Naibu wa Rais William Ruto amefutilia mbali taarifa kuwa anapinga uamuzi wa kinara wa ODM Raila Amollo Odinga wa kupitisha BBI kupitia kura ya maamuzi itakayofanywa na wananchi.
Tamko lake la kukubali kura ya maamuzi ni mshangao mkubwa baada ya wandani wake kuapa kutumia utaratibu wa bunge la kitaifa kuipitisha.
Mbunge Moses Kuria na Aden Duale walikuwa katika mstari wa kwanza kupinga wazo la kura kutoka wananchi.
Moses alikuwa anahoji kuwa uchaguzi utagharimu kiwango kikubwa cha hela.
Wengi wanahofia kuwa huenda uchaguzi ukagawanisha wakenya zaidi.
Ruto amesema kuwa mapendekezo ya BBI yanaweza kuamuliwa kupitia kura ya wananchi kama itafikia kiwango hicho.
(+ Picha) Tuzo la Victor Wanyama kwa Country Bus FC, Muthurwa Club
Aidha, Ruto amesema tatizo lililopo ni vitisho vinavyotolewa na wanaounga mkono ripoti ya BBI .
“Maoni yanayokinzana yametolewa kuhusu BBI. Ripoti tayari imewekwa wazi na wanajopo. Tumeona mapendekezo yote na tutafanya majadiliano ya kuiidhinisha.” Amesema Ruto.
+ Video) Visanga vya BBI na nyufa za Jubilee, Ruto akiombea ripoti ya BBI
Ruto alikuwa akizungumza katika hafla ya David Sankok iliyofanyika katika shule ya msingi ya Enkare-Ngiro kaunti ya Narok.
“Sio vizuri kutishiana. Vitisho havisaidii chochote. Taasisi zipo za kuhakikisha kuwa wakenya wamepata wanachotaka kwenye ripoti hiyo…”
Ruto amesema kuwa ni jambo la busara wanasiasa kukubali na kufuata sheria zilizopo katika katiba.