Angalau vijana 200 wajawazito wapatwa na virusi vya ukimwi Murang’a

Kulingana na mtendaji mkuu wa afya Joseph Mbai,  angalau vijana 200 wajawazito katika kaunti ya Murang’a wamepatikana na virusi vya ukimwi.

Katika data iliyochukuliwa katika hospitali kuu ya Murang’a level 5, vijana 4,000 wamo wajawazito katika umri wao mdogo.

5b23a5a6ac0563167cb02c67

Pia kulingana na Mbai nambari ilirekodiwa kwa wasichana waliona na virusi vya ukimwi iko juu kuliko hali ya kawaida. Murang’a ina watu 16,000 wanaoishi na virusi vya ukimwi huku 4000 wakiwa ni vijana wa jinsia zote mbili.

Kaunti ya Murang’a imeanzisha kampeni ya kuwapima vijana virusi hivyo na hata kuwashauri endapo watapatikana na virusi hivyo.

“Mpango huu utatusaidia kupata data za ndani ambazo zinawakilisha hali sahihi katika upimaji wa virusi hivyo.” Alizungumza Mbai.

Pregnant 16-year old girl from a village in Baringo North sub-county spotted in Kabarnet town, Baringo County on Thursday. /JOSEPH KANGOGO

Vijana watakaopatikana na virusi hivyo watawekwa katika ratiba ya matibabu huku wakipewa dawa za ukimwi (ARV’s) ili kuzuia mtoto kuambukizwa.

Mazuri yaja! Peter Kenneth akutana na wanasiasa kutoka Murangá

Wanasiasa kutoka Murang’a wamefanya mkutano na mbunge wa zamani wa Gatanga Peter Kenneth katika hatua inayoonekana kama ya kumweka katika kapu la upande wa rais Uhuru Kenyatta baada ya mgombeaji huyo wa zamani kukutana na kiongozi wa ANC  Musalia Mudavadi anayedaiwa kutafuta ushirikiano na naibu wa rais William Ruto kwa uchaguzi mkuu wa 2022.

Mashakani: Mahakama yakataa kuzuia hoja ya kumuondoa Ngilu afisini

Seneta Irungu Kang’ata,  mbunge wa Maragua Mary Wamaua, Wangari Mwaniki wa Kigumo  na mbunge wa Gatanga  Nduati Ngugi  walikutana na PK katika hoteli ya   Greens huko Thika.

Wakati wa mkutano huo wa saa tatu waliahidi kushirikiana na Kenneth kuendeleza ajenda ya rais na kuliunganisha eneo la Mlima Kenya kabla ya uchaguzi mkuu ujao.

Kasuku nje ndani kimya: Sudi, Wako hakusema neno hata moja bungeni mwaka wa 2019 – Mzalendo

Kenneth amekuwa akipigiwa upato kwa uwezekano wa kujiunga na baraza la mawaziri na hata kutajwa kuwa miongoni mwa wanoweza kumrithi rais Uhuru Kenyatta katika eneo la Mlima Kenya.

Wiki jana, Kenneth alikuwa katika mkutano mwingine uliowaleta pamoja spika wa bunge  Justin Muturi,  waziri wa kilimo  Peter Munya,  magavana  Kiraitu Murungi (Meru), Ndiritu Muriithi (Laikipia),  na kiongozi wa wengi bungeni  Amos Kimunya  katika dhifa ya chakula cha mchana kwenye hoteli ya Panafric Hotel, Nairobi.

Magavana  Lee Kinyajui (Nakuru), Muthomi Njuki (Tharaka-Nithi)  na seneta wa  Kirinyaga Charles Kibiru pia walikuwepo katika mkutano huo.

Kenneth anatayarishwa  kuwa mgombea mwenza au kwa nafasi ya ngazi ya juu  serikalini katika  muundo mpya wa utawala wa kisiasa utakaoundwa  endapo mapendekezo ya BBI yatapitishwa.

 

 

 

 

Hofu Murang’a huku mwili wa mwathiriwa wa virusi vya corona ukizikwa usiku

Hatua ya kuzika mwathiriwa wa virusi vya corona usiku kaunti ya Murang’a imeibua hisia mseto miongoni mwa wananchi huku visa vya maambukizi katika jimbo hilo vikiendelea kuripotiwa .

Tahadhari kwa wakaazi wa Lamu! KWS yasema huenda Mamba na Kiboko wakavamia makaazi yao kutokana na mvua kubwa

Baada ya mwili wa mwendazake kuondolewa katika hifadhi ya maiti ya hiospitali ya Thika,familia ya jamaa huyo ilitarajia kuwa huenda angezikwa 3 jioni japo ratiba hiyo ikabadilishwa .

Body-buried-at-Night

mwili uliwasilishwa usiku ukiwa na maafisa wa afya ambao waliendesha shughuli hiyo haraka wakiwa wamevalia magwanda ya kuwakinga dhidi ya maambukizi.

78352776_3039714856123416_8652800509347889152_o

Mzozo wa shamba,jamaa amuuwa mamake kutokana na ugomvi wa shamba

Aidha waziri wa afya kaunti ya Murang’a ameshutumu vikali uongzi wa hospitali ya Thika kwa kutuma ujumbe wakiwa wamechele kuwa mwathiriwa huyo alifariki kutokana na virusi hivyo hatari.

 

Sabina Chege atoa msaada wa chakula kwa makahaba

Mwakilishi wa wanawake kaunti ya Murang’a Sabina Chege amewapa msaada wa chakula zaidi ya makahaba 100 na kuwafanya wafurahie sana.

Kupitia ukurasa wa Facebook, Chege alisema makahaba hao walimuelezea kuwa janga la virusi vya corona limeathiri sana biashara yao na hata kufanya wakose chakula.

Sabina chege 5

“Kundi kadhaa la wanawake wanaofanya biashara ya ngono kupitia kwa mwenyekiti wao waliniomba msaada wa chakula wakidai hali ngumu ya maisha na kwamba janga la corona limeathiri biashara yao.” Aliongea Sabina.

Chege alisema chakula hicho kitawatosheleza makahaba hao kwa muda wa juma moja na ataendelea kuwasaidia hadi hali iwe nzuri. Ni virusi ambavyo vimeathiri uchumi wa nchi hasa kwa wafanyabiashara wa hali ya chini.

” Tumeafikiana na makahaba hao kuwa tutatafuta suluhu la kudumu ambalo litawasaidia hao kupata chakula kwa urais na kuahidi kuasi biashara hiyo na kufanya biashara nyingine kama ya saluni na ya kushona nguo.” Aliongea Sabina Chege.

Swali ambalo linazidi kugonga vichwani mwa wananchi ni je, hali ya kawaida itarudi lini na mambo yatakuwa sawa lini licha ya janga la corona na nchi kurekodi visa vipya kila siku.

Madhara ya pombe! Msamaria mwema ajitokeza kuwasaidia jamaa wanaokunywa vitakasa mikono

Baada ya taarifa kushamiri katika mitandao ya kijamii kuhusiana na jamaa watano ambao wamekuwa wakinywa vitakasa mikono almaarufu kama hand sanitizers eneo la Mathioya kaunti ya Murang’a, msamaria mwema kwa jina Stanley Kamau wa shirika la Ahdai Kenya amejitokeza na kusema atawasaidi jamaa hao.

Image

Kamau amesema atatumia hela zake kuwapeleka jamaa hao walioathirika na unywaji wa pombe katika kituo cha kubadili tabia yaani Rehab ili wapewe ushauri nasaha.

Hivi sasa!China yafadhili mradi wa kujenga kituo cha kukabili corona- Xi Jinping asema

Kutokana na hatua ya serikali kuongeze vigezo kwa wamiliki wa mikahawa na hata vilabu, halaiki ya watu waliokuwa na mazoea ya kunya vileo wamejipata katika njia panda kwani asilimia kubwa ya maeneo hayo yangali mahame na hayajafunguliwa.

Aidha masharti ya kuonya watu kutangamana katika eneo moja zaidi ya watu 15 imechangia watu wengi waliokuwa wamezoea kunya pombe kuwa katika njia panda kwani maagizo hayo yamekuwa magumu kwa asilimia kubwa ya vilabu nchini kuyatimiza.

 

 

Vichwa Maji! Watu 9 waliohepa Nairobi kupitia njia za mkato wanaswa

Watu tisa waliofaulu kuondoka katika eneo la Nairobi na viunga vyake ambalo limefungwa wamekamatwa katika kaunti ya Murang’a. Wanaume hao watano, wanawake watatu na mtoto mmoja walikamatwa katika kizuizi siku ya Jumatatu, Mei 11, baada ya kushindwa kutoa stakabadhi za kuwaruhusu kusafiri.

Nairobi

Itakulazimu kufanyiwa vipimo vya Corona kabla ya kulazwa katika kituo cha afya-Wizara ya Afya yasema.

Akithibitisha kukamatwa kwao, OCPD wa Murang’a Mashariki, Alex Muasya, alisema washukiwa walikuwa wameabiri matatu kutoka Kenol, kaunti ya Kiambu na kutumia njia za mkato kuingia Kaunti ya Murang’a.

“Wakati waliwasili katika kizuizi, waliulizwa stakabadhi zao za kusafiri na kuibuka hawana.”Amesema Alex Muasya

Washukiwa sasa wamepelekwa katika makao makuu ya polisi kaunti ya Murang’a kabla ya kuhamishwa hadi kituo cha karantini huku wakisubiri kupelekwa kortini baada ya siku 14.

Makachero wa DCI wamtia mbaroni jamaa wa miaka14 kwa kuhusishwa na mauwaji ya mwanahabari.

Hata hivyo, si mara ya kwanza kwa kisa sawia na hicho kuripotiwa Murang’a, ambayo imeibuka kuongoza katika kukiuka maagizo ya serikali kukabiliana na COVID-19 na pia kutumia mbinu za kiasili kukabili ugonjwa huo.

Madereva 9 ni miongoni mwa wale waliopatikana na corona – Aman

Mnamo Aprili 15, zaidi ya wafanyakazi 52 ambao walikuwa wanasafari katika lori moja walikamatwa eneo la Maragua wakiwa safarini kuelekea shambani. Walipelekwa katika kituo cha polisi cha Maragua kabla ya kuhamishwa hadi katika Shule ya Wavulana ya Chania ambapo waliwekwa karantini kwa siku 14.

Rasmi sasa! Wakaazi wa Murang’a kuanza kuhudumiwa baada ya chumba cha kuangazia Corona kufunguliwa

NA NICKSON TOSI

Ni afueni kwa wakaazi wa kaunti ya Murang’a baada ya uongozi wa jimbo hilo kufungua kituo kilichojengwa kwa siku 21 kuanza kutoa matibabu na hata kuwapima wakaazi wa eneo hilo kuhusiana na virusi hatari vya Corona.

Kituo hicho maalum na ambacho kimewekwa mashine maalum kama vile ICU sasa kitakuwa na wajibu wa kuwapokea wagonjwa kutokwa kaunti jirani za Mkoa wa Kati.

Wakenya 84 warejea nchini kutoka Uingereza kwa gharama yao

Kituo hicho kilifunguliwa baada ya viongozi wa kidini kuombea wote watakaokuwa wanahudumu hapo.

ImageImage

Yawa! We are a poor economy. Total lock down itaangamiza wakenya – Gavana Mutua

ImageImage

Kariobangi North yageuka kuwa mtaa wa wakimbizi-Tazama

Sekta ya afya imekuwa na changamoto kuu kwa serikali za kaunti ambapo baadhi ya wananchi wamekuwa wakilazimika kusafiri hadi jiji kuu la Nairobi kupata tiba.

Kituo hicho sasa kina uwezo wa kuwalaza wagonjwa kutoka kaunti zingine eneo hilo.

21 Days! Kaunti ya Murang’a yajenga eneo la wagonjwa wa virusi vya corona kwa siku 21

NA NICKSON TOSI

Katika baadhi ya kaunti nchini, wakenya wanaendelea kuvuna matunda ya ugatuzi miaka 7 baada ya kuanzishwa. Hii ni baada ya kaunti ya Murang’a kujenge kituo cha kuwahudumia wagonjwa wa virusi vya corona kwa siku 21 na kuweka vitanda takriban 35.

Kaunti hiyo aidha imeweka mashine ya wagonjwa mahututi yaani ICU kama njia ya kujiandaa tu iwapo hali ya maambukizi ya virusi hivyo hatari vitabisha hodi katika kaunti hiyo.

ImageImageImageImageImage

Ujenzi huo sasa unawapa wakaazi wa eneo hilo matumaini ya kupata tiba bora pasi ya kuabiri hadi jijini Nairobi wakitafuta matibabu.

Mtoto wa miezi 6 ni miongoni mwa watu 25 walioambukizwa virusi vya corona nchini

Ni hatua ambayo serikali kuu imekuwa ikiwataka magavana wote nchini kuhahakikisha kuwa wametenga maeneo maalum ya kuwahudumia waathiriwa wa virusi vya Corona .

 Hofu ya  Virusi vya  Corona  yazuia  ulevi Murang’a

Gavana  wa Murang’a  Mwangi wa Iria amefutilia mbali leseni za  wamiliki wa mabaa waliokaidi  agizo la kuyafunga maeneo hayo ya burudani  kama ilivyoagizwa na  kundi la kushughulikia dhrura katika kaunti hiyo .

Covid 19:Kenya yasajili kisa cha 4 cha virusi vya Corona

Siku ya jumatatu  gavana huyo na kamishna wa kaunti Mohamed Barre  walisema  mrundiko wa watu  na hali mbaya ya usafi huenda ikalazimu kufungwa kwa baadhi ya baa .waliwashauri wakaazi kuburudi kwa kwa vinywaji vyao wakiwa nyumbani .

Coronavirus:Kisa kingine charipotiwa Kericho na mwanamme kutengwa

Wawili hao walisema watu walevi hawataweza kujikinga dhidi ya virusi vya corona .Kufikia jumanne gavana wa Iria alisema leseni za baa hio zimefutiliwa mbali baada ya wenyewe kukosa kuafikia mahitaji yaliyotolewa kama mojawapo ya njia za kuzuia kusambaa kwa virusi vya corona .

 

 

Watu watatu kulazwa Murang’a baada ya kupatikana na dalili za kipindupindu

Watu watatu wamelazwa katika hospitali ya Murang’a baada ya kuonyesha dalili za kipindupindu, Afisa mkuu wa afya  Joseph Mbai alisema kuwa watu hao ni msichana wa miaka kumi na wanaume wawili.

Mbai pia alisema watatu hao wanatibiwa katika wadi za kipekee ili wachunguzwe zaidi kama wanaugua kipindupindu.

Jamaa aumia vibaya katika ajali kwenye barabara ya Waiyaki

Aliongeza kusema kuwa wagonjwa hao wamekuwa wakiugua kuendesha na kutabika lwa muda sasa lakini wamo katika hali thabiti.

Mmoja wa wagonjwa ni eneo la mjini slum, mwingine ametoka eneo la Kayole na wa mwisho ni wa kijiji cha Wango mbai alisema.

Joseph pia alisema maafisa wa afya wametumwa katika familia za wagonjwa hao ili kufanyiwa mafusho.

“Tumezuiwa kuingia kwa kaburi la bwanangu..” Mkewe bilionea Reginald Mengi alia

“Tumewakubalisha baadhi ya maafisa wa afya kutembelea maeneo ambayo yameadhiruwa ili kubaini kiini cha ugonjwa huo.” Alisema Mbai.

Aliwasihi na kuwauliza wenyeji wa vijiji hivyo pia waweze kuchemsha maji yao ya kunywa ili kuzuia ugonjwa huo.

Wizara  ya afya pia imesema kuwa itasimamsha uuzaji wa vyakula ambavyo si visafi, na pia kukomesha watu ambao wanaingia katika kaunti hiyo bila ruhusa huku wakiwapigia maafisa wa afya waliokuwa katika likizo simu ili warejee kazini.

Mwaka wa 2015 watu wawili waliaga dunia kwa sababu ya ugonjwa unaotokana na maji katika  kijiji cha Kabati kaunti ndogo ya Kandara.

Mwaka wa 2017 watu zaidi ya watu hamsini kutoka kijiji cha Kiunyu kaunti ndogo ya Gatanga  walilazwa hospitali kwa sababu ya ugonjwa huo.

Serikali ya kaunti hiyo imetoa njia mbalimbali ili kuzuia ugonjwa huo kuenea sana na watu wasiweze kuugua.