PATANISHO: Bwanangu Afaa Aamue Kama Ni Mimi Au Mke Mwenza

Bi Martha alituma ujumbe akiomba apatanishwe na mke mwenza bi Maria akidai kuwa wawili hao walikosana baada ya kumtusi.

Ilifika wakati nikiwa na mimba ya bwanangu tukakosana na nikaamua kurudi nyumbani. Hapo ndipo watu wa kwao walinieleza kuwa bwanangu alikuwa na mke mwingine kule mashambani na wawili hao wana watoto watatu.

Jambo hilo liliniudhi sana.

Sasa ikafikia mahali tukaanza kurushiana cheche za matusi na yule mwanadada maneno makali.” Alidai akisema kuwa kama mke mwenza atasalia na bwanake yeye atajiondoa.

Maria alidai kuwa hawezi msamehe kwani alimtusi vibaya huku akiwatusi wazazi wake na isitoshe alimnyang’anya.

Pata uhondo kamili.