Bibi yangu aliniroga na nimekuwa nikimbebea mimba – Kenyan man narrates

I have always known that the the world is a strange place but now I am more than convinced that Kenya is it’s headquarters.

This is because of the number of bizarre stories that people share involving witch craft and rituals, total madness!

One man by the name Martin has taken ‘madness’ to a whole different level, am talking outer space level.

Video of the day: Massawe Japanni’s dancing skills are top notch!

Martin left many in shock when he narrated how he used to carry his wife’s pregnancies. I am talking five of them. I know this is where all of you scientists start thinking am bluffing but he attests all these to witch craft.

He says his aunt brought him a wife whom he did not love and for that reason, he used to beat her in order to get rid of her for good. Instead, the lady sought mganga services in Uganda in retaliation.

He says his wife was given some weird medicine which she was instructed to apply on his belly, and the result would be that everytime his wife was expectant, Martin would carry the child for eight months then ‘hand over’ the duties to his wife.

Martin says he did this five times and had to run away from his matrimonial home because he had ‘bebad’ enough!

Kutana na familia ya mtangazaji maarufu Massawe Japanni (Picha)

Read his confession below.

Nilioa bibi ambaye nililetewa na dada ya mamangu na ilifika mahali akaenda kwa mganga. Alipewa dawa ambayo yeye akipata mimba mimi ndio nitabeba.

Kuna dawa eti anakupaka kwa tumbo na akipata mimba wewe ndio unabeba kwa miezi minane.

Nilikuwa nampiga kwani sikuwa nampenda kwa sababu nililetewa bure, sasa nilikuwa nampiga ili aende na badala aende alienda kwa mganga.

Nilitoroka kwani niko Ng’ong kazini naye ako western. Nimebeba mimba ya watoto watano kwani ukiniona nikivaa koti unadhani nimenona lakini ni mimba nimebeba na unaona kitu inatembea tu.

Mbele ya mungu ni ukweli alienda kwa mgongo fulani sijui kutoka Uganda.

Nikiwa nimebeba mimba mimi hujihisi mzito na kitu inatembea na pia hutaki kuona mke wako, sasa baada ya miezi minane anasema sasa anachukua mwezi mmoja kisha anazaa.

Tuna watoto watano na sijaongeza kwa sababu nilibeba nikaona hiyo imezidi.

Massawe Japanni cries on air after a domestic violence victim narrated her ordeal

listen to the audio below.

 

PATANISHO: Mke wangu ameavya mimba mbili akiogopa kufutwa kazi na muhindi

Ochieng alituma ujumbe akiomba apatanishwe na mkewe bi Grace, waliyekosana mwaka uliopita mwezi wa kumi na moja.

“Kuna kazi nilisafiri kidogo na wakati nilirudi kuna msichana alikuwa rafiki yangu ambaye tulipata njiani na bahati mbaya mke wangu alikuwa hapo karibu.

Sasa kwenda nyumbani tukagombana kidogo na nilipotoka kwenda nyumbani nilipata ameondoka na kwenda kwa shangazi yake.” Alijieleza Ochieng.

PATANISHO: Nilimpiga mke wangu hadi nikamvunja mkono

Wawili hao walikuwa kwa ndoa ya miaka minne na bado hawajajaliwa watoto.

Ochieng alieleza mbona wawili hao bado hawana watoto na sababu yake iliwashtua wengi.

Amekuwa na tabia ya kuavya mimba kila mara anashika mimba.

Kuna siku alikuja kwa nyumba akanidanganya kuwa alianguka na akaanza kuzoa damu. Kumpeleka hospitalini daktari aliniambia kuwa alikuwa anajaribu kuavya mimba na mtoto akafariki.

Isitoshe kuna siku yeye mwenyewe akiniambia kuwa aliavya mimba eti anaogopa kuwa atafutwa kazi na muhindi aliyemuajiri.

PATANISHO: Sitasema kama namtambua Beryl kama mke wangu

Babangu alipumzika wiki iliyopita na twapaswa kumzika wiki ya tarehe ishirini na tatu na kulingana na wazazi hatuwezi fanya mazishi kama mke wangu hayuko kwa boma.

Wakati tulizungumza alisema atakuja lakini bado hajaja, jana nilimpigia lakini aliruka hayo yote.

Hata hivyo, juhudi zetu za kumfikia bi Grace hazikufua dafu.

PATANISHO: Nahisi kujitia kitanzi kwa sababu ya mume wangu

Patanisho: Mke wangu alipachikwa mimba na mpango wa kando

Bwana Otieno aliyekiri kuwa mkewe bi Betty, alienda nje ya ndoa, alituma ujumbe akiomba apatanishwe. Isitoshe, katika harakati ya mipango ya kando alipachikwa mimba.

PATANISHO: Pastor alimdanganya mke wangu eti alimuombea akapata mimba

“Mke wangu alienda nje ya ndoa na nikagundua kuwa ana mimba ya yule mpenzi wake. Kisa hicho kilinikasirisha na niliondoka na kwenda akiwa miezi kadhaa kabla hajajifungua.” Alieleza Otieno akisema anataka apatanishwe na mkewe huku akidai aligundua kuwa haoni kama atapata mke mwingine kama yeye.

Otieno alifichua kuwa wawili hao waliingia kwa ndoa huku mkewe akiwa na watoto watatu tayari.

Mke wangu alikuja akanidokezea kuwa mkewe alidanganywa na msichana wa kazi aende nje ya ndoa.

Wawili hao wamekuwa kwa ndoa ya miaka mitano.

PATANISHO: Mke wangu nimekuwa mchafu tangu uende

Betty alipo ombwa msamaha alikiri kuwa hana shida kwani yuko tayari kurudiana na mumewe.

“Ni sawa sina shida wacha nishughulike mambo na watoto shule tutaongea.” Alisema Betty akiongeza, Sina shida naye tumesameheana.”

Cha kushangaza ni kuwa Betty alisema kuwa mimba ni ya Otieno na kuwa aliyemdanganya mimba sio yake ni kama alikuwa na nia ya kumuoa. Swala hilo lilimfurahisha mumewe Otieno.

Pata uhondo kamili.

PATANISHO: Mume wangu alinitenga baada ya kukataa kuavya mimba

Anne Jepkorir alituma ujumbe akiomba apatanishwe na mumewe akidai kuwa ana watoto wawili na kuwa anapanga kuwapeana baada ya maisha kuwa mazito.

Mara ya mwisho kuzungumza naye alisema anaenda Nairobi lakini hakuwa huko na nikimpigia hakuwa anashika simu. Alisema Anne

Tuna watoto wawili, baada ya kupata mtoto mmoja nikashika mimba ya pili baada tu ya miezi mitano.

Nikama hakuwa anatarajia kwani kuna siku alikuwa anadai nitoe mimba na nikakataa.

Hapo alikasirika na kunieleza kuwa sifai kumhesabu ndani ya maisha yake, hapo nikamnyamazia na nikaondoka. Baada ya kurudi miezi tisa baadaye alianza kulia alipomuona mtoto kwani aliamini ni wake na akapata machungu kuwa karibu aue mwanawe.” Alieleza Anne.

Bwanake alikatisha mawasiliano nasi pindi tu aliposkia sauti ya mkewe.

Pata uhondo kamili.

Familia Yalilia Haki Baada Ya Binti Yao Kubakwa Na Kupewa Mimba Na Baba Wa Kambo

Familia moja kutoka eneo bunge la Tongaren kaunti ya Bungoma inalilia haki baada ya mwanao wa miaka kumi na minne kubakwa na kupachikwa mimba na babake wa kambo.

Vincent Wanyonyi ambaye ni mwalimu mkuu wa shule ya upili ya Mwibale anadaiwa kumtendea unyama huo bintiye wa kambo mwaka jana mwezi wa Oktoba aliporejea nyumbani kutoka shuleni ili kupokea matibabu baada ya kuwa mgonjwa.

Msichana huyo aliyekuja na mamake kwa ndoa hiyo pindi tu mamake alipooleka kama bibi wa pili kwa Wanyonyi, alielezea jinsi babake wa kambo alimlazimisha kufanya ngono naye alipokuwa mgonjwa akiwa amelala kitandani wakati mamaye alikuwa ameenda sokoni.

Kwa sasa mamake na familia hio inataka mwalimu huyo achukuliwe hatua kali za kisheria.

-Brian Ojamaa

#ToboaSiri: Nilinyang’anya Baba Yangu Mke Na Nikampa Mimba

Kila siku ndani ya stesheni ya Radio Jambo waskilizaji zaidi ya milioni kumi hupata fursa murua ya kujieleza, kuburudishwa na cha muhimu kuelemishwa kwa mambo chungu nzima.

#ToboaSiri: Nilinajisiwa Nikiwa Darasa La Pili Na Hakuna Anayejua (AUDIO)

Na katika kipindi cha Mbusii na Lion Tekeke, wanajambo hupata fursa muhimu ya kufungua roho zao na kutoboa siri ambazo wamekuwa wamezificha kwa miaka na mikaka bila hofu ya ubaguzi.

Jamaa mmoja aliwashtua watangazaji Mbusii na Lion pamoja na waskilizaji alipofichua kuwa alimnyang’anya babake mzazi bibi, na isitoshe tayari amempachika mimba.

#ToboaSiri: Ex Wangu Anasema Atajiua Nisipo Muoa

Kulingana na jamaa yule, alimtongoza mamake mdogo baada yake kudai kuwa bwanake hangeweza mtosheleza kitandani.

Pata uhondo kamili.

Soma habari zaidi kama hizi HAPA

Kalameni Ajitoa Uhai Baada Ya Kupachika Dadake Mimba

Kalameni mmoja amehamua kujitoa maisha kwa kujitia kitanzi baada ya kumpachika dadake wa kambo mimba katika kijiji cha Minyenya, kata ya Kamwango Kaskazini katika kaunti ndogo ya Rongo.

Kennedy Odhiambo wa miaka 21 ambaye anafanya kazi za sulubu katika mashamba ya miwa katika kijiji chao alihasi kuoa na kuanza mapenzi na dadake huyo ambaye ni mwanafunzi wa miaka 12 na wa darasa la tano.

PATANISHO: Bwanangu Alitaka Nizae Kila Mwaka Akiona Majirani Wana Mimba

Odhiambo alikatazwa na wazee kuhusu mapenzi hayo pamoja na tabia ya kuwamezea mate watoto wa shule.

Kulingana na chifu wa eneo hilo, Okech Boi familia yake ilikataa kumchukulia hatua za kisheria ikitaka kusuluhisha kifamilia kabla ya maji kuzidi unga.

Boi alisema babake msichana huyo Joel Omare ambaye ni ndugu wa toka nitoke wa babake mwenda zake alikwenda kwa mwenda zake na kuharibu mali za nyumbani huku akiapa kuchoma Nyumba yake.

PATANISHO: Bwanangu Alipachika Mwanadada Mimba Kisha Akaniita Tasa

Mkuu wa polisi katika eneo la Rongo, Jonathan Kisaka alisema kalameni huyu alionelea kujitia kitanzi kuhepa aibu kwa kitendo chake.

Kisaka ameomba Wakenya kutojihusisha kimapenzi na watu wa karibu wa kifamilia akisema huo ni utovu wa kimila.

Mwiili wa mwenda zake umehifadhiwa katika chumba cha maiti cha hospitali ya Rosewood mjini Rongo ukingoja upasuaji wa kimaabara na uchunguzi zaidi.

-Manuel Odeny

PATANISHO: Bwanangu Alipachika Mwanadada Mimba Kisha Akaniita Tasa

Douglas alituma ujumbe akiomba apatanishwe na mkewe bi Lilian ambaye pamoja waliishi kwa miaka mitano bila kubarikiwa na mtoto.

Wawili hawa walikosana mwezi wa Agosti mwaka uliopita na kutengana.

“Nimezaliwa pekee yangu katika familia yetu na sasa kuna pressure nyingi kutoka kwa nyumba yetu na mke wangu alikataa kunizalia.” Alielezea Douglas.

Sasa nikapata mwanadada mwingine na nikampachika mimba kwani nilikuwa najaribu kama mimi ndiye niliyekuwa na shida ya uzazi na hapo nikampachika mimba. Nimekubali nilimkosea sana.”

Alipopigiwa simu bi Lilian, alikiri kuwa mwanadada huyo aliyepachikwa mimba ndiye bibiye na anaishi mashambani.

“Alimpea mwanamke huyo simu akanitusi mara kadhaa kwani alipompachika mimba alianza kuniita tasa na hapo nikaamua niondoke nimngoje mungu kwani sikutaka chuki.” Aieleza Lilian.

Nilienda hospitali na nikapimwa lakini nikakosa fedha za uchunguzi zaidi lakini naye Douglas alikuwa anasukumwa sana na mamake na hapo nikaamua nijiondoe. Labda wakati wangu haujafika siwezi harakisha mambo kwani mungu ndiye anayejua mipango yake.” Aliongeza huku akikataa katakata kurudiana na aliyekuwa mumewe kwani hataki kudharauliwa na mama mkwe.

Pata uhondo kamili.

 

AUDIO: Kasisi Azuiliwa Na Polisi Baada Ya Kunajisi Na Kupachika Wanafunzi Wawili Mimba

Kasisi mmoja anazuiliwa katika kituo cha polisi cha Voi kwa tuhuma za kuwanajinsi na kuwatunga mimba wanafunzi wawili wa shule moja ya upili wenye umri wa miaka 16 huko Voi kaunti ya Taita Taveta.

Mlinzi Wa Kanisa Auwawa Huku Kasisi Akinusurika Kifo

 Kwa mujibu wa kamanda wa polisi kaunti ya Taita Taveta, kasisi huyo kutoka Wongonyi eneo la Tausa anadaiwa kuwanajisi wanafunzi hao tangu mwaka jana.

Makasisi wapinga ndoa za jinsia moja

Polisi wameomba mahakama siku tatu kufanya uchunguzi kabla mshukiwa kujibu mashtaka.

Skiza kanda ifuatayo

Mwalimu Adaiwa Kumbaka Mwanafunzi Na Kumpachika Mimba

Mwalimu mmoja katika shule ya msingi ya Nyikendo kwenye kaunti ya Migori anadaiwa kumbaka mwanafunzi wa miaka kumi na sita wa darasa la nane na kumpachika mimba.

Kulingana na babake mwanafunzi huyo Peterlis Omutu, mwalimu huyo anadaiwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanafunzi huyo wa darasa la nane kuanzia mwishoni mwa mwaka jana.

Mzazi huyo anataka haki kutendeka na mwalimu huyo kuchukuliwa hatua za kisheria kwa kumpachika mimba na kumbaka kinyume cha sheria.

Mwanafunzi huyo pia alikiri kuwa mwalimu huyo amekuwa akimchukua kutoka kwao nyumbani na kumpeleka mjini Migori katika vyumba vya burudani ambako wawili hao wamekuwa wakifanya mapenzi.

Juhudi za kutafuta majibu kutoka kwa mwalimu mkuu wa shule hiyo hazikufua dafu baada yake kuwa kwenye mkutano na wasimamizi wa shule hiyo na kusema kuwa bado anafanya uchunguzi kuhusu kisa hicho na kuwa hangezungumzia swala hilo hadi uchunguzi huo kukamilika.