Babake Diamond Platnumz kukiwasha Stejini Itungi Hotel

Babake staa na fundi wa muziki Afrika nzima Chibu Dangote atakuwa anadondosha burudani miongoni mwa mastaa wengine Tanzania katika hoteli ya Itungi usiku wa leo tarehe 21. Babake Mondi amekuwa kifua mbele kuzamia katika tasnia ya muziki baada ya kuona mwanawe akivuna makubwa katika muziki wa Bongofleva.

Soma hadithi tofauti hapa:

Dah! Hatari sana Bahati amnunulia Diana Marua chumba kipya

Mkurugenzi wa WCB Diamond Platnumz na ambaye ni mwanawe Mzee Abdul walipatana juzi kati katika studio ya Wasafi FM na kuonekana kuzima tofauti zao za awali. Abdul aliomba msamaha mwanawe kwa madai ya kuwatelekeza yeye na Bi. Sandra Sanura Kassim.

Soma hapa hadithi nyingine:

Weka mbali mondi sasa! Babake aonyesha mngurumo wa simba mkubwa

 Kukutana kwa wawili hawa kunaonekana kulifanya ili kuzima bidii za vyombo vya habari nchini hum kukuza uadui kati ya baba na mwanae. Babake Diamond Platnumz kwa sasa anatamba vizuri na ngoma hatari inayokwendwa kwa jina Unanijua akimshirikisha Chada Boy. Happy_moment_as_Diamond_Platnumz_meets_his_father_Abdul_Juma-minxelufwd969n5hw0k5cbff4ecd6463

Tazama hapa:

Babu Tiffah pia ameweza kuzama studio na kudondosha ngoma kama Umeniteka ambayo inafanya vizuri katika mtandao wa kijamii.

Tazama hapa:

 

Diamond Platnumz na babake wakutana na kuzima tofauti zao

Msanii na staa mkubwa Afrika Diamond Platinumz ameweza kukutana katika redio ya Wasafi FM na babake na kuonekana kuzima tofauti zao za awali.

Mzee Abdul alimtaliki mkewe miaka ya awali kijana huyu akiwa kidato cha kwanza. Naseeb alitangulia kwa kusema kuwa ubaridi unaonekana kati yao na baba mzazi umechochewa na kutokua pamoja kwa kipindi kirefu.

“Kiukweli siwezi kusema nina ukaribu na mzee. Hatujakuwa na bond kubwa naye ila mimi sina matatizo naye…tukiwa kuna issue tutakutana naye tuongee” Diamond alisema katika mahojiano.

diamodn and his parents
Diamond Platnumz na wazazi

Ukaribu wa Naseeb na mamake umeonekana kwa muda mrefu kunoga huku babake akionekana kusahaulika na msanii huyu.

Katika kitengo cha Block 89 cha shoo ya redio ya Wasafi, babake Platnumz anaonekana kutokea ghafla katika mahojiano  ya mtoto wake na kituo hiki.

Mwanae anamiliki chumba hiki cha habari pamoja na runinga bila kusahau lebo ya Wasafi (WCB)  inayojivunia kusimamia wasanii wakubwa Afrika mashariki na Afrika ya kati kama Rayvany,  Harmonize, Lavalava, Mbosso na Queen Darleen.

Baada ya kuugua kwa muda mrefu, babake Chibu alipata ufadhili kutoka kwa mtendawema aliyeguswa na hali yake ya ugonjwa.

diamondplatnumzinyellow
Diamond

Yule sio mtoto wangu kunizaa ila niseme kuna watu hawana wazazi na wana hela.Aliniangalia katika mitandao ya kijamii katika hali sio nzuri na akatokea kutoa usaidizi”

Diamond anadai kuwa baadhi ya vyombo vya habari vinamtumia babake kupata ufuasi mkubwa wanapokwenda kumhoji kuhusu tofauti zao.

“Naamini vyombo vya habari vinakuzakuza na kutengeneza matatizo kati yangu na baba.”

diamond platnumz madale
Bongo singer Diamond Platnumz

Kwa upande mwingine anaona kuwa babake anamweka katika kicheko kwa watu wengi hususan wapinzani wake anapoonekana kama hamsaidii mzazi.

Babake alimwomba msamaha na wote kuonekana wameridhiana katika mazungumzo yao

Kama nimekukosea naomba unisamehe na ujaribu kuangalia utanisaidia vipi mimi babako.”

Diamond alionya kuwa kuna baadhi ya vyombo vya habari vinavyomtumia babake kwa maslahi yao na hawamsaidii. Mkali huyu wa kibao kipya The one  alimaliza kwa kuomba msamaha.

“Well mimi siwezi kusema nina  matatizo na babangu. Naamini utofauti wake na mama unafanya tuwe hatuna ukaribu…Naomba anisamehe pia kwa sababu sijui akiwa na mama walikosana kwa misingi gani.”

Also read more here