile wanakisema ni ” Bedroom yao”.

“Tumikomboa Bedroom ya Baba, hatua inayofuata ni pale siitngroom (Langata) hawa wageni wametuozea sana!” ujumbe wake ulisoma.

Kijana Ashtakiwa Na Kufanya Mtihani Wa KCSE Kortini

Ujumbe wake ulisoma Hivi ;

Mgombea wa chama cha ODM Imran Okoth aliwabwaga wagombeaji wengine 23 kwa kuzoa jumla ya kura 24, 636, alifuatwa na McDonald Mariga wa Jubilee kwa kura 11,230, Eliud Owalo wa ANC alikuwa wa tatu kwa kura 5,275, huku Khamisi Butichi wa Ford Kenya akifunga nne bora kwa kura 260.

Hata hivyo McDonald Mariga alikubali kushindwa huku akipongeza Imran Okoth.

Alisema kwamba yuko tayari kumuunga mkono Imran kuhakisha kwamba wakaazi wa Kibra wanahudmiwa ipasavyo

Kivumbi Ndani Ya “Bedroom” Huku Raila Akimlambisha Ruto Sakafu

 

Mariga akubali kubwagwa, amualika Imran chakula cha mchana – Video

Mgombeaji wa Jubilee katika uchaguzi mdogo wa Kibra McDonlad Mariga amekubali matokeo ya uchaguzi.

Mariga akimpongeza mshindi wa uchaguzi huo Imran Okoth wa ODM alisema kufurahishwa na jinsi uchaguzi huo ulivyoendeshwa.

Kulingana na kanda ya video, Mariga anaonekana akisema, “Ni Mariga, nimepiga nikuambie congratulations. Kura imekua poa hatujapigana, meeting tulikuwa pamoja na pia niko ready for lunch.”

Alisema kwamba yuko tayari kumuunga mkono Imran kuhakisha kwamba wakaazi wa Kibra wanahudmiwa ipasavyo.

Kivumbi Ndani Ya “Bedroom” Huku Raila Akimlambisha Ruto Sakafu

Baada ya uchaguzi, tuendeleze maisha yetu ya kawaida na kudumisha urafiki wetu,” Mariga alisema.

Akijibu salamu hizo za pongezi na pongezi, Imran kupitia ukurasa wake wa Twitter alimlibikizia sifa Mariga kwa kukubali matokeo na hata kumuunga mkono katika utendaji kazi wake.

Katika uchaguzi huo, Imran Okoth wa ODM ndiye  mshindi kwa kura  24,636, akifuatiwa na mwaniaji wa Jubilee McDonald Mariga aliyepata kura 11,230.

Eliud Owalo wa ANC alipata kura elfu 5,275.

Uchaguzi Kibra: Imran Okoth Apata Ushindi, Mariga Ampa Kongole

Waiguru ampongeza Imran, asema ni ‘zao la Handshake’

Gavana wa Kirinyaga Anne Waiguru amempongeza mbunge mteule wa Kibra Bernard Imran Okoth kwa ushindi katika uchaguzi mdogo uliofanywa Alhamisi.

Kupitia mtandao wake Twitter, Waiguru alimpongeza Imran Okoth huku akisema ni “Zao la Handshake’ katika uchaguzi huo mdogo.

Makosa Aliyofanya MacDonald Mariga, Angembwaga Imran Okoth

Waiguru ambaye ni miongoni mwa wanasiasa wa Jubilee waliojitokeza hadharani kumpigia kampeni Imran Okoth wa ODM licha kwamba kulikuwa na mgombeaji McDonald Mariga wa chama chake.

PATANISHO: Baba Alibomoa Nyumba Yangu Na Kupeleka Mabati Kwa Chifu

Gavana wa zamani wa Kiambu pia alimpongeza ushindi wa Imran.

IEBC imemtangaza rasmi Imran Okoth wa ODM kuwa mshindi wa uchaguzi mdogo wa Kibra. Okoth alipata kura elfu 24,636, akifuatiwa na mwaniaji wa Jubilee McDonald Mariga aliyepata kura 11,230.

Eliud Owalo wa ANC alipata kura elfu 5,275.

 

Kivumbi ndani ya “Bedroom” huku Raila akimlambisha Ruto sakafu

Bernard Okoth ‘Imran’ wa ODM sasa ndiye mbunge mteule wa Kibra kuchukuwa nafasi ya marehemu ndugu yake Ken Okoth.

Afisa mkuu wa uchaguzi katika eneo bunge la Kibra Beatrice Muli alitangaza matokeo rasmi ya uchaguzi huo siku ya Ijumaa asubuhi.

Uchaguzi Kibra: Imran Okoth apata ushindi, Mariga ampa kongole

 Okoth aliwabwaga wagombeaji wengine 23 kwa kuzoa jumla ya kura 24, 636, alifuatwa na Macdonald Mariga wa Jubilee kwa kura 11,230, Eliud Owalo wa ANC alikuwa wa tatu kwa kura 5,275, huku KHamisi Butichi wa Ford Kenya akifunga nne bora kwa kura 260.

Akihutubia wananchi punde tu baada ya uchaguzi kutangazwa Imran aliahidi kushirikiana na wapinzani wake wote ili kuleta maendeleo katika eneo bunge la Kibra.

Imran alisema yeye ni mbunge wa kwanza wa ‘Handshake’na kuapa kuunganisha jamii zote katika eneo la Kibra bila kujali vyama vyao vya kisiasa.

“Mimi ni mtoto wa kwanza wa Handshake kati ya baba Raila Odinga na Rais Uhuru Kenyatta, ajenda yangu kuu itakuwa kuunganisha jamii zote katika eneo bunge la Kibra na kutumikia wananchi wote,” Imran alisema.

Alipongeza wanachama wa vyama vingine chini ya Handshake kwa kumuunga mkono.

Imran aliungwa mkono na wanachama wa Jubilee Gavana wa Kirinyaga Anne Waiguru, Maina Kamanda mbunge maalum, Spika wa Kaunti ya Nairobi Beatrice Elachi na aliyekuwa mbunge wa Dagoreti South Dennis Waweru.

Orodha ya wagombea wa viti mbalimbali ambao hawakujipigia kura wakati wa uchaguzi

 Pia aliungwa mkono na magavana Alfred Mutua wa Machakos ambaye ni kinara wa chama cha Maendeleo Chap Chap, Charity Ngilu wa Kitui ambaye pia ni kiongozi wa chama cha Narck na Kivutha Kibwana wa Makueni.

Boni Khalwale arushiwa mawe na kufurushwa Kibra – Video

Seneta wa zamani wa Kakamega Boni Khalwale amefurushwa na wakaazi wa Kibra  alipowasili katika Wadi ya Laini Saba.

Kulingana na video iliyochapishwa kwenye Twitter, Khalwale anaonekana akitoroka makundi ya watu waliokuwa wakimrushia cheche za matusi.

Aidha, watu hao wanaonekana wakirushia mawe kwa Seneta huyo wa zamani.

Afisa Wa CDF Akamatwa Kwa Tuhuma Za Kuhonga Wapiga Kura Kibra

Baadhi yao walisikika wakisema “”Hapa ni bedroom ya Baba bwana. Hatutaki mchezo”

Kabla ya vurugu hizo, Khalwale alikuwa ametangaza kwenye Twitter kwamba alikuwa katika maeneo ya Kibra.

 

“Deep inside Kibra. Mambo iko bara bara kabisa!”  taarifa kutoka mtandao wake ulisoma.

Masaa chache baada ya kisa hicho, Khalwale aliwahutubia wanahabari kuwa uchaguzi wa Kibra unaendelea vyema ila woga wa ODM unawafanya kutoa malalamishi kuhusu madai ya wapiga kura kuhongwa.

Utacheka Ufe! Tazama Jinsi Wapigaji Kura Walivyojitokeza Kibra

“Tumepiga kampeni ya kutosha ndiyo maana ODM wanatuogopa kinachowapelekea kutoa madai ya rushwa,” alisema.

Baadaye Polisi walimwamuru Khalwale kuondoka maeneo hayo.

Awali  Kiongozi wa ODM Raila Odinga amewataka wapiga kura wa Kibra kulinda kura zao katika uchaguzi mdogo unaoendelea.
“Tuko katika chumba chetu cha kulala ‘bedroom’ na nataka kuuliza watu wetu kulinda bedroom yetu dhidi ya watu wa nje,” Raila alisema.

Uchaguzi mdogo wa eneo bunge la Kibra umevutia jumla ya wagombeaji 24.

Uchaguzi Wa Kibra: IEBC Yatoa Onyo Kali Dhidi Ya Usambazaji Wa Picha Za Kura

Uchaguzi wa Kibra: IEBC yatoa onyo kali dhidi ya usambazaji wa picha za kura

Tume ya IEBC imewaonya wapiga kuzingatia siri za upigaji kura na kukoma kusambaza mtandaoni picha za kura zilizopigwa.

Kupitia mtandao wa Twitter, tume huru ya uchaguzi na na mipaka imeonya kwamba ukiukaji wa sheria hiyo

 

 

Fahamu Wagombea 24 Waliojitokeza Katika Uchaguzi Mdogo Wa Kibra

Hii ni baada ya mpiga kura wa Kibra kupiga picha ya karatasi za kura na kuchapisha katika mtandao wake Alhamisi.

Ballot 2-compressed

Mpiga kura katika eneo la Kibra baada ya kupiga kura.

Wapigakura walijitokeza asubuhi na mapema katika wadi tano za Kibra huku milolongo mirefu ikishuhudiwa.

Chama Cha ODM Chamwonya Musalia Mudavadi Dhidi Ya Kujipendekeza

Sheria za uchaguzi zinaeleza kuwa kila mtu aliye katika kituo cha kupigia kura anafa kudumisha na kuzingatia sheria ya usiri wa upigaji kura.

 

Ballot 3-compressed

 

Yeyote anayekiuka sheria za siri za kura ni kosa la jina na anaweza kushatkiwa na kuhukumiwa kifungo kisichozidi miaka mitatu au faini ya shilingi milioni moja au yote mawili.

Kiti cha ubunge cha Kibra kiliachwa wazi baada ya kifo cha aliyekuwa mbunge Ken Okoth.

MacDonald Mariga Atua Lindi, Hana Uwezo Wa Kujipigia Kura