PATANISHO: Mke wangu nimekuwa mchafu tangu uende

Bwana Ng’etich alituma ujumbe akiomba apatanishwe na mkewe Faith Jepkorir ambaye walikosana mwaka uliopita mwezi wa Oktoba kwa kile hakujua ni kipi.

Alisema kuwa aliondoka kwao Kericho na kuja Nairobi kufanya kazi na baada ya mwezi mmoja, alipata mkewe ameondoka bila kufahamishwa.

PATANISHO: Niliogopa kuwa mume wangu anaweza niua

 

Tulikosana na mke wangu Oktoba mwaka uliopita. Tulikuwa tunaishi Kericho na nikaenda Nairobi kikazi kwa mda wa mwezi mmoja, tulikuwa tumekosana kidogo na kurudi nyumbani sikumpata.

Hakunielezea sababu ya kuondoka, nilijaribu kumpigia simu lakini alikuwa amezima simu kwa miezi mitatu. Alinipigia simu juzi akaniambia anahitaji picha ya mtoto na nikamtumia lakini hataki turudiane.

Chanzo chao kukosana kilikuwa kipi?

Kuna siku alikuwa mgonjwa na akaniambia nimpeleka hospitalini lakini huo wakati mdosi alikuwa amenipigia simu sasa nikamwambia aende pekee yake ili niende kazini. Hapo aliona nikama sina haja naye na hapo akakasirika licha ya kuwa ilikuwa mara moja pekee.

Wawili hao wamejaliwa mtoto mmoja katika ndoa yao ya miaka mitatu.

PATANISHO: Bibi yangu anatetea mpango wake wa kando

Bi Faith Jepkorir shabiki sugu wa patanisho alisema kuwa wanadada wana shida kama alichopitia ni kwa ajili ya mapenzi.

Bibi yangu mimi naendanga kazi nyumba inabaki tu hivyo, nimekuwa mchafu tangu uende. Alijitetea bwana Ng’etich.

Chenye nilifanya nitoke kwako ni kuwa mimi nilikuwa mja mzito na nilitoka kwako kwani niliona huna uwezo wa kutunza mwanamke mja mzito ulikuwa unanipa stress. Alisema Faith.

Pata uhondo kamili.

 

 

PATANISHO: Niligundua Kuwa Mke Wangu Aliingia Kwa Ndoa Akiwa Mja Mzito

Alex alituma ujumbe akiomba ndoa yake ya miaka minne iokolewe kwani inasambaratika.

PATANISHO: Mke Wangu Hupotelea Kwa Kichaka Kila Ninapoenda Kwao

“Tulikosana na mke wangu mwezi wa Novemba mwaka uliopita. Shida ilitokea wakati tulianza kukorofishana na nyanyake.

Nilimuoa mke wangu na mtoto mmoja kisha nikaja kugundua kuwa aliingia kwa ndoa akiwa na mimba. Nikakubali na nikamweleza kuwa nitamshughulikia mtoto.

Mtoto mmoja aliwachwa kule mashambani na hapo nyanya yangu alianza kutumia fursa ile kama biashara akidai kuwa nafaa kumtumia kama shilingi elfu moja mia tano kila wiki.

PATANISHO: Bibi Yangu Alininyima Tendo La Ndoa Akidai Amerogwa

Nilipokasirika nyanyangu akanitishia kuwa atampeleka mke wangu kwa wanaume wataomshughulikia.” Alielezea Alex.

Alipopigiwa simu bi Helen alidai kuwa hataki maneno yake kwani shemeji wake walimfanyia mambo makubwa.

Mojawapo ya mambo hayo ni kugombana na nyanyake Alex na pia kupigwa na bwanake.

Pata uhondo kamili.