‘Nilibeba maiti ya mtoto wangu kwa handbag’ Mwanamke asimulia mateso ya kukosa pesa

Hebu fikiria kuhusu kumpoteza mwanao kisha ukose usaidizi wa kuweza kuisafirisha maiti yake hadi   eneo unalotaka kumzika.Hayo ndio masaibu yaliyomkumba  Ziporah Chiti ambaye aliubeba mwilia wa mtoto wake wa mwaka mmoja kutoka Nairobi hadi Kwale .

Matatizo yake yalianzia  katika hospitali moja hapa Nairobi ambapo mwanawe alikosa kuhudumiwa na madaktari kwa wakati   na kuaga dunia .  kwa sababu alikuwa ametumia pesa nyingi kwa matibabu ya mtoto hakuwa na pesa za kutosha  kutafuta jeneza na kufanikisha usafiri wa mwili wake kutoka jijini hadi Kwale . Chiti alijaribu kutafuta  usaidizi kutoka kwa jamaa na rafiki zake lakini kiasi cha fedha zilizokusanywa hakikutosha kuweza kuusafirisha mwili wa mwanawe .Ni katika hali hiyo alipoamua kwamba liwe liwalo kwani  alipanga kuubeba mwili wa mtoto wake katika mfuko wake wa mkononi kutoka Nairobi hadi kwale .

Gay Husband! Mwanamke agundua mumewe ni mpenzi wa jinsia moja

Aliuchukua mwili  ule hospitalini na kuuweka katika  karatasi na kisha  akaukunja katika  leso na kutumbukiza kwenye begi lake .Hakuna aliyeweza kujua amebeba nini lakini moyoni mwake alihuzunika  sana  kuona kwamba hali ya uchochole ilikuwa ikimlazimu kuusafirisha mwili wa mtoto wake kwa njia ile.

‘Majambazi waliwabaka mamangu na dadazangu nikishuhudia’ Jamaa asimulia

Alifika katika kituo cha mabasi ya kwenda Mombasa mwendo wa saa moja jioni na gari lile  likaondoka .  Akiwa safarini  Chiti alikuwa akibubujikwa machozi abiria wenzake wasijue nini kulikuwa kikimliza na waliotaka kujua zaidi aliwaambia  alikuwa mgonjwa na hivyo basi  maumivu yalikuwa yamemzidi . Begi yake iliyokuwa na mwili wa mtoto wake iliwekwa ndani ya gari katika vyuma vilivyokuwa juu ya kiti chake .Alikumbuka jinsi mlinzi lkwenye mlango wa gari alipomuuliza amebeba nini alimuambia kwamba alikuwa amebeba nguo zake .

Nilihofia kwamba iwapo angeamua kuikagua ile begi basi angeupata mwili wa mtoto  wangu,ingekuwa kesi  kwa sababu hakuna angeyeweza kuamini kwamba nimeshindwa kupata pesa za kuusafirisha mwili huo’ anasema Chiti .

Fungua duka! Aliniacha ‘ocha’ pekee yangu nikaamua kufungua miguu

Alipofika Mombasa , Chiti hakuwa na muda wa kupumzika na safari ya kwenda Kwale ikaanza .Alichukua gari jingine hadi kwale huku jamaa zake wakimgonja kwa maazishi .Hawakujua kwamba  mwili wa mtoto ulikuwa ukisasafrishwa katika  mkoba wa mkoni na wengi walishangaa walipomuona Chiti akiingia bomani bila jeneza wala msafara wa magari . Alipoingia chumbani aliutoa ule mwili ambao sasa ulikuwa umeathiriwa na joto baada ya safari ndefu iliyoanza siku iliyotangulia .  Baada ya maazishi Chiti hakuweza kupata nguvu za kuja Nairobi kwa sababu wiki mbili zilizopita kabla ya mwanawe kuaga dunia zilikuwa ndefu kwake .Kifo cha mtoto wake kwa sababu ya utepetevu wa madaktari pia kilimpa kumbukumbu ambazo alitaka saba kuzifuta akilini mwake .

SUTI ZA MWILI WA MOI :Mwili wa Mzee wavalishwa suti tofauti kila siku unapotazamwa .

Mwili wa marehemu Mzee Daniel Moi  ulivalishwa suti tofauti kila siku ambayo ulipelekwa bungeni kutazamwa na wananchi .

  Siku ya jumatatu ambayo ndio ya mwisho mwili huo kuwekwa katika majengo ya bunge ili kutazamwa na umma , mwili wa Moi ulivalishwa  suti ya rangi ya kijivu (grey) ,viatu vya  rangi ya  kahawia(brown) ,shati jeupe na  tai yenye vistari vya  manjano . Kirungu kidogo cha mzee Moi al maarufu fimbo ya nyayo  kiliwekwa katika mkono wake wa kulia kinyume na siku mbili za awali ambapo kiliwekwa kando yake . Siku ya kwanza ya kuutazama mwili huo jumaosi  ,ulivalishwa  suti ya  rangi ya kijivu  shati jeupe na viatu vya  rangi ya kahawia  na tai yenye maua . Siku ya jumapili iliyokuwa ya pili kwa mwili wake kutazamwa na umma ,alivalishwa  suti nyeusi ,shati jeupe ,tai ya rangi nyekundu na  viatu vyeusi .

 FIMBO YA MZEE MOI YAONEKANA: Rungu ya Hayati Mzee Moi haijaachwa nyuma

 Viongozi ambao tayari wameuona mwili wa Mzee Moi ni pamoja na rais Uhuru Kenyatta ,naibu wake William Ruto ,rais mstaafu  Mwai Kibaki ,mabalozi ,wabunge  na maseneta,magavana na viongozi wa kidini .

MBOCH PIA NI BINADAMU:‘Nilikuwa nikiosha chupi za mwajiri wangu na kutupa ‘pads’ zake’-Mfanyikazi wa nyumbani asimulia masaibu yake .

Rais huyo wa zamani atapewa taadhima zote za kijeshi   wakati wa maazishi yake ikiwemo saluti ya milio 19 ya risasi . Siku ya jumanne misa ya madhehebu mbali mbali itafanyika katika uwanja wa Nyayo Nairobi . Moi atazikwa nyumbani kwake Kabarak siku ya jumatano .

 

MERU: Kichwa cha mwanamke chakatwa kabla ya kutupwa shambani

Mchana wa Jumatano, wananchi wa kijiji cha Nkabune, Meru walishuhudia kifo kingine cha kinyama baada ya mwanamke kukatwa kichwa na kutupwa mita 30 mbali na mwili wake.

Mwanamke ambaye anajulikana kama Justa Mungania, mwenye umri wa miaka 25 na mama wa mtoto wa miaka miwili, alikuwa anaelekea kula chakula cha mchana nyumbani kwa nyanyake.

Uhuru aagiza kusitishwa kwa mikutano ya La Mada

Mwanamke huyo alikuwa anafanya kazi za juakali na nyinginezo katika kituo cha Nkabune na alikuwa anaelekea kumyonyesha mwanawe.

Hata hivyo, hakufika na inakisiwa kuwa aligongwa kutoka nyuma na kifaa kikali.

Wanahabari na polisi walipofika katika eneo hilo, damu yake bado ilikuwa inaonekana katika eneo la tukio hilo na pia kutoka kichwani na mkononi mwake.

Wananchi ambao walifika hapo bado hawaelewi mbona mtu aliye na utu anaweza fanya jambo la kinyama kama hilo huku wengine wakikisia kuwa huenda ilikuwa ni kisa cha mzozo wa mapenzi, huku wengine wakihusisha mauji yale kama njia ya kutoa dhabihu.

Chifu wa eneo hilo, Kaari Muguna alisema kuwa aliambiwa kuhusu mauaji yake mda mchache baada ya saa saba siku ya Jumatano.

Karibu 33!! Grace Msalame asherehekea siku yake ya kuzaliwa

“Nilipokea simu kuwa mwanamke aliuawa na nilipofika katika eneo hilo nikapata mwili bila kichwa. Tulipofuata matone ya damu tukapata kichwa kati shamba lililoko hapo karibu.” Muguna alisema.

Muguna aliwahakikishia wakaazi kuwa ataboresha usalama.

Chifu huyo alisema kuwa kijana wa shule alisema kuwa alimuona mtu akiingia shambani ambapo kichwa cha mwanamke huyo kilipatikana.

-Dennis Dibondo

 

 

Maisha ya raha mstarehe aliyoishi Monica Kimani

Wakenya wamepata jipya la kuangazia kutoka kwenye kesi ya mauaji yake Monica Kimani.

Monica alikuwa mfanyi biashara maarufu hapa nchini. Alipatana na mauti yake nyumbani kwake eneo la Lamuria Gardens. Monica alitambulikana sana kwa maisha yake ya kistaarabu pamoja na kuendesha magari makubwa ya kifahari.

Afisa wa polisi aliyefika eneo hilo mapema, Jennifer Sirwa alitoa picha za sehemu ya shingo ya marehemu Monica. Mdomoni alikua amefungwa na kamba nyeusi huku miguu ikifunganishwa nyuma nayo mikono ikafungwa nyuma.

Moja kati ya picha zilizotolewa zilimwonesha monica akiwa kwenye bafu huku amevalia vazi refu ya kijani kibichi, miguu yake ikiwa imeinuliwa juu na mkato wa sentimita sita kwenye shingo lake.

Kwenye mkono wake uliojaa michoro mlikua na huku kamba za kushindilia  paa la nyumba. Sirwa alidai kuwa Monica aliuliwa sebuleni mwake kisha mwili wake ukavurutwa hadi bafuni.

“Mlikua na taulo iliyolowa damu ambayo tunashuku ilitumika kuosha damu kutoka sebuleni.” Alieleza Sirwa.

Hata hivyo wakili wake Joseph Irungu,Hassan Nandwa, alidai kuwa huenda Monica aliaga dunia kutokana na njaa kwani uchunguzi wa mwili ulionesha ukosefu wa chakulab mwilini mwake.

“Je, mlifugua umio wake ili kubaini alichkuwa kale hio siku? Je, mlifumgua tumbo lake? Je, twaweza kusema kuw kifo chake ni sababu ya kukosa kula kwani hamkua na chakula tumboni mwake?

Monica KimaniMonicah Kimani
Marehemu Monica Kimani

Wakili Hassan pia alikuwa amedai kuwa labda shingo lake monica ilikatika baada ya kupiga dunia teke.

Ndegwa alisema,”Mwili ulikua unatoa damu. Hakuna mwili mfu hutoao damu. Alikuwa na mkato kwenye shingo lake ulionekana  na damu iliyojaa kwenye mapua.”  Uchunguzi wa mwili ulifanyika tarehe 24 kwenye chumba cha kuhifadhi maiti cha Chiromo. kulinganan na uchunguzi ,monica aliaga dunia kutokana na kidonda cha kitu chenye makali. viuno vyake vyote vilikuwa na vimefungwa na kanda nyeusi.

“Mwili huo ulikuwa wa mtu mwenye umri wa miaka 28, alikuwa kavaa nguo ya rangi ya samawati  na alikuwa na vazi refu la kijani kibichi,” Ndegwa alisema. kulikuwa na wakati ambapo jaji aliuliza,”Je, mlikuwa mnaitazama kana ya soap  ama cinema ya Nigeria? Hii ni baada ya daktari wakufanya uchunguzi wa wafu kuleta picha nyingine..

 

Mwili wa mwanaume aliyejirusha kwa mto wapatikana

Mwili wa mwanaume mmoja aliejirusha kwenye mto Sio karibu na soko la Matayos wikendi iliopita umepatikana.

Mwili huo umepatikana leo asubuhi na wapiga mbizi ambao wamekuwa wakikesha kwenye mto huo wakiutafuta.

Wapiga mbizi hao wameomba serikali kuingilia kati na kuwapa vifaa vya kisasa vya kutafuta miili.

Kwingineko sare za shule za wanafunzi wawili wa shule ya msingi ya Nambale AC waliotoweka juma moja lililopita zimepatikana kichakani kilomita mbili kutoka shuleni humo.

Mzazi wa watoto hao anasema walienda shuleni wakihofia kuchapwa na mwalimu baada ya kudaiwa kuiba vitabu vya wenzao.

Kando na hayo, chama cha kutetea maslahi ya walimu KNUT tawi la Taita Taveta kimeonya kuwa huenda mtaala mpya wa elimu ukakosa kutekelezwa kikamilifu iwapo wizara ya elimu haitahusisha wadau wote.

Katibu wa chama hicho Lenox Mshila anasema shurutisho la kufunza mtaala huo mpya kilazima huenda zikaathiri pakubwa kiwango cha elimu nchini na kushauri wadau wote kujadiliana kwa kina na kuafikiana kuhusiana na mtaala huo kwa lengo la kufanikisha elimu.

Mwili Wa Mwanaume Wapatikana Bungoma

Maafisa wa Polisi mjini Bungoma wameanzisha uchunguzi kufuatia kupatikana kwa mwili wa mwanaume mmoja akiwa ameuawa katika eneo la shell viungani mwa mji huo.

Akidhibitisha kisa hicho OCPD wa Bungoma kusini David Kirui amehoji kuwa walipashwa kupatikana kwa mwili huo na mwanamke mmoja mwendo wa asubuhi alipokuwa akipeleka mwanawe shuleni ambapo ulikuwa umelazwa langoni pake ukiwa na majeraha kichwani.

Kiruia amewataka wananchi kupasha maafisa wa usalama visa vyovyote visivyo vya kawaida hasa nyakati za usiku.

Mwili wa mwanaume huyo umehifadhiwa katika hifadhi ya hospitali ya rufaaa ya kaunti ya Bungoma.

-Brian Ojamaa

 

Mwili Wa Mwanaume Mwenye Umri Wa Makamu Wapatikana Migori

Polisi huko Kuria magharibi kwenye kaunti ya Migori wameanzisha uchunguzi baada ya mwili wa mtu mmoja kupatikana ameuawa katika kijiji cha Getonganya kwenye kaunti hiyo.

Kulingana na OCPD wa Kuria magharibi Evans Wanyonyi mwili wa marehemu Marwa Kerato wa umri wa miaka arobaini na miwili ulipatikana umekatwa kichwani na kifaa butu baada ya kuvamiwa na watu wasiojulikana nyumbani kwake usiku wa kuamkia leo.

Wanyonyi alisema kuwa polisi wameanzisha uchunguzi kuhusu kisa hicho baada ya watu hao kuvamia mtu huyo bila ya kuiba chochote katika nyumba yake na pia hawakujeruhi mtu mwingine ila tu mwenye boma.

Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika chumba cha maiti cha hospitali ya kibinafsi ya Pastor Machage mjini Migori ukisubiri kufanyiwa upasuaji.