PATANISHO: Naomba nipatanishwe na mpango wa kando lakini sitaki mke wangu ajue

Peter alituma ujumbe akiomba apatanishwe na mpenzi wake ‘Alice’ akidai kuwa, I fell in love with a certain lady who indeed drove me crazy despite me being married.

We have lived together for three years till this year and I had planned to introduce her to my people. Please hide my names since I do not want my elder wife to notice me.

Licha ya bwana ‘Peter’ kuzungumzia jinsi anavyompenda Alice ambaye ni wa umri wa juu kumliko na kuwa na watoto watatu, bi Alice alikataa kuzungumza naye.

 

Pata uhondo kamili.

PATANISHO: Mke wangu aliondoka na kusema watoto wetu wanaweza ishi kama yatima

Vincent alituma ujumbe akiomba apatanishwe na mkewe wa miaka mitano, Bi Lydia ambaye hivi majuzi aliamua kufunga virago na kuondoka nyumbani kwao na kumuachia watoto watatu.

Patanisho: Nilitoweka Kwangu Na Kumuacha Mke Wangu Na Mtoto

 

“Hatukuwa tumekosana. Mimi nilikuwa nimeelekea kazini na nikapigiwa simu kuelezwa kuwa mke wangu amefunganya virago na kuondoka.

Kumpigia simu mamake alinitusi sana akidai kuwa nilimtesea mtoto kwani kazi yangu ni kukaa tu nyumbani na kula fedha za mke wangu.” Alieleza Vincent akidai kuwa mkewe alimueleza kuwa atafute mke mwingine ambaye atalea wanawe.

 

Patanisho: Mke Wangu Alidai Kuwa Haja Yake Ni Kula Fedha Za Wanaume Wengine

Alipopigiwa simu bi Lydia, alidai kuwa mumewe alimtesa sana na hata bado hajamuoa ki rasmi na kuwa hataki lolote kumhusu.

“Mimi nafanya kazi yeye hushinda tu ameketi na akipata fedha kiasi hushinda ame bet bila usaidizi wowote. Isitoshe kazi ni kunitusi kwa simu akiniita majina yote.” Alidai Lydia.

PATANISHO: Tangia mke wangu aende kupiga kura hajawahi rudi nyumbani

Fredrick alituma ujumbe akiomba apatanishwe na mkewe Joyce ambaye aliondoka Agosti mwaka jana.

“Ilikuwa ni wakati wa uchaguzi sasa akanieleza kuwa ameenda kupiga kura na alipofika huko, baada ya mwezi mmoja akaanza kudai atarudi lakini akakawia.

Sasa nikamuuliza shida ni gani lakini hakunieleza shida iliyofanya yeye asije hadi wa leo.” Alieleza Fredrick.

Wawili hao wamekuwa kwa ndoa ya miezi mitano.

 

Sema Na Raey: Nilifukuzwa na bibi yangu wa miaka ishirini

Jamaa kwa jina Steve alituma ujumbe katika kipindi cha ‘Sema Na Annitah Raey’ akidai kuwa mkewe wa miaka ishirini alimfurusha kwake nyumbani.

Kulingana na Steve, wawili hao walikuwa wametengana na mkewe akahamia maeneo mengine na watoto wao. Steve alipopoteza kazi alielekea kwa mkewe kumtembelea pamoja na watoto wao wanne.

Yote yalitendeka baada ya mkewe kumuonesha madharau nyumbani kwa kupigia wanaume wengine akiwaeleza waje wamfurushe huku akimuita ‘Takataka.’

Pata uhondo kamili.

Patanisho: Mke Wangu Alidai Kuwa Haja Yake Ni Kula Fedha Za Wanaume Wengine

Bwana Joseph alituma ujumbe akiomba apatanishwe na mkewe bi, Susan akiomba msaada kwani anapitia maisha magumu.

“Mwaka uliopita tulikosana na mke wangu kidogo na akatoweka akarudi nyumbani. Sasa wazazi wake wakaona anapitia maisha magumu na wakamrudisha Nairobi. Nikamweleza aje nyumbani tulee watoto wetu.

Sasa aliporudi shida kuu ilikuwa tabia ya kuongea na wanaume wengine usiku wa manane tukiwa na yeye kitandani. Nikimuuliza anadai kuwa hawataki ila anataka tu kula fedha zao.” Alieleza Joseph.

Wawili hao wamekuwa kwa ndoa ya miaka minne na wamejaliwa na watoto wawili.

Susan ambaye ni shabiki wa Radio Jambo hakutaka kuzungumza nasi.

Pata uhondo kamili.

PATANISHO: Nashuku Mtoto Wangu anasumbuliwa na Majini Na Bwanangu Hataki Kutushughulikia

Maureen alituma ujumbe akiomba apatanishwe na mumewe akidai kuwa alipoenda nyumbani kupiga kura mumewe alimueleza asirudi na vitu vyake.

Isitoshe mtoto wao ni mgonjwa na mumewe alipata mke mwingine.

“Nilienda ushago kupiga kura na bado mtoto alikuwa mgonjwa sasa nikamueleza mume wangu kuwa ninamshughulikia mtoto. Kumpigia simu akanielezea nisirudi na dadake alinieleza kuwa nisijishughulishe kwani Abu ameoa tayari.” Alieleza Maureen akidai kuwa anashuku kuwa mtoto wao anasumbuliwa na majini.

Maureen aliongeza kuwa kuna siku alimpeleka mtoto hadi kwa jamaa fulani ambaye alimshauri kuwa kuna kitu mama mkwe walimfanyia mtoto.

Pata uhondo kamili.

PATANISHO: Mimi Na Mke Wangu Tulikunywa Damu Yetu Mwingine Kumaanisha Hatutatengana

Kyalo alituma ujumbe akiomba apatanishwe na mkewe Nduku ambaye wameoana miaka minane sasa, akidai kuwa ameshindwa naye na angependa kumuuliza mkewe mpango wake ni upi kwani alimpata na mpango wa kando na aliondoka na watoto wao.

“Huyu ni mke wangu wa pili na mimi mwenyewe wakati tulipatana aliniambia nimuoe lakini nikamwambia siwezi kwani wakati huo nilikuwa na wake wawili, na nikamweleza kuwa ile vita nimepigwa na mke wa pili staki mambo ya wanawake.

Sasa baada yetu kuoana alirudi kazini na huko ndipo alianza uhusiano na jamaa flani kwani niligundua kupitia ujumbe.” Alieleza Kyalo huku akidai wawili hao walijikata mikono na kunywa damu kumaanisha kuwa hawatawahi tengana.

Pata uhondo kamili.

Kama Wataka Kumuoa Silphrosa Haya Ndiyo Masharti Unayopaswa Kutimiza

Katika kipindi cha ‘Auntie Boss’ muigizaji, Sandra Anyango Dacha almaarufu ‘Silphrosa’ anajulikana kama mjakazi wake Mayweather. Isitoshe anajulikana kama mama mlafi aliye na watoto saba.

Katika mahojiano yetu naye mwezi mmoja uliopita, Silphrosa aliwashangaza wengi alipofichua kuwa bado hajaolewa ila hana mpenzi na isitoshe hajazaliwa mtoto.

Haya yalibainika wakti tulipomhoji kuhusu mambo ambayo mashabiki wake hawajui kumhusu na alikuwa na haya yakusema.

“Kitu moja ambacho watu hawajui ni kuwa naweza nengua kiuno vizuri sana.”Alisema.

Kingine ni kuwa kama Silphrosa katika kipindi cha ‘Auntie Boss’ watu huona nikiwa nimeolewa na watoto wengi, wacha niwashtue. Sina watoto na bado sijaolewa, kwa hivyo kama kuna mtu ambaye anaona nikama anawezana na hii lori, anawezza tuma application nitakubali. Aliongeza kabla ya kupeana mukhtasari wa vitu anavyo angalia kwa mwanaume.

Cha kwanza napenda mwanaume anayeamini mungu, mwanaume ambaye ana heshima kwa mwanamke kwani mapenzi huja ukiwa na heshima.

 

PATANISHO: Niligundua Kuwa Mke Wangu Aliingia Kwa Ndoa Akiwa Mja Mzito

Alex alituma ujumbe akiomba ndoa yake ya miaka minne iokolewe kwani inasambaratika.

PATANISHO: Mke Wangu Hupotelea Kwa Kichaka Kila Ninapoenda Kwao

“Tulikosana na mke wangu mwezi wa Novemba mwaka uliopita. Shida ilitokea wakati tulianza kukorofishana na nyanyake.

Nilimuoa mke wangu na mtoto mmoja kisha nikaja kugundua kuwa aliingia kwa ndoa akiwa na mimba. Nikakubali na nikamweleza kuwa nitamshughulikia mtoto.

Mtoto mmoja aliwachwa kule mashambani na hapo nyanya yangu alianza kutumia fursa ile kama biashara akidai kuwa nafaa kumtumia kama shilingi elfu moja mia tano kila wiki.

PATANISHO: Bibi Yangu Alininyima Tendo La Ndoa Akidai Amerogwa

Nilipokasirika nyanyangu akanitishia kuwa atampeleka mke wangu kwa wanaume wataomshughulikia.” Alielezea Alex.

Alipopigiwa simu bi Helen alidai kuwa hataki maneno yake kwani shemeji wake walimfanyia mambo makubwa.

Mojawapo ya mambo hayo ni kugombana na nyanyake Alex na pia kupigwa na bwanake.

Pata uhondo kamili.

PATANISHO: Bwanangu Afaa Aamue Kama Ni Mimi Au Mke Mwenza

Bi Martha alituma ujumbe akiomba apatanishwe na mke mwenza bi Maria akidai kuwa wawili hao walikosana baada ya kumtusi.

Ilifika wakati nikiwa na mimba ya bwanangu tukakosana na nikaamua kurudi nyumbani. Hapo ndipo watu wa kwao walinieleza kuwa bwanangu alikuwa na mke mwingine kule mashambani na wawili hao wana watoto watatu.

Jambo hilo liliniudhi sana.

Sasa ikafikia mahali tukaanza kurushiana cheche za matusi na yule mwanadada maneno makali.” Alidai akisema kuwa kama mke mwenza atasalia na bwanake yeye atajiondoa.

Maria alidai kuwa hawezi msamehe kwani alimtusi vibaya huku akiwatusi wazazi wake na isitoshe alimnyang’anya.

Pata uhondo kamili.