Patanisho: Mume wangu alitaka kujinyonga kanisani

Stephen alituma ujumbe akiomba apatanishwe na mama Faith ambaye ni mke wake na mama wa mtoto wao mmoja.

“Tulikosana tarehe 28 baada ya kusafiri nyumbani. Niliporudi nilipata amefunganya virago na kuondoka bila sababu na sina habari nilimkosea aje.

Alinituma nyumbani na akaniambia nimletee dawa ya kienyeji kwani alikuwa mja mzito na amepoteza mtoto bila kujua kuwa ni uwongo.” Alielezea Stephen.

Kwa nyumba alichukua kile alichoona ni chake na nikamwachia mungu kwani nampenda na mungu ametujalia mtoto mmoja.”

Huyo ni baba wa mtoto wangu, unajua mahali tulikosania ni kwamba kuna siku tulikosana na akachukua kamba akitaka kujinyonga kwa compound ya kanisa. Alieleza mama Faith.

Sasa kila mara tukikosana huwa akidai kuwa niokote nilichotaka kwa ile nyumba na niondoke, hapo siku moja nikaamka nikachukua nilichokinunua na kuondoka.

Tukasuluhisha yote na tukaombewa na tukasahau lakini kuna siku alitaka kuniua kwa kutumia chuma kwani kuna siku alimuumiza mtoto na akafura mguu. Huyu sio jamaa wa kuishi naye.

Aliongeza mkewe Stephen akidai kuwa kuna wakati alilala nje na hakuwa na mavazi na hata alikuwa anaomba hadi mavazi ya ndani.

Alijawa na huzuni akidai kuwa hataki kuzungumza na mumewe kwa hasira kwani amezungumza na watangazaji kwani anawapenda.

Pata uhondo kamili.