United yailaza Derby, Uingereza yapiga marufuku kusalimiana kwa wachezaji

Manchester United ililaza Derby county 3-0 katika raundi ya tano ya kombe la FA na kunyakua tikiti ya mwisho ya robo fainali.  Luke Shaw alifunga bao la kwanza kunako dakika ya 33 huku Odion Ighalo akiongeza mawili katika dakika ya 41 na 70 na kukamilisha kichapo hicho.

Mfungaji bora wa Mancheter United katika historia ya klabu hio Wayne Rooney ambaye anachezea Derby alikua karibu kufunga kupitia mikwaju ya adhabu lakini kipa wa United Sergio Romero alihakikisha hakukua na goli la kufuta machozi. United sasa itacheza dhidi ya Norwich katika robo fainali baadae mwezi huu.

Tanzania yaagiza wachezaji kutosalimiana ili kuepuka Coronavirus

Wasimamizi wa ligi ya Uingereza FA wamepiga marufuku kusalimiana kwa wachezaji na maafisa wa mechi za ligi ya Uingereza kuanzia wikendi hii, ili kuzuia kuenea kwa virusi vya corona. Haya yanajiri baada ya serikali kuwataka waweke mikakati ya kupambana mchipuko wa janga hilo ambalo linatishia kusambaa kote duniani.

Mshambulizi wa Real Madrid Eden Hazard amefanyiwa upasuaji wa kidole cha mguu, na anazidi kupata nafuu. Mbelgiji huyo ambaye alijiunga na  Los blancos kutoka Chelsea mwanzoni mwa msimu huu alijeruhiwa wakati walipoteza 1-0 dhidi ya Levante mwezi Februari.

Hio ilikua mechi yake ya pili tu baada ya kupona jeraha lingine mwezi wa Januari. Haijulikani atarejea lini lakini madaktari wanaamini huenda asicheze tena msimu huu.

‘Ngono imeharibu umaahiri wa wachezaji,’ Mmiliki wa klabu ya Bucharest asema

Uwanja wa Kasarani utafungwa ili kufanyiwa ukarabati mwezi huu, ili kuwa tayari kwa mbio za vijana wasiozidi umri wa miaka 20 mweji Julai 2019.  Kenya iliandaa mbio za kinda wasiozidi umri wa miaka 18 mwaka wa 2017 na wananuia kuandaa mbio za kufana tena. Waziri wa michezo Amina Mohammed anadai serikali imeweka mikakati kabambe kuhakikisha wanaendeleza rekodi nzuri ya kuanda michezo nchini.

Mshambuliaji wa Tottenham Harry Kanemwenye umri wa miaka 26, atafikiria kuhamia Manchester United msimu huu. Kane hana mpango wa kutia saini mkataba mwingine na Tottenham. Kwingineko Arsenal wanaweza kufungua njia kwa John Stones, kuondoka Manchester City mwishoni mwa msimu.

 

Man United wakubaliana mkataba wa kumsajili Bruno Fernandes

Manchester United wamekubaliana mkataba wa kumsajili kiungo wa kati wa Ureno Bruno Fernandes kutoka Sporting Lisbon.

United watalipa kitita cha kwanza cha takriban Uro milioni 55 kwa mchezaji huyo wa miaka 25, ingawaje marupurupu huenda yakafanya kitita hicho kufikia Uro milioni 80.

Uhamisho wa Fernandes utakamilika baada ya uchunguzi wa kimatibabu na masuala mengine ya kibinafsi. Vilabu hivyo vimekua vikijadiliana wakati wote wa dirisha la uhamisho huku makubaliano yakiafikiwa Jumanne.

Mkusanyiko wa habari za spoti

 

Mohamed Salah alikuwa nyota wa mechi Liverpool walipoongeza uongozi wao kileleni mwa jedwali la ligi ya Primia kwa alama 19 baada ya kuwanyuka West Ham 2-0. Salah alianza kufunga kunako kipindi cha kwanza kabla ya Alex Oxlade-Chamberlain kuongeza bao la pili.

Vijana wa Jurgen Klopp sasa wamewanyuka wapinzani wao wote wa ligi angalau mara moja msimu huu. Ushindi huo unawawacha West Ham katika nafasi ya 17 kwenye jedwali.

Manchester City walifuzu kwa fainali ya kombe la Carabao licha ya kupoteza 1-0 katika mkondo wa pili wa nusu fainali kwa Manchester United.  Ilionekana kama itakuwa rahisi kwa City baada ya kushinda mkondo wa kwanza 3-1 ugani Old Trafford wiki tatu zilizopita, lakini bao la Nemanja Matic kunako kipindi cha kwanza likabadilisha mambo.

City walikosa nafasi nzuri katika kipindi cha pili lakini jitihada zao za kufika fainali ya mashindano hayo zilipigwa jeki baada ya Matic kupewa kadi nyekundu na kuwawacha United na wachezaji 10.

Arsenal haitakubali kumuuza mshambuliaji wao raia wa Gabon Pierre-Emerick Aubameyang mwenye umri wa miaka 30, kwa dau la chini ya pauni milioni 50.

PATANISHO: Alisema ataniendea kwa mganga ili niwe wake – Mercy

Barcelona inaripotiwa kumnyatia mshambuliaji huyo. Kwingineko Sheffield United ndiyo klabu pekee ambayo imepeleka ofa ya usajili kwa kiungo wa klabu ya Genk na taifa la Norway Sander Berge ambaye ana thamani ya pauni milioni 27.

Mashindano ya riadha ya dunia mwaka 2020 ambayo hufanyika ukumbini huko Nanjing yameahirishwa, kutokana na hofu ya kusambaa kwa virusi vya coronavirus nchini Uchina.

Mashindano hayo yalikuwa yafanyike kuanzia Machi tarehe 13 hadi 15 lakini bodi ya usimamizi wa riadha duniani ikaiahirisha kwa miezi 12. Bodi hio ilitafuta ushauri kutoka kwa shirika la afya duniani na kukataa ofa kutoka kwa miji mingine.

Mabingwa watetezi Gor Mahia walifungua mwanya wa alama mbili kileleni mwa jedwali la KPL baada ya kupata ushindi 2-1 dhidi ya Sofapaka jana mjini Kisumu. Mechi hio ilipelekea Gor, ambao wana mechi moja mkononi kumuanzisha mchezaji wao mpya waliomsajili raia wa Uganda Juma Balinya, ambaye mchango wake ulimpelekea kusifiwa na kocha Steven Polack.

Lawrence Juma na Kenneth Muguna walifungia Gor huku Jedinal Ameyaw akiwapa Sofapaka bao lao.

Waogeleaji wa Kenya wanapowania kuiwakilisha nchi katika mashindano jijini Tokyo wana kila sababu ya kutabasamu, baada ya kamati ya kitaifa ya Olimpiki kufichua kuwa malumbano yanayolikumba shirikisho lao, hayataathiri kushiriki kwao. Waogeleaji hao walikua wako katika hatari ya kufungiwa nje ya Olimpiki baada ya shirikisho la Kenya kupigwa marufuku na lile la kimataifa la uogeleaji kwa kukosa kulainisha masuala yao.

Kenya tayari imewataja waogeleaji wanne kushiriki mashindano hayo. Ni pamoja na Emily Muteti, Issa Abdulla, Danilo Rosafio na Maria Brun-lehner.

Masaibu ya Waititu: James Nyoro kuapishwa kama gavana wa Kiambu

Fomu mbaya ya United yaendelea baada ya kubwagwa na Burnley

Fomu mbaya ya Manchester United iliendelea jana walipopoteza 2-0 nyumbani, kwa Burnley. Burnley waliongoza kabla tu ya muda wa mapumziko wakati Chris Wood alipofunga bao.

Jay Rodriguez kisha akaongeza bao la pili na kuwapa ushindi wao wa kwanza Old Trafford. United walizomewa wakati wa mapumziko na baada ya mechi kuisha huku mashabiki wakiondoka uwanjani ikiwa imesalia dakika tano mechi kutamatika.

Manchester United huenda ikamsajili kiungo wa kati wa Ureno Bruno Fernandes kwa mkataba wa pauni milioni 55m mwisho wa wiki hii baada ya kuafikiana na Sporting Lisbon.
Fernandes aliwapuuza mashabiki wa Sporting na kusukuma kamera za televisheni baada ya kupoteza mechi dhidi ya Braga siku ya Jumanne katika kile kilionekana kuwa mechi yake ya mwisho katika klabu hiyo. 

Cristiano Ronaldo alifunga bao lake la 13 katika mechi 10 alizocheza Juventus walipowanyuka AS Roma 3-1 na kufuzu kwa nusu fainali ya Coppa Italia. Mshambulizi huyo wa Ureno alianza kufunga kunako kipindi cha kwanza kutoka kwa pasi ya Gonzalo Higuain. Rodrigo Bentancur na Leonardo Bonucci kisha wakaongeza mabao mengine na kufanya mambo kuwa 3-0 kabla ua muda wa mapumziko. Roma ilipata boa lake kupitia kwa Cengiz Under.

Juventus watakabana na aidha AC Milan au Torino kwenye nusu fainali.

Shirikisho la soka barani Afrika CAF limeialika Libya kushiriki katika michuano ijayo ya fainali za ubingwa wa mataifa Afrika huko Cameroon.

Caf wanatafuta timu itakayochukua nafasi ya Tunisia, ambao wamejiondoa kutoka kwa kipute hicho, baada ya vilabu vya nchi hiyo kudinda kuwawachlia wachezaji wake. Wanahoji kuwa mishuano hio haiku katika kalenda rasmi ya FIFA na kwa hivyio wanataka kulinda afya ya wachezaji wao.

Cameroon au Ivory Coast haitashiriki katika kombe la dunia mwaka 2022 nchini Qatar baada ya timu hizo kuwekwa katika kundi moja kwenye raundi ya pili ya michuano ya kufuzu kwa kombe la dunia. Indomitable lions imewakilisha Afrika mara saba katika kombe la dunia, huku Ivory Coast ikishiriki katika kombe hilo mara tatu.

Ghana na Afrika Kusini zitakutana katika kundi G pamoja na Zimbabwe na Ethiopia huku Misri na Angola pia zikikutana katika kundi F pamoja na Gabon na Libya.

Misri ilikuwa miongoni mwa wawakilishi watano wa Afrika katika kombe la dunia pamoja na Morocco, Nigeria, Senegal na Tunisia na zote zinaamini kwamba zina fursa nzuri ya kufika katika raundi ya tatu na ya mwisho mnamo mwezi Novemba mwaka huu.

Takriban pauni bilioni 7.35 zilitumika katika uhamisho wa wachezaji soka wanaume mwaka wa 2019, kulingana na ripoti ya FIFA. Kiwango hicho kimeongezeka kwa asilimia 5.8 mwaka wa 2018 za uhamisho kote duniani.

Vilabu vya Uingereza vilitumia pauni bilioni 1.5 ambalo ni punguzo la asilimia 11 kutoka mwaka 2018, huku kukiwa na ongezeko la asilimia 16 kwa kiwango kilichotumika kwa uhamishi wa wachezaji wa kike.

 

Pigo kwa United huku Maguire akitarajiwa kuwa nje kwa mda

Beki wa Manchester United Harry Maguire ataendelea kukaa nje kwa muda bila kushiriki mechi yoyote.

Hii ni kutokana na jereha la mfupa wa nyonga analouguza. Kufikia sasa michuano ambayo hatashiriki haijulikani. Lakini wasiwasi wa United ni kwamba hawakutarajia angekaa nje kwa muda mrefu baada ya kupewa moyo na Ole Gunnar Solskjaer, aliyesema kuwa jeraha hilo lilikuwa dogo. Maguire aliumia Manchester United ilipokuwa ikicheza na Wolves jumamosi iliyopita.

Borussia Dortmund haipo tayari kumwachilia nyota wake Jadon Sancho kununuliwa mwezi huu na baadhi ya vlabu vinavyommezea mate hususan vile vya Uropa.

Wachezaji ghali waliosajiliwa nchini Uingereza msimu huu

Borussia inahofia kwamba hawana mchezaji atakayechukua nafasi yake endapo atagura ikiongeza kuwa kandarasi yake klabuni humo itakamilika mwishoni mwa mwaka 2022.

Miongoni mwa klabu zilizoonyesha nia ya kumnunua Sancho mwenye umri wa miaka 19 ni pamoja na Chelsea, Manchester City, Manchester United, PSG Real Madrid na Barcelona.

Tusker ilipanda kileleni mwa ligi ya KPL baada ya kuilaza Kisumu All stars 2-0, huku Kakamega Homeboyz wakiwapiga Zoo Kericho 1-0 na kupanda hadi nafasi ya pili.

Ulinzi stars nao waliwanyuka Wazito FC 1-0 , huku KCB ikitoka nyuma na kuibwaga Sofapaka 2-1 nao Kariobangi Sharks waliwafunga Bandari 1-0. Western Stima waliwaadhibu Mathare United 2-1.

Chemilil sugar nao walisalia kushikilia mkia licha ya kupata ushindi wao wa kwanza msimu huu wa 1-0  dhidi ya Nzoia Sugar. Katika mechi ya mwisho hapo jana goli la dakika la mwisho la Sammy Odero, liliisaidia Posta Rangers kuilaza AFC Leopards 2-1.

Kocha mkuu wa timu ya Posta Rangers Sammy Pamzo Omollo anadai licha ya kuwalaza AFC Leopards 2-1 katika mechi ya ligi jana timu zote mbili zilicheza vizuri na yeyote angeshinda mechi hio.

Kutoka Mahrez hadi Pepe: Wachezaji ghali zaidi barani Afrika

Pamzo pia amewapongeza Ingwe kwa mchezo wao na anawapigia upato kufanya vyema msimu huu.

Mshambulizi Leroy Sane, anakaribia kurejea kwenye mazoezi ya Manchester City baada ya kuwa nje kwa miezi mitano akiuguza majeraha.

Mzaliwa huyo wa Ujerumani mwenye umri wa miaka 23 alikua nguzo katika timu hio na kocha mkuu Pep Guardiola anasema kurejea kwake kutawapiga jeki wanapoelekea wakati mgumu wa msimu.

 

Video ya siku: Mashabiki wa Man U humu nchini waiombea timu yao mlimani

Siku ya leo katika ligi kuu ya Uingereza, kuna mechi bomba kabisa ambayo inatazamiwa na mashabiki wengi duniani. Mechi hii ni dhidi ya Manchester United na Manchester City, al maarufu, Manchester derby.

Mechi hii kama ilivyo desturi huwaleta wapinzani hawa wakuu kutoka mtaa wa Manchester na kila wakati huwa ya kusisimua zaidi.

Manchester City ambao ni mabingwa kwa mika miwili sasa hawajakuwa wakionesha mchezo bora kama misimu iliyopita na wanashikilia nafasi ya tatu nyuma ya Leicester City, na wako nyuma ya viongozi Liverpool kwa alama 11.

United kwa upande wao walionesha ubabe wiki hii baada ya kumuadhibu aliyekuwa kocha wao, Jose Mourinho 2-1 alipoiongoza Tottenham hadi Old Trafford.

Hii ikiwa mechi kuu, mashabiki wa Kenya wa Man U wakiongozwa na mcheshi Eric Omondi wamechukua hatua ya kuiombea timu yao ili waibuke washindi baada ya kuwa na msururu wa matokeo mabaya.

Kanda hii imesambaa sana duniani na inawafurahisha wengi haswa mashabiki wa Red Devils.

Tazama kanda hii,

Man United waandikishwa ushindi wao mkubwa zaidi tangu Agosti

Meneja wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer anasema kikosi chake kilikua na mpango wa jinsi wangecheza msimu huu waliwapowanyuka Partizan Belgrade na kufuzu kwa 32 bora katika ligi ya Uropa.

Mabao ya kipindi cha kwanza ya Mason Greenwood na Anthony Martial yalifuatiwa na la Marcus Rashford baada ya mapumziko na kutamatisha ushindi mkubwa zaidi wa United tangu Agosti. Ushindi huo unakiweka kikosi cha Solskjaer kileleni mwa kundi L.

Aaron Ramsey amekiri kua alimwomba radhi Cristiano Ronaldo kwa kukatiza na kumnyima rekodi nyingine ya ligi ya mabingwa.

Raia huyo wa Wales aliwaweka waItalia mbele baada ya dakika tatu tu za mechi yao waliowanyuka Lokomotiv Moscow 2-1 jumatano baada ya kuzuia mkwaju wa adhabu wa Ronaldo.

Ligi ya mabingwa Uropa: Man United watashinda?

Katika mchakato huo Ramsey alimnyima mreno huyo rekodi ya Champions League ya kufunga dhidi ya vilabu vingi zaidi lakini akakiri kuwa hisia zake ziliingilia kati ili kuhakikisha timu yake inafunga.

Mabao mawili ya kipindi cha pili yaliwapa Rangers ushindi dhidi ya Porto na kukaribia kufuzu kwa awamu ya mchujo ya mishuano ya ligi ya Uropa.

Vijana wa Steven Gerrard Alfredo Morelos na Steven Davis walifunga mabao ya Rangers. Matokeo haya yana maana kuwa Rangers wako kileleni mwa kundi G pamoja na Young Boys wa Uswizi wakiwa na mechi mbili zilizosalia, huku Porto na Feyenoord wakiwa alama tatu nyuma.

Orodha ya wagombea wa viti mbalimbali ambao hawakujipigia kura wakati wa uchaguzi

Kocha wa Harambee Starlets David Ouma ametoa wito kwa wakenya kujitokeza kuwashabikia kinadada hao katika mechi yao ya kufuzu kwa michuano ya Olimpiki dhidi ya Shepolopolo ya Zambia hii leo ugani Kasarani.

Hakuna ada ya kiingilio ya mchuano huo kwani FKF inataka mashabiki wengi zaidi kujitokeza kuwashabikia Starlets. Mechi ya marudio itachezwa Lusaka siku ya Jumatatu.

Arsene Wenger amekanusha fununu kuwa anajadiliana na Bayern Munich kuwa meneja wao mpya lakini amejiepusha kujiondoa kutoka kwa kinyang’anyiro hicho. Miamba hao wa Ujerumani wanamtafuta meneja mpya baada ya kumfuta kazi Niko Kovac, baada ya kunyukwa mabao 5-1 na Eintracht Frankfurt.

Wenger alishinda ligi ya Primia mara tatu na kombe la FA Cup mara saba katika tajriba yake ya miaka 22 North London kabla ya kuondoka mwaka wa 2017-18.

Aina mpya ya virusi vya HIV yagunduliwa na wanasayansi

 

Madrid iko tayari kuipatia Man United £90m pamoja na Gareth Bale

Real Madrid iko tayari kuipatia Manchester United £90m pamoja na mshambuliaji wa Wales Gareth Bale, 30, ili kumsajili Paul Pogba, lakini inataka mchezaji huyo wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 26 kuimarisha kiwango chake cha mchezo uwanjani . (El Desmarque, in Spanish)

Real Madrid ina mpango wa kumuuza mshambuliaji Bale na kiungo wa Colombia James Rodriguez 28 ili kupata fedha za kumsajili mshambuliaji wa Ufaransa na PSG Kylina Mbappe 20. (Calciomercato).

Zidane: Lazima Bale aondoke Madrid

Wakati huohuo, rais wa Real Madrid Florentino Perez ana mpango wa kufanya kila kitu katika uwezo wake ili kumnyakua Mbappe katika uwanja wa Bernabeau msimu ujao. (AS)

Washauri wa kiungo wakati wa Arsenal Mesut Ozil, 31, wanajaribu kumshawishi mchezaji huyo wa zamani wa Ujerumani kuhamia katika ligi ya MLS. (Mail)

Ruthless Zidane to axe 14 Real Madrid players including Bale

Hatahivyo imeripotiwa kwamba Ozil amejiandaa kuendelea kuichezea Arsenal kwa muda mrefu. (Star)

Mkufunzi wa Manchester City Pep Guardiola anasema kwamba wanaweza kumnunua kiungo wa kati wa Brazil Douglas Luiz ,21, ambaye alijiunga na Aston Villa msimu huu. (Manchester Evening News)

Bayern Munich inafikiria uhamisho wa mwezi Januari wa beki wa Atletico Bilbao na Uhispania Unai Nunez na wamefanya mazungumzo na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20 ambaye pia anahusishwa na uhamisho wa kuelekea Arsenal na Everton. (Goal.com)

No room for Bale as Ronaldo and Eriksen feature in UEFA goal of the season nominations

-BBC

‘Kuna uwezekano mashetani wekundu watashushwa daraja,’ – Allardyce

Kuna uwezekano Manchester United ikashuka daraja msimu huu, kwa mujibu wa kocha wa zamani wa England, Sam Allardyce.

Hayo yakijiri, Kocha wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer atafutwa kazi endapo timu yake itafungwa na Norwich mwishoni mwa mwezi, ripoti zinaeleza. (Sun)

Je, Uhuru anamzubaisha Raila huku akimuunga mkono Ruto?

Hata hivyo, vyanzo vingine vinaarifu kuwa uongozi Man United upo tayari kumvumilia na kumpa muda zaidi Solskjaer wa kufanya mageuzi klabuni, licha ya kiwango kibovu cha matokeo ya mwanzo wa msimu kwa miaka 30. (Telegraph)

United wanapanga kuwasajili kiungo wa West Ham na England Declan Rice, 20, na beki wa Napoli na Senegal Kalidou Koulibaly, 28, bila kujali mustakabali wa Solskjaer. (Goal)

Kalidou Koulibaly

Kocha wa Tottenham Mauricio Pochettino napanga kuwauza wachezaji kadhaa wa klabu hiyo baada ya kuanza msimu kwa kiwango kibovu. Wachezaji watakaowekwa sokoni mwezi Januari ni; Eric Dier, 25, Christian Eriksen, 27, Serge Aurier, 26, Victor Wanyama, 28, pamoja na Danny Rose, 29. (Times – subscription required)

Yote utakayo kujua kuhusu bingwa Eliud Kipchoge

Kocha David Moyes yupo tayari kurudi kuifunza klabu yake ya zamani ya Everton, katika kipindi ambaco kocha wa sasa Marco Silva akiwa katika shinikizo kubwa baada ya timu hiyo kuwa chini ya mstari wa kushuka daraja. (Mirror)

Crystal Palace watalazimika kulipa pauni milioni ili 22 wamsajili mshambuliaji wa Chelsea na timu ya taifa ya Ubelgiji Michy Batshuayi, 26,ambaye yupo kwa mkopo Palace toka Januari mwaka huu. (Express).

-BBC

Alexis Sanchez akiri kuwa hajutii uhamisho wa Man United

Mshambuliaji Alexis Sanchez “hajutii” kujiunga na na klabu ya Manchester United lakini anasema hakupata muda wa kutosha wa kucheza na kuonesha makali yake.

Mchezaji huyo raia wa Chile, 30, amejiunga kwa mkopo na miamba ya soka nchini Italia, klabu ya Inter Milan, baada ya kudumu Old Trafford kwa miezi 19.

Siendi ng’o!: Alexis Sanchez akiri hataondoka Man United

Sanchez alikuwa akilipwa mshahara mkubwa zaidi United wa pauni 400,000 kwa wiki – lakini amefunga magoli matano tu katika mechi 45 alizoichezea United toka alipoihama Arsenal Juanuari 2018.

“Ni furaha kwangu kuwa nilijiunga na Manchester United,” Sanchez ameiambia BBC.

“Nimekuwa nikisema hivyo kila siku. Ni klabu iliyoshinda zaidi England.

“Nilipojiunga Arsenal ilikuwa ni jambo kubwa na zuri – Nilikuwa mwenye furaha pale (Arsenal) – lakini United ilikuwa ikitanuka, walikuwa wananua wachezaji ili kushinda kitu.

“Nilitaka kujiunga nao ili nami nishinde kila kitu.”

Sanchez alipachika magoli 80 katika mechi 166 alizoichezea Arsenal ambao walimnyakua kutoka Barcelona kwa pauni milioni 30 Julai 2014.

Mwaka 2017, alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa ligi ya Primia.

Hata hivyo, kujiunga kwake na United kumeandamwa na kuporomoka kwa kiwango chake dimbani.

Alexis Sanchez yuko tayari kubakia ugani Old Trafford

Alifunga magoli mawili tu katika mechi 27 za ligi alizocheza msimu uliopita. Japo aling’ara na timu ya taifa ya Chile kwenye kombe la Copa America akipachika magoli mawili nusu faiali.

Sanchez alianza kwenye michezo 31, kati ya 77 kwa United, na alimaliza michezo 13 tu.

“Naamini huwa na furaha sana ninapochezea timu yangu ya taifa,” amesema.

“Nilikuwa mwenye furaha nikiwa na Manchester United pia, lakini nimekuwa nikiwaeleza rafiki zangu: nataka kucheza.

“Kama wataniruhusu kucheza nitafanya kila niwezalo. Wakati mwengine nacheza dakika 60 kisha mechi inayofuata sichezi, na sijui kwa nini.”

Kabla ya kujiunga na Inter Milan, Sanchez hakucheza hata mchezo mmoja wa kirafiki wa kabla ya msimu na hakuwemo kwenye kikosi cha kocha Ole Gunnar Solskjaer kwenye michezo mitatu ya mwanzo huku klabu ikisema alikuwa majeruhi baada ya kuumia akiwa na timu ya taifa.

Hata hivyo, Sanchez anasema alikuwa tayari kuchezea klabu yake baada tu ya Copa America.

“Nilikuwa tayari na nimepona. Nilifanya vizuri. Baada ya hapo yalikuwa ni maamuzi ya kocha kunipanga nicheze. Inabini umuulize yeye (kwa nini hakupangwa) na si mimi.”

Alexis Sanchez fears a two-month absence at Manchester United

-BBC

Siendi ng’o!: Alexis Sanchez akiri hataondoka Man United

Mshambuliaji wa Manchester United na Chile Alexis Sanchez, 30, amekataa uhamisho wa kuelekea Roma, licha ya klabu hiyo ya Old Traford kukubali kulipa kitita kikubwa cha mshahara wake wa £560k kwa wiki.{Mirror)

Hatahivyo Sanchez huenda akaelekea katika ligi ya serie A baada ya Man United kumruhusu kufanya mazungumzo na Inter Milan, ambapo huenda akakubali kupunguza mshahara wake. (Mail)

Liverpool huenda ikafaidika na £18m iwapo mshambuliaji wa zamani wa klabu hiyo na raia wa Brazil Philippe Coutinho, 27, ataelekea Bayern Munich kwa mkopo. (Mail).

Everton imetoa ofa ya kumsaini winga wa Ufaransa Franck Ribery, 36, ambaye yupo huru baada ya kuondoka Bayern Munich baada ya kuhudumu kwa miaka 12 katika klabu hiyo ambayo ndio mabingwa wa ligi ya Bundesliga . (90Min)

Kwengineko, Kiungo wa kati wa Portugal Renato Sanches, 21, anataka kuondoka Bayern kwa kukosa muda wa kucheza katika klabu hiyo. (Sport1 – in German).

Mesut Ozil

Mesut Ozil, 30, huenda akaondoka Arsenal na kujiunga na klabu ya DC United iwapo klabu hiyo ya ligi ya MLS inaweza kumshawishi kiungo huyo wa Ujerumani kuhamia Washington. (Star)

Beki wa kulia wa Ivory Coast Serge Aurier, 26, huenda akaondoka Tottenham na kuelekea AC Milan iwapo beki wa timu hiyo Andrea Conti, 25, ataondoka ligi ya Serie A kabla ya kukamilika kwa dirisha la uhamisho la Ulaya. (Calciomercato)

Na mchezaji wa Everton Yannick Bolasie, 30, yuko tayari kurudi katika uwanja wa Goodison Park, huku klabu za Uturuki Besiktas na Trabzonspor zikiwa na hamu ya kumsajili mchezaji huyo wa Congo . (Sun)

Mchezaji wa zamani wa Manchester City na Liverpool Mario Balotelli, 29, anakaribia kujiunga na klabu ya Serie A Brescia. (Sun via La Gazzetta)

Mshambuliaji wa Paris St-Germain Neymar, 27, hakuorodheshwa katika kikosi cha timu hiyo kitakachocheza dhidi ya Rennes kutokana na jeraha na sio kwamba raia huyo wa Brazil anataka kurudi Barcelona. (AS – in Spanish)

Mshambuliaji wa Barcelona Kevin-Prince Boateng, 32, amefichua ni kwa nini Sir Alex Ferguson hakumsajili kujiunga na Manchester United mapema wakati wa kipindi chake cha mchezo. (Goal)

-bbc