Swingers: Soma kuhusu watu wanaobadilishana wapenzi ,mambo ya kisasa

Mambo ya usasa na vitu vya uzunguni vimefika hapo nyumbani na vingine  vinashangazana . umezuka mtindo wa watu katika uhusiano wa kimapenzi au hata ndoa kubadilishana wapenzi.  Lengi inadaiwa ni kuzidisha ‘ladha’ katika mahusiani yao na hili hufanywa baada ya mwanamke na mwanamme kukubaliana kutafuta wenzao katika uhusiano kisha kubadilisha kwa usiku mmoja wa mapenzi .

‘Alikuwa akinifuata hadi kazini’ Jua unaanza mahusiano na mtu wa aina gani

Awali ungesimuliwa kwamba kitu kama hicho kinafanyika basi ungesema labda katika filamu lakini masimulizi ya wahusika yamethibitsha kwamba kweli  tabia hiyo inafanyika hapa kenya . Elimily* na  Karis  ambao wamejiunga kundi hilo la siri wanasema walipatana na pendekezo hilo kupitia rafiki yao mmoja ambaye aliwaambia jinsi mtindi huo  hutekelezwa na baada ya kuwashawishi kuhusu umuhimu wa kufanya hivyo ili kuboresha ndoa yao ,basi walikubali na wakawekwa katika kundi moja la whatsapp ambalo lilikuwa na wanachama wengine  wanaofanya hivyo na waliojipa jina ‘Nairobi Swingers’.

Jamaa katoroka na mamake wa kambo na kumuacha babake hoi

Mwanzoni walipatwa na hofu kuhusu watakavyojiingiza katika mtindo kama ule kwamba  Emily angelala na mwanamme mwingine kisha Karis afanye mapenzi na mwanamke mwingine .Walikaribishwa katika kundi hilo katika mkutano uliofanyika kwenye mtaa moja wa kifahari kisha wakatambulishwa kwa wanachama wengine . Pale ,zililetwa picha za wanawake wote ambao wapo katika lile kundi na Karis alitakiwa kumchagua mmoja. Aliambia wkamba mume wake alikuwepo pale pia lakini hilo halikufaa kumpa wasi wasi .Wakati unapomchagua mwanamke wa mwenzio ,basi huyo ndiye unayefaa kulala naye kwa usiku mmoja na mkeo pia atachaguliwa na mwanamume mwingine . Kulikuwa na masharti kwamba huwezi kufanya mapenzi na mke wa mwenzio bila kinga na wote walisaini  stakabadhi ya kueleza hilo .

Sema kuteswa! Aliniacha kwa hoteli bila kulip na sikuwa na pesa-Wanawake wasimulia mateso mikononi mwa wanaume

Emily naye aliletewa picha za wanaume ambapo alifaa kumchagua mmoja wa kulala naye usiku mmoja .mke wake alikuwepo katika kundi hilo  na baada ya kuchagua sasa walijumuika pamoja huku kila mmoja sasa akijua ni yupi aliyemchagua mke wake au mume wake .Ilipangwa safari ya kwenda karamu ya kujivinjari Naivasha ambako  Elimy na Karis walikaribishwa kwa kundi la swingers kwa kulala na  watu wan je .Tangia hapo wamezoea na sasa ni wanachama wa kundi hilo ambapo kila wanapopiga safari ,wao huchaguana upya kila mmoja akiamua yuataka kulala na mke au mume wa nani .Majabu!a

 

 

 

 

 

Mama aliyewaua wanawe 4, kupewa hatima yake

Mahakama ya Naivasha imempa maagizo atakayofuata Beatrice Mwende, mwanamke ambaye alikiri kuwaua wanawe wanne  ya kwenda katika taasisi ya akili.

Jaji aliyeongoza kesi hiyo alisema Beatrice aweze kupelekewa kwenye taasisi ya Mathare baada ya ripoti kuonyesha kuwa hayuko timamu kiakili.

Watoto 4 waliouawa na mama yao wazikwa

Mwende hakutoa ombi lolote baada ya ripoti hiyo kutokea na kusema kuwa kiakili si mtulivu kutoka hospitali ya akili ya Gilgil mashtaka tayari ilikuwa limearifu jaji mkuu Lyna Sarapai liko tayari kumshtaki mshukiwa na mashtaka ya mauaji.

“Due to the prevailing Covid-19 conditions, the High Court will not be seating for the next two days and we want to hold her until then before charging her with four counts of murder.”

Hayo ni Mapepo! Mwanamke aliyewaua watoto wake 4 alaumu mapepo kutoka kwa mpenziwe wa zamani

Beatrice aliiambia mahakama kuwa alikuwa amepagawa na mapepo kwa hivyo hakufahamu alichokuwa anafanya baada ya kuomba mahakama huruma.

Alikiri kuwaua wanawe wanne waliofahamika kama Melody Warigia (8yrs), Willy Macharia (6yrs), Samantha Njeri (4yrs) na Whitney Nyambura (2yrs).

Mama awauwa wanawe kisha kujiua baada ya kugombana na mumewe

Alidai kuwa mpenzi waliotengana naye mwaka jana amekuwa akimuamuru kufanya vitendo visivyostahili. Baada ya kutekelez kitendo hicho mwende alisema kuwa alienda kumtafuta aliyekuwa mpenzi wake Naivasha.

Watoto 4 waliouawa na mama yao wazikwa

Wakaazi wa Kinangop hatimaye wamezika watoto wanne walioangamizwa na mama yao mzazi wiki ililyopita.

Watoto hao Melody Warigia (8 ), Willy Macharia (6), Samantha Njeri (4 ) na  Whitney Nyambura (2 ), wamezikwa hii leo katika kaburi la pamoja.

Hotuba ya waathiriwa ilikuwa imeandikwa kwa ufupi kama njia ya kuonyesha kuwa maisha ya watoto hao yalikatizwa kighafla

 “The late met her death on the night of Friday, June 26 under unclear circumstances, shine all the way in the land of the living untill we meet again, rest in peace.”

Children poisoned by mother, naivasha

Miili ya watoto 2 yapatikana ikiozea ndani ya gari katika kituo cha polisi cha Athi River

Mshukiwa mkuu na ambaye ni mama yao mzazi Beatrice Mwende alisema kilichomfanya kuwauwa watoto hao ni shetani na mpenziwe wa zamani.

Akiwa mbele ya mahakama ya Naivasha, mwanamke huyo wa miaka 42 aliomba mahakama kumuonea huruma ila akasema yupo radhi pia kufungwa gerezani.

 

Children poisoned by mother, naivasha

Mwanamke huyo alisema kuwa siku ya kutekeleza uovu huo alishikwa na mapepo chanzo ambacho kilimpelekea kutekeleza tukio hilo.

 

Hayo ni Mapepo! Mwanamke aliyewaua watoto wake 4 alaumu mapepo kutoka kwa mpenziwe wa zamani

Mwanamke aliyekamatwa kwa kuwaua watoto wake wanne huko naivasha amesema aliongozwa kufanya hivyo na mapemo ya mpenzi wake wa zamani .

Beatrice Mwende, 42, amesema  alikuwa ameingilia na mapepo na yungali anafikiri yupo kwenye ndoto baada ya kutekeleza mauaji ya wanawe  na sasa anamlaumu mpenzi wake huyo waliyetangana naye mwaka jana . Mwende  amesema anapitia uchungu nab ado hajaelewa kilichofanyika .Alifikishwa kortini  jana mbele ya hakimu mkaazi wa Naivasha   Yusuf Baraza.

Horror: ‘ Nimewanunulia nguo za kuwazika’ asema mwanamke aliyewaua watoto wake wanne kupitia barua

Mama huyo wa watoto sita  alisimulia jinsi walivyowauawa  watoto wake wanne siku ya ijumaa kwa kuwapa sumu kabla ya kwenda kulala .

Mwende,  mwalimu wa hesabu  aliyekuwa akifanya kazi na shirika moja lisilo la serikali mjini Naivasha  aliomba msamaha kwa hatua hiyo yake na kutaka ahurumiwe  akisema hakujua alikuwa akifanya . “ Mpenzi wangu wa zamani alikuwa na nguvu za mapepo alizotumia kunielekeza kufanya unyama huo  na kusababisha niwaue watoto wangu wanne’ alisema

“ Nataraji kwamba ndoto hii mbaya itakamilika na nitaamka niipate familia yangu katika nuzri ya afya kwa sababu siwezo hata kumdhuru nzi’

Watoto waliouawa wametambuliwa kama  Melody Warigia (8), Willy Macharia (6) —  wote wanafunzi wa shule ya  Milimani Primary School, Samantha Njeri (4)  na Whitney Nyambura (two).

Polisi huko Naivasha wameruhusiwa kumzuilia Mwende kwa siku saba  ili kukamilisha uchunguzi wao .

Mshukiwa atafikishwa tena kortini Julai tarehe 6 .

Nilifanya ngono na pepo- Vennie amepitia mazito na ya kushangaza

Polisi watategemea ripoti ya uchunguzi wa miili ya watoto hao na ripoti wa hali yake ya kiakili .Akikumbuka uhusiano wake wan a mpenzi wake ,Mwende amedai kwamba alikuwa na nguvu za kumfanya atekeleze mambo ambayo hakutaka .

Amesema kwamba  tarehe  26 ya kila mwezi  alikuwa akiingiliwa na mapepo yaliyomfanya  kufanya vitu  bila kuweza kujithibiti . Alimtaka mungu na familia yake kumsamehe kwa mauaji aliotekeleza ya wanawe .

Mwende  amesema jumamosi asubuhi baada ya kugundua alichofanya alienda naivasha kumtafuta mwanamme huyo ambaye hufanya kazi mjini Naivasha . Kupitia barua alioandika Mwende  amesema alishangazwa na hatua hiyo yake na kwamba alikuwa tayari kwenda jela kwa makosa aliofanya .

 

 

 

Horror: ‘ Nimewanunulia nguo za kuwazika’ asema mwanamke aliyewaua watoto wake wanne kupitia barua

Mwanamke alaiyewaua watoto wake wanne huko Naivasha ameandika barua ya kuogofya inayosimualia yote yaliyotokea na kumfanya kutekeleza unyama huo ambao umeiacha familia yake na butwaa na kuwashangaza wenyeji wa eneo hilo.

Barua hiyo aliomwandikia mtoto wake wa kiume ambaye yupo katika chuo kikuu  inaeleza jinsi alivyozongwa na fikra tangia mwezi Aprili baada ya kushindwa kulipa kodi. Pia alikuwa ameshindwa kulipa bili ya stima ya shilingi 1,400.

Nilifanya ngono na pepo- Vennie amepitia mazito na ya kushangaza

Mama huyo wa watoto sita yameonekana alikuwa mtulivu na hakuwa amemueleza yeyote kuhusu  matatizo aliokuwa akipitia yakiwemo ya kifedha.

“ Najua nastahili kuwa jela .. na huenda nikafungwa maisha yote lakini nimejitayarisha kwa hilo ‘ barua yake imesema

Amemshtumu mpenzi wake kwa kumsaliti akisema ‘ Nilimpenda sana, usijihusishe naye kwa sababu alijifanya kuwa mtu mwingine’ alimuonya mwanawe

Kupitia barua hiyo amemtaka mwanawe kumtunza kaka yake mdogo na pia aendelee na masomo. Pia amefichua alikotaka watoto wake aliowaua wazikwe akisema tayari alikuwa ameshawanunulia nguo mpya.

Kaka mshukiwa Jackson Kimotho amesimulia jinsi dadake mkubwa alivyoweka picha za watoto wake hao katika kundi la familia  la whatsapp siku ya Jumamosi.  Alikuwa akitaka maoni kuwahusu watoto wake  mmoja wa wanachama wa kundi hilo alisema walikuwa wakipendeza.

Kwa msururu wa haraka  aliandika  ‘ Chukueni muda na kunyamaza, wapeni  heshima za mwisho watoto wangu, sielewi kilichofanyika. nimewaua.’

Triple Trouble : Wasichana watatu wa shule kutoka familia moja wapachikwa mimba

Muda mfupi baadaye alituma picha yake ya zamani  yenye maandishi

‘Betty the murderer — Pray for the soul to have peace here on earth.”

Msimamizi wa kundi hilo la whatsapp alimuondoa kwa haraka  lakini tayari kila kilichofanyika kilikuwa kimeitumbukiza familia hiyo katika lindi la sintofahamu.

Baadaye alimpigia kakake Kimotho simu kumueleza aende kwake akiwa na polisi na walipofika huko walipata miili ya watoto  hao.

Mshukiwa aliwapa sumu watoto hao  siku moja tu baada ya jamaa zake kutaka kuwachukua wanawe lakini akakataa. Watoto wake wawili wa kiume hawakuwa nyumbani wakati wa tukio hilo.

 

UNYAMA!Polisi wamtia mbaroni mwanamke kwa mauwaji ya wanawe wanne

Aliwaacha wengi midomo wazi na kupigwa na butwaa baada ya kukiri kuwa kuwaua wanawe wanne kwa kuwapa sumu na kisha kuwanyonga Jumamosi Juni 27. Polisi mjini Naivasha walimkamata mwanamke huyo wa miaka,42, kwa kutekeleza kitendo hicho cha unyama. Mama huyo wa watoto sita alikiri hayo kwa rafiki yake ambaye aliwaambia polisi Jumamosi jioni, kamanda wa polisi mjini Naivasha Samuel Waweru alithibitisha kisa hicho na kusema kuwa mama huyo yuko mikononi mwa polisi.

“Mshukiwa alimwambia rafiki yake kuwa wanawe wamelazwa katika hospitali ya Naivasha wakiugua kifua, baada ya saa chache alikiri kuwa aliwanyonga,” Alisema Waweru.

Wanne hao walizirai wakiwa sebuleni na akawapeleka katika chumba cha kulala na kisha akatoweka kwenda mafichoni. Wawili kati ya sita hao walikuwa wameenda wakati wa kisa hicho, polisi aliyechunguza mauaji hayo alisema kuwa mama huyo alichukua muda akiwanyonga wanawe.

“Mshukiwa alichukua muda akiwanyonga wanawe na akalala na wao chumbani kimoja hadi Jumamosi asubuhi.”

Kamanda wa polisi alisema kuwa wanaendelea na uchunguzi wa mauaji hayo ili kubaini nini haswa kilipelekea mama huyo kuwaua wanawe.

Je wazazi wamechoka kukaa na wanao wakati huu wa janga la corona, na kitendo hicho kinahashiria nini haswa?

 

MHARIRI: DAVIS OJIAMBO

Maafisa 8 wa polisi wanusurika kifo baada ya kambi yao kuteketezwa Naivasha

Maafisa wanane wa polisi wamenusurika kifo baada ya kambi yao kuteketezwa eneo la Naivasha wakati wa mandamano ya kukashifu udhalimu wa polisi.

Kisa hicho cha Alhamisi, Juni 11 asubuhi, kiliwashuhudia maafisa hao wakipoteza mali yenye thamani ya pesa.

Kulingana na wakazi, waliotekeleza kitendo hicho walianza kwa kufungia nje mlango wa afisa aliyekuwa zamuni kabla ya kuwasha gurudumu nje ya mlango wake.

Moto huo ulianza kusambaa katika nyumba zingine huku maafisa hao wakihangaika kutorekea usalama wao, moto huo ukichukua masaa mawili kuzima.

“Walikuwa wanalenga nyumba ya Inspekta ambaye hakuwepo lakini moto huo ulichoma nyumba yake kabla ya kusambaaa kwa nyumba zingine,” alisema mkazi mmoja.

Mdosi ageuza mbochi kuwa mke, aaibishwa hadharani

Inaaminika kuwa wakazi wa eneo hilo wamekuwa wakilalamikia kudhulumiwa na maafisa wa polisi wa kambi hiyo jambo ambalo linasemekana lilichangia tukio hilo.

 

Mtindo wa nywele aina ya ‘box’ wamsababishia mwanamke kifo

Mwanamke auawa kwa upanga aliotumia katika jaribio la kumuua bintiye Naivasha.

Ijapokuwa stakabadhi za mahakama zilionyesha kuwa  kifo cha Esther Wambui hakikuwa cha maksudi,lakini Gideon Kibunje atasalia gerezani kutumikia kifungo cha miezi 14 kwa kosa la kuua bila kukusudia.

Kibunje ambaye awali alikuwa ameshtakiwa kwa kosa la mauaji, alijitetea kwamba hakuua kwa kukusudia na ombi lake kortini likakubaliwa.

Maajabu! Jamaa ajitia kitanzi baada ya kujichimbia kaburi, Homa Bay

Akijitetea mbele ya Jaji Richard Mwongo kwenye mahakama ya Naivasha, mshukiwa mwenye umri wa miaka 28 alijitetea kwamba alitekeleza mauaji hayo ili kumkinga bintiye.

Aliambia korti kuwa mnamo Januari 14 saa 7 usiku, alifika nyumbani kwake mtaa wa Site mjini Gilgil na Wambui akamwambia alihitaji mboga na maziwa ya jioni.

Kibunje alitoka na kununua bidha hizo muhimu na aliporejea aligundua kuwa mke wake alikuwa amenyoa nywele mtindo wa ‘box’. Mtindo huo haukumfurahisha mumewe.

“Nilimwambia kuwa mtindo wa nyewele aliyokuwa amenyoa haufai mwanamke aliyeolewa na hakufurahishwa na maneno hayo,” alisema.

Kibunje alisema kwamba ugomvi ulizuka na Wambui akakereka zaidi. ” Alifungua begi langu na kutoa simi na kumdunga binti wetu. Nilichukua hatua za haraka na kumwepesha mtoto,” alisema.

Lakini wakati Kibunje alipokuwa anajaribu kufungua mlango, ili kumhepesha mtoto, Wambui alimdunga na simi mgongoni. Na katika hali ya vuta ni kuvute ili ajiokowe na pia kumuokoa mwanawe, Kibunje alimdunga mkewe kifuani.

Familia hiyo ina watoto wawili wenye umri wa mwaka moja na mitatu.

Ruto avunja kimya kirefu kuhusu mkutano wa Gema Sagana

“Nilikimbia nje na kuomba usaidizi kutoka kwa majirani. Walipofika walimpata akiwa katika kidimbwi cha damu huku amekata roho,” alisema.

Hatimaye polisi waliwasili wakamtia mbaroni na kuchukua mwili wa marehemu..

Upasuaji ulifanya na daktari Titus Ngulungu na uchunguzi ulibaini kuwa aliaga dunia kutokana na majereha kwenye mbavu zake kutoka na jeraha la kudungwa kisu.

“Familia yangu imesambaratika na nahitaji kupanga upya maisha yangu na ya familia, hususan watoto wangu ambao hawakuhsika kivyovyote vile katika kisa hicho.

ODM yatoa kauli kuhusiana na mkutano uliofanyika Sagana IJumaa

 

 

Vurugu baada ya mtoto mwenye Autism kuzama Naivasha

Maskini wa Mungu! Watoto wasiojiweza walikuwa wameenda kwenye ziara ya shule, na walipokuwa wakicheza karibu na mto Malewa, mmoja wao akateleza na kusombwa na maji.

autism child

Familia ya Bwana na Bi Paul Macharia Gichimu wanaishtaki shule ya Little Hands Academy iliyo karibu na mji wa Naivasha kwa uvivu wa kutowaangalia watoto hawa wasiojiweza baada ya mtoto Dalton Gichimu, kusombwa na maji.

Mwili wa mtoto huyu ulipatikana na polisi pamoja na wanakijiji ukielea kwenye mto Malewa jumatatu jioni. Wazazi wa mtoto huyu Dalton, walikuwa na simanzi na huzuni kwani hawakuwa wanaamini yaliyotendeka.

Jamaa na marafiki walikuwa na huzuni pia  na kusema mengi huku wakisisitiza kuwa, shule ndiyo iliyokuwa na makosa kwa kutowaangalia watoto hawa wasiojiweza mpaka mmoja wao akasombwa na maji.

Paul Macharia Gichimu, baba ya mtoto huyu alishangaa mbona shule hii ilichagua kuwapeleka watoto hawa mtaaa huo wakijua fika kwamba mtaa huo, huwa ni mtaa hatari sana si kwa watoto pekee bali pia kwa watu wazima. Vile vile,alisema kuwa wazazi hawakuwa wamejuzwa kuwa watasafiri na kuenda kwenye kambi hiyo.

“The area has a very steep cliff that drops into the river and it’s even unsafe for adults. I wonder why the management settled for the location in the first place,” Paul Macharia alisema.

PATANISHO: Mke wangu akirudi lazima tuongeze watoto wawili

Zaidi ya hayo, baba ya mtoto huyu alisema kua mtoto wao alikuwa anahitaji kutunzwa kwa njia spesheli na ndio maana yeye na mke wake, waliamua kumpeleka kwenye shule hiyo. Kwa huzuni tele, Paul Macharia alisema kuwa iliwachukua saa moja walimu kujua kuwa, kuna mtoto aliyekuwa amepotea na walipompata walipata mwili wake ukielea majini.

Baba huyu mwenye watoto watatu alisema kuwa wakati huu ndio uliokuwa wakati wa uchungu zaidi maishani mwake na kusema kuwa, alikuwa na matumaini mengi sana kwa mtoto wake Dalton na ni ombi lake mzazi wowote asipatwe na janga kama hilo.

“Despite suffering from autism Dalton had special talent and was a joy to the family and my prayers is that no other parent will undergo the pain that we are currently undergoing,” alisema.

Daah! Fred Omondi afunguka na kusema ameokoka

OCPD wa Naivasha, Bwana Samuel Waweru alithibitisha kitendo kilichofanyika na kusema kuwa, iwapo watapata ushuhuda wa kutosha na kuona kuwa ni ukweli shule hii ilikuwa na negligence, basi hatua kali itachukuliwa.

“We have embarked on our own investigations to determine if there was negligence on the part of the school and if there was any definitely the law will take its course,” alisema

Mwalimu wa shule hii ambaye hakutaka jina lake litajwe, alisema kuwa bado wanashangaa kwani hakuna kitendo chochote kama hichi ambacho kimewahi fanyika shuleni humo.

Vilevile, tumeamua kuomboleza na familia hii na kisa hiki ni kisa ambacho kimetutikisa sote kwani hakuna mwalimu ambaye aligundua kuwa mtoto huyo hakuwa na wenzake.

“We have decided to mourn in silence with the parents and it’s an incident that has left us shaken as none of the teachers realised that the minor had slipped from the other students,” mwalimu alisema.

Mwanaume apatikana ameuawa na mwili wake kutupwa Naivasha

Idadi ya watu wanaopatikana wakiwa wameuawa na mili yao kutupwa huko Naivasha imeongezeka hadi nne hii leo, baada ya mwanamme mmoja kupatikana ameuawa na mwili wake kutupwa katika barabara ya Moi North Lake.

Visa viwili vya kwanza viliripotiwa siku ya Jumatatu na siku moja baadaye kisa cha tatu kika ripotiwa ambapo mwili ulipatakina kichakani huku uso ukiwa na majeraha.

Mwili wa mwanamme huyo ulipatikana mikono ikiwa imefungwa nyuma na kulingana wakaazi huenda alinyongwa na waya kabla ya mwili wake kutupwa katika bara bara hiyo.

Kulingana na kiongozi wa eneo hilo Boniface Waiganjo, mwanamme huyo hakuwa stabadhi yoyote ya kumtambua. Aliongeza kuwa watu wote wanne si wakaazi wa eneo hilo na huenda waliuawa mahala kwingine kisha kutupwa eneo hilo.

Mwanamke raia wa Kenya apatikana amefariki Australia

Wakaazi sasa wanantaka uchunguzi wa kina kufanywa kuhusu mauaji hayo na wahalifu wanaotekeleza unyama huo kukamatwa.

“Hii ni mara ya kwanza tumeshuhudia visa kama hivi eneo hili na tunaomba polisi kuanzisha uchunguzi mara moja,” Waiganjo alisema.

OCPD wa Naivasha Samuel Waweru alithibitisha kisa hicho na kusema kuwa mwili umepelekwa katika chumba cha kuhifadhi maiti.

Huku hayo yakiarifiwa shughuli ya kumtafuta mwanamke mmoja huko Mia Mhiu iliishia majonzi baada ya mwili wake ulokuwa ukioza kupatikana umefungiwa nyumbani kwake.

Inakisiwa kuwa mwanamke huyo aliaga dunia siku ya Jumatatu kabla ya mwili wake kupatikana leo.

Chifu wa eneo hilo alidhibitisha kisa hicho.