Zari Hassan apata kipenzi kipya

Baada ya ukimya wa muda mrefu, Zari ameweza kutokea katika mitandao ya kijamii na mwanaume ambaye amtamrithi msanii na mkurugenzi wa WCB Diamond Platnumz. Katika chapisho siku ya ijumaa, mrembo huyu na mama wa watoto watano amesema kuwa mwanamume aliyempata kwa sasa ni baraka kubwa kwake.

Zari na Diamond waliachana mwaka uliopita tarehe 14 Februari siku ya wapendanao kwa kuchapisha ua jeusi lililoambatana na ujumbe mzito wa kuonyesha hawapo tena katika mahusiano.

zariposeswithdiamond
Zari na mpenzi wa zamani Diamond

Mama Tiffah alionekana kukasirishwa na tendo la mzazi mwenzake kukiri katika runinga na redio kubwa nchini Tanzania kuwa aliweza kufanya tendo la ndoa na kupata mtoto na mwanamitindo Hamisa Mobeto.

Patanisho: Jombi aapa kutopiga bibi yake

Zari The Bosslady ametupia picha ya mpenzi wake mpya katika mtandao wake maridhawa wa Instagram. Katika chapisho  hilo, mama Tiffah ameonekana kummiminia sifa kedekede mume huyu mpya na kubana jina lake kabisa na kumwita Bwana M.

Mrembo huyu ambaye ni msanii kutoka nchi jirani ya Uganda baada ya kumtema staa wa muziki Chibu Dangote alionekana kusononeka sana kwa kumpoteza mpenzi aliyempenda kwa dhati.

From Verona to Venice! Check out how Massawe Japanni is slaying in Italy

Katika mitandao ya kijamii, anadokeza kwamba mshikaji wake mpya amemkubali pamoja na watoto wake watano. Zari amezaa watoto wawili na Diamond platnumz na watatu na aliyekuwa mmewe marehemu Ivan Ssemwanga.

Zari amefunguka sana maneno matamu kwa mpenzi wake.

“Nimebarikiwa sana kukupata wewe. Nakupenda sana Bwana M… Sio kwa vitu unazoninunulia wewe kwa kuwa nimeona tena kubwa na nzuri maishani mwangu ila naupenda moyo wako na jinsi unavyonifanya nijihisi vizuri pamoja na watoto wangu.” Anasema mrembo huyu.

Akionekana kuwa amepitia katika mahusiano ya mateso,  mrembo huyu amesema kuwa yeye huwajenga wanaume na wala sio sampuli ya wanawake wanaotegemea kupewa na wanaume.

“Mimi sio sampuli ya wanawake wanaochukua kutoka kwa wanaume ila nawajenga.”

zari with teddy bear
Zari Hassan

Anasema Bwana M ni tofauti na wapenzi wa jadi na kwamba ana upole na utulivu mwingi ambao unafanya ampende zaidi. Mzazi mwenza Simba  anaonekana kuzama katika mahaba mazito na mtangazaji wa redio Tanasha Donna kutoka hapa nchini.

Penzi lake diamond na Tanasha linaonekana kunoga zaidi baada ya mkali huyu kumpeleka Donna nyumbani Madale na kumtambulisha kwa  familia. Dadake Platnumz anapenda sana mahusiano haya na anajuta kuwa wawili hawa wangekutana zamani.

PATANISHO: Mume wangu hutaka tufanye mapenzi hadi nikiwa na periods

Faith alituma ujumbe akiomba apatanishwe na mumewe bwana Sam ambaye walikosana sana Jumatatu iliyopita.

Mzee wangu tumekuwa tukisumbuana kuhusu mapenzi kwa nyumba kwani hutaka tufanye mapenzi kila siku, hata nikiwa na period zangu yeye hajali. Alieleza.

Patanisho: Mpango wa kando wa bibi yangu anampigia simu tukiwa tumelala

Nikamwambia haya maisha yamekuwa ngumu kwani nalima kwa shamba na nalea watoto na sitaweza. Isitoshe nilimuomba aoe mke wa pili anisaidie kwani siwezi.

Siku moja niliamka kwenda kumshughulikia mtoto na alinizaba kofi akisema namwonesha madharau. Hapo nikatoroka na niakenda nyumbani. Aliongeza Faith huku akiwa na wingi wa huzuni.

Wawili hao wamekuwa kwa ndoa ya miaka minane na wamefanikiwa na watoto.

PATANISHO: Ndugu yangu alihepa majukumu ya kuwasaidia wazazi

Bwana Sam alipopigiwa simu alisema kuwa mkewe alimtishia kuwa atamuua na atampa madawa fulani.

Faith alisema kuwa anampenda mumewe na kuwa aliwacha shule ili aolewe na bwana Sam licha ya wazazi wake kupinga ndoa hiyo.

Siko tayari kurudiana naye kwani nina machungu, aniwache nitulie na nifikirie ili nijue kama tutarudiana, kwa sasa mapenzi yako kwa watoto.

PATANISHO: Mume wangu akilewa hutishia kuniua na nikaamua nikimbie

PATANISHO: Mke wangu hanipii furaha kwani mimi mnyama?

Lucy kutoka Malindi alituma ujumbe akiomba apatanishwe na mumewe bwana Mohammad Ali, akisema ni makosa kidogo yaliyotoke kwa nyumba.

PATANISHO: Mume wangu hata nguo za ndani hanishughulikii

“Naomba tu apigiwe simu nipatane naye niweze kuomba msamaha. Ndio aende tuliwachana asubuhi nikienda kazini na kurudi nyumbani kuandaa chakula cha jioni.

Mzee aliingia na mzigo na kuuweka kwa kiti na nikaupeleka kwa nyumba, kutoka jikoni kurudi nikapata ameuchukua ule mzigo na kuondoka. Sasa sielewi shida ni gani.” Alieleza Lucy.

Kisa hicho kilitokea wiki iliyopita na mwanadada hajui cha kufanya.

Wawili hao wamekuwa kwa ndoa ya miaka kumi na miwili.

PATANISHO: Ndugu yangu alinipeleka kwa polisi nikatwangwa twangwa

“Mipaka umenipitishia kabisa, mimi hutoka na furaha kwenda kusherehekea na bibi yangu kurudi umenuna huzungumzi nami hatuna furaha kwani mimi ni mnyama?” Alisema Ali.

Hatuna furaha yoyote, miaka miwili mimi nawe hatujuani haya basi, mimi sina neno lakini unayoyafanya sina neno.” Aliongeza akiwa na wingi wa msononeko.

Kulingana na Ali, miaka miwili hajapata raha ndani ya ndoa kwani yeye hupakuliwa tu chakula na ndio hivo, hapo aliamua kuondoka.

Mimi mwenyewe nina pressure nina sukari na anaye nituliza ni wewe na sasa nikiona hunishughulikii naenda kutafuta mapumziko kwani maudhiko siyawezi.” Aliongeza mzee.

PATANISHO: Babangu alitutoroka tukiwa wadogo kwa miaka 11

PATANISHO: Niliogopa kuwa mume wangu anaweza niua

Patrick alituma ujumbe akiomba kupatanishwe na mkewe Sylvia, mwenye umri wa miakaa 28, mbaye alipata amefunganya virago vyake na kuondoka mwezi wa Disemba tarehe 30.

PATANISHO: Bibi yangu anatetea mpango wake wa kando

Kuna kijana fulani ambaye alikuwa anamtaka na mimi kuja kugundua hayo maneno, kumuuliza ikawa tunakosana naye na baadae akaja akaniambia huyu kijana alikuwa anamtaka, lakini alimueleza kuwa yeye ni mpwa wake na hawawezi pelekana mahali. Alijieleza Patrick.

Sasa nikamweleza kuwa sikuwa naelewa hayo maneno na sasa kwa ajili nimeelewa basi hayo maneno tuyaache. Na hapo baadae akanitumia ujumbe akisema nimsamehea maneno yote aliyonifanyia.

Nikamwambia nishamsamehe na tuishi na amani, sikujua on Sunday nikitoka kazini nitamkosa. Nilipata amekusanya vitu vyake na ameenda huku watoto akiwa amewapeleka kwa mamake. Aliongeza akidai kuwa hajui kwenye mkewe aliko kwani alimwambia yuko Naivasha.

Kulingana na Patrick 31, wawili hao wamekuwa kwa ndoa ya miaka mitano lakini bado hawajaona ki rasmi.

PATANISHO: Bwanangu alikatwa kichwa na mpango wa kando na bado akamrudia

Unajua Gidi wacha nikuambie, mapenzi inakuanga ya watu wawili lakini mtu wa tatu, nne akiingia inakuwa tu hivo. Kwa hivyo mimi niliboeka. Alisimulia Sylvia.

Mimi niligundua kuwa tukivuruga kidogo yeye huenda kuambia ndugu zake mpaka anaingiza wazazi wake na tukimaliza maneno, hatukai hata wiki moja kabla ya kurudisha yale maneno. 

So niliona hakuna haja ya kuendelea na yeye, unajua mtu anaweza kuambia amekusamehe na kwa roho hajakusamehe. Mimi niliogopa kwani mtu hata anaweza kuua. Aliongeza.

 

Pata uhondo kamili.

PATANISHO: Jamaa kazi ni kunitesa na hadi paka hajawahi peleka kwetu

Japhet kutoka Nairobi alituma ujumbe akiomba apatanishwe na mkewe Sarah.

PATANISHO: Nasikitika Nilimuibia Tajiri Wangu Elfu Tisa

 

Mke wangu ametoweka miezi minne sasa na nikimpigia anadai atakuja lakini amekuwa muongo sana.

Mke wangu alipata ujumbe kwa simu yangu lakini haukuwa wangu lakini pia nilipata ujumbe kwa simu yake ya mapenzi huku wakizungumza na jamaa fulani wapatane na hapo tukakosana.

Ujumbe aliopata ulikuwa umetumwa na jamaa fulani mfanyikazi mwenzangu akiungumza na mpenziwe.

Kumuuliza akadai kuwa aliponipata sikumwambia chochote na kwa hivyo kila mmoja ajishughulishe. Alidai Japhet ambaye amekuwa kwa ndoa kwa miaka saba.

PATANISHO: Mke wangu alikuwa anakatiwa na caretaker

Wawili hao wamejaliwa mtoto mmoja.

Alipopigiwa Sarah alikiri Japhet alikuwa na shida ya kukwepa majukumu ya nyumba.

“Hataki kusomesha mtoto, ukimwambia mambo ya kujenga nyumbani hataki, tumeoana miaka saba na huyu mwanaume hajui kwetu lakini anataka niishi Nairobi bila kushughulika na mambo ya nyumbani.” Alieleza Sarah.

Hata haikuwa mambo ya mpango wa kando, nilitoka nyumbani na pindi tu nilipofika nyumbani majirani walinipigia kunieleza alikuwa na vituko chungu nzima huko Nairobi.” Aliongeza.

PATANISHO: Kila nikichelewa mke wangu hudhani nina mpango wa kando

Eric alituma ujumbe akiomba apatanishwe na mkewe ambaye walikosana mwezi uliopita na kwenda kwao.

Huwa natoka nyumbani kwenda kazini na kurudi nikiwa nimechelewa kwa ajili ya msongamano wa magari barabarani. Sasa kila wakati huwa shida tupu nyumbani kwani mke wangu hudhani nina mpango wa kando. Nafanya kazi ya mechanic.

Wakati mwingine mimi hurudi nyumbani nikiwa nimechoka na akiniongelesha mimi hujipata nimemjibu vibaya.

Wawili hao wana watoto wawili pamoja.

Alipopigiwa simu bi Sheila alimueleza achague kati ya wanawake wawili aliyozaa nao nani mke wake akiongeza kuwa mume wake amepachika wanawake kadhaa mimba. “Nimemwachilia afanye kenye anataka.” Alisema.

Pata uhondo kamili.

PATANISHO: Nikimtumia mke wangu ujumbe wa mapenzi hunijibu ‘Go to hell’

Joash alituma ujumbe akiomba apatanishwe na mkewe bi Consolata akidai anapitia magumu sasa hivi.

Bibi yangu alitoka nyumbani Aprili mwaka uliopita akielekea Embakasi na kabla aende kulikuwa na mgogoro kwa nyumba. Sielewi mbona hazungumzi nami na nikimtumia ujumbe wa mapenzi ananitusi ‘Go to hell’.

Mke wangu alikuwa anadai kuwa sikuwa nampa mda wake na pia anadai kuwa mimi ni mkali.

Pata uhondo kamili.

PATANISHO: Mke Wangu Aliondoka Alipogundua Nina Mpango Wa Kando

Felix alituma ujumbe akiomba apatanishwe huku akidai mkewe aliondoka baada ya kugundua kuwa ana mpango wa kando.

‘Bibi yangu Cate nilimuoa akiwa na watoto na tumevumiliana na sasa watoto wamekuwa wakubwa. Mimi ni mpishi na siku moja katika hali ya kuchokora simu yangu aligundua kuwa kuna wanadada nimekuwa nikizungumza nao.

Sasa akapata msichana fulani ambaye tulijuliana Facebook na ilifika wakati nikama tulikuwa tunatongozana. Sasa mke wangu akakasirika na akaondoka na hadi wa leo hajawahi rudi na hajibu simu zangu.” Alieleza Felix.

Alipopigiwa simu bi Cate, alidai mumewe alimtishia akidai kuwa ataharibu watoto wake.

 

PATANISHO: Mume wangu alinitenga baada ya kukataa kuavya mimba

Anne Jepkorir alituma ujumbe akiomba apatanishwe na mumewe akidai kuwa ana watoto wawili na kuwa anapanga kuwapeana baada ya maisha kuwa mazito.

Mara ya mwisho kuzungumza naye alisema anaenda Nairobi lakini hakuwa huko na nikimpigia hakuwa anashika simu. Alisema Anne

Tuna watoto wawili, baada ya kupata mtoto mmoja nikashika mimba ya pili baada tu ya miezi mitano.

Nikama hakuwa anatarajia kwani kuna siku alikuwa anadai nitoe mimba na nikakataa.

Hapo alikasirika na kunieleza kuwa sifai kumhesabu ndani ya maisha yake, hapo nikamnyamazia na nikaondoka. Baada ya kurudi miezi tisa baadaye alianza kulia alipomuona mtoto kwani aliamini ni wake na akapata machungu kuwa karibu aue mwanawe.” Alieleza Anne.

Bwanake alikatisha mawasiliano nasi pindi tu aliposkia sauti ya mkewe.

Pata uhondo kamili.

Patanisho: Mume wangu alitaka kujinyonga kanisani

Stephen alituma ujumbe akiomba apatanishwe na mama Faith ambaye ni mke wake na mama wa mtoto wao mmoja.

“Tulikosana tarehe 28 baada ya kusafiri nyumbani. Niliporudi nilipata amefunganya virago na kuondoka bila sababu na sina habari nilimkosea aje.

Alinituma nyumbani na akaniambia nimletee dawa ya kienyeji kwani alikuwa mja mzito na amepoteza mtoto bila kujua kuwa ni uwongo.” Alielezea Stephen.

Kwa nyumba alichukua kile alichoona ni chake na nikamwachia mungu kwani nampenda na mungu ametujalia mtoto mmoja.”

Huyo ni baba wa mtoto wangu, unajua mahali tulikosania ni kwamba kuna siku tulikosana na akachukua kamba akitaka kujinyonga kwa compound ya kanisa. Alieleza mama Faith.

Sasa kila mara tukikosana huwa akidai kuwa niokote nilichotaka kwa ile nyumba na niondoke, hapo siku moja nikaamka nikachukua nilichokinunua na kuondoka.

Tukasuluhisha yote na tukaombewa na tukasahau lakini kuna siku alitaka kuniua kwa kutumia chuma kwani kuna siku alimuumiza mtoto na akafura mguu. Huyu sio jamaa wa kuishi naye.

Aliongeza mkewe Stephen akidai kuwa kuna wakati alilala nje na hakuwa na mavazi na hata alikuwa anaomba hadi mavazi ya ndani.

Alijawa na huzuni akidai kuwa hataki kuzungumza na mumewe kwa hasira kwani amezungumza na watangazaji kwani anawapenda.

Pata uhondo kamili.