Jambo Massawe: Bwanangu alinifukuza na akaoa dadangu (AUDIO)

Je mume wako akikufukuza na kuoa dadako utahisi vipi? Je waweza wasamehe kweli?

Akizungumza katika kipindi cha bustani la Massawe, Mama Chwele ni mmoja wa wanawake wanaopita masaibu hayo kwani alisimulia jinsi mzee wake alimfukuza pamoja na watoto wanne na kuoa dadake mkuu.

Isitoshe, wawili hao walipo oana walitorokea nchi jirani ya Uganda na hajawahi zungumza nao tangia mwaka wa 2011.

Bustani la Massawe: I have been smashing my boss’ wife for the last 6 years

Mungu naye alimbariki mama Chwele na bwana mwingine ambaye naye mabibi zake walikuwa wamemkimbia. Wawili hao walipendana na yule bwana akachukua wale watoto kama wake na huwa anawasomesha bila ubaguzi.

Soma usimulizi wake, kisha uskize kanda ifuatayo.

Mimi nilikuwa na mke wa ndoa ambaye tulioana tukiwa virgins. Tukazaa naye watoto wanne halafu tukawachana, akaja akaoa dadangu mkubwa nikawachana naye na akanifukuza na watoto, hata sahii hawezi shughulikia watoto lakini niko kwa ndoa ya pili.

Nikamwachia na hatujawahi kutana tangia mwaka wa 2011 mpaka sahii. Sasa wakatoroka na mzee hadi Uganda mimi nikaenda Nairobi nikaona maisha ya maid siwezi na nikarudi nyumbani. Nikapata mwanaume mwenye naye bibi alimuacha, nikamkubali naye akanikubali na mzigo wangu.

Nina watoto wanne, kijana amefanya form four, wasichana wawili last born na second last wako form two, huyu mwingine ako na shida tu ya kidunia sasa yeye ako tu nyumbani.

Lakini huyu mzee mwenye niko naye sahii, walahi namwombea mungu ampe miaka mingi kwa sababu anasomesha watoto wenye sio wake na sijawahi zaa nayewatoto.

‘I can’t support crap if it’s dirty, I won’t play it’ Massawe explains why she attacked Khaligraph

PATANISHO: Niliogopa kuwa mume wangu anaweza niua

Patrick alituma ujumbe akiomba kupatanishwe na mkewe Sylvia, mwenye umri wa miakaa 28, mbaye alipata amefunganya virago vyake na kuondoka mwezi wa Disemba tarehe 30.

PATANISHO: Bibi yangu anatetea mpango wake wa kando

Kuna kijana fulani ambaye alikuwa anamtaka na mimi kuja kugundua hayo maneno, kumuuliza ikawa tunakosana naye na baadae akaja akaniambia huyu kijana alikuwa anamtaka, lakini alimueleza kuwa yeye ni mpwa wake na hawawezi pelekana mahali. Alijieleza Patrick.

Sasa nikamweleza kuwa sikuwa naelewa hayo maneno na sasa kwa ajili nimeelewa basi hayo maneno tuyaache. Na hapo baadae akanitumia ujumbe akisema nimsamehea maneno yote aliyonifanyia.

Nikamwambia nishamsamehe na tuishi na amani, sikujua on Sunday nikitoka kazini nitamkosa. Nilipata amekusanya vitu vyake na ameenda huku watoto akiwa amewapeleka kwa mamake. Aliongeza akidai kuwa hajui kwenye mkewe aliko kwani alimwambia yuko Naivasha.

Kulingana na Patrick 31, wawili hao wamekuwa kwa ndoa ya miaka mitano lakini bado hawajaona ki rasmi.

PATANISHO: Bwanangu alikatwa kichwa na mpango wa kando na bado akamrudia

Unajua Gidi wacha nikuambie, mapenzi inakuanga ya watu wawili lakini mtu wa tatu, nne akiingia inakuwa tu hivo. Kwa hivyo mimi niliboeka. Alisimulia Sylvia.

Mimi niligundua kuwa tukivuruga kidogo yeye huenda kuambia ndugu zake mpaka anaingiza wazazi wake na tukimaliza maneno, hatukai hata wiki moja kabla ya kurudisha yale maneno. 

So niliona hakuna haja ya kuendelea na yeye, unajua mtu anaweza kuambia amekusamehe na kwa roho hajakusamehe. Mimi niliogopa kwani mtu hata anaweza kuua. Aliongeza.

 

Pata uhondo kamili.

PATANISHO: Nilitoroka kwangu kwani niliogopa watoto wangu watanipiga

Bwana Charo aliomba apatanishwe akidai mkewe bi Edith, aliondoka baada ya wawili hao kukosa kuelewana akidai kuwa shetani aliingilia kati ndoa yao.

“Huyu bibi mimi nilikuwa nampenda sana lakini sasa kadri tunapoishi, unajua shetani ana majaribio yake. Huyu shetani alinichezea mchezo ambao sio lakini ashindwe!.” Alijieleza.

Bwana Gidi huyu mke wangu tulikuwa tunaishi Mombasa na nikimwambia twende kwetu nyumbani Mariakani huwa hakubali, lakini kwao hupenda kwenda kila baada ya mwezi miwili. Sasa ikabidi saa zote akienda namwambia sipendelei.

Siku moja nikamwambia hivo vyenye wewe huenda wewe baki huko nitakufuata, yeye akaniambia hata asubuhi nitamwona amefika huko. Sasa aliporudi mimi nikamchapa. Sasa nikitaka kumchapa nikakumbuka ana vijana wakubwa na nikaogopa watanichapa na nikatoroka.

Mke naye akakaa Mombasa nami nikarudi Nairobi na hatujakuwa tukizungumza hata kiasi.

Wawili hao wamekuwa kwa ndoa ya miaka ishirini.

Alipopigiwa simu bi Edith alisema kuwa aliskia kutoka kwa dadake Charo kuwa alikuwa amefunga ndoa mara mbili huku akidai kuwa haoni wawili hao wakirudiana.

“Kurudiana sioni kwani nitakuwa naingilia nyumba nyingine ya bibi wa pili. Msamaha nilikusamehe kitambo sana na nikakuacha uishi maisha yako mimi niishi yangu.” Alisema.

Pata uhondo kamili.

 

 

Msanii Ali Kiba afichua jinsi alivyokutana na mkewe nchini Kenya (AUDIO)

Ali Kiba ambaye yuko nchini kwa mikutano ya kuhakikisha kuwa uzinduzi wa kinywaji chake ‘ nchini Kenya utakuwa timamu, aliweza kuketi chini na mtangazaji Massawe Japanni siku ya Jumatatu.

Mwimbaji huyo ambaye alitamba baada ya kuzindua wimbo wake ‘Cinderella’ takriban miaka kumi iliyopita, alizungumzia maswala mengi katika mahojiano yake lakini kilichofurahisha wengi ni pindi alipofichua jinsi alivyo patana na mkewe Amina.

amina khalef 1

Ali Kiba alifunga pingu za maisha na mpenziwe wa siku nyingi, Amina Khalef Aprili mwaka huu katika sherehe ya kukata na shoka, katika uga wa Diamond Jubilee, Mombasa. Sherehe hiyo ili walete watu mashuhuri akiwemo gavana wa Mombasa, Hassan Joho.

Lakini wawili hao walipatana wapi?

“Ushawahi skia msemo unaosema mapenzi ni majani huota kokote hata juu ya nyumba aisee. Mkee wangu nilikutana naye hapa Kenya mjini Nairobi. Alikuwa anasomea USIU na nikabahatika kuwa naye tukafahamiana tukawa marafiki kwa mda mrefu.

I believe alikuwa shabiki wangu na alikuwa anapenda mziki wangu kwa mda mrefu. ” Alieleza Ali Kiba.

amina khalef

Alipoulizwa iwapo mkewe anahofia kuwa jinsi alivyopatana na star huyo ndivyo huenda akapatana na mwanadada mwingi humo nje, alisema;

“Ki ufupi anaelewa jinsi maisha yangu yalivyo na ananijua vilivyo ananiheshimu na ananipenda nami nampenda sana.

Hiyo haina shida kwani anaelewa mume wake ni mtu wa aina gani, ni msanii na nashukuru kuwa anajiheshimu ndio maana mpaka sasa hivi hukuskia chochote kimetokea iwapo ni mda mfupi.” Alisema.

Ali Kiba’s ex girlfriend lands a government job

Miezi saba baada ya wawili hao kuoana, wapendwa hao wawili tayari wanatarajia mtoto wao wa kwanza ambaye atakuwa mtoto wa nne wa msanii ambaye ana watatu na wanawake watatu tofauti.

“Katika dini yetu we believe kwamba ni faida kubwa ya ndoa wakati tumemaliza kufunga ndoa tukikaa kidogo tupate baraka. Mungu akipenda atajifungua mwakani lakini bado hatujui kama ni wa kike.

Wakati mwingine hufika na huwezi ishi na mtu bila makubaliano so ni ivo tu. Naishi na mtoto mmoja ambaye nilimchukua akiwa na miezi sita. Mwingine ambaye ni first born anaishi UK mwenye umri wa miaka tisa na wa mwisho ana miaka mitano.”

Yafuatayo ni baadhi ya maswali mengine ambayo aliweza kujibu.

Ali Kiba’s baby mama reveals why she sued Ali Kiba after his wedding

Je wataka kuingia kwenye siasa nchini Kenya?

Kiba: Hapana sina nia ya kuingia kwenye siasa, hizo ni fununu tu.

Changamoto gani kubwa umepitia?:

Kiba: Challenges ziko nyingi lakini siku yangu ya harusi kuna vitu vilitokea kama kuna watu nilitarajia watakuja lakini baada ya harusi nilipata lawama nyingi sana, ‘kwa nini hukunialika na kadhalika’. Halafu maybe on social media kuna vitu ambavyo wengi hunizungumzia.

Pata mahojiano yote kati ya Ali Kiba na Massawe Japanni katika kanda ifuatayo.

PATANISHO: Mke wangu aliniambia atanitesa kwa miaka kumi

Bwana William aliomba apatanishwe na mkewe wa miaka ishirini ambaye walikosana mwaka jana.

“Tumeishi na yeye kwani nilimuoa akiwa mdogo baada yake kumaliza kidato cha nne. Tumejaliwa watoto watatu ambao wako shuleni.”Alisema William.

Sasa tumeishi na amani na hatujawahi kosana naye halafu nikaskia 2017 mwezi wa nne wakati walikuwa wanaandika wanajeshi. Sasa mkora alitoka Nairobi akaja akamweleza naandika watu kazi na akaambiwa atafutiwe watu watatu kazi.

Sasa mke wangu akatafuta watatu ambao walitoa elfu mia tatu kwa kila mtu na akapatia huyo jamaa. Lakini mke wangu hakunijulisha kuna mpango anafanya pale kwa miezi minane na kuna watu walikuja kunitafuta wakidai fedha.

Sasa tulikosana na mke wangu na huwa tunazungumza naye saa zingine anacheka na kuna siku aliniambia atanitesa miaka kumi kwani sahii yuko raha.” Alieleza William.

Alipopigiwa simu bi Mary alisisitiza kuwa atampa mke wake kichapo cha miaka kumi.

“Character zake ndio zilinikasirisha. Alikuambia ana mwanamke? NIlimsamehe alipo zaa mtoto mmoja nje ya ndoa sasa ya pili akarudia. Halafu kilicho nichosha zaidi ni nililea watoto niliompata nao hadi wakamaliza shule lakini wangu hakuwa anataka kuwaona.” Alijieleza.

Pata uhondo kamili.

PATANISHO: Bibi yangu alihama na watoto

George alituma ujumbe akiomba apatanishwe na mkewe bi Hellen, ambaye walitengana na kwenda na watoto na kwenda Nairobi.

“Ilikuwa mwezi wa nane mimi nafanya kazi Siaya na bibi anafanya Nairobi. Sasa nilikuwa nimeenda likizo pamoja na watoto Nairobi, sasa siku nilikuwa nirudi nyumbani nilipata kijikaratasi kilikuwa kimeandikwa mke wangu alikuwa ameenda Uganda.” Alieleza George.

Sasa kumuuliza alikataa kujieleza na nikamwambia kama amekataa kuniambia ukweli, ukirudi nyumbani tutaongea. Sasa wakati wa kuja alipeana watoto kwa ndugu yake na aliporudi akachukua watoto na baadaye ndio akaniambia ndoa yetu imeishia hapo.

Sasa on Sunday, nikasafiri Nairobi ili tuongee na nikapata tayari ameshahama. Nikaspend the whole day kumtafuta na sikumpata kwani sijui alikohamia. Jana nilimpigia simu lakini bado hajaniambia aliko.” Aliongeza jamaa mwenye umri wa miaka 30.

Wawili hao wamekuwa kwa ndoa ya mika saba na wamejaliwa watoto wawili.

Alipopigiwa simu bi Hellen alikiri amehama lakini atarudi tu kwani hamna tatizo haliwezi tatuliwa.

“Mimi nilikuwa nimemwambia kama anaweza ji sort na aendelee na maisha yake, nilikuwa tu nafeel nikae kivyangu. Gidi unajua kuna maneno mengine huwezi sema kwa redio, hadi nilimueleza mambo ya Uganda sio yalifanya tuachane.” Alisema Lenny.

Pata uhondo kamili.

Jambo Massawe: Rafiki ya mume wangu alinitoa kwangu na kunioa

Mwanamke mmoja kwa jina Nancy aliwaacha wengi vinywa wazi akiwemo mtangazaji Massawe Japanni alipopiga simuna kusimulia jinsi rafiki wa mumewe wa dhati alivyo mtoa kwa ndoa yake na kumuoa.

“I am back bigger and better!” Massawe Japanni announces her comeback

“Nilimpenda tu na nikaona mapenzi yake iko juu sana.” Alisema baada ya kuwa na yule jamaa kwa mda wa miaka mitatu lakini bado hawajafanikiwa na mtoto.

“Mimi alishanioa alikuwa rafiki ya mzee. Alinitoa kwangu.” Alisimulia.

Nilikuwa nafanya biashara na mzee alikuwa anamuamini huyo jamaa na kutuacha naye.

Nilimuacha mume wangu kwani nilimpenda huyo rafiki yake nikaona mapenzi yake yako juu sana. I am happy, very happy!” Aliongeza Nancy akidai kuwa ndoa yake ya pili ilivunja urafiki kati ya jamaa hao wawili.

Proof that Radio Jambo Presenter Massawe Japanni has fun in the studio

Pata uhondo kamili.

 

 

PATANISHO: Siwezi olewa na Mwanaume hana makao!

Silas alituma ujumbe akiomba apatanishwe na mke.

“Mwaka wa 2015 tulikosana na mke wangu na akaondoka na kwenda Nairobi kwani nilikuwa nimejenga nyumba karibu na boma lao. Sasa nikashikwa na uwoga kwani niko karibu na kwao na ameniwacha.” Alieleza.

Mama mkwe anapita ananiona nikiosha watoto, nikiosha vyombo sasa hilo jambo likanisumbua sana.

Sasa nikaamua niuze ile shamba ninunue kwingine na nijenge boma lingine na nikafanya hilo na nikaelekea Nairobi kutafuta kibarua. Nairobi tukatafutana na tukaenda tukajenga naye mahala nilinunua.

Kutoka mwezi wa nane mwaka uliopita akaanza kubadilika tena.” Aliongeza Simon mwenye umri wa mika 34 akidai anataka tu kujua msimamo wa mkewe.

“Yeye mwenyewe kitambo akuje anajua makosa ni yepi.” Alieleza Lydia.

Mimi sikumwacha kwa kutaka, kitu kilinikasirisha ni kuwa niliolewa naye na tukanunua shamba na shida lakini tulipotoka kwao aliona amefika na akaona atafute wanawake. Nilipojaribu kumuongelesha akadai kuwa pia mimi nifanye hayo na nikiuliza ananipiga.” Alieleza akidai kuwa mumewe aliuza lile shamba na akala zile fedha.

Pata uhondo kamili.

Toboa Siri: Bwanangu Huniita Jina La Mamangu, Sikujua Anampiga Kuni Pia

Mrembo mmoja aliwashangaza watangazaji Mbusii na Lion katika kitengo cha ‘Toboa Siri’ alipofichua kuwa mumewe amempachika mamake mimba.

Mwanadada huyo alikiri kuwa shida ilianza wakati mmoja mumewe alirudi nyumbani akiwa mlevi chakari na badala amuite jina lake alikuwa anamuita jina la mamake.

Toboa Siri: My wife has no idea I have been sleeping with her younger sister

Hapo alianzisha uchunguzi na ndipo aligundua kuwa wawili hao wana uhusiano. Isitoshe amempachika mimba.

“Mimi nimeolewa na nina mtoto moja. Nimekaa kwa ndoa kwa miaka miwili sasa tulikuwa tunakaa vizuri na mume wangu na ilifika mahali akaanza kubadilika, mara hali kwa nyumba na nikimuongelesha anajibu na hasira.” Alisimulia mwanadada huyo.

Siku moja kwenye harakati zake za ulevi alianza kuniita jina la mama yangu. Sasa nikashindwa nini inaendelea na aliendelea kuniita ivo siku kadhaa. Naishi na yeye lakini mamangu yuaishi kivyake kwani ni single mother.

Toboa Siri: Nina Sugar Mummy Na Bibi Yangu Hana Shida

Nikakuja nikachunguza nikapata wana uhusiano pamoja na hata sahii mamangu (mwenye umri wa miaka 40) ana mimba na nashuku ni yake. Niliangalia message zenye hutumiana na hata mamangu humuita sweetheart.” Aliongeza akidai kuwa hajui kama mamake mzazi anajua uhusiano wao.

Skiza uhondo wote.

PATANISHO: Jamaa akubali kuwa na uhusiano na mama pima

Anne kutoka eldoret alituma apatanishwe na mumewe Zeblon.

Kulingana anadai kuwa walikosana mwezi uliopita na akaenda nyumbani kwao lakini amerudi hivi majuzi. Alidai kuwa bado hamna amani kwa nyumbani.

“Ilianza mwezi wa tatu ambapo bwanangu alianza kubadilika na kumuuliza shida ni gani anadai ako sawa lakini ikafika mahali alikuwa anafika nyumbani, anabadilisha mavazi halafu anaenda kubwaga pombe.” Alisimulia mwanadada.

Kumbe alikuwa ameshikana na mama flani wa pombe ambaye alikuwa anaenda kunywa pombe na analala huko. Kazi ya huyo mwanamke ana tabia ya kuchukua wanaume wa wenyewe kwa miezi mitatu kisha anawaacha.

Sasa ilibidi nimemshikia kisu ili nione kama atabadilisha, ametulia lakini nataka akiri kuwa amewacha tabia zake.” Aliongeza bi Anne.

Ni kweli Gidi nilikuwa na uhusiano na huyo mwanamke lakini sasa kulikuwa na vile tulikuwa tumependana na ilikuwa bahati mbaya mke wangu aligundua lakini niliomba msamaha na hayo yakaisha.. Alikuwa ni msichana mdogo na nilianguka kwa mtego. Alijitetea bwana Zeblon.

Pata uhondo kamili.