Mbunge aandamana na wake zake 4 na watoto 27 Bungeni kuthibitisha uwezo wake

Mwanamume mmoja Mnigeria ambaye anawapenda wake zake wote bila kubagua amewaacha watu wengi wameduwaa baada ya video yake akiwatambulisha wapenzi wake bungeni kusambaa.

Alhassan Ado Doguwa anajivunia kuwa baba ya watoto 27 na ana wake wanne ambapo hujigamba nao kila mahali.

Katika video ya kusisimua iliyopakiwa na Gavana wa Nairobi, Mike Sonko,kiongozi huyo wa wengi katika Bunge la Kitaifa la Nigeria, anaonyeshwa akiwaomba wake zake wasimame.

Wanawake hao wanne ambao nyuso zao zilikuwa zimejaa tabasamu walisimama na kupunga mikono.

Kiongozi huyo alikuwa anajaribu kuwaonyesha wabunge wenzake kuwa ni mtu mwenye nguvu pande zote na wake zake wanne ni thibitisho kuwa ni mwanamume kamili.

Doguwa alikuwa amerejea tu bungeni baada ya kushinda uchaguzi mdogo na kutaka kurejea kwake kuwacha historia.

Toto limekua!, Kiuno kimekubalika, Tazama picha za Joy Muigizaji wa Machachari

Kiongozi huyo ambaye ushindi wake wa awali ulikuwa umefutwa, aliwataka viongozi wenzake kutambua kwamba anazingirwa na nguvu za uongozi popote aendapo.

“Bwana Spika, ningependa kukujuza kwamba hii leo pamoja nami ni wake zangu wanne wapendwa, Halima waeza kusimama, Umma simama,” Ado alisema.

Jamaa akamatwa akikojoa kwenye jiwe la kumbukumbu ya polisi aliyeuawa

Alianza kujigamba kwamba barafu hao wa moyo wake wamemzalia watoto 27 warembo na tena wenye afya ambapo pia ni ishara ya mamlaka kulingana na Ado.

“Na sababu nyingine ni kukujuza kwamba wakati wananiita mtu mwenye nguvu, mimi sina mamlaka bungeni pekee lakini pia nina mamlaka nyumbani kwa sababu ninakabiliana na wake wanne,” aliongezea Ado.

Jamaa aliyewabaka wanawake 40 chini ya mwaka mmoja akamatwa na polisi

Polisi nchini Nigeria wamemkamata mwanamume mmoja anayedaiwa kuwabaka wanawake 40 chini ya mwaka mmoja. Jamaa huyo alikamatwa baada ya mwanamke mmoja mkaazi wa mji wa Dangora kaskazini mwa Nigeria kumpata akiwa amejificha katika chumba cha watoto cha kulala.

Kiongozi wa mji huo, Ahmadu Yau, alisema kukamatwa kwa mshukiwa huyo ni hatua kubwa ambayo wamepata katika kukabiliana na uhalifu huo.

“Watu wa Dangora wanafurahia sana hatua zilizochukuliwa na tunatumaini haki yao itatekelezwa,”alisema Yau.

Wakaazi wa Dangora walidokezea kwamba walikuwa wakiishi kwa woga mwaka 2019 na wengine hata kuchagua kusalia ndani ya nyumba zao kwa sababu wabakaji walikuwa wanaruka ua na kuingia majumbani kuwabaka wanawake.

227bb8830bd57876

Visa vya ubakaji na mauaji ya wanawake nchini Nigeria vimekuwa vikikithiri siku za hivi karibuni hali ambayo imewapelekea wananchi kumeza funda chungu la mate.

Kulingana na dada yake marehemu, Judith Omozuwa, Uwavera alikuwa anajisomea vitabu vyake ndani ya kanisa la Redeemed Christian Church of God(RCCG), karibu na nyumbani kwao Benin City wakati wa tukio hilo.

Judith alifichua kwamba dada yake mpendwa alibakwa kabla ya kuuawa na wahalifu hao. Uwavera alikimbizwa hospitalini baada ya mlinzi kumpata sketi yake ikiwa imechanika na blauzi yake ikiwa imelowa damu.

Mwanafunzi huyo ambaye alikuwa na ndoto ya kuwa muuguzi, alikata roho hospitalini siku ya Jumamosi, Mei 30, kutokana na majeraha aliyopata baada ya kushambuliwa.

Wananchi walizua hamaki mitandaoni kufuatia mauaji hayo ya kinyama huku kampeni ya kutaka atendewe haki ikienea nchini humo.

‘Si jambo la kawaida!’ Vifo vya wazee vyatia hofu watu Nigeria

Mashirika na asasi zingine katika taifa la Nigeria Kaskazini haswa katika jimbo la Yobe yamesema watu 471 wamefariki kufikia sasa chini ya wiki tano, yakisema kuwa idadi hiyo ya watu ni ya kutiliwa shaka wakati huu ambao taifa hilo linakabiliana na corona.

Haijabainika wazi iwapo visa hivyo vinatokana na virusi hivyo.

Aliyefariki kutokana na corona Bomet azikwa usiku

Nigeria kufikia sasa limethibitisha visa vya maambukizi 5,000 huku watu 164 wakiwa wamefariki.

 

Mkuu wa Yobe Muhammad Lawan Gana ameliambia shirika la BBC kuwa baada ya utafiti kufanyika na bainika kuwa asilimia kubwa ya watu waliofariki ni wazee huku magonjwa kama kisukari yakiwa yanaendelea kuripotiwa.

BUHARI-730x414

Muwe macho! Msiruhusu watu kutoka Tanzania kuvuka ovyo ovyo – Wamalwa asema

Ameongeza kuwa baadhi ya watu hao wanaofariki walikuwa wameonyesha dalili za virusi vya corona.

 

Tumekuwepo na taarifa  kuwa asilimia kubwa ya vifo kutoka jimbo hilo la Yobe imekuwa ikifichwa swala ambalo limewapa wakaazi hofu.

Kwendeni kabisa! Madereva 25 waliopatikana na corona kwenye mpaka wa Namanga warudishwa katika mataifa yao

 

Hatua ya kupima idadi ndogo ya watu katika taifa la Nigeria kubaini ni wangapi walioambukizwa virusi hivyo imetia hofu mashirika hayo yakisema huenda asilimia kubwa ya watu wanaishi na virusi hivyo

 

 

Polisi Nigeria wabomoa hoteli zalizokiuka sheria za kukaa nyumbani

Maafisa wa polisi nchini Nigeria wamebomoa hoteli mbili kwa madai kuwa zilikiuka sheria za kukaa nyumbani. Gavana wa jimbo la Rivers, Nyesom Wike alisema kuwa wamiliki wa hoteli ya Edemete na Prodest walikamatwa kwa kuendesha biashara kinyume na masharti yaliyowekwa kwa ajili ya kukabiliana na COVID- 19.

6f59bfd70de19d7a

Nyesom alisema visa vya hivi karibuni vya maambukizi ya COVID-19 vilitokana na watu waliokuwa katika hoteli mbalimbali katika jimbo hilo.

Aidha, gavana huyo hakusema iwapo hoteli hizo mbili zilikuwa zimeripoti maambukizi ya virusi vya corona.

Mmoja wa wamiliki wa hoteli hizo alikanusha madai kuwa hoteli yake ilikuwa ikiendesha biashara kinyume na masharti ya COVID-19.

“Hoteli haikua ikifanya kazi na asilimia 70% ya wahudumu walikua wamerudishwa nyumban.” Alisema.

Licha ya kujua hatari za virusi vya corona wanakiuka sheria na kufanya mambo yasiyostahili.

Flight baby: Mwanamke kutoka Nigeria ajifungua mtoto katika ndege ya kumrejesha nyumbani

Mwanamke mmoja amejifungua mtoto akiwa safarini katika ndege kurejeshwa  Nigeria  kutoka  Dubai UAE.

dunai 2

Abike Dabiri-Erewa,  mwenyekiti wa   jamii ya wanigeria walioko nje ya nchi  amesema  Kafayat Amusan  alimzaa mtoto wa kiume dakika 30  baada ya ndege kuondoka  uwanja wa ndege. Ndege hiyo ililazimika kurejea Dubai ili kuhakikisha kwamba mama na mtoto wapo salama .

Kenya yafikisha watu 582 walioambukizwa virusi vya Corona-Mutahi

Amusan na mwanawe wapo katika hali nzuri kiafya  na wamelazwa katika hospitali moja Dubai. Wanatarajiwa kurejea Nigeria pindi cheti za  kuzaliwa cha mtoto huyo  kitakapotolewa  na stakabadhi nyingine za usafiri kutayarishwa. Mwanamke huyo alikuwa katika kundi la kwanza la raia wa Nigeria  waliotolewa UAE kurejeshwa nyumbani kwa sababu ya janga la virusi vya Corona .

Watu 256 waliwasili katika uwanja wa ndege wa   kimataifa wa Murtala Muhammed  jijini Lagos  Jumatano saa moja jioni. Maamlaka za Nigeria zimesema zimefaulu kupata sehemu ambazo raia wake wanaorejea watakapotengwa katika karantini.

 

 

Sio Movie? Mwanamke mwenye umri wa miaka 68 ajifungua mapacha Nigeria

Mwanamke mwenye umri wa miaka 68 huko Nigeria amejifungua mapacha  katika  Hospitali ya mafunzo ya chuo kikuu cha Lagos(LUTH)

Aliekewa mimba kutumia njia ya kisayansi IVF.

Wasiu Adeyemo,  kutoka hospitali hiyo amesema  mwanamke huyo alikuwa  akipata mimba kwa mara ya kwanza

Bwana Adeyemo amesema mwanamke huyo alijifungua kupitia njia ya upasuaji tarehe 14 Aprili  baada ya kuibeba mimba yake kwa wiki 37 .

Ameongeza kwamba, yai la uzazi la mwanamke huyo lilitundikwa katika eneo tofauti na alikojifungulia mwanamke huyo

 

 

Kizaazaa baada ya mwanamke kuolewa na wanaume wawili Nigeria

Mgogoro mkali wa kimapenzi umeibuka katika jimbo la Kano nchini Nigeria ambapo wanaume wawili walimuoa mwanamke mmoja wakati tofauti.

Katikati ya mgogoro huo ni mwanamke kwa jina Hauwa Ali Mariri mwenye umri wa miaka 32 ambaye sasa anahofia adhabu iwapo atapatikana na hatia ya kuwadanganya wanaume hao.

Kano ni mojawapo ya majimbo kadhaa ya Nigeria ambayo yanaongozwa kupitia sheria ya Kiislamu na ni makosa kwa mwanamke kuolewa zaidi ya mwanamume mmoja.

Mambo yalibadilika na kuwa mabaya wakati Bello Ibrahim mwenye umri wa miaka 40, mume wa kwanza wa Mariri aliporudi nyumbani na kumpata mwanamume mwengine amelala katika kitanda chake.

Ibrahim alikuwa ameugua kwa muda mrefu na alikua amesafiri kijijini ili kupata matibabu ambapo alikaa huko kwa takriban miaka miwili.

Anamtuhumu Mariri kwa kufunga ndoa bila yeye kujua. Lakini aliambia BBC kwamba walitalakiana.

”Alisema kwamba ameniwacha kabla aende kijijini. Ndio maana nilifunga ndoa na Bala, nilihisi kwamba nilikuwa huru aliposema kwamba amenipa talaka”, alisema.

Hatahivyo Ibrahim amekana hilo akisema kwamba hakumpa talaka na kwamba bado anamchukulia kama mkewe.

Walioana kwa takirban miaka 17 na wakajipatia watoto sita.

”Sikumuwacha. Iwapo anasisitiza kwamba nilimpa talaka ushahidi uko wapi, barua niliomuandikia iko wapi?”,

Talaka nyingi nchini Nigeria hutolewa kwa mdomo ama kupitia barua.

Wanawake Waislamu wakibeba zawadi zao katika harusi moja katika mtaa wa mabanda wa Kibera nchini Kenya

Ibrahim aliyevunjika moyo aliwasilisha malalamishi yake kwa polisi wa jimbo hilo ambapo kisa hicho k inachunguzwa na wote watatu wamechunguzwa.

Bala Abdulsalam mwenye umri wa miaka 35 ,mwanamume wa pili katika hadithi hiyo, alisema kwamba Mariri alimwambia kwamba alikuwa amewachana na mumewe na kwamba alikuwa tayari kufunga naye ndoa.

Anasema kwamba alimtumia dola 50 za Marekani kusimamia ndoa hiyo pamoja na mahari.

”Nilikuwa nje ya mji wakati nilipomtumia fedha hizo, niliporudi Kano alikuwa mke wangu”, aliambia BBC.

Anahofia kuadhibiwa iwapo mahakama za sheria zitampata na hatia za kumuo mke wa mtu mwengine.

Uhusiano huo wa miaka miwili ulisababisha mtoto kuzaliwa na sasa Mariri ni mjamzito na mtoto wa pili.

Mariri ameondoka katika nyumba hiyo, akiwawacha nyuma watoto sita na Ibrahim, huku Bala akiambiwa na polisi kutoondoka Kano kwa kuwa wanaendelea kuchunguza kesi hiyo.

Gwani Murtala , kamanda wa kituo cha polisi cha Kumbotso ambapo tukio hilo lilitokea aliambia BBC kwamba kesi hiyo ni ya kwanza kuwahi kufanyika na kwamba hakujua jinsi itakavyoisha.

-BBC

Matata sana!Wahubiri hawa ni wazushi ,matajiri na sarakasi zao kuhusu Neno la mungu ni tele

Afrika  imeshuhudia  aina mpya ya wahubiri ambao wamejipata katika vichwa vya habari kwa njia mbazo sio za kawaida .wengi wao ni kutoka Nigeria ,Afrika kusini na hata hapa nyumbani Kenya .Kutoka miujiuza bandia ,hadi kuwa na mali nyingi kupundukia –baadhi ya wahubiri hawa wana ushawishi mkubwa sana  kwa waumini wao na wanachosema ni sheria au hata hutumika kama neon kutoka kwa Mungu .

Heart-broken:Nilimpata girlfriend yangu na mwanamme mwingine siku ya Valentine!

Vitendo  vya baadhi yao hata hivyo  vimetilia doa ukweli wao na hata hadhi zao hasa machoni pa watu .Kinachoshangaza hata hivyo ni kwamba licha ya  mkinzano wa vitendo na mahubiri yao ,bado wanaaminika sana na wafuasi wao ambao huwatetea na kuwafuta kote . Kuna baadhi ya watu hasa wanawake ambao huamini na kuogopa kila wanachoambia na wahubiri wao.Kuna visa ambavyo vinajulikana  vya watu kungoja wataoana lini au ahata kuoa nani watakapoambiwa na mhubiri wao! Hii hapa orodha ya baadhi ya wahubiri wazushi na wanaojulikana kwa sababu  moja au nyingine –nzuri au mbaya .

Alph Lukau
Alph Lukau

1.Alph Lukau

Mhubiri huyu kutoka Afrika  kusini  alidai kutekeleza muujiza wa  kumreejsha hai mwanamme aliyekuwa amefariki  lakini aliamua kuondoa madai yake baada ya  kutishiwa na uwezekano wa kushtakiwa kwa kuharibu  sifa na majina ya kampuni kadhaa . Raia huyo wa Congo  kutoka kanisa la  Alleluia Ministries International  aligonga vichwa vyq habarai baada ya tukio hilo zima kunaswa katika picha za video . kando na kisa hicho , Lukau anafahamika sana kwa mambo yasio ya kawaida katika kanis ahilo huku waumini wake wakimwogopa sana kwa imani kwamba  yeye huzungumza na Mungu .

Nigel Gaisie
Nigel Gaisie

2.Nigel Gaisie

 ‘Nabii’ huyu kutoka Ghana ,aligonga vichwa vya habari mwezi uliopita kwa kusema kwamba ana uwezo wa kumrejesha hai  nyota wa mchezo wa basketball  Kobe Bryant  na binti yake Gianna walioafriki katika ajali ya helikopta. Alisema Mungu alimpa ujumbe huo kwa sharti kwamba  familia ya Kobe impe asilimia kumi ya mali yake .Wengi walioekana kuhamakishwa na matamshi yake wakisema kwamba alikuwa sasa ameingiza mzaha katika kazi ya Mwenyezi Mungu .

 

Okotie.
Okotie.

 3. Rev. Chris Okotie

  Mhubiri huyu wa kanisa la  Household of God Church, Ikeja, Lagos,  alianza sarakasi zake  za utabiri mwaka wa 2003 nchini Nigeria wakati wa uchaguzi aliposema kwamba Mungu alizungumza naye na kumtaka awanie kiti cha urais . Alishindwa na Olesegun Obasanjo . Okotie tena alirejea mwaka wa 2007 akigombea kiti cha urais chini ya chama cha  Fresh Democratic Party.  Alishindwa na  marehemu  Umaru Yar’Adua. Mwaka wa 2014 alirejea tena kwamba Mungu amemtaka awanie urais kwa mara ya tatu mwaka wa 2015   lakini akashindwa na rais  Muhammadu Buhari.

Oh No!Tazama Video Inavyoonyesha ukatili wa Jamaa akimpiga mfanyikazi wake

 

Pastor Nganga  na mkewe
Pastor Nganga na mkewe

4.Pastor James Ng’an’ga

Mhubiri wa kanisa la Neno Evangelism James Ng’ang’a  anafahamika sana nchini Kenya kwa kugonga vichwa  vya habari kwa sababu zisizo   nzuri .kutoka kwa matusi yasiofaa kutoka kwa mtu wa mungu hadi kwa majibizano na kila anayemkosoa ,James Ng’ang’a amejitambulisha kama  mhubiri mwenye uzishi sana .  Alijipata  katika kila gumzo wakati alipowakemea wahubiri wenzake wa kanisa hilo kumheshimu mke wake .Hapo ndipo jina lake la utani  ‘rubish’ ambalo yeye alilitamka kama ‘lubish’.‘ Nikikohoa mnaitika’ aliwaambia  wahubiri hao wa matawi mbali mbali ya kanisa la Neno . Hadhi  yake imegeuka sasa na kuwa kama muigizaji au mwanasarakasi .Siku hizi wengi wanamfuatilia sio kwa sababu ya mahubiri yake bali kwa ajili ya uwezekano wake kuwa mcheshi na mwanavituko  mahiri akiwa jukwaani .

Lucy Natasha
Lucy Natasha

5.Lucy Natasha

 Reverend Lucy Natasha ilidaiwa alinunua ndege ya kibinafsi Aprili mwaka wa 2019 na tangia hapo  wengi hawakoma kutaka kujua mengi kumhusu . Ingawa waumini wake wengi wanaishi katika maisha ya uchochole ,jinsi na kiasi cha ukwasi na mali anaopepesa mitandaoni ,ni hatua itakayokufanya ufikiri kwamba ni muigizaji au mwanamuziki maarufu kutok Hollywood . Ndege hiyo anayoripotiwa kununua ni sehemu tu ya vitu vingi vya bei ghali anavyodaiwa kumiliki na wengi wanahoji alikotoa mali yote hiyo katika umri wake mdogo lakini ametoa jibu akisema .

“ KUNA MAKUNDI YA WATU AMBAO WANAAMINI KUHUSU KAZI TUNAYOFANYA  KATIKA MIKUTANO NA WARSHA MBALI MBALI .MAELFU WAMEGUSWA NA WAMETOA MICHANGO YAO .PIA MKUMBUKE MIMI NI MWANDISHI WA VITABU 12  NA NINA BIASHARA NYINGI AMBAZO ZINALETA MAPATO MAKUBWA’

  Kuna wanaodai kwamba maisha yake ya kifahari yanafadhiliwa na gavana wa Nairobi Mike Sonko .Lakini anasema Sonko ni mcha mungu na muumini katika kanisa lake .

Fake Lover? Mpenzi wangu alinitoroka alipoona afya yangu imezoroteka- Jahmby Koikai asema

 

Pastor Kanyari
Pastor Kanyari

5.Victor Kanyari aka Bishop Mwangi

  Pastor Kanyari  anajulikana sana kwa miujiuza yake ‘feki’ na hata alijipata pabaya wakati makala maalum ya runinga yalipomuangazia akifanya utapeli wake .Pia amefahamika sana kwa wito na ombilake la sadaka ya shilingi 310. Baada ya kuvurugika kwa sifa  na jina lake .aliamua kubadilisha jina lake na sasa anafahamika kama  Bishop Mwangi . Chini ya  jina jipya na sifa tofauti siku hizo anaitisha sadaka ya shilingi 250  .wakati alipokuwa katika kilele cha utapeli wake ,alifanya miujiza yake kutumia kemikali ya  potassium permanganate,  iliyokuwa ikgeuka rangi kuwa ya zambarau  inapowekwa majini .

 

 

 

 

 

 

Ukahaba sio dhambi! Mahakama ya Nigeria yasema

Jaji wa mahakama kuu katika mji mkuu wa Nigeria, Abuja, amewapa wanawake elfu 16,000 za Nigeria (naira) au ($ 275) kila mmoja baada ya uamuzi kwamba kukamatwa kwao mwaka wa 2017 kulikuwa ni ukiukwaji wa haki yao ya faragha.

 

Hii ni sawa na jumla ya Sh444,000 kwa wanawake wote 16. Inaaminika kuwa wanawake hao walifungwa kwa sababu walishtumiwa kuwa makahaba.

Mahakamani, Babatunde Jacob ambaye ndiye alikuwa wakili wa wanawake hao, alisema kwamba kazi ya kufanya ukahabba haijawahi tambulika kama uhalifu, Nigeria.

Jacob also argued thatwas a violation of their “dignity… and right to private life”, a summary of the judgement says.

Jacob pia alisema kwamba “”the act of pulling down the doors of the applicants [and] indecently searching them was a violation of their dignity… and right to private life” , muhtasari wa uamuzi unasema.

Jaji Binta Nyako alisema haki za wanawake chini ya katiba zilikuwa zimekiukwa.

Katika utetezi wao, viongozi walidai kuwa wanawake hao walikuwa wamefungwa kizuizini baada ya kukiuka sehemu ya sheria ya mazingira ya Abuja, uamuzi unasema.

But Justice Nyako said constitutional rights overrode the local regulations.

She did not, however, specifically state that sex work was not a crime.

Lakini Jaji Nyako alisema haki za kikatiba zinapita zaidi ya kanuni za mitaa.
Hakusema, hata hivyo, kuwa  kazi ya ukahaba ni hatia.

 

 

Wanaume 26 waliovalia kama wanawake wakamatwa Nigeria

Wanaume 26 waliovalia kama wanawake wamekamatwa katika sherehe za siku ya kuzaliwa katika mtaa wa Kano, kaskazini mwa Nigeria, polisi wamesema.

Naibu kamanda wa polisi Tasiu Ishaq alisema vijana hao waliovalia kama wanawake, walitiwa mbaroni siku ya Jumapili.

“Ni aibu kwamba wanaume na raia wema wanaweza kuwa na tabia kama hii na kujifanya kuwa wanawake,” alisema.

Kamanda Ishaq alisema wanaume hao walikuwa “wamehubiriwa” juu ya athari za kiroho za matendo yao na wataachiliwa kwa wazazi wao.

 Mmoja wa watu walioshtakiwa aliiambia BBC kuwa rafiki yake alikuwa amemwalika kwenye sherehe hiyo na kwamba mtu ambaye ndiye mwenye sherehe alitoroka wakati polisi wa Kiisilamu walipofika.
 “Wametuhubiria na tumeomba tangu watukamate. Ninajuta kilichotokea na nitaacha tabia hii kwa neema ya Mungu, “alisema.

Kano ni moja wapo ya majimbo kaskazini mwa Nigeria ambayo inasisitiza Sharia, sheria ya dini ya Kiisilamu, ambayo imekuwa hapo tangu 2001.

Polisi wa Kiislamu wana nguvu ya kuwakamata watu wanaoamini kuwa wana vitendo ambavyo ni kinyume na sheria za Kiislamu.