Ligi ya Europa: Makali ya Pepe yaokolea Arsenal

Nicolas Pepe aliokolea Arsenal kwa free-kicks mbili katika dakika kumi za mwisho za mechi yao ya makundi ya ligi ya Uropa dhidi ya Vitoria Guimaraes waliposhinda mabao 3-2 ugani Emirates.

Walikua wanapoteza 2-1 wakati Pepe alipofunga bao kunako dakika ya 75th na lingine dakika tano baadae. Kwingineko Manchester United walipata ushindi wa 1-0 dhidi ya Red Star Belgrade.

Hayo yakijiri, wachezaji wa ligi ya Premier huenda wakabiliwa na uwezekano wa kucheza mechi siku sita kabla ya kuanza kwa olimpiki ya majira ya baridi mwaka 2020 huko Qatar.

Nameless ampasha Massawe baada ya kuanguka katika jangwa la Dubai

Mipango ya awali inaonyesha ratiba ya ligi hio kupangwa wakati wa mashindano hayo yatakayoanza Novemba tarehe 21 hadi Disemba tarehe 18. Mechi za ligi huenda zikachezwa kuanzia Novemba tarehe 12 na kuregelewa tarehe 26 Disemba, siku nane baada ya fainali. Suala hili litajadiliwa katika mkutano ujao wa wadau wa ligi hio mwezi ujao.

Polisi wa Merseyside wamewasaidia Liverpool kumtambua mhuhusika aliyechapisha bango la Divock Origi lililotajwa kuwa la kukera na la kibaguzi. Polisi wa Ubelgiji sasa wanasema wanachunguza kisa hicho ambapo picha ya Origi ilichapishwa mwishoni mwa mechi ya ligi ya mabingwa waliyowanyuka Genk jumatano, huku Uefa ikisubiri ripoti kutoka kwa shirika la kukabiliana ubaguzi wa rangi FARE.

Mwandishi afungwa kwa kushiriki ngono nje ya ndoa

Huenda Harambee Stars wakakabiliwa na sintofahamu katika siku chache zijazo wanapojitayarisha kwa michuano ya AFCON mwaka 2021 kwa kua FIFA imetishia kupiga marufuku FKF baada ya George Mwaura kuwasilisha kesi katika mahakama kuu kuahirisha uchaguzi unaokuja. Kanuni za FIFA zinaashiria kuwa masuala ya soka hayapaswi kushughulikiwa na mahakama za kawaida bali mahakama za spoti. Iwapo Mwaura hataondoa kesi hio anajiweka katika hatari ya kupigwa marufuku ya shughuli zote za soka.

Ligi ya Kenya cup inaanza kesho katika maeneo kadha. Mabingwa watetezi  KCB wataanza kampeni yao na mechi dhidi ya Western Bulls. Huko Nakuru katika uwanja wa maonyesho ya kilimo, Menengai Oilers watakabana na majirani zao Nakuru RFC huku Homeboyz wakichuana na Kenya Harlequins. Mechi zingine zitakua kati ya Kabras watakaowaalika Kisumu RFC, Mwamba watachuana na Blak Blad huku Impala wakikabana na Nondies katika uwanja wa Jamhuri.

 

 

Arsenal wakamilisha usajili wa Nicolas Pepe kwa kitita cha pauni milioni 72

Arsenal wamekamilisha usajili wa wing’a wa Ivory Coast Nicolas Pepe kutoka Lille kwa kitita cha pauni milioni 72, kwa mchezaji huyo wa miaka 24 anayeaminika kutia saini mkataba wa miaka mitano.

Pepe alikua na msimu mzuri na Lille, akifunga mabao 23 katika mechi 41. Arsenal wanaaminika kuwapiku Napoli kumsajili Pepe na kiungo huyo atavaa sare nambari 19 ugani Emirates.

PATANISHO: Ndugu yangu alitumia simu ya mzee kufuliza

Ni mchezaji wa nne kusajiliwa na Gunners msimu huu wa joto baada ya Dani Ceballos, Gabriel Martinelli na William Saliba.

Napoli wamejipanga na kitita cha Euro milioni 60 kwa ajili ya winga wa Crystal Palace na mchezaji wa kimataifa wa Ivory Coast Wilfried Zaha baada ya kumkosa Pepe.

Kwingineko Barcelona wanataka kumuuza Mbrazili Philippe Coutinho, lakini wanahofia kuwa kuwa hawajapata ofa yoyote kumhusu mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27.

Ole Gunnar Solskjaer anasema Manchester United bado wanajitahidi kusajili wachezaji kabla ya msimu mpya kuanza na kuwa anafurahishwa na bishara ya uhamisho ya klabu hiyo.

United wamemsajili Daniel James na Aaron Wan-Bissaka msimu huu wa joto na wako katika majadiliano kumsajili kiungo wa Juventus Paulo Dybala na mlinzi wa Leicester Harry Maguire.

Tukisalia Uingereza, Tottenham wameanzisha majadiliano na Sporting Lisbon kwa ajili ya Bruno Fernandes. Wawakilishi wa Spurs walikutana na maafisa wa Sporting jijini Lisbon jana.

PROOF:Niko tayari kwa uchunguzi wa DNA,asema ‘mke wa pili ‘ wa Ken Okoth

Majadiliano hayo yanaaminika kuwa ya awali lakini Fernandes anadhaniwa kuweza kuchukua nafasi ya kiungo wa kati wa Real Betis Giovani Lo Celso, ambaye amekuwa akiwaniwa na Mauricio Pochettino msimu huu wa joto.

Manchester United pia wanamtaka Fernandes lakini hajapewa kipa umbele na huenda mkataba wa Old Trafford usitokee.

Dirisha la uhamisho la la ligi ya Premier litafungwa Agosti tarehe 8.

 

Kocha wa Gor Mahia aruhusiwa kwenda nyumbani kushughulikia maswala ya kibinafsi

Gor Mahia jana ilithibitisha kwamba kocha mkuu Hassan Oktay amepewa siku kadha za mapumziko kushughulikia masuala ya kifamilia nyumbani kwao Uturuki.

Kocha huyo ataondoka kuelekea Uturuki hii leo na mabingwa hao wa KPL hawakusema anatarajiwa kuregea lini. Kocha huyo ameahidi kurudi kwani sio mara ya kwanza kwa kocha wa Gor Mahia kuondoka nchini kushughulikia masuala ya kibinafsi na kukosa kuregea.

Mwaka uliopita Dylan Kerr aliondoka nchini kwa sababu kama hizo na akaishia kujiuzulu.

Kiungo wa Gor Mahia Dennis Oliech ameregelea mazoezi na klabu hio baada ya kupona jeraha. Oliech aliyesajiliwa Gor Mahia mapema mwaka huu alikatazwa kukamilisha msimu Mei baada ya kuvunjika mkono na alidhaniwa kuwa huenda angekaa nje kwa miezi mitano.

Hata hivyo anaripotiwa kupona na kuanza mazoezi na timu hiyo kabla ya kuanza kwa msimu mpya. Kogallo itamtegemea sana Oliech msimu huu baada ya kuondoka kwa Jacques Tuyisenge ambaye amehamia Angola.

Kwingineko, Nicolas Pepe anatarajiwa kufanyiwa uchunguzi wa kimatibabu na Arsenal katika kipindi cha siku chache zijazo baada ya mkataba kuafikiwa na Lille.

Mchezaji huyo wa umri wa miaka 24 anatarajiwa kuwa mchezaji wa Arsenal wiki hii na atakua wanne kusajiliwa na msimu huu wa joto. Pepe alifunga mabao 22 katika Ligue 1 msimu uliopita, na kuibuka wa pili nyuma ya Kylian Mbappe wa Paris- Saint Germain, na kusaidia mara 11, Lille ilipomaliza nyuma ya PSG.

Gareth Bale hajajumuishwa katika kikosi cha Real Madrid kitakachosafiri kuelekea Ujerumani kabla ya msimu kuanza. Miamba hao wa Uhispania wamesema katika tovuti yao kuwa Bale hajafanya mazoezi nje ya kikosi hicho, badala yake amefanya mazoezi ndani na mchezaji mwenzake aliye na jeraha Luka Jovic.

Real ilitangaza kwamba kikosi hicho kinachoelekea Munich na jina la Bale halikuwa kwenye orodha hiyo ya wachezaji 24. Inaarifiwa kwamba Bale hayuko tayari kucheza baada ya rais wa Real Florentino Perez kumzuia kujiunga na Jiangsu Suning.

Everton imewasilisha ombi la pauni milioni 55 pesa taslimu kumsajili kiungo wa Crystal Palace Wilfried Zaha huku kukiwa hakuna mchezaji wanayejitolea kubadilishana na wapinzani wao katika ligi ya Premier.

Palace inataka pauni milioni 60m awali ili kumuachia mchezaji huyo wa kimataifa wa Ivory Coast na pia ina wasiwasi kuhusu namna Everton inavyotaka kupangia malipo katika makubaliano yoyote yanayowezekana kuidhinishwa.

Inter Milan bado wanafanya majadiliano ya kumsajili mshambulizi wa Manchester United Romelu Lukaku kwa mujibu wa mkurugenzi wa Inter Beppe Marotta.

Lukaku amewachwa nje ya kikosi cha United kilichosafiri kwa mechi ya leo ya kirafiki dhid ya Kristiansund huko Norway, na amekosa mechi zote nne za kabla ya msimu kuanza huko Australia, Singapore na Uchina kutokana na jeraha dogo.

Juventus wanatayarisha ofa ya kumtaka Lukaku na wako tayari kumjumuisha Paulo Dybala kama sehemu ya makubaliano yao, lakini raia huyo wa Argentina anataka kusalia Turin.