Massawe Japanni na mumewe waadhimisha miaka 13 ya ndoa

Mtangazaji wa Massawe Japanni na mumewe Tom Japanni wanaadhimisha miaka 13 ya ndoa tangu waoane kwa kufunga fungate.

Wanandoa hao wamekuwa kwa tasnia ya uanabari kwa zaidi ya miaka 1o.

Akizungumza na mtandao mmoja wa humu nchini, Massawe alisema ndoa ni kitu cha kujitolea na watu lazima waweze kutumia muda wao kila wakati ili kufanikisha malengo yao kwa ndoa yao.

“It is resilience. In it, you discover your elasticity and capacity to do more than you ever gave yourself credit for,” she said.”It is a sacrifice because you learn to make concessions therein. It is a vulnerability, a high-stakes gamble, where your heart is the prize or the price.”alisema Massawe.

massawe krisimasi 1

Aliongeza kuwa ndoa si tofauti na maisha.

“Different seasons, some joyous, some sad, some unexpected, some planned for. And as it is for life, marriage also calls for giving it your all and making sure you enjoy the ride,” aliongezea

Kiambu kaunti kuanza kupima halaiki ya watu virusi vya corona-James Nyoro

Mama huyo wa watoto watatu wakati wa kuadhimisha miaka hiyo 13 ya ndoa aliandika hivi.

“May the grace of God for a blessed family continue to shine on our marriage. And may wisdom be our constant companion! Happy 13th Anniversary #17together #mpakamilele.” 

Massawe and Tom Japanni

Kuongeza mapenzi zaidi kwa ndoa yao, Japanni alimnunulia Massawe pete nyingine.

“When he knows what to get you… I’m here blushing😊😊😊 and it’s fascinating him….More rocks to the years lived…A journey it has been…😘😘@tjapanni #mpakamilele♥,”aliandika Massawe baada ya kupokea pete hiyo.

Safari ya mahaba ya Massawe: Massawe Japanni na mumewe washerehekea miaka13 katika ndoa

Mtangazaji Massawe Japanni anafahamika sana kwa weledi wake wa lugha ya kiswahili. Massawe na mumewe Tom Japanni wanasherehekea miaka kumi na tatu katika ndoa yao.

Wawili hao wamekuwa katika uanahabari kwa zaidi ya miaka kumi.

Screenshot-from-2020-05-12-21_08_38

Massawe na Japanni wamebarikiwa na watoto watatu wa kike. Haya basi wakisherehekea siku hii kila mmoja wao amedhihirisha mapenzi yake kwa mwenzake na ni wazi kuwa mapenzi kati ya hao wawili yamenoga.

Ndoa yao kwa hakika ni ya kupigiwa mfano na wengi.

“HAPPY ANNIVERSARY!! IT HAS TAKEN NOT ONLY LOVE, BUT PAIN AND GRIT, LAUGHTER AND TEARS AS WELL AS THE HELP OF GOD TO GET US TO THIS POINT. MAY THE GRACE OF GOD FOR A BLESSED FAMILY CONTINUE TO SHINE ON OUR MARRIAGE. AND MAY WISDOM BE OUR CONSTANT COMPANION! HAPPY 13TH ANNIVERSARY
#17TOGETHER #MPAKAMILELE♥️.” Massawe Aliandika.

massawe daugh

Tom naye hakuachwa nyuma bali alimnunulia mkewe pete ambayo Massawe aliposti na kuandika ujumbe mfupi;

“WHEN HE KNOWS WHAT TO GET YOU…I’M HERE BLUSHING😊😊😊 AND ITS FASCINATING HIM….MORE ROCKS TO THE YEARS LIVED…A JOURNEY IT HAS BEEN…😘😘@TJAPANNI #MPAKAMILELE♥️.”

Screenshot-from-2020-05-12-23_19_47

Mashabiki wake hawakuachwa nyuma walituma jumbe za kuwatakia kila la heri katika ndoa yao wanaposherehekea siku hii ya maana.

chriskirwa 🙌🙌🙌🙌😀😀😀😀 Our people happy Anniversary 🔥🔥🔥

annengugi Happy Aniversary Queen and King

jackyvike Happy Anniversary Beautiful!!

wilson_malaba Happy anniversary good people

massawe krisimasi 2

kaundaabigail9 Congratulations 13 yrs si kdgo hyo ni yenu🍰🍷

evelynwanjiru_a Happy anniversary my sister…

billymiya Following footsteps every step of the way! Kongole jamani boss lady!

kendi_gichuru Happy anniversary Massawe❤❤

beldingambani Happy for you mungu awalinde

nimmomilka Wow to many more years

 

MHARIRI: DAVIS OJIAMBO

Uko na ujinga! Lulu Hassan amwambia Massawe Japanni baada ya kumpigia simu

Mtangazaji Massawe Japanni aliwapigia watangazaji Lulu Hassan na mumewe Rashid Abdalla katika kipindi chake cha bustani katika radio jambo.

Massawe alimpigia Rashid asubuhi na kumuuliza achague mtu mmoja ambaye angetaka kuongea naye wakati huo.

Rashid hakusita na alimchagua rais Uhuru Kenyatta ili aongee kuhusu janga la corona ambalo linahangaisha wakenya.

LULU 3

” Ningependa kuongea na rais wa Kenya Uhuru Kenyatta, kwa maana mimi ni mwanahabari ningetaka kuongea naye ili nimweleze  jinsi wanafanya kazi vizuri na mahali ambapo wamekosea.” Rashid Alisema.

Massawe alimshangaza Rashid kwa kumpigia mkewe Lulu badala ya rais Uhuru Kenyatta, kwa mara ya kwanza Lulu alikuwa anaongea na heshima lakini alicheka aliposikia sauti ya mumewe na na kumwambia Massawe,

“Uko na ujinga.” Lulu Alisema.

lulu hassan

Baada ya Rashid kuwekwa kwa laini alisema kuwa anataka kuongea na rais wa nyumba yake yaani Lulu.

Baadae Massawe alimuuliza Lulu nini hicho anataka kubadili katika maisha yake, naye Lulu alimuuliza mumewe ni nini ambacho hajawahi kupenda na angetaka kibadillishwe.

Kwa mengi zaidi sikiza mazungumzo yao kwenye mtandao;

https://www.instagram.com/tv/B_2xNkigr4O/?igshid=1dyig122e28fg

 

MHARIRI: DAVIS OJIAMBO

Mazoezi ni afya! Massawe, Akothee na ma celeb wanaopiga tizi!

Mwaka wa 2020 umeanza kwa mpigo huku ma celeb wengi wakiamua kuingia gym na kufanya mazoezi, lengo lao likiwa kuboresha afya yao kwa kuongeza au kupunguza uzani.

Kwa wakati fulani, Gidi alikuwa mmoja wa ma celebs ambao walikuwa wanapiga tizi huku lengo lake likiwa kupunguza utambi na juhuzi zake zilizaa matunda baada ya miezi kadhaa.

Mwenzake Ghost Mulee ambaye ana shule yake ya kukuza vipaji vya soka, anajulikana kwa juhudi zake za kufanya mazoezi kwani mara kwa mara yeye huchapisha picha zake akiwa gym.

Kenyan celebrities who have been hitting the gym 2019

Massawe Japanni naye amekuwa katika safari ya kupunguza uzani na ili kuhakikisha kuwa ndoto yake imetimika, yeye hupiga tizi kila siku asubuhi kabla ya kuja kazini na pia wikendi ambapo huungana na marafiki zake.

Ifuatayo ni orodha na picha za ma celebs wengine ambao hupiga tizi kila siku bila kuhata.

Akothee

akothee

Soma ujumbe wa Ghost Mulee kwa wanaokejeli kitambi chake

2. Massawe Japanni

japanni 1 japanni

3. Talia Oyando

Image result for Taliya oyando working out

4. Yvonne Okwara

Related image

5. Khaligraph Jones

Image result for khaligraph jones

6. Nadia Mukami

7. Ghost Mulee

View this post on Instagram

Life is short.ENJOY

A post shared by Jacob "Ghost" Mulee (@ghost_mulee) on

8. Gidi Gidi

View this post on Instagram

Weather imekubali……kabumbu ibambe

A post shared by Gidi (@gidiogidi) on

‘YAUMA’,Mke wangu aliniachia mtoto siku chache baada ya kujifungua

Katika Bustani ya Massawe Japanni leo mwanamume mmoja alipiga simu akilalamikia hatua ya mkewe kujifungua mtoto na kumuachia.

“Nilikaa na yeye kwa miaka miwili na tukaachana, lakini aliniachia mtoto hadi wa leo hataki kujua mtoto wake anaendelea aje,” Alieleza mwanamume huyo.

Gidi na magwiji wengine duniani kote wamkumbuka Kobe Bryant

massawe

Sijafanya lolote baya:Ajitokeza kusema Gladys Shollei baada ya picha na mzungu kusambaa mtandaoni

Ni jambo ambalo lilifanya mashabiki wachangie na kila mmoja kutoa maoni yake, si wazazi wa kike pekee ambao wanaachiwa watoto bali hata wa kiume huachiwa wana na kuwalea bila usaidizi wa mama mtoto.

Yafuatayo ni baadhi ya maoni ambayo yalitolewa;

” Mimi niliacha mtoto wangu kwa babake akiwa na miezi mitano na sasa hivi ana miaka mitano anaenda shule sasa, nilimuacha kwa sababu huyo mwanamume alikuwa msumbufu sana,” Alisema shabiki wa kwanza.

Sema Kurukwa! Gavana Tolgos asema hatamuunga mkono Ruto kuwa rais 2022

“Niliachiwa mtoto kwa sababu ya mzozo wa kifamilia na bibi yangu alienda kabisa,” Shabiki wa pili aliongeza.

Wengi walipiga simu na kusema kuwa hawawezi kuacha mtoto wao heri waende na wao.

“Mimi siwezi muacha mtoto wangu heri niende na yeye”.

massawe-ilikuaje-300x200

Kweli waswahili hawakukosea waliposema kuwa uchungu wa mwana aujuaye ni mzazi

Ni watoto wangapi wamewachwa na mama au baba zao? lakini cha kustaajabisha ni mzazi wa kiume kuachiwa mtoto na kisha mzazi wa kike kutoweka kabisa bila haja ya kumuona mtoto wake.

STILL FRIENDS? RAIS Uhuru na naibu wake Ruto wakutana kwa mara ya kwanza baada ya mwezi mmoja

Inamaanisha kuwa hawapendi watoto wao ama tutasema kuwa hawana utu ndani yao wanapoamua kuwaacha wana wao?

Hata katika wakati huu wengi wanaacha huku wengine wakiwatupa na kuendelea na maisha yao kwingineko bila kujali.

“Niliachiwa mtoto akiwa na wiki moja lakini baadaye mamake akarudi na kumchukua,” Shabiki mmoja alizungumza.

“Massawe hata mimi niko na mpango wa kumuacha,” Mama mmoja alipiga simu na kusema.

 

 

Bwanangu aliniletea bibi mwingine na watoto kwa nyumba

Kwa kweli mapenzi ni kihozi na hayafichiki na wapendanao hufanya kila namna kuhakikisha kuwa mapenzi yao yanadumu na wanafurahishana.

Hata hivyo, kuna mahali mambo hufika na mapenzi yanaisha, madharau yanaingilia ndoa na hivo ndivyo ndoa husambaratika.

Mwanamke mmoja kwa jina Lucy, aliwashangaza waskizaji alisimulia jinsi mume wake alivyomletea watoto wanne kutoka ndoa ya zamani na kumtenga pindi tu walipojaliwa watoto wawili pamoja.

Ilikuaje: Beth na mwalimu Alice waongelea changamoto za wasichana

Kulingana na Lucy, alipatana na mumewe wakati alikuwa hohe hahe na wawili wakavumiliana bila yeye kujali kuwa analea watoto wa mke wake wa kwanza. Hata hivyo, wawili walijaliwa na mali na hapo ndipo bwanake alianza kujionesha ngozi yake kamili.

Jamaa aliwacha kushughulikia familia yake, na ilimbidi Lucy kuanza kufanya vibarau kadhaa wa kadhaa ili awashughulikie watoto sita. Kuzidisha, bwanake alienda nje na kupachika mke mwingine mimba na wakapata watoto mapacha.

Bila heshima aliileta ile familia kwake jambo lililomkera Lucy na kumpelekea kutaka kujitoa uhai kwa kunywa sumu.

Soma usimulizi wake.

Massawe mimi nikiolewa nilipata bwana yangu ameoa bibi wa kwanza ameenda amewacha watoto wanne, nikiolewa na yeye alikuwa mtu wa kuchunga ng’ombe.

Nimehangaika na watoto nimefanya vibarau kwa mashamba ya watu, nimeenda forest nikitoa kuni nikiuza kusudi hawa watoto wapate chakula.

Bwanangu ilikuwa Jumapili  ameniletea mwanamke na watoto wawili, Massawe jambo hilo limeniuma. Kando ya hao watoto wanne, ameoa, amepatia mwanamke mimba na amezaa mapacha wawili. Nashukuru mungu kwa sababu maisha yenye nimepitia ni mungu tu anajua hata ilifika mahali nikanywa sumu kwani moyo wangu unaniuma zaidi.

Tumezungumza na mume wangu na akasema mtu akitaka kujiua ajiua mtu akitaka kwenda aende kwani hana shughuli.

Bwanangu alileta watoto kunyoa kisha akarudi nao na akaniwachia wanne pamoja na wawili tulioa naye. Mmoja wa miezi sita na mwingine wa mwezi mmoja. Napanga mungu akinifungulia mlango kidogo nijiondee kwani dalili ya mvua ni mawingu.

Kutana na familia ya mtangazaji maarufu Massawe Japanni (Picha)

Kinachomuudhi Lucy ni kuwa baba mkwe ndiye anayeingilia ndoa yake na hana mtu yeyote wa kuendea kila anapotaka kutatua shida za ndoa yake.

Aliongeza: Kitu kinachoniuma ni eti bwanangu hana wazazi kwani wote waliaga na mwenye alibaki ni babake mdogo na ndiye kunipangia hayo yote, imeniuma sana. Baba mkwe ameingia kwa ndoa yangu kwa kichwa na miguu.

Nilikuwa napigwa na kumwagiwa maji kitandani na mume wangu – Peninah

Lakini jameni, uwe mume au mke ambaye yuko kwenye ndoa ya mateso na matusi, itakuchukua mda gani kabla uamue kuondoka?

Wengi huvumilia wakiwa na imani kuwa wapendwa wao huenda wakabadilika huku wengine kwa bahati mbaya wakifuatwa na mauti, yote kwa ajili ya mapenzi.

Kisa ambacho unasoma ni cha mwanadada kwa jina Peninah ambaye alijipata taabani mikononi mwa mumewe mkatili. Mumewe alianza kumpiga kila siku bila hata sababu.

Cha kushtua ni kuwa hamna aliyemuamini nyumbani kwao.

Jamaa alikuwa anamuamsha usiku na kumwagia maji kitandani kabla ya kumpa kichapo cha mbwa. Isitoshe alikuwa anacheza nje ya ndoa na rafikiye wa dhati ambaye alikuwa mke wa wenyewe.

Soma usimulizi wake;

Mimi nilikuwa nimeoleka hapa Webuye mahali panaitwa malaha, na kupigwa ndio ilikuwa kazi na nilichoka.

Yeye ni mtu wa bodaboda na alikuwa anatoka asubuhi vizuri jioni akirudi hazungumzi, ukiamka kumpakulia chakula kisha ukirudi kitandani ananimwagia maji kitandani naloa mpaka na godoro yote.

Hapo nikajijazia kuwa labda ametoka mwingine huko town alikotoka, iliendelea hivyo na kuna wakati tukilala kama hajanipiga ikifika saa tisa usiku alikuwa anaamka ananitoa kwa mattress na kuniambia kuwa sijui alikotoa pesa na alivyo nunua na ananiamrisha niamke nilale chini ya simiti.

Nina mtoto mmoja lakini mimba ya pili alinipiga ikatoka, ya tatu ikatoka.

Nilikuwa naenda narudi kwani mbele ya wazazi walikuwa wanaona mimi ndio mbaya kabla ya mwishowe kugundua yeye ndio mbaya.

Ile kitu ilifanya nitoke aki nilikuwa na rafiki yangu ambaye tulikuwa tunauza naye vitu, sasa ile wakati nilikuwa napigwa na kufukuzwa naye alikuwa anarudi kwangu.

Kumbe alikuwa mke wa wenyewe na alipopatikana nyumba ikachomwa na kila kitu kuharibiwa na hapo ndipo kila mtu nyumbani alijua ukweli wote.

‘Naomba mume wangu aambukizwe kisonono afariki!’ – Cynthia

Je wewe kama mwanaume ukaskia kwamba mkeo hukuombea mabaya ili uage dunia utafanya nini? Utamuombea abadilike au utamtema kama viazi moto?

Katika kipindi cha Bustani la Massawe, mwanadada mmoja aliwaacha wengi vinywa wazi alipopiga simu na kulalamikia tabia za mumewe.

Kulingana na mwanadada yule kwa jina Cynthia, alisimulia jinsi mumewe amekuwa fisi mla wanawake njia ya ndoa, jambo ambalo linamkera sana moyoni mwake.

Chris Martin na mastaa wawili zaidi kutoka Jamaica wawasili nchini

Alidai kuwa mumewe ana mipango ya kando wengi na huwabadilisha kila siku kama nguo.

Cha kushangaza ni kuwa Cynthia ambaye amekuwa kwa ndoa ya miaka minane na jamaa huyu, humuombea usiku na mchana apate maambukizi ya kisonono.

Anadai ombi lake ni kuwa akipata kisonono atakosa zile nguvu za kutongoza wanawake na mwishowe aage dunia.

Ila alichosahau Cynthia ni kuwa kisonono kina dawa na waweza kupona ukinywa dawa vilivyo.

Hata hivyo soma usimulizi wake;

Je ni haki? Kocha wa Enugu FC afutwa kazi kwa njia tatanishi

Wangu amefika mwisho yaani naombanga mungu kila siku apate kisonono agonjeke ashindwe kutongoza wanawake. Amenifika mwisho aki ya mungu huyu mwanaume ni malaya anatembea kwa wanawake kila siku ananibadilisha kama nguo.

Je si akipata kisonono atakuambukiza?

Hapana hawezi juu mimi hatuwezi shiriki na yeye ndoa, tumeishi naye miaka minane na baada ya kujua ana hao wasichana nimekaa karibu miezi sita hivi hatushirikiana.

Niko tu sawa lakini mimi huomba usiku na mchana apate kisonono agonjeke akufe!

‘Shinda tuzo kadhaa kisha tuongee!’ Dadake Ronaldo amfokea Van Djik (Picha)

Maisha ya huntha! changamoto za kuwa na sehemu mbili za siri

Katika kitengo cha Ilikuaje na Massawe Japanni, Kwamboka alijitokeza na kusema waziwazi  vile maisha yake yalikuwa magumu  alipokuwa mchanga kabla ya kukubali mambo yalivyokuwa.

IMG_9926

Kwamboka alisema kuwa, wazazi wake walikataa kutimiza wajibu wao  na hata kumwambia ajue atakavyojisaidia.

Taarifa ya Habari Toleo la saa saba 23/10/2019

Visa vya  wazazi kukataa kutimiza wajibu wao kwa watoto waliozaliwa huntha ni vingi sana lakini Kwamboka anatupa moyo leo kutuonyesha kuwa yote yanawezekana.

Kwamboka alisema, alipokuwa mdogo alijaribu kumwambia mamake lakini alikuwa akimchapa kila wakati alipomueleza kuhusu jambo hili na kushindwa ni yupi angemsaidia.

Ajali! 2 waaga katika ajali barabarani, Voi.

Hivyo basi, Kwamboka alisafiri mpaka Nairobi huku akidhani kuwa atafika na maisha yatakuwa mazuri lakini alipofika Nairobi, mambo hayakuwa alivyotarajia.

Kwamboka alipofika Nairobi alishindwa kujikimu maishani na hapo ikambidi awe chokora.

Baada ya siku nyingi za kuteseka jijini, alikutana na mama mmoja ambaye alikuwa huntha pia na huyo mama akaamua kumchukua na kumpeleka shuleni ambapo alikubaliwa na kupendwa.

Mwenzake Kwamboka  pia alisema kuwa maisha yalikuwa magumu sana kwa upande wake,  mamake alikuwa anampenda lakini watu wa kwao hawakumkubali.

Cha kusikitisha ni kuwa, mama yake alikuwa anaficha chakula na kumpelekea kwa sababu hakuwa anataka aonekane na watu wengine kwani  ingekuwa tatizo kubwa katika jamii yake.

Vilevile  alisema, maisha  yake shuleni ni magumu kwani ikiwa yuko katika hedhi yeye hupata damu nyingi sana.

Zaidi ya hayo, walisema kuwa kushiriki tendo la ndoa ni changamoto kwake kwani huwa anaogopa kuwa mpenzi wake anaweza kuona na kushtuka ama kumwacha.

Amini usiamini Kwamboka alisema kuwa yeye ana mke na anampenda sana kwani alimkubali alivyo.

 

 

 

 

 

 

Ilikuaje:Ya Mungu ni Mengi!Mwanamke aliyepoteza maisha ya watoto nane ajieleza

Susan Wanjiru Ndung’u aliyekuwa mgeni wa kitengo cha Ilikuaje na Bi Massawe Japanni,alifunguka mwanzo mwisho na kueleza yaliyompata kila wakati alipojaribu kujifungua mtoto.

Bi huyu ambaye ni mama,mhubiri na hata mwanasayansi alisema kuwa,maisha hayo yalikuwa magumu  na alikuwa mwanamke mwenye huzuni sana.

Susan alisema kuwa alizaliwa na shida ya jeni (genes) na alipokuwa tayari kuwa mama ndipo akagundua ana shida ile baada ya kuwa na shida ya kutoweza kubeba ujauzito kwa miezi inayotakikana.

Amini usiamini,Susan alipoteza watoto saba kwa sababu ya kuharibikiwa na utumbo (Miscarriage) na wengine wawili wakazaliwa na kufariki.

Patanisho:Daah! Wapenzi wakosana na kukata uhusiano baada ya miaka

Vilevile,binti huyu alisema kuwa hakupoteza matumaini ya kupata mtoto hata baada ya kupatwa na matatizo mengi ya ujiauzito kwa sababu alikuzwa katika familia ya kikristu ambapo mama yao aliwafunza kutokata tamaa maishani.

”Sikuwa nakufa moyo kwa sababu mama yangu alikuwa ametufunza tusiwe watu wa kukata tamaa kwani hata Ayubu alijaribiwa na hakukata tamaa.”Susan alisema.

Licha ya hayo,mhubiri huyu alisema kuwa, mume wake alijitolea mzima mzima kumsaidia na kumuunga mkono kwani hata kuna wakati ambao hakuwa anajiweza kabisa na bado mume wake alizidi kumpa msaada wowote ule alihitaji.

Je ni yeye kweli? Tazama picha za Betty Kyallo bila vipodozi

Aisee!Ni wazi kabisa kuwa Mungu hamuachi mja wake kwani baada ya kutibiwa ugonjwa huo binti huyu aliweza kujifungua watoto na kwa sasa ana mapacha na mtoto mmoja ambao wote wamekuwa wakubwa.

Mwisho kabisa,alizidi kuwaambia kina mama ambao wanapitia changamoto hili la kutopata watoto wasife moyo,waende hospitalini na  pia waombe Mungu na mambo yatakuwa shwari.