[Picha ] KQ yafanya ziara ya kwanza London baada ya zafari za kimataifa kuanza

Shirika la safari za ndege nchini Kenya Airways  limerejea usafiri wa kwenda nje ya nchi  kufuatia kulegezwa  kwa mashari ya usafiri wa kimataifa kama ilivyoagizwa na rais Uhuru Kenyatta .

Ndege ya kwanza ya KQ kufnya safari ya kimataifa  KQ100  imeondoka mapema leo kwenda lOndon ,Uingereza

Mwenyekiti wa bodi ya shirika hilo Michale Joseph  amesema ziara hiyo ya kwanza ni muhimu sana na yenye hisa nyingi  akisema kwamba hali imekuwa ngumu kwa wafanyikazi wa kampuni hiyo .

Joseph ni miongoni mwa walio katika ndege hiyo kwa safari ya kwenda London .

KQ 2

KQ 3

Mwezi huu kutakuwa na  ongezeko la safari za kimataifa kwenda katika miji ya Paris , Mumbai na Amsterdam .

Barani Afrika KQ itafanya safari za kwenda  Accra, Dzaoudzi, Freetown, Harare, Kilimanjaro, Lagos, Monrovia, Moroni, Nampula  na Zanzibar.  Kulingana na uhitaji ,safari  zaidi zitafanywa katika maeneo mengine  duniani .

Katibu wa utawala wa mashauri ya Kigeni Ababu Namwamba amesema ni jambo zuri kushuhudia hatua za kuanza kufunguliwa kwa uchumi .

 

Shirika hilo linata sanitizer kwa wasafiri wote walio katika ndege hiyo  na wafanyikazi wake .

Janga la covid 19 limekuwa na athari kubwa kwa sekta za usafiri  wa ndege na utaii baada ya mataifa mengi kupiga marufuku safari za kimataifa .

Kulingana na IATA  mapato yatonakayo na usafiri wa ndege yamepungua kwa dola bilioni 6 ikilinganishwa na mwka jana .

Sekta ya utalii nchini Kenya nayo imepoteza  shilingi bilioni 80  kufikia sasa .

 KQ 4

KQ 5

Michael Joseph ateuliwa mwenyekiti wa bodi ya Safaricom

Safaricom imemetua Michael Joseph kuwa mwenyekiti mpya wa bodi yake. Anaichukua nafasi hiyo kutoka kwa Nicholas Ng’ang’a ambaye anastaafu baada ya kuiongoza bodi ya kampuni hiyo kwa miaka 16.

Safaricom itatoa tangazo hilo rasmi kwa umma wakati wa mkutano wake wa kila mwaka   siku ya Alhamisi.

Michael Joseph achukuwa nafasi ya Bob Collymore

Mwenyekiti wa bodi ana jukumu la kusimamia oparesheni na uongozi wa  bodi  ili kuunda ajenda ifaayo kwa ufanisi wa kampuni hiyo.

Michael Joseph ndiye afisa mkuu mtendaji wa kampuni hiyo, nafasi ambayo aliishikilia kuanzia  Julai mwaka wa 2019 hadi machi mwaka huu. Alijiunga na  kampuni hiyo Septemba tarehe 8 mwaka wa 2008.

Awali aliwahi kuwa afisa mkuu mtendani wa safaricom  kuanzia Julai mwaka wa 2000  wakati kampuni hiyo ilipozinduliwa upya kama biashara ya pamoja ya  Vodafone UK  na Telkom Kenya  hadi alipostaafu Novemba mwaka wa 2010.

Michael Joseph achukuwa nafasi ya Bob Collymore

Michael Joseph ameteuliwa kaimu afisa mkuu mtendaji wa Safaricom kufuatia kifo cha Bob Collymore. Kampuni hiyo imetangaza kwamba Joseph atashikilia wadhifa huo hadi pale bodi ya kampuni hiyo itakapotangaza afisa mkuu mpya wa kudumu.

joseph
“Bodi inaimani kwamba, Joseph atatoa muongozo na uongozi unaofaa wakati huu wa mpito,”,” Katibu wa kampuni hiyo Kathryne Maundu alisema katika taarifa.

Harambee Stars yanyukwa na Senegal

 

Michael Joseph alikuwa afisa mkuu mtendaji mwanzilishi wa kampuni hiyo kabla ya kustaafu na kumwachia majukumu Bob Collymore aliyefariki siku ya Jumatatu baada ya kugua saratani kwa kipindi cha miaka miwili.