Eric Omondi alinipa shavu kimuziki, Bahati hakuweza- Madini Classic

Staa wa muziki nchini Madini Classic amefunguka katika kikao cha Papa Na Mastaa kuwa mchekeshaji Eric Omondi alikuwa wa kwanza kumshika mkono na kumpa moyo wa kufanya muziki. Muimbaji huyu alimtaja Eric kama nguzo muhimu katika maisha yake ya sanaa. Madini Classic aliirithi jina lake kutoka kwa babu yake ambaye alikuwa mchimbaji migodi katika kitongojiduni cha Migori.

 

Soma hapa:

King Kaka afunguka kuhusu kufanya collabo na mzazi mwenzake Sage

Madini alimueleza Papa mwanzo mwisho jinsi alivyotoka kijijini na kuja Nairobi kujituma kwenye haso zake za kimziki.

“Kipindi natoka nyumbani kweli sikuwa na muziki. Nimekuja kuimba nikiwa hapa Nairobi . Muziki ulionitambulisha kwenye mainstream media unaitwa Nikaribishe. Kikawaida safari ya muziki huwa ndefu sana. Sio kitu unaweza ukabumburuka na ghafla utusue.” alisema Madini.

Madini aliweza kueleza ukaribu wake na Eric Omondi na jinsi alivyomhimiza afanye muziki mkubwa.

“Eric Omondi ni mtu na ambaye anapendana sana kipaji changu. Alimuuliza Bahati huyu Madini ni nani. Bahati akamwambia kuwa mimi ni rafiki yake. So akamwambia mbona usisaidie huyu jamaa atoke kimuziki kwa sababu bahati alikuwa ashatoka na akawa mkubwa lakini inaonekana mikakati za Bahati na shughuli zikawa nyingi mpaka akasahau.” Madini alimueleza Papa.

Pata uhondo hapa:

 

“Nikiingia Mombasani nione Fatuma sitambania” – Mbusii

Madini alisema kuwa anatamani sana angefanya muziki na mastaa kama Sauti Sol, Alikiba na Diamond Platnumz. Kupitia kuwashirikisha kwenye ngoma, staa huyu alisema anaweza jifunza mengi kimuziki.

 

 

 

Rayvanny adaiwa kuiba idea ya wimbo wake Willy Paul

Msanii wa nyimbo za injili na mwenye utata Willy Paul amechapisha kipande cha video akionekana kulalamika kuwa mwenzake wa Tanzania Rayvanny kamwibia idea ya nyimbo yake Chuchuma. Nyimbo hii haijaweza kurekodiwa beat zinakwenda sawa.

 

Kulingana na Pozze, mipango ilikuwepo ya kuzama studio na kufanya bonge la collabo ila mambo yakashindikana. Katika Insta story yake staa Rayvanny anaonekana akiuimba muziki huo wa chuchuma na kuandika caption kuwa akiingia studio anadondosha hits tu.

Tumekusogezea hapa:

King Kaka afunguka kuhusu kufanya collabo na mzazi mwenzake Sage

000

Willy Paul alifanya ngoma na staa huyu wa Tanzania muda mchache uliopita. Nyimbo hii inayofahamika kama Mmh inatamba na kufanya vizuri katika mtandao wa Youtube na upigwaji mkubwa katika redio na runinga mbalimbali.

“Simama wakuone kijana mfupi round” – Mbusii amuita Uche

Ushikaji wa dogo hawa wawili unaonekana haupo tena baada ya madai haya ya wizi wa nyimbo. Katika kipande hicho cha video, Willy Poze anaonekana akipiga mistari ya kikwake akitaja baadhi ya mastaa hapa nchini.

Msanii Rayvanny hajaweza kujibu madai hayo ya kuifanya ngoma yake Pozze.

 

Massawe atarudi kuwapasha polisi Industrial

Baada ya ajali ya jumatano iliyofanyika kati ya gari ya staa wa redio Massawe na basi ya sacco ya Orokise, mtangazaji huyu ameapa kufika kituo cha polisi Industrial na kuwapasha.

Akizungumza jana katika kipindi anachopeperusha kuanzia saa nne hadi saa nane alasiri, mtangazaji huyu alionekana kutopendezwa na wanapolisi hao.

“Am still going for my abstract and I think I will give them peace of my mind.” afoka Massawe.

Soma hapa:

Baadhi ya maneno Massawe huyatumia hewani na maana yake

Massawe akionekana kukerwa na tabia ya wanapolisi hao, amefunguka walivyomnyamazisha na kumtaka asiongee. Alikuwa ameandamana na maafisa wa polisi hadi kituo hicho baada ya tukio hilo.

Massawe aligongwa na gari kutoka nyuma na kuvunja kioo cha gari lake. Kulingana naye gari hiyo ya sacco ya Orokise ndio walivunja sheria za barabarani.

“Unajua wakati mwingine unaweza ukawa careful barabarani lakini mwenzako hafuati sheria.”

Baada ya kupatikana na bima pana ya gari lake, afisa mmoja alimueleza kuwa asiwe na hofu.

Pata uhondo hapa:

Massawe afunguka kuhusu ajali – Jumatano

“Madam insurance yako ni comprehensive wacha insurance isort.” amesema Massawe.

Hali kadhalika Massawe amedokeza alivyotaka kukimbia na kutoweka baada ya kisa hicho lakini msamaria mwema akamsihi asifanye hivyo.

“Nilitoka mbio. Nilikuwa nataka kutoroka. Msamaria mwema akaniambia nisifanye hivyo.”

Massawe ameongeza kusema kuwa wanapolisi hawafai kuwadhulumu wananchi na kuwa uwepo wao ni kuhakikisha usalama kwa watu wote.

 

Baadhi ya maneno Massawe huyatumia hewani na maana yake

Utangazaji wa redio ni mojawapo ya sanaa duniani zinazohitaji ubunifu mkubwa na ukakamavu wa kuwashika na kuwagandisha wasikilizaji katika spika za redio zao.

Sanaa yoyote lazima msanii achombeze maneno matamu yanayofanya kazi yake ionekane bora na ya kuvutia zaidi.

Soma hapa:

Massawe afunguka kuhusu ajali – Jumatano

Mwimbaji wa nyimbo za mapenzi atapenda sana kuchonga mistari inayokwenda freshi na maudhui na lengo anayokusudia kwa mashabiki wa jinsia tofauti. Hali kadhalika anapofanya maonyesho jukwaani atakuwa na baadhi ya maneno kinywani ambayo wafuasi wake humtambua nayo.

Mtangazaji Massawe hajaachwa nyuma katika mtindo huu na kuna baadhi ya maneno anayoyatumia katika kipindi chake cha Bustani la massawe ili kuvutia mashabiki.

Pata uhondo hapa:

Sababu Massawe Japanni hatokuwa hewani kwa mda

Tumekusogezea hapa baadhi ya tungo virai (phrases) anazopenda kutumia:

  1. “Nafurahi kuwa tupo pamoja nawe”

Baada ya nyimbo inayocheza hewani kumalizika, mtangazaji huyu anapenda sana kuanza na maneno haya kama kitambulisho cha kufungua shoo.

     2. “Ngwenee”

Hili ni tamko ambalo lina asili ya lugha ya Kikamba na huwa na maana ya ‘Nakuona’. Kwa haraka haraka unaweza toa ubashiri wako na kusema kuwa Massawe husema hivi labda kwa sababu anatoka maeneo ya ukambani au labda ni mbinu ya kugeuza ndimi na kuwavuta wasikilizaji kutoka jamii hiyo.

    3 .” Uko hii town? Au niko hii town au labda hii ni town”

Massawe hutumia maneno haya mara kwa mara. Staa huyu huwa anataka kujua mashabiki wake wanategea kipindi wakiwa maeneo gani.

 

Soma pia:

‘Safiri salama dadangu’ Massawe Japanni mourns her best friend

Massawe afunguka kuhusu ajali – Jumatano

Mtangazaji wa kipindi cha majira ya mchana – Bustani la Massawe  na kinachopeperushwa kuanzia saa nne hadi saa nane alasiri katika mawimbikasi ya Redio Jambo amechapisha ujumbe  kwa mashabiki wake katika mtandao  maridhawa wa Instagram.

Staa huyu amezamia insta story yake na kutoa ushauri wake kwa mashabiki wake kuwa wakae ange muda wowote wanaposafiri.

“Siku iliyoje! Ndo nafika chumbani baada ya kuhusika katika ajali ndogo ! Mafunzo nimeyasoma muda wowote chochote kinaweza kufanyika. Funga mkanda wa usalama kila wakati.”

 

 

massawe

Tumekusogezea hapa:

Massawe Japanni anusurika baada ya kuhusika katika ajali mbaya (PICHA)

Mtangazaji Massawe alipigwa na butwaa na kuingiwa na kibuhuti baada ya tukio la jana. Wasikilizaji walimkosa Jumatano ila leo (Alhamisi) yupo yupo kuwakonga nafsi wasikilizaji wake.

Zamia uhondo hapa:

Sababu Massawe Japanni hatokuwa hewani kwa mda

Kipindi chake huangazia sana matatizo yanakumba familia katika jamii hususan wanaume wanaopachika mabinti mimba na kuwazimia data ghafla. Massawe huwapigia simu na kuwasaidia kwa kuwaelekeza katika kituo cha kusaidia kina mama.

Jilie utamu hapa:

Video of the day: Massawe Japanni’s dancing skills are top notch!

 

Gabu amsifia msanii Diamond Platnumz

Msanii mkubwa Afrika mashariki Gabu almaarufu kama Bugubugu alipata nafasi na kufika kwenye kikao cha Papa Na Mastaa kinachoruka kupitia mtandao wa youtube wa Redio Jambo.

Kikao hiki huongozwa na mtangazaji Rais Papa  na huwa ni kitengo maridhawa cha mazungumzo na mastaa wakubwa nchini.

Gabu ameweza kuzungumzia nyimbo yake na msanii Mbosso kutoka lebo ya WCB huku akimsifia msanii nguli Afrika na mmiliki wa Wasafi FM na Wasafi TV Diamond Platnumz.

“He’s a good businessman. Very sharp. Anajua chenye anafanya.”

Soma habari kemkem:

King Kaka afunguka kuhusu kufanya collabo na mzazi mwenzake Sage

Staa Gabu ameweza kuzungumzia nyimbo inayotamba kwa sasa Koroga na sababu kubwa za kuichapisha katika mtandao wa Vevo.

“Vevo inalipa vizuri. Vevo ni ya mastaa. Na pia watu wengi wanatoka Youtube na kwenda kwa Vevo. Halafu ina rangi nzuri katika TV yako nyumbani. Nimependa tu vevo.”

Katika nyimbo hii inayofanya vizuri katika mtandao huo, Gabu alifunguka jinsi walivyoshirikiana na staa kutoka Uganda Addy Andre na Arrowboy.

Soma hadithi hapa:

“Nikiingia Mombasani nione Fatuma sitambania” – Mbusii

“Niliita Arrowboy akakuja kwa studio nikampatia collabo nikamwita Addy andre kutoka Uganda ni producer na bado mi msanii amefanyia Jose Chameleone kwa hivyo akakuja Kenya tukafanya muziki. Tukasafiri Tanzania tukafanya video na Kenny kwa siku 3.  Kenny anafanya na Zoom Production Wasafi alafu video ikatoka.”

Mkali huyu wa Koroga pia alizungumzia kuhusu collabo yake na Mbosso kutoka lebo ya WCB, Mastory huku akionekana kubana kiwango cha hela alichomlipa.

Soma mengine hapa:

“Simama wakuone kijana mfupi round” – Mbusii amuita Uche

“Mambo ya hela sitataja. Chenye nitakwambia ni tuliclick vizuri mambo yakawa sawa ile siku alikuwa amekuja Nairobi. Tukaclick vizuri alikuja kwa studio yangu Kompakt Records tukarekodia audio hapo alafu tukaenda Tanzania kushoot video. Tuko na uhusiano kati ya Kompakt na Wasafi.”

Hali kadhalika Gabu alimzungumzia msanii Kristoff na jinsi anavyomwona kisanii

“Kristoff tumetoana mbali nimeweza kum_advise hapa na pale. Na Kristoff sasa ni one of the biggest artistes hapa Kenya. Sisi ni marafiki tu, family friends na business men.

Soma hapa:

Musician Vivian opens up on being in an abusive relationship

Msanii huyu alieleza kimya cha kundi la Punit ambayo wengi wamekuwa wakihisi kuwa kuna ubaridi ambao ni dalili ya kuvunjika kwa kikundi hiki.

“Timu tupo lakini tuko na bigger fish to fry. Mimi niko na studio yangu hapo nmeshikana na Steve Ongechi. Boneye na studio yake pale Decimal Records ameshikana na Musyoka. Frasha alikuwa ndani ya Pacho. Idea yetu ni kushikilia industry in various ways but tunakuja pamoja tunafanya kama Punit na kila mtu ni brand kivyake.”

Gabu amesema kuwa yupo na mpango imara wa kuhakikisha kuwa anawasaidia wasanii chipukizi kupitia studio yake

“Kwa studio kuna wasanii tunawabring up hapo Kompakt Records  in the few months hivi mtakuwa mnawaskia. Kuna nyimbo ya kimataifa nafuatilia ila chenye nafuatilia sai ni my new artiste anatoa ngoma”.

Soma hapa:

Gidi amkosoa rapa Khaligraph Jones

 

King Kaka afunguka kuhusu kufanya collabo na mzazi mwenzake Sage

Msanii na rapa mkubwa Afrika mashariki King Kaka amefunguka sana kuhusu kufanya muziki na aliyekuwa mpenzi wake Sage.

Katika mahojiano na mtangazaji Rais Papa katika kipindi kinachoruka katika mtandao wa youtube ya Redio Jambo, mkali huyu ameweza kusema kuwa hana matatizo na mzazi mwenzake baada ya wao kutengana huku akisema nafasi ikitokea wanaweza ingia studio na kufanya ngoma.

“Tukikutana studio tunaweza fanya ngoma. Muziki inafanywa tu si ni muziki.” Alisema King Kaka.

Soma mengine:

Musician Vivian opens up on being in an abusive relationship

Papa Na Mastaa ni kipindi na ambacho kimetengwa kwa mahojiano ya kipekee na mastaa wa muziki, mkali huyu ambaye ni mjasiriamali, rapa na mwimbaji pia ameanzisha juhudi za kuwasaidia wasanii chipukizi inayofahamika kama Empires Gold na tayari wasanii watatu wapo katika mpango huo.

King Kaka pia ameweza kuweka wazi sababu iliyomfanya yeye kuacha kufunza masomo ya biashara katika chuo kikuu cha Zetech. Staa huyu aliweka pembeni kazi hii kwa misingi ya kazi nyingi zinazomwandama.

“Nilikuwa mhadhiri Zetech University. Nilikuwa nafunza business na kwa vile schedule yangu ilikuwa tight nkaacha. For almost 2 years sifunzi.”

Mkali huyu aliweza pia kuzungumzia safari yake ya Marekani inayofahamika kama Eastlando Royalty US Tour. Ziara hii ya marekani iliweza kumfanya aingie studio na kumshirikisha msanii wa kimataifa Cassidy katika nyimbo inayofanya vyema ya Far Away.

“The fact that nikona Cassidy kwa ngoma ni ushindi ukubwa,” King Kaka alieleza katika kikao cha Papa Na Mastaa.

Pata uhondo hapa:

My hubby pinned me down and shaved my hair – Cries Woman

Audio ya nyimbo hii ilifanywa hapa nchini na Musyoka na video ikihaririwa na mkenya anayeishi Marekani, Hussein Njoroge.

King Kaka alifunguka zaidi kuhusu mahusiano yake na msanii Sage na jinsi anavyotenga wakati kuongea na watoto.

“I think you’re talking about sage yeye akona my other daughter. Lazima niende kumwona mtoto wangu ambaye ni Ayana lakini naishi na Nana. You’ve to create time for your kid.”

King Kaka hali kadhalika alisema kuwa yupo freshi na Msanii Khaligraph na kumsifia sana.

“Ni jamaa anafanya vizuri tunashukuru mungu. Tukiona vijana wanatia bidii tunafurahia. Anatia bidii kwa kazi zake. Tunaongeaongea ikifika time tutaingia studio.”

Soma hapa:

‘Kijana fupi amenona..’ Compilation of the best quotes by lonyang’apuo