Wee! Cheza na slayqueens wa Nairobi ukipate,Mwanamke afikishwa mahakamani kwa madai ya wizi

Mwanamke katika mtaa wa mabanda wa Kibra jijini Nairobi amefikishwa mahakamani baada ya kudaiwa kumwibia Miss World 1997 Diana Hayden shilingi 209,809.

Akifikishwa mbele ya hakimu wa mahakama hiyo Joyce Gandani, mshukiwa Ashpal Boghal Ghir anashukiwa kuchukuwa hela hizo kutokana na uhusiano wao waliokuwa nao wawili hao.

Hata kama anakulipua lungula hatujui sisi, Tanasha akana madai kuwa Jamal ni mpenziwe

Mahakama iliarifiwa kuwa Hayden na Ghir walikuwa marafiki wa kufa kuzikana kwa muda mrefu kabla ya kisa hicho kutokea mnamo Machi 30 na Apri 9, mwaka  huu katika eneo la Galleria Gardens, Lang’ata jijini Nairobi.

Woman charged for stealing Ksh.200,000 from Miss World in Nairobi

Mshukiwa alikataa makosa hayo na kuachiliwa kwa dhamana ya shilingi 70,000.

Hayden alishinda tuzo ya Miss World mwaka 1997.

Alidhani albamu yetu haitafana! Ethics na Octopizzo wajibizana

Ni raia wa India ambaye kufikia sasa amewahi kushinda tuzo hiyo.

 

Polisi watawanya watu eneo la Mlango Kubwa kwa kujaribu kuingia Eastleigh

Maafisa wa usalama asubuhi hii wamelazimika kutumia vitoa machozi ili kuwatawanya wakaazi wa mtaa wa Mlango Kubwa waliokuwa wanataka kuvuka vizuizi vilivyowekwa na polisi kuvuka katika mtaa wa Eastleigh uliofungwa na serikali kama njia ya kupunguza usambaaji wa virusi hatari vya corona.

Ni mara ya pili sasa polisi kulazimika kuwatanya wakaazi katika maeneo hayo ambao wamekuwa wakijaribu kwende kiunyume na sheria kuhusiana na utaratibu uliowekwa na serikali.

Jinamizi jingine kwa taifa! Watu 13 wamefariki kutokana na kipindupindu

Mtaa wa Easytleigh na Mji wa Kale Mombasa uliendelea kufungwa na serikali hadi Juni tarehe 6.

Image

Kwengineko ni kuwa, mwili wa mwanafunzi wa darasa la tano katika mitaa ya Kibra jijini Nairobi umetolewa katika Kidimbwi kilichojaa maji eneo la Soweto.

Image

Shughuli zimesitishwa katika mpaka wa Malaba baada ya madereva kufunga njia

Image

Shughuli ya kuopoa mwili huo imefanikishwa na wakaazi wa mtaa huo.

Mkono wa mhisani! Evans Oluoch asambaza barakoa Kibra

Evans Oluoch ambaye ni nduguye Ken Okoth ambaye alikuwa mbunge wa Kibra, ameamua kuwasambazia wakaazi wa mtaa wa Soweto eneo hilo barakoa na vitakasa mikono kama njia ya kuwasaidia wakaazi hao kudumisha usafi wakati huu ambapo virusi hivyo vinaendelea kupenya katika vitongoji mbalimbali nchini.

ImageImageImage

Mtaa wa Kibra umeanza kuipa serikali changamoto hasa baada ya jamaa mmoja aliyefariki katika kaunti ya Bomet kubainika kuwa alikuwa anaishi mtaa huo.

Wahudumu wa kliniki katika soko la Toi Kibra wawekwa kwenye karantini

Visa kadhaa vimekuwa vikiripotiwa kutoka Kibra hatua ambayo imewafanya baadhi ya wahisani kujitokeza na kuwapa wakaazi ufadhili wa barakoa.

 

Mvulana wa miaka 14 akamatwa kuhusiana na mauaji ya mwanahabari Kibra

Polisi wamemkamata mvulana mwenye umri wa miaka 14 kuhusiana na amuaji ya mtangzaji wa kituo cha redio cha Pamoja FM mtaani Kibra  Mohamed Marjan.

Penzi la sumu? Tazama waliopendana licha ya pingamizi kutoka kwa jamii-Kuanzia kwa Tecra Muigai hadi kwa Wambui Otieno na Princess Diana

Mohamed  alipatikana ameuawa Mei tarehe 4 na mwili wake ukiwa barabarani eneo la Makina karibu na mahakama ya Kibera. Makachero wamemkata mshukiwa huyo baada ya kuitathmini kanda ya video yaa ya CCTV. Alikuwa akielekea nyumbani  alfajiri baada ya kufanya kipindi cha usiku cha ‘ Ukumbi wa Kiislamu’ 

Picha hiyo ya video ilimuonyesha mvulana huyo mwenye umri wa miaka 14 akiwa pamoja na watu wengine wane wanaoshukiwa kuwa majambazi  wanaohudumu katika mtaa huo wa mabanda. Polisi wanasema washukiwa hao walimshambulia marehemu akiwa anaenda nyumbani. Kundi hilo kisha lilimwibia  kabla ya kumdunga kisu kifuani na kumuua papo hapo.

Usaliti ama ni siasa? Ruto atembea kwenye wembe wenye makali huku Uhuru akianza kuchukua udhibiti

Mshukiwa mmoja alivamiwa na  wananchi kabla ya kutoroka. Polisi wanaendelea kuwasaka washukiwa wengine  watatu na mwanamke anayeaminika kuwapa hifadhi washukiwa hao. Polisi wamesema  kwamba mshukiwa wa pili alikamatwa na ndiye aliyetambua majina ya wenzake. Marijan  alikuwa mwanahabari aliyejituma na alikuwa nguzo muhimu kuanzisha kituo hicho cha redio mwaka wa 2006.

Jamaa anayeshukiwa kuhusika na mauwaji ya mwanahabari Marjan atiwa mbaroni

NA NICKSON TOSI

Jamaa wa miaka 19 anahusishwa na mauwaji ya mwanahabari Mohammed Hussein Marijan ametiwa nguvuni na maafisa wa polisi.

Mwanamke anayesemekana alipanga njama na kikundi cha watu sita pia anatafutwa na maafisa wa usalama.

 

“We still have a lot to do and we cannot disclose more details. We are, however, optimistic that all the people responsible for the killing will be brought to book,”Lucas Ogara OCPD wa  Kilimani amesema .

Marjan alikumbana na kifo chake eneo la Makina, mtaa wa Kibra mita chache tu kutoka kwa mahakama za Kibra akiwa anatoka kazini..

Marjan-730x414

Polisi waanzisha uchunguzi kuhusiana na Kifo cha Mwanahabari Marijan

Taarifa zinasema kwamba mwanahabari huyo alikuwa mmoja wa wanakamati wa shirika la Kibera Policing Committe na aliuwawa kwa kudungwa kisu mara sita na kufa papo hapo.

Ogara aidha amesema wanaoendesha uchunguzi huo wataangazia sana kamera za siri ili kubaini waliotekeleza mauwaji hayo.

 

Polisi waanzisha uchunguzi kuhusiana na Kifo cha Mwanahabari Marijan

NA ICKSON TOSI

Maafisa wa usalama sasa wameanzisha uchunguzi kuhusiana na kifo cha mwanahabari wa stesheni ya Pamoja Fm Mohamed Hassan Marijan ambaye aliuwawa asubuhi ya leo akitoka kazini karibu na mahakama ya Kibra.

Naibu Kamishna wa Kibra Gideon Ombogi amesema maafisa wa polisi wametumwa kuanzisha uchunguzi kuhusiana na kisa hicho.’

Kifo cha Marijan kilisababisha wananchi kuanzisha uchunguzi wao wa yule aliyetekeleza unyama huo. Mmoja wa washukiwa anayehusishwa na mauaji hayo ametiwa mbaroni huku maafisa wa polisi Kibra wakishutumiwa kwa kulaza damu na wananchi.

Tanzia! Mwanahabari wa stesheni moja Kibra auwawa akirejea nyumbani

 

Mwili wa Marijan umepelekwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha City huku uchunguzi wa kubaini kilichosababisha kifo chake ukitarajiwa kutolewa na wapasuaji.

Kwingineko ni kuwa katika kaunti ya Kirinyaga, maafisa wa polisi wameanzisha uchunguzi kuhusiana na kifo cha kutatanisha cha mtoto wa miaka 4 msichana  kilichotokea eneo la Gitoo.

Hasira ni Hasara: Mwanamke akamatwa Kayole kwa kuwaua watoto wake 2

Inadaiwa kuwa mama mzazi wa mtoto huyo alikuwa anakunywa bia katika nyumba ya mwanamume mmoja eneo hilo wakati tukio hilo lilipojiri.

Akidhibitisha tukio hilo, mkuu wa polisi Mwea Magharibi Aden Alio amesema tukio hilo liliripotiwa katika kituo cha polisi cha Kangai na Thomas Chomba, mjomba wa mwendazake.

 

 

Tanzia! Mwanahabari wa stesheni moja Kibra auwawa akirejea nyumbani

NA NICKSON TOSI

Mwanahabari wa kituo cha Pamoja Fm Mtaani Kibra Mohamed Hassan Marijan amepatikana kama ameuwawa na genge la wahalifu mtaani Kibra, eneo la Makina asubuhi ya leo.

Mpenziwe Tecra Muigai Omar Lali akamatwa kuhusiana na kifo chake

Marijan alikutana na kifo chake usiku alipokuwa ametoka kufanya kipindi cha Ramadhan .

Image

Alikuwa amehudumu katika stesheni hiyo kuanzia mwaka 2016.

 

Bando zinayeyuka Insta, Mwonekano wa Stivo Simple Boy unakosha wengi (+Picha)

Picha za mwanamuziki kutoka mtaa wa mabanda wa Kibra zinayeyusha bando za watu Insta .

Kijana huyu sasa ndio gumzo kitaani baada ya kuvuma na bonge la ngoma.

Stivo Simple Boy aliteka vichwa vya habari alipovamia tansia ya muziki na mkwaju wa Mihadarati.

Ngoma hii ilipokelewa vizuri katika mitandao ya YouTube huku wengi wakionyesha kuipa shavu talanta yake.

Soma hadithi nyingine;

Drama za Ng’ang’a zashika kasi Marekani, Snoop Dogg atupa dongo (+Video)

Kwa sasa Stivo amekuwa gumzo Insta na suti za bluu;

Mastaa nchini akiwemo Chipukeezy, Khaligraph Jones walionyesha nguvu kubwa ya kuinua talanta ya Simple Boy.

Stivo alikuwa anafanya kazi ya mjengo kabla avume zaidi katika mitandao ya kijamii.

Rapa Khaligraph aliwahi kufoka jinsi vyombo vya habari vilikuwa vinamshobokea kijana huyu katika mahojiano.

Soma hadithi nyingine;

George Magoha atoa kauli, NBI yataja jumba la Precious Talent pango la kifo

Kulingana na Khaligraph, baadhi ya vyombo vya habari vingemtumia kupata hadhira na baadaye kumtema.

“Kila mtu sasa anataka kuoenekana na huyu kijana…kumuita katika interviews ili kuzidisha pato badala ya kuongea naye kuhusu muziki.” Khaligraph

Khaligraph alikuwa wa kwanza kumuomba Chipukeezy kuhakikisha kuwa Stivo yuko sawa.

Chipukeezy alimjibu kuwa,

“Stivo ni msanii wa kawaida, kwa hivyo akiitwa katika interview anapaswa kufika ili auze muziki wake.”

“Nimefanya nilichopaswa kufanya na sasa Simple Boy ni balozi wa Nacada…” Alisema chipukeezy.

Kwa sasa Stivo Simple Boy anatesa zaidi katika mitandao Insta.

Soma hadithi za Abraham Kivuva

 

‘Alinilazimisha kulamba uume wake, akanibaka na kuiba pesa zangu,” asimulia kortini

Mwanaume ameshtakiwa kwa kosa la kumshambulia mhudumu wa kike wa mkahawa kwa kisu, akamlazimisha kulamba uume wake, akambaka na kisha kumwibia shilingi 630 kutoka akaunti yake ya M-Pesa.

Charles Mbusiro hata hivyo alikana mashtaka hayo mbele ya hakimu mkaazi wa Kibera Boaz Ombewa.

Mbusiro anadaiwa kumnajisi kidosho huyo baada ya kumlazimisha kumvuta hadi kichakani katika eneo la Uthiru jijini Nairobi Disemba 4.

Aidha, alishtakiwa kwa kumshika sehemu za siri za Angela (silo jina lake rasmi) na kumwibia shilingi 130 kutoka begi lake na shilingi 600 kutoka akaunti ya M-Pesa.

Ripoti ya polisi inasema kuwa Mbusiro alimshambulia mwanamke huyo alipokuwa akitoka kazini.

ODM Yateua Jopo La Kurahisisha Mapendekezo Ya BBI

“Nilitoka kazini Githurai ninapofanya kama mhudumu wa mkahawa na nilipofika Uthiru nilinunua chapati na mayai na kisha kutembea kuelekea kwangu. Kulikuwa na mwanaume wa umri wa makamo mbele yangu,” ripoti ya polisi inasema.

Anasema kuwa Mbusiro alimtishia kwa kisu na akalazimika kukubali amri zake bila hiari ili kunurusu maisha yake.

“Alinishika kutoka nyuma nilipogeuka kumwaangalia. Alinitishia kwa kisu huku akisema nikubali au aniue,” alisema.

Kisha jamaa huyo alimpeleka kwenye msitu na kumnajisi na kumwibia.

“Alinivuta hadi kichakani chenye mahindi na nyasi nyingi, akanilazima nilambe uume wake na kunibaka mara kadhaa kisha akaiba pesa zangu,” alisema.

Kidosho huyo anasema kuwa alilazimishwa kuvua nguo zake na kuweka juu ya mti wa parachichi.

Gavana Sonko Apelekwa Hospitalini KNH Kwa Matibabu Ya Dharura

Baada ya kumaliza haja yake, msichana huyo alilazimishwa kujipangusa kwa nguo zake na kutishia kutotoa siri hiyo kwa mtu yeyote.

“Alinilazimisha kutoa pin yangu ya mpesa na kujitumia pesa zote kisha akatoa simcard yangu,” alisema.

Mbusiro alikana mashtaka hayo na kupewa bondi ya shilingi 600,000 na mdhamani wa kiasi hicho.

Kesi hiyo itasikizwa tena Machi 3 mwaka ujao.

Watu Watano Wafariki Dunia Kutokana Na Mlipuko Wa Volkano

Utacheka ufe! Tazama jinsi wapigaji kura walivyojitokeza Kibra

Kwa kweli wazungu wa zama za kale hawakukosea waliposema kuwa kucheka ndio dawa bora.

Basi leo siku ambayo wakazi wa Kibra walikuwa wamengoja kwa hamu na ghamu, iliwadia na walijitokeza kwa maelfu ili wakampigie kura mgombea wa kiti hicho cha Kibra, wanayemu enzi.

PICHA: Mamake Ken Okoth apiga kura katika uchaguzi mdogo Kibra

Basi baadhi ya wana Kibra waliojitokeza walikuwa na mavazi na mitindo ya kipekee ambayo kwa uhakika yalivunja baadhi ya shingo katika maeneo hayo ya kupigia kura.

Jamaa mmoja aliwashtua wengi alipovalia suruali refu ajabu ambayo ilikuwa imefungiwa kifuani kinyume na kawaida yake, ambapo ni kiunoni.

Tazama picha zifuatazo.

Uchaguzi wa Kibra: IEBC yatoa onyo kali dhidi ya usambazaji wa picha za kura

kibra 4 kibra 3 kibra 2 kibra