Ni nani mshambulizi bora katika ligi ya Uingereza?

Ligi ya Uingereza ambayo inajulikana sana barani Ulaya kwa kukuza washambulizi bora duniani umeendelea kushuhudia ushindani mkubwa kutoka kwa wachezaji mbalimbali wanaochezea klabu tofauti.

Katika msimu huu wa mwaka 2019/2020, washambulizi wengine wapya wamejitokeza na kuthibitisha makali yao kwa kutikisa nyavu zaidi ya mara tano.

Wachezaji hao ni Tammy Abraham na Teemu Pukki ambao wanachezea klabu ya Chelsea na Norwich.

Wabunge wa ODM waagizwa kufika mbele ya NCIC

 Ligi hiyo ya Uingereza bado haujakamilika lakini wafuatao ni wachezaji ambao wamefunga mabao zaidi tangu msimu huu uanze;

Jamie Vardy

Mshambulizi huyu anachezea klabu ya Leicester na vile vile ameweza kufunga mabao 17.

jamie

Sergio Kun Aguero

Mshambulizi huyu ambaye ametajika kwa muda wa karibu miaka tano katika ligi ya Uingereza kwa makali yake anaichezea klabu ya Manchester City.

Kwa sasa anaongoza katika orodha hilo la wachezaji ambao wamefunga bao huku akiwa ametikisa nyavu mara tisa.

aguero

Tammy Abraham

Ni mshambulizi katika klabu ya Chelsea. Vile vile ameweza kufunga mabao kumi na moja msimu huu.

tammy

Pierre Emerick Aubameyang

Anachezea klabu ya Arsenal. kwa sasa Aubameyang ameweza kupachika mabao 11.

Aubameyang

Raheem Sterling

Muingereza huyu anachezea klabu ya ManCity na ameweza kutikisa nyavu mara tisa.

raheem

 

‘Je wakumbuka tulichokubaliana?’ Ruto amuuliza Uhuru leo ikiwa birthday yake!

 

 

Arsenal vs Man City: Baada ya kupokea kichapo dhidi ya Man United, Guardiola ataandikisha ushindi leo?

Klabu ya Manchester City hii leo watakuwa wanachuana na klabu ya Arsenal Ugani Fly Emirates. Ni mechi ambayo mashabiki wa soka wamengoja kwa hamu  lengo likiwa kuthibitisha nani bora zaidi.

Man City waliweza kupoteza mechi dhidi ya Man United wikendi iliyopita nyumbani kwao Etihad baada ya bao ya Marcus Rashford na Anthony Martial kuwahakikishia United ushindi.

City kwa sasa wanashikilia nafasi ya tatu wakiwa na pointi 32.

(+ Picha) Diamond Platnumz abuni njia mpya ya kuwaongea na watoto wake

 Arsenal kwa upande wao wameweza kuonyesha kuwa bado wapo katika shindano ya kumaliza nne bora katika ligi hiyo ya Uingereza hii ni baada ya kuambulia ushindi ya mabao 3-1 dhidi ya Westham wikendi iliyopita.

Arsenal kwa sasa wapo katika nafasi ya tisa wakiwa na pointi 22.

Nani ataibuka mshindi? Yote hayo yatathibitishwa leo.

Mechi zingine zitakazochezwa leo ni;

Manchester United vs Everton

rash

Wolves vs Tottenham

LONDON, ENGLAND - DECEMBER 29:  Adama Traore of Wolverhampton Wanderers battles for possession with Christian Eriksen of Tottenham Hotspur during the Premier League match between Tottenham Hotspur and Wolverhampton Wanderers at Tottenham Hotspur Stadium on December 29, 2018 in London, United Kingdom.  (Photo by Marc Atkins/Getty Images)

(+Mistari, Video) King Kaka atangaza kuitoa ngoma ya ‘Wajinga Nyinyi’ YouTube

 

Derby ya Manchester: City ama United, nani ataibuka mshindi?

Leo ni leo kwani msema kesho atabaki kuwa muongo.

Derby ya Manchester katika ligi ya Uingereza itakuwa inachezwa leo huku ushindani mkubwa ukitarajiwa kutoka kwa klabu hizo mbili, Manchester City na Manchester United.

Klabu gani bora? wachezaji wa kutazamiwa hii leo ni kina nani? Mkufunzi yupi ni bora? Wachambuzi wamechambua, mashabiki wametoa ubashiri, lakini leo yote hayo yatathibitishwa.

Sonko akamatwa na maafisa wa DCI Voi akiwa kwa SGR

Vijana wake Pep Guardiola watakuwa wanawakaribisha Man United nyumbani kwao Etihad.

Kwa sasa Man City wanashikilia nafasi ya tatu wakiwa na pointi 32, huku Man United kwa upande wao wanashikilia nafasi ya 6 wakiwa na pointi 21.

Man United waliweza kuwanyuka Tottenham mabao 2-1 katika mechi iliopita, je leo watawaadhibu Man City?

Mume wangu anataka watoto ila hataki nipate periods – Ruth

 

Baada ya kumpiga kalamu Unai Emery, Arsenal wataandikisha ushindi leo?

Klabu ya Arsenal hii leo watakuwa wanachuana na Brighton katika ligi ya Uingereza.

Arsenal walisitisha ukufunzi wa Unai Emery wiki jana baada ya matokeo duni katika msimu huu na kwa sasa wanashikilia nafasi ya 10 wakiwa na pointi 19.

Afisa wa polisi atuhumiwa kumbaka mwanawe na kujificha Tanzania

 Katika mchuano uliopita dhidi ya Norwich, Arsenal waliambulia sare ya mabao mawili, na hii leo watakuwa wanategemea huduma ya washambulizi wao Pierre-Emerick Aubameyang, Alexandre Lacazette, na Nicholas Pepe kushinda mechi hiyo.

Brighton kwa upande wao wanashikilia nafasi ya 16 wakiwa na pointi 15.

Nani ataibuka mshindi? Yote hayo yatathibitishwa leo usiku.

Samuel Eto’o arejea chuoni Harvard, nia ni ‘kupata ujuzi na kuinua jamii’

Ligi ya Uingereza: Man City wataweza kutetea taji lao?

Klabu ya Manchester City hii leo watakuwa wanachuana na Newcastle uwanjani St James Park.

Pep Guardiola ambaye ni mkufunzi wa City ana matumaini kuwa vijana wake bado wanaweza kutetea taji hilo kwani kwa sasa City wanashikilia nafasi ya tatu wakiwa na pointi 28 nyuma ya Liverpool na Leicester ambao wako na pointi 37 na 29 mtawalia.

Fred Matiang’i awazomea TangaTanga Kirinyaga, atoa onyo kali

 Newcastle kwa upande wao wanashikilia nafasi ya 14 huku wakiwa na pointi 15.

Mechi zingine zitakazochezwa hii leo ni;

Liverpool vs Brighton

trent

Burnley vs Crystal Palace

cahill

Chelsea vs Westham

LONDON, ENGLAND - APRIL 08: Chelsea's Ngolo Kante and West Ham United's Angelo Ogbonna during the Premier League match between Chelsea FC and West Ham United at Stamford Bridge on April 8, 2019 in London, United Kingdom. (Photo by Rob Newell - CameraSport via Getty Images)

Tottenham vs Bounermouth

son

 

Tujitayarishe kupiga kura ya BBI, Kinara wa ODM Raila Odinga

Ligi ya Uingereza: Mechi kali ya kutazamwa wikendi

Ligi ya Uingereza itakuwa inasakatwa hii leo baada ya mapumziko mafupi ya juma moja. Klabu mbalimbali zimejiandaa vilivyo ili kuhakikisha kuwa wikendi hii wataandikisha ushindi.

Wikendi hii ni ya kusisimua kwani mechi kali zaidi itakuwa Manchester City dhidi ya vijana wake Frank Lampard Chelsea. Kumbuka Pep Guardiola ambaye ni mkufunzi wa Mancity aliweza kuadhibiwa vikali na Liverpool kule uwanjani Anfield kwa kunyukwa mabao tatu kwa moja.

Uhuru afoka! ni mjinga asiyejua maana ya BBI

Ni kichapo ambacho kilichangia klabu ya City kushushwa daraja hadi nambari nne katika ligi hiyo wakiwa na pointi 25.

Chelsea kwa upande wao wanashikilia nafasi ya tatu wakiwa na pointi 26 baada ya kuandikisha ushindi katika mechi yao dhidi ya Crystal Palace.

Je, nani mkali zaidi? Mancity ama Chelsea? yote hayo yatathibitishwa wikendi hii.

azpli

Mechi nyingine ya kutazamiwa wikendi hii ni ya klabu ya Tottenham ikichuana na Westham.

Si mechi kali vile lakini umuhimu wa mechi hiyo ni je, Jose Mourinho ambaye ni mkufunzi wa sasa wa Tottenham baada ya Mauricio Pochettino kupigwa kalamu ataweza kuandikisha ushindi wake wa kwanza na klabu hiyo?

jose

Kumbuka Tottenham kwa sasa wanashikilia nafasi ya 14 wakiwa na pointi 14 huku mashabiki wa klabu hiyo wakiwa na matarajio kuwa Mourinho atachangia pakubwa kurudisha makali ya klabu hiyo.

Mwanahabari wa K24 afariki dunia akiwa safarini kumwona mkewe aliyejifungua

 Mechi zingine ambazo zitachezwa wikendi hii ni;

Arsenal vs Southampton

laca

Brighton vs Leicester

leic

Crystal Palace vs Liverpool

zaha

Sheffield United vs Manchester United

digea

Ligi ya Uingereza: ushindani wa kumaliza katika nne bora

Ligi ya Uingereza itakuwa inachezwa wikendi hii huku klabu mbali mbali zikiwa na matarajio ya kumaliza katika orodha ya nne bora katika msimu huu wa mwaka 2019/2020.

Vijana wake Pep Guardiola waliweza kumaliza kileleni katika msimu uliopita baada ya ushindani mkali kushuhudiwa kati yao na Liverpool.

Mariga akubali kubwagwa, amualika Imran chakula cha mchana – Video

 Kwa sasa  klabu ya Liverpool inaongoza kwenye ligi hiyo ikiwa na pointi 31, wakifuatiwa na Manchester City ambayo wameweza kupata pointi 25, huku Leicester na Chelsea wakifunga orodha ya nne bora kila mmoja akiandikisha pointi 23.

Michuano ambayo itachezwa wikendi hii itachangia pakubwa kuthibitisha klabu ambazo huenda ikamaliza katika nafasi ya nne bora msimu huu.

‘Mungu anayesababisha mwanamke “tasa” kuimba,’ Kambua apeana sababu za kusifu

 Manchester United, Tottenham, na Arsenal pia ni miongoni mwa klabu ambazo zinatarajiwa kuleta ushindani mkubwa.

Mechi kubwa wikendi hii itakuwa baina ya Liverpool na Mancity ambao wanashikilia nafasi ya kwanza na pili mtawalia.

Mechi zingine ni;

Chelsea vs Crystal Palace

chelsea

Tottenham vs Sheffield Utd

dele

Leicester vs Arsenal

auba

Man United vs Brighton

pogba