(+Picha )Harmonize aifunika tatoo aliyochora ya Diamond kwa michoro

Ni wazi na bayana kuwa staa wa muziki Harmonize hataki kabisa kuonekana na tatoo aliyojichora ya bosi wake Diamond Platnumz.

Tatoo hii aliichora kipindi na ambapo alikuwa chini ya lebo ya Wasafi.

Alikuwa ameichora kuonyesha ni kwa kiasi gani anavyothamini nafasi aliyopewa ya kujulikana kuwa ana kipaji duniani.

Image result for harmonize diamond

(+ Video) Kero kwa Zari The Boss Lady ,Diamond Platnumz na Tanasha kwenye penzi moto

Diamond alikuwa mtu wa kwanza kugundua kipaji cha Harmonize na akawekeza katika kipaji chake katika hali ya kumsaidia atoke kimuziki.

Mcheshi Chipukeezy ashangaza wengi na hili vazi la kufuzu chuo kikuu

Hatimaye Harmonize aliitema lebo hii na kuanzisha yake ya Konde Gang.

Kwa kile kinachoonekana kama kujisahau na kuingiwa na ustaa mwingi, Harmonize amefunika tatoo hiyo na michoro mingine.

Image result for harmonize tattoo

Ushikaji umepotea kati ya mastaa hawa wawili.

Katika fiesta iliyofanyika uwanja wa Uhuru Dar Es Salaam, Konde Boy alikosa kumtaja Diamond katika phrase aliyomtaja ya ngoma ya Uno.

 

UNO ya Harmonize yatolewa YouTube, ubishi wa Magix Enga na Konde Gang

Meneja wa lebo ya Konde Gang ya Harmonize amefunguka kuhusu ngoma ya UNO kufungiwa.

Hii ni baada ya ubishi kuzuka kuwa midundo ya mkwaju huu ni ya producer wa hapa nchini Magix Enga.

Meneja wa Harmonize amefunguka kupitia mtandao maridhawa wa Insta,

“Tumepata taarifa kutoka mtandao wa YouTube kwamba producer wa Kenya ametuma baruapepe kudai umiliki wa ngoma ya UNO…”

(+Video ) Size 8 afunguka A-Z alivyopata presha akijifungua, video ya kinyonge

“Kwa utaratibu wa mtandao huu, ni lazima wafungie nyimbo hii kuonekana wakiendelea na juhudi za kufuata madai hayo…”

Meneja huyu aidha aliwaomba wafuasi na mashabiki wawe watulivu swala hili likifuatiliwa ili kubaini ukweli.

Alichokisema babake kuhusu mauaji ya Monica Kimani,Jowie ni mhusika mkuu

Magix Enga ni producer mkubwa hapa nchini na alitoa lalama zake kuhusu midundo ya ngoma hii.

“1 Week Imeisha and The song Uno is no longer on YouTube Don’t sample magix Enga Beats. I repeat, dont! Like I said i’m not going to allow this to happen not in 254 🇰🇪..” Alichapisha Magix punde tu ngoma hiyo ilipofungiwa.

 

Harmonize ni msanii namba moja kwa sasa Tanzania – Q Chief

Staa mkongwe wa Tanzania Q Chief sasa anahoji kuwa Harmonize kwa wakati huu ndiye staa mkubwa Tanzania.

Katika mahojiano, Q Chief ambaye anaonekana karibu sana na Konde Boy amezungumza mengi kuhusu maisha yake ya muziki.

Aidha, staa huyu amesema kuwa kutoka kwa Harmonize WCB ni ishara ya mwana kukua.

“Kuna kipindi mtoto analelewa na baba. Kikubwa unachotakiwa kujua ni kumheshimu baba. Harmonize sijawahi sikia akimzungumzia Diamond vibaya…”

Soma hadithi nyingine:

Rayvanny aweka wazi taarifa za kusaliti Mkewe Fayma kwa Elizabeth Lulu

Q Chief amesema kuwa yupo kwenye usimamizi wa  Konde Gang ya Harmonize.

“Konde Gang ni lebo yangu. Nyuma ya hizo projects yupo mwenyezi Mungu…”

Kama mwandani wa Harmonize, staa huyu amekana taarifa za uhasama kati ya Diamond na msanii aliyemtengeza.

“Tangu hizi issues zianze, Harmonize sijawahi sikia akizungumza kitu negative kumhusu Diamond…”

“Ni kwa sababu anaheshimu. Watu wanatakiwa kuona vile ana akili kubwa.”

Kuhusu iwapo anajua kilichofanyika kupelekea Harmonize kuitema WCB, Q Chief amesema kuwa ana ufahamu wowote.

Soma hadithi nyingine:

Swaleh Mdoe atokwa na povu, siasa za uanahabari zimemchosha

‘Nyuma ya pazia hatujui ni nini kinaendelea. Ukaribu wangu na Harmonize haunipi kujua kabisa kinachofanyika.”

Aidha, amewaonya watu wanaomchamba staa huyu katika mitandao ya kijamii.

“Inaniuma sana mtu anaposema atakwama. Kwa nini mtu hafikirii kuwa Mungu atamsaidia apae juu.”

“Comment mbaya zinamjenga na hata comment nzuri zinamfanya awe imara zaidi.”

“At least naona furaha iliyopotea miaka mingi. Nawashukuru sana waandishi wa habari, nimshukuru Harmonize, Diamond kwa kuipeleka game juu.”

“Lakini sisemi kuwa msanii wangu Harmonize hana mchango wowote. Kama unavyoona sasa,yeye ndiye msanii namba moja Tanzania.”

 

Harmonize ataja mastaa Tanzania waliojunga na Konde Gang, aitaja WCB

Staa na nyota wa Bongo Harmonize ametaja baadhi ya majina ya watu ambao watakuwa katika lebo ya Konde Gang.

Ikumbukwe kuwa staa huyu ndiye kifungua mimba cha lebo kubwa Afrika Mashariki ya WCB iliyopo mjini Dar nchi jirani ya Tanzania.

Harmonize almaarufu kama Konde Boy amekuwa mkubwa kwa kupiga nyimbo hatari na kushirikisha mastaa wakubwa kutoka nchi jirani kama Uganda na Nigeria kati ya nyinginezo.

Matamasha anayoyafanya ni makubwa sawa na bosi wake Diamond Platnumz.

Soma hadithi nyingine;

(+Meseji zavuja ) Willy Paul aonywa, meseji za ufisi Insta

Dogo ana mpenzi wa haiba ya juu sana Sarah.

Ana walinzi sawa na idadi ya Diamond. Kumewahi kutokea vyombo vya habari nchini Tanzania zinazowalinganisha wawili hawa.

Katika mahojiano, staa huyu aliitetea Konde Gang na kutaja watu walio katika lebo hiyo,

“Sisi tunakuwa kila siku na watu wanatupenda. Jamii inatupenda na inatufuatilia sana. Konde Gang ni still WCB.”

“Konde Gang itakuwa na mastaa wa wengine sio mastaa. Nadhani kwa sasa umeona Jose wa Mipango Jabulanti, Choppa,Mnyama Mkali, Budda na Mchachambo .”

“You know Young Money right, you know cash money right. Come on why are you asking?” Alisema Harmonize.

Kwa usemi huu, staa huyu anasema hana matatizo na WCB.

Soma hadithi nyingine;

Zitakavyofanyiwa noti mzee za elfu, M-Pesa kukoma kuchukua Alhamisi

 Hii inatokea kuwa tofauti na matendo yake baada ya kufanya hafla ya ndoa na kukosa kuwaalika mastaa wa WCB

Wanandoa hawa walihakikisha wameipanga hafla hiyo kwa mbwembwe zote na hawakuwaalika mastaa wa WCB.

Soma hadithi nyingine;

Mkali wa “Lubbish” apigwa faini ya 1M kwa kuonyesha video chafu, ajitetea

Mzee Abdul anahoji kuwa dalili za Harmonize kuwa ana uwezo wa kufanya na kusimamia fiesta zake nje ya nchi ni ishara kuwa mwana kashakua na kwa hivo kutoka kwake ni kwema kwa maslahi yake.

Anadokeza kuwa labda dogo kapewa ushawishi na marafiki wake ili kufanya uamuzi huo.

”Kwanza Naseeb alimuangaikia sana. Kamtufuta kampa sapoti kubwa kamtoa kimuziki,” Mzee Abdul.

“Harmonize sio mtoto. Ukiona mtu anatoka kashakomaa tayari.

Konde Gang ya Harmonize yaachilia mdundo. WCB yadondosha ya Mbosso

Staa na fundi wa muziki nchini Tanzania Harmonize amedondosha ngoma ya kwanza Inabana tangu adondoshe barua ya kuvunja mkataba wake na lebo inayoongozwa na Diamond Platnumz. Ngoma hii iliyochapishwa kwenye mtandao wa YouTube masaa 10 yaliyopita amemshirikisha Eddy Kenzo kutoka nchi jirani ya Uganda.

Soma hapa:

Eric Omondi atokwa na povu insta. Afunguka jinsi Ebru ilivyomtesa Chipukeezy

Harmonize ameanzisha lebo yake Konde Gang ambayo anapania kuwasaini mastaa wengine wa muziki. Aidha, katika mahojiano Meneja wa WCB Babu Tale alisisitiza kuwa chochote Harmonize atakwenda kuanzisha kinachohusiana na burudani, kutakuwepo na pato itakayokuwa inaingia Wasafi.

Hii ni kufuatia makubaliano katika mkataba wao na staa huyu ambao unatajwa kama ulikuwa wa miaka 15. Katika mahojiano hayo, Tale alitoa tamko kuwa mtu yeyote hawezi siku moja dhubutu kung’ara zaidi ya bosi wake. Hii ni ishara kuwa labda kinachopelekea mtifuano katika Wasafi na Konde Boy huenda dogo alionyesha makali ya kumtoa Diamond Platnumz kwenye game.

Soma hapa:

Inspekta Mwala anusurika kichapo cha umati. Agonga na kuua mtu papo kwa hapo

Kando na kuchonganishwa na vyombo vya habari, Harmonize anapata kero kubwa kwa mashabiki katika mitandao ya kijamii baadhi yao wakihapa kuzima stima za ushabiki kwake.

Lebo ya WCB imedondosha ngoma Shilingi ya Mbosso akimshirikisha Reekado masaa 5 baada ya Harmonize kutoa. Hii inaweza kutafsiriwa kama njia moja ya kufunika ngoma ya Harmonize. Mondi pia anatarajiwa kudondosha ngoma yake muda usio mrefu ili kuonyesha ubabe katika tasnia ya muziki wao.