PATANISHO: Bibi yangu anatetea mpango wake wa kando

Paul aliomba apatanishwe na mkewe bi Elizabeth akidai kuwa wawili hao walikosana baada yake kumpiga mpango wa kando.

PATANISHO: Bwanangu alikatwa kichwa na mpango wa kando na bado akamrudia

Akieleza kisa hicho, bwana Paul alidai kuwa wawili hao walikuwa wametengana kwa mda na kila mmoja akaanza uhusiano wa kando na baada yao kurudiana, aliyekuwa mpango wa kando wa mkewe hakusita kumfuata.

Jambo hilo lilimkera haswa baada yake kumtumia picha za mkewe kwa mtandao wa Whatsapp na alipopatana naye alimpa kichapo cha mbwa, jambo ambalo halikumfurahisha mkewe.

Kwa hasira na kero kuu, Paul alimfukuza Elizabeth.

Soma usimulizi wake.

PATANISHO: Nilienda Kuwatch mpira kurudi nyumbani bibi amenuna hadi leo haongei

 

Tulikuwa tumekosana hapo mbeleni na tuka separate kidogo. Katika hali ya ku separate akapatana na mtu mwingine halafu tukaja tukarudiana. Baada ya kuishi naye yule jamaa bado alimfuata na baada ya kuzungumza na mke wangu tukamaliza hayo maneno, na nikampigia yule jamaa na nikamkanya.

Sasa hakuacha na akaendelea kumfuata na ikafika mahali akaanza kutuma picha za bibi yangu kwa Whatsapp na hiyo kitu iliniuma sana.

Nikamwambia bibi yangu anipatanishe na yule jamaa, tukazungumza na nikakasirika zaidi nikampiga yule mwanaume na bibi yangu nikama lile jambo halikumfurahisha na akaanza kumteta yule mwanaume na kwa machungu ikabidi nimfukuze mke wangu. Aliondoka na kwenda kwao nyumbani na hawazungumzi na yule jamaa.

Wawili hao wana watoto wawili mmoja alimuoa naye na wamekuwa kwa uhusiano wa miaka minane.

Bi Elizabeth naye alidai kuwa Paul alimtumia fedha za kununua sare za shule lakini pindi tu zilipofika akazirudisha. Alisisitiza mumewe ana madharau sana na hadai kurudiana naye.

Hata hivyo alimuomba ashughulikie watoto huku akimpa mda.

Patanisho: Nililala kwa sitting room baada ya mke wangu kugeuka kwa kitanda akaface upside down

Pata uhondo wote.

PATANISHO: Bwanangu alikatwa kichwa na mpango wa kando na bado akamrudia

Bwana Charles, aliyewachwa na mkewe takriban miaka miwili iliyopita kwa kuwa na uhusiano wa kando na mke wa mwenyewe, alituma ujumbe akiomba apatanishwe.

Isitoshe, alifichua kuwa alikuwa kwa uhusiano na mwanamke mwingine kwa mda wa miaka mitano bila mkewe kufahamu, na cha kushangaza ni kuwa wawili hao wamejaliwa mtoto mmoja.

Soma usimulizi wake.

PATANISHO: Nilienda Kuwatch mpira kurudi nyumbani bibi amenuna hadi leo haongei

 

Bwana Gidi, ilikuwa wakati mmoja nikawa na mpango wangu wa kando takriban miaka mitano ivi na tulikuwa pamoja kwa miaka miwili kabla mke wangu kujua. Na alipojua, mimi na yule mpango wa kando tulikuwa tushafanikiwa na mtoto.

Mke wangu alipojua alikasirika lakini nikamuongelesha na akatulia kidogo nami nikaenda kazi nje. Nikiwa kule aliposikia bado naendelea na huyu mpango wa kando, akafunganya virago na kwenda kwao nyumbani. Sasa imetimia miaka miwili tangia aondoke na hajawahi rudi.

Charles alidai kuwa mkewe Salome, ambaye pamoja wamejaliwa watoto wanne wamekuwa wakizungumza lakini hataki kumrudia licha yake kushughulikia watoto wake.

Wawili hao walikuwa kwa ndoa ya miaka tisa.

Patanisho: Nililala kwa sitting room baada ya mke wangu kugeuka kwa kitanda akaface upside down

Hakuna kitu naweza kukusamehea, hakuna kurudi! Sirudi na sirudi. Bi Salome alisema pindi tu aliposkia sauti ya aliyekuwa mumewe.

“Alinitesa sana alinitesa hadi nikifikiria bado nina hasira, alinitesa sana hadi nina ma alama za kunipiga. Nimevumilia sana kwanzia 2013 mpaka wa leo, nilikuwa hata karibu kujiua na watoto lakini nikasema wacha tu nitoke huko kuliko kujiua.” Alieleza Salome akidai kuwa Charles alikuwa hadi na tabia ya kumpiga mamake mzazi.

PATANISHO: Gidi ambia huyo mwanaume tupatane 2021 simtaki sahii

Pata uhondo kamili.

 

 

 

PATANISHO: Jirani yangu aliniseti kwa bibi nina mpango wa kando

Douglass alituma ujumbe akiomba apatanishwe na mkewe Irene.

PATANISHO: Mke wangu huleta wanaume nikiondoka

“Sasa Ghost nilikuwa naishi Kisii na bibi yangu, sasa kuna dem mwingine nilikuwa naye wa kando ambaye alikuja kuniona kwa jirani yangu. Tukaingia kwa nyumba na huyu mwenye nyumba ambaye ni rafiki yangu akapigia bibi yangu simu na kumwambia nina msichana kwa nyumba.” Alifichua Douglass.

Mke wangu akatufumania tukiwa tunatoka na tangia siku hiyo mke wangu hajawahi niongelesha, tangia mwezi wa saba mwaka huu. Nikimpigia simu anakataa kuniongelesha akidai hanitaki kamwe.” Aliongeza akisema kuwa aliyemuuza ni mzee wa miaka hamsini.

Mkewe alienda kwao na kubeba mwanao.

PATANISHO: Bibi yangu alinishika na mpango wa Kando

 

Aliniletea msichana hadi kwa jirani yangu alipo omba room. Mimi nilikuwa nampigia simu nikiwa nimesimama nje na nikaona pikipiki ikipita na nikamuona na msichana mwingine.

Sasa nilienda huko na nikaingia walimokuwa. Douglass alinitusi na nikamuacha na nikamwambia ‘I just came to witness.’ Alisema bi Irene akisisitiza aliondoka bila hata kumtusi mumewe.

Mimi naweza tu kusamehe mwendelee na huyo msichana wala sio eti turudiane, madharau ulinionesha mimi sijawahi ona hii dunia tafuta tu mwingine lakini sio mimi. Alisema Irene.

PATANISHO: Bibi yangu alinishika na mpango wa Kando

Bwana Mwadime alituma ujumbe akiomba apatanishwe na mkewe akidai mkewe ameondoka nyumbani kwa mda wa wiki mbili baada ya kumpata na mpango wa kando.

“Aliskia tu nikiongea na simu na after nimeingia kwa nyumba nikaacha simu kwa meza, nikatoka nje akachukua number akapiga ingawa yeye hakushika. Sasa tukagombana kiasi , nikamwambia kama ni kwenda siwezi kuruhusu kwenda usiku sasa nikamwambia alale kama ni kuondoka ataenda asubuhi.

Aliamka akaniwacha nimelala akajipanga na akaenda.” Alieleza akisema kuwa mawasiliano yao hayajakuwa sawa kwani juzi mkewe alimtumia ujumbe akisema anataka kurudi kuchukua vitu vyake.

Wawili hao wamekuwa kwa ndoa ya miaka minne huku mpango wa kando wamekuwa pamoja kwa miezi minane.

Alipopigiwa simu mama Agnes alisema kuwa mumewe alikuwa anazungumza na wanawake wengine wakiwa kitandani pamoja.

“Nikamuuliza na aka kana, nikamwambia number ndio hii imepigwa alipopigiwa nikashika na yule mwanamke aliposikia sauti yangu akakata simu. Kumuuliza nani huyo akakasirika na akataka kunipiga, hiyo number nikachukua na nikaweka kwa simu yangu lakini nikimpigia yule mwanadada hukata simu akiskia sauti langu.” Alieleza.

Sikiza uhondo kamili.

PATANISHO: Bibi yangu alinifumania na mpango wa kando

Bwana Samuel alituma ujumbe akisema kuwa mkewe bi Milkah, alimfumania akiwa na mpango wa kando na akaondoka.

“Alienda mwezi wa nane na nikajaribu kuongea na wazazi nikaomba msamaha na akarudi, lakini uaminifu au amani kwa nyumba haijarudi kwa sababu ya nilichotenda.” Alisema akiongeza, Naona kila wakati hatuelewani nikiongea kitu inakuwa ngumu kuniskiza.”

Mimi nilifika mahali ujanja wangu ukajulikana na sikuwa na lingine ila kukubali hata kwa wazazi na kwake na akarudi lakini kurudi kwake bado haniamini nimebadilika.

Sometimes tunazungumza vizuri lakini inafika mahali anasema bado anakumbuka nililofanya. mke wangu sijui ni nini lakini kila wakati najaribu kuwa na mpango wa kando huwa simalizi wiki moja.

Hii ya mwisho nilikuwa naongea na delete message lakini nikama alikuwa ame record hata sahii nikama ana record. Sasa siku moja akaniwekea volume kumbe ame record kila kitu.

Samuel ana umri wa miaka 28 na mkewe ana mika 23 na wawili hao wamekuwa kwa ndoa ya miaka mitano.

Ni mhanyaji wa siri na bado anapatikana, nampata tu hata kama yeye ni muongo hakuna siku nitakosa kumpata hata awe wa wapi.” Alisema bi Milkah.

Unamuuliza tu maswali kumbe napeleleza.

Mume wangu huhubiri kanisani na siku moja akasema naomba mke wangu na Metrine waje hapa mbele waimbe wimbo wa sadaka kumbe alikuwa anatuita atulinganishe.” Aliongeza Milkah.

Pata uhondo kamili.

‘Kitandani Mwanaume Akikwambia Ugeuke, geuka!,’ Serial Mpango Wa Kando Advises Wives

On Tuesday, Annita Raey probably had one of the best moments on radio while interacting with her fans.

This happened when she received a very interesting call from a lady who identified herself as Kate, who chose to openly speak about her role as a serial ‘mpango wa kando.’

Kate chimed in on the day’s hot conversation which revolved around infidelity and mpango wa kando and she literally left Annita rolling on the floor with laughter, thanks to her charisma and hilarious comments.

Annita saw an opportunity to milk all the necessary information about why mpango wa kando do what they do and she surely succeeded in that. Smart lady!

Kate started out by confessing that she is a proud mpango wa kando who has stuck by the same guy for three years, all for one reason – financial gains.

Read her confession below.

“Wacha nikuambie kitu moja. Mimi sijaoleka bado lakini nina mtu ambaye tumekuwa naye kwa miaka mitatu na huyu mwanaume hulalamikia mke wake kila siku. Husema mara mke wake sio mtamu, ana uchafu, hampokei vizuri na kila wakati wakilala naye hudhani amefariki.

Hawezi kumuacha eti anioe kwani wazazi wake wataleta maneno na isitoshe sikuhizi mapenzi ni pesa. Tunasema pesa kwanza mapenzi baadaye, pesa ikiisha mapenzi inaisha naye.” Said Kate.

Mwanaume muweke vizuri, mbembeleze kwanza akiwa na pesa usimuache hata akikwambia umuoshe mguu muoshe, mfanyie kila kitu anakumambia. Mkifika kwa kitanda akikuambia geuka hivi wewe geuka kwani unajua chenye unatafuta. She added.

PATANISHO: Bwanangu Alichukua Simu Yangu Na Kumpa Mpango Wa Kando

Mama Chantelle akiomba apatanishwe na baba Chantelle.

“Hapo nyuma tulikuwa tunakosana na mume wangu kwani alikuwa anatoka nyumbani, anarudi saa sita ya usiku na nikimuuliza ananichapa na nina mtoto mdogo wa mwaka mmoja unusu.

Kuna mwanadada mmoja ambaye alikuwa anampigia saa sita za usiku, anajifunga taulo na kwenda kuongelea nje ya nyumba. Nikimuuliza ananipa na nikimuuliza hiyo ni vita. Alikuwa ananitandika na kunitolea vitu vyangu nje ya nyumba huku akidai yule mwanadada ana haki ya kumpigia simu.

Kitu kingine watu wao hawanipendi hata, isitoshe simu ambaye alikuwa ameninunulia alimpelekea yule mwanadada. “ alijua Mama Chantelle ambaye aliongeza kuwa bwanake hakuwa anashughulikia familia yake.

Kumpigia simu siku fulani akanieleza kuwa ameoa mke mwingine baada ya kuondoka kwake jambo ambalo lilisisitizwa na watu wake wakidai kuwa nijipange.” Aliongeza.

Juhudi za kumpata Baba Chantelle hazikufua dafu.

Pata uhondo kamili.

 

‘Mwanamke ukizeeka ondokea slay queen! ‘ Says mpango wa kando

We are living in an age where things which used to be considered barbaric or uncultured are now the new norm and one would be considered stupid not to follow the very things today.

One of those things are acts of prostitution, adultery, abortion among others.

It seems like even after Radio Jambo presenter, Annitah Raey went off air for a while, her loyal and crazy fans were eagerly waiting for her return to dish out some more juicy secrets.

One loyal listener left the mid-morning presenter in stitches when she narrated how she has been able to specialize living as a mpango wa kando and how she has managed to convince someone’s husband to ditch his wife for her.

‘Kitandani Mwanaume Akikwambia Ugeuke, geuka!,’ Serial Mpango Wa Kando Advises Wives

Read her confession below,

Mimi kuoleka? Mimi bado nina sponsor. Kwanza sahii ndio nataka kumuoa kirasmi kwa ajili bibi alienda. Unajua niliamua kumpima akili nione kama ananipenda, nikamwambia huyu bibi si umfukuze tubaki mimi na wewe.

Na yeye akatumia hiyo akili kumfukuza na watoto pia na sahii ni mimi tu na yeye. Time yake imeisha, ukizeeka unawachia wale wengine kwa sababu umezaa watoto na umechapa, wachia sisi. Mimi bado nakula life kama wazimu. She confessed.

To make things tricky, she revealed that the man left his wife for her but he doesn’t know that his lover is also seeing a mheshimiwa somewhere.

Listen to her confession below.

PATANISHO: Mke Wangu Aliondoka Alipogundua Nina Mpango Wa Kando

Felix alituma ujumbe akiomba apatanishwe huku akidai mkewe aliondoka baada ya kugundua kuwa ana mpango wa kando.

‘Bibi yangu Cate nilimuoa akiwa na watoto na tumevumiliana na sasa watoto wamekuwa wakubwa. Mimi ni mpishi na siku moja katika hali ya kuchokora simu yangu aligundua kuwa kuna wanadada nimekuwa nikizungumza nao.

Sasa akapata msichana fulani ambaye tulijuliana Facebook na ilifika wakati nikama tulikuwa tunatongozana. Sasa mke wangu akakasirika na akaondoka na hadi wa leo hajawahi rudi na hajibu simu zangu.” Alieleza Felix.

Alipopigiwa simu bi Cate, alidai mumewe alimtishia akidai kuwa ataharibu watoto wake.

 

PATANISHO: Mke wangu alinitenga alipogundua natongoza mwanafunzi

Bwana Mark alituma ujumbe akiomba apatanishwe na mkewe mama Pesh akidai hana amani.

“Kuna wakati tulikuwa tunaishi maeneo ya Kitale na kuna wakati alinipata na msichana tukiwa tunatembea naye, mwanafunzi jirani na hapo alikasirika.

Nilikuwa namtongoza lakini hatukuwa tumefanya lolote naye.” Alikiri bwana Mark.

Bwana Mark ana miaka 25 huku mkewe akiwa na miaka 22 na wawili hao wana watoto wawili.

Alipopigiwa simu mama Pesh alidai kuwa walikosania mambo kidogo kidogo ya nyumba na ilifika mahali akachoka.

Alikuwa akinipiga sana na bado akaanza mipango ya kando kinyume na chenye nilikuwa nimemfanyia kwani nilikuwa nampenda kama mume wangu.” Alieleza Pesh.

Niliwapata na huyo msichana wakiwa wanazungumza na huyo msichana alikuwa na sifa mbaya na isitoshe alikuwa rafiki yangu. Isitoshe yule Rozie alidai kuwa hamuachi mume wangu na hapo nikaamua kujipa shughuli.” Alifichua Pesh.

Pata uhondo kamili.