Mpende msipende,niko hapa! Maraga asema hatang’atuka hadi muda wake ukamilike

Jaji mkuu nchini David Maraga amesema hatang’atuka mamlakani hivi sasa hadi pale hatamu yake ya kuhudumu itakapokamilika.

Akizungumza alipokuwa anazindua mpango wa dijitali wa kusajili kesi mbalimbali mahakamani, Maraga amesema hatatoka kamwe katika wadhifa wake kwani kuna mengi ambayo yanahitajik kufanywa.

 

“I noticed when the president of LSK spoke it was like he was bidding me goodbye but I am still here,” he “When a judge goes on retirement, he or she gets a letter to go on leave from the chief Registrar of Judiciary and that I think will be in November.” maraga

Deputy Chief Justice Philomena Mwilu and Chief Justice David Maraga during the launch of electronic filing on July 1,2020

Kufikia sasa wahudumu wa afya 186 wameambukizwa virusi vya corona

Chini ya mfumo huo mpya, mawakili, polisi, DPP na wananchi kwa ujumla wanatarajiwa kujisajili kupitia mfumo huo ili kuwa ndani ya data za mahakama.

Maraga amesema mfumo huo utapunguza siku za kusikilizwa kwa kesi na hata wakati wa kuandikisha kesi mahakamani na hivyo kuwasaidia wananchi walioko nchini na kimataifa.

 

David Maraga atofautiana na mabadiliko maalum ya rais Uhuru

Jaji Mkuu David Maraga, ametoa maoni yake kuhusiana na maagizo maalum ya Rais Uhuru kuvunja taasisi ya rais ambayo ilifanya mabadiliko katika serikali.

Katika taarifa mnamo Alhamisi Juni 4, Maraga alisema mabadiliko hayo hayawezi kutekelezwa katika idara ya Mahakama kwani taasisi zote ni tofauti.

Jaji Mkuu David Maraga alisema mabadiliko hayo hayawezi kutekelezwa katika Idara ya Mahakama kwani taasisi zote ni tofauti.

maraga

Maraga alikosoa mabadiliko hayo maalum ambayo yameweka Idara ya Mahakama chini ya Serikali Kuu. “Taasisi hiyo haiwezi kusimamia huduma za idara nyingine tofauti na tume zingine zinazojisimamia.

Serikali kuu haiwezi kubadilisha ama kutoa mwelekeo kwa Idara ya mahakama ama kwa Jaji Mkuu,” alisema Maraga katika taarifa hiyo.

presidentuhurgreetschiefjusticedavidmaragaatthemashujaadaycelebrationsatuhurupark

View image on Twitter

Guys! Wacheni nile bana, Hii corona ilinipeleka teke teke

View image on Twitter

Jaji huyo Mkuu aliomba Ofisi ya Rais kubainisha bayana mabadiliko hayo mapya kwa umma huku akidai kwamba huenda kulikuwepo na makosa.

“Huku ikiwa agizo maalum haijaanza kutekelezwa kisheria, katiba yaelezea vyema kuhusu kubuniwa kwa Idara ya mahakama na Tume ya Huduma za Mahakama na mamlaka yao, ni vyema umma kuelewa kwa demokrasia ya katiba,” Amesema Maraga

Mkutano watibuka! Wamalwa na wenzake kutoka Magharibi wahofia usalama wao

“Kwa hivyo ni wazi kwamba Agizo hilo ni la kutekelezwa katika idara za Serikali Kuu, ninataka kuamini kuwa kulikuwepo na makosa na Ofisi ya Rais itarekebisha makosa hayo,” aliongezea Maraga.

cjmaraga

Haya yanakujia baada ya Rais Uhuru mnamo Jumatano Juni 3, alitia saini agizo maalum na kufutilia mbali taasisi ya rais maarufu kama ‘presidency’.

Muigizaji Celina Njoki awekwa ICU Kijabe

Maana ya hatua hiyo ni kuwa sasa naibu rais hatakuwa na mamlaka yake kando kama vile uajiri wa wafanyikazi wake.

rsz_maraga

Jukumu hilo sasa litachukuliwa na afisi ya rais sawa na bajeti zingine zilizokuwa zikitengewa afisi yake chini ya mpango wa awali.

 

Wanansiasa na watu mashuhuri waliowahi kuhusika katika ajali

Kweli ajali haina Kinga na haibagui tajiri na maskini siku yako ikitimia huwezi ibadili. Hawa ni baadhi tu ya watu amshuhuri waliohusika katika ajali za barabarani na kuachwa na majeraha mabaya.

Mwai Kibaki

Rais Mustaafu Mwai Kibaki alihusika katika ajali mbaya ya barabarani siku chache kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2002. Kibaki ambaye alikuwa mgombea urais wa Narc katika uchaguzi mkuu dhidi ya mgombezi wa KANU Uhuru Kenyatta alisafirishwa ughaibuni kwa matibabu zaidi. Ajali hiyo ilimuacha na majeraha mabaya na hata baada ya kushinda uchaguzi Kibaki aliapishwa akiwa kwa kiti cha magurudumu.

 

1.Raphael Tuju

Tuju ni katibu mkuu wa chama cha jubilee hivi majuzi alihusika katika ajali alipokuwa safarini kuhudhuria mazishi ya rais mstaafu hayati Moi.

TUJU

Habari za ajali yake zilitangazwa asubuhi na mapema na vyombo vya habari. Ilibidi ahamishiwe nchini Uingereza kwa matibabu zaidi.

Itakumbukwa kwamba Tuju pia alihusika katika ajali ya ndege mjini Busia maka 2003 abbda ya kuhudhuria hafla ya kuchaguliwa tena kwa aliyekuwa makamu wa rais Moody Awori. Alijuruhiwa sana na kusalia mkekakani kwa muda.

 

2.David Maraga

Jaji mkuu David alihusika katika ajali ya barabra wakiwa na mkewe, mwaka wa, 2018, Desemba katika eneo la Ngata kaunti ya Nakuru.

cjmaraga

3.David Rudisha

Rudisha alikuwa anaelekea nyumbani kwao alipohusika katika ajali ya barabra, hii ni baada ya gurudumu la dari lake kutoa pumzi na gari kukosa mwelekea huku akiandika katika mtandao wa kijamii na kusema yupo sawa na Kkumshukuru Mola kwa kwa uhai wake.

gettyimages-589987050-e1525805245419

Baada ya hapo rudisha alipelekwa hospitalini.

4.Nameless

Alihusika katika ajali alipokuwa akirudi nyumbani baada ya onyesho katika eneo la Nakuru na kuzungumzia kisa hicho na kusema,

I DID NOT KNOW FROM THE TIME I WAS TAKEN TO HOSPITAL WHEN IT ALL HAPPENED. I WAS TOLD HE WAS IN A DIFFERENT HOSPITAL.

nameless

I HAD NO PHONE OR OTHER WAY OF REACHING HIM. MY BRO CAME FROM NAIROBI. I ASKED EVERYONE AND NO ONE TOLD ME.” Alisema Nameless.

5. Millicent Wambui

MCA Wambui alihusika katika ajali ya barabarani mwaka wa 2017, aki nusurika pekee katika ajali na watu wanne kupoteza maisha yao.

millicent-wambui

6. Yussuf Hassan

Mbunge huyo wa Kamukunji alihusika katika ajali iliomuacha akiwa hali mahututi katika eneo la Eastleigh baada ya kutoka sala.

Yusuf_Hassan

7.Richard Chacha

Mwanahabari Chacha alihusika katika ajali ya barabarani mwaka 2012. Ajali hiyo ilimuacha chacha na majeraha mabaya na kwa sasa hana uwezo wa kutembea.

idsbk5d30cvcvipyrg4q56a31a93d4bf3

 

Maraga kuunda jopo kusikiliza kesi yake Omtatah

Jaji Weldon Korir amelitaja kesi iliyowasilishwa na mtetezi wa haki za kibinadamu Okiya Omtatah kuwa na uzito mkubwa.

Korir ameongeza na kusema kuwa maswala yaliyotajwa mle ndani yanaibua maswali muhimu ya kisheria.

Jaji huyu ametuma ombi kwa  jaji mkuu David Maraga kuunda jopo la majaji litakalosikiliza kesi hiyo.

omtatah
Okiya Omtata

Soma hapa:

Simon Mbugua aipeleka CBK mahakamani

Okiya Omtata mapema jana alifika mahamakani kupinga swala la kuidhinisha noti mpya zitakazotumika nchini kuanzia tarehe 1 Oktoba. Katika stakabadhi alizowasilisha mbele ya mahakama, Okiya anahoji kuwa ni ukiukaji wa sheria katika mpya ya 2010 kuchapisha hela iliyo na picha ya muasisi wa taifa la Kenya Mzee Jomo Kenyatta.

Mwingine aliyefika mahakamani ni mbunge wa EALA Simon Mbugua mapema jumatatu ili kukataa katakata uidhinishwaji wa noti mpya. Mashtaka ya Simon dhidi ya Benki Kuu ya Kenya (CBK) yanaendana sawa na yake Okiya Omtatah.

Soma hadithi nyingine hapa:

Wabunge wataka noti za 1000 kuondolewa mara moja

Gavana wa CBK, Patrick Njoroge katika kikao na wanahabari alisema kuwa yupo tayari kukabiliana na mashtaka yoyote mahakamani. Njoroge alisema kuwa sheria imefuatwa katika mchakato huo na kwamba lengo kuu ni kuzima moto wa ufisadi na wizi wa pesa nchini.

Noti za awali za elfu moja zitapigwa marufuku na kuacha kutumika tarehe mosi Oktoba. Wananchi wanaombwa kubadilisha noti mzee katika tawi la benki iliyo karibu kabla ya muda huo kufika.

Mengine yanafuata…

Nilikua mnywaji mkubwa wa pombe kwa miaka 20, Jaji Mkuu Maraga afichua

 

Jaji mkuu David Maraga, amewashauri vijana wenye uraibu wa mihadarati kutafuta usaidizi kwa wataalamu au kutoka kwa Mungu.

Alipokua akizindua Kampeni ya Uhamasisho kuhusu mihadarati Jumamosi katika Chuo Kikuu cha JKUAT, Maraga amekiri kwamba miaka 20 ya maisha ilipotea kwa ulevi.

‘Nilibatizwa Oktoba tarehe 30 mwaka wa 1965 nikiwa bado katika shule ya msingi lakini nikapata marafiki wa kupotosha nikiwa shule ya upili. Wakati mwingine hata nilikunywa kwa mkopo’ Maraga alisema.

Wanawake wananyanyaswa kwenye matatu, ripoti yafichua

Maraga alisema bado alikunywa pombe kupita kiasi alipokua katika chuo kikuu na hata wakati alipoanza tajriba yake ya uanasheria.

‘Kwa zaidi ya miaka 20 sikuwa na maendeleo yoyote maishani kwa ajili ya pombe. Ningeenda nyumbani saa tisa alfajiri na kuitisha chakula. Mke wangu angeniuliza iwapo kweli ilikua chakula cha usiku au kiamsha kinywa nilichotaka. Singekua Jaji Mkuu iwapo singemgeukia na kumfuata Yesu Kristo’ alisema.

maraga

Maraga amewataka wanafunzi wa vyuo vikuu kujizatiti katika vita dhidi ya mihadarati kwani jamii kwa sasa inawaruhusu walanguzi kuishi miongoni mwai na kuifanya kuwa rahisi kupata mihadarati.

“Kwa kupenda pesa, walanguzi wanawauzia watu mihadarati na kusababisha uraibu huo kuwa miongoni mwa changamoto kuu zinazoikumba nchi hii.

6 notorious criminals arrested by DCI detectives in Kilimani house

Jaji mkuu amelalama kwamba licha ya sheria zilizopo zinazonuiwa kuthibiti ulanguzi wa mihadarati, uraibu huo bado unazidi kuongezeka.

Katika hotuba yake Maraga amefichua athari za utumizi wa mihadarati miongoni mwa vijana.

Hii ni pamoja na kudorora kwa masomo na kuwa na fikra za kujitoa uhai, ukosefu wa ajira, umaskini na maradhi ya akili na kisakolojia.

 

PATANISHO: Mke Wangu Alidai Ni Maraga Pekee Anayeweza Kumrudisha Kwangu

Nicholas alituma ujumbe akiomba apatanishwe na mkewe mama Stano akidai walikosana jumamosi iliyopita kwa ajili ya dadake na akaondoka na kwenda kwao.

Dadake anaishi karibu na kwetu Sasa ikawa siku choo yangu ika block na mke wangu hakuwa. Sasa nikamtumia dadake ujumbe nikimweleza Kuna fundi anakuja kutengeneza na mke wangu hayuko. Hakujibu ile simu.

Nikapigia mke wangu kumuuliza kama yuko karibu kurudi nyumbani na akadai bado hajarudi, hapo nikamtumia dadake ujumbe tena na akakubali na alipofika nyumbani alimpata mke wangu amefika.

Sasa nilipomtumia ujumbe dadake ujumbe akalenga na hapo nikamtumia ujumbe wa hasira na kumbe alionesha mke wangu.

Siku iliyofuata nikamtumia dadake ujumbe nikimwambia kuwa twafaa kupatana tusuluhishe Yale maneno, kumbe alimuonesha mke wangu ule ujumbe na akanikasirikia.

Kurudi nyumbani nikapata mke wangu amefunganya virago na kuondoka.

Kumpigia simu akadai kwangu hatarudi labda nimuendee na maraga.

Pata uhondo kamili.